Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Serikali kupitia wizara ya ulinzi na JKT imesema kuanzia sasa utaratibu wa majeshi kuajiri raia na kuwapeleka kwenye mafunzo utasitishwa na utaanza utaratibu mpya wa kuajiri kutoka JKT. Uamuzi huo umetolewa na Waziri Nahodha ambaye pia ametoa wito pia kwa wizara ya mambo ya ndani kuagiza jeshi la polisi, magereza na zimamoto kuajiri wahitimu wa JKT na kuachana na utaratibu wa kuajiri raia wa kawaida.
Mchungaji Msigwa alikuwa sahihi aliposema akili ndogo kuongoza akili kubwa.
Ajira za raia katika sekta za jeshi haziepukiki kwa sabaubu wanajeshi kazi yao ni ile waliyochukulia mafunzo. Papo hapo jeshi linahitaji makarani, wataaalamu mbalimbali katika fani ambazo si zautendaji wa kijeshi bali wa kiofi na utal;amu mwingine katika ofisi za jeshi. Hilo lipo po pote vinginevyo huyu waziri ni mzuzu anayeongea kisiasa zaidi. Ukichukulia jambo lenyewe lilivyo haliepukiki.
Wenzetu utaona jeshi la polisi ofisi za record, na shughuli nyingine wamejaa raia wa kawaida ambao wamesomea mambo ya uhaziri na sheria. Polis ni kwenye majukumu yao huko.
Tuache siasa, tuje kwenye hali halisi ya maisha na utendaji.