Naibu Waziri Kihenzile Akagua Upanuzi wa Bandari ya Pangani, Bandari ya Kipumbwi na Bandari ya Mkwaja Zilizopo Pangani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Naibu Waziri Kihenzile Akagua Upanuzi wa Bandari ya Pangani, Bandari ya Kipumbwi na Bandari ya Mkwaja Zinazotumika Kusafirisha Ndani na Nje ya Nchi Bidhaa za Mifugo, Saruji, Mbao

"Nikiwa nimeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Abdallah tumetembelea Ujenzi (upanuzi) wa Bandari ya Pangani, Bandari ya Kipumbwi na Bandari ya Mkwaja pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Viongozi" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Ziara hii imesukumwa na tukio Kubwa lilioandaliwa kwa umahiri mkubwa na Uongozi wa Wilaya ya PANGANI INVESTMENT FORUM lililofanyika Mliman City, lenye lengo la kuvutia uwekezaji Wilayani Pangani" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Imekuwa wakati mzuri kuona Bandari zinazotumika kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kwenda ndani na nje ya nchi ikiwemo Mifugo, Saruji, Mbao nk na hivyo kuunganisha nguvu katika kusukuma Maendeleo ya wana Pangani na Taifa kwa ujumla" - Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi
WhatsApp Image 2024-01-06 at 15.17.54(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-06 at 15.17.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-06 at 15.17.54.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-06 at 15.17.55.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-06 at 15.17.55(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-06 at 15.17.55(2).jpeg
 
Back
Top Bottom