Naibu Waziri Kihenzile: Serikali Kujenga Kujenga Matenki ya Kuhifadhi Mafuta (Tani 360,000)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,858
930
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imepanga kujenga matenki ya kuhifadhi mafuta (Farm Tanks) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 360,000 kwa wakati mmoja ili kufanya Meli za mafuta zisikae bandarini muda mrefu hivyo kuongeza ufanisi na kupunguza gharama kwa wateja.

Hayo yamebainika Septemba 26, 2023 wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile katika bandari ya Dar-es-Salaam.

Mhe. Kihenzile ametembelea eneo yatakapojengwa matenki ya kuhifadhi mafuta, eneo la kuhifadhi mizigo inayoharibika (perishable goods), Gati la Mafuta (KOJ), Gati Na. 1-7, Gati la Magari na Gati la Meli za kwenda Zanzibar na Visiwa vya Comoro.

Mhe. Kihenzile ameipongeza Menejimenti ya TPA na kuitaka kusimamia miradi kikamilifu ili ikamilike kwa wakati, pamoja na kuhakikisha thamani ya uwekezaji (value for money) inapatikana.

Mhemishiwa Naibu Waziri alikuwa katika ziara yake ya kwanza TPA kufuatia uteuzi wake katika nafasi hiyo hivi karibuni.

WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.11(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.14.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.15.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.15(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.16.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-28 at 16.03.17.jpeg
 
Mtajenga mnayakusanya afu yanashuka bei, mtamuuzia nani?

Twenda na data. Pipa moja la mafuta ni litters 156, hapo tuna tani 360000 ambapo tani 1 ni litter 1000.

Jumla ya mafuta yakayo kuwa store kwenye hayo matenk ni litter million 360 (360,000 × 1,000).


Last year kama sijakosea kipindi vita ua Ukraine inaendea na Russia kawaziuwa kuuza mafuta, na bei ya mafuta kuanza kupanda kutokana na scarcity h

bodi ya twakimu au ewura waliota twakwimu za matumizi ya mafunta nchi, by that time Tanzania nzima tulikua tunatumia mafuta litter 10M litter per day (ukitoa matumiazi ya migodini na uzalishaji wa umeme)

Sasa chukulia sasa tumefika litters 10 - 12M per day.

Haya ma tenk ya store litter 360M na sisi matumizi yetu ni 12M per day. Ivyo itatuchukua siku 30 kumaliza mafuta yote tani 360,000.

Ukichukua matenki yalipo na haya mapya tutakua na stock ya mafuta kwa siku 50 - hadi 60, hii economically ni sawa kwa maana bei za mafuta zina tend ku fluctuate karibia 5 - 6 month

Kumalizia tu, kujenga hayo matenki hakuta athiriwa na bei za mafuta (5% error term)
 
Back
Top Bottom