figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 27,594
- 62,331
Kazi ni kwenu
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza rasmi nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya sekondari hadi elimu ya juu, hatua inayolenga kuongeza nguvu kazi na kuendeleza taaluma mbalimbali ndani ya jeshi.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, vijana watakaofanikiwa kuandikishwa watapatiwa mafunzo ya kijeshi pamoja na mafunzo ya kuwaendeleza kitaaluma, ili kuwajengea uwezo wa utendaji ndani na nje ya jeshi.
JWTZ imeweka masharti kwa waombaji kuwa raia wa Tanzania wa kuzaliwa, wenye umri usiozidi miaka 25 kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita, na miaka 28 kwa wahitimu wa elimu ya juu.
Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa na afya njema, akili timamu, tabia nzuri na asiwe na historia ya makosa ya jinai mahakamani.
Pia, waombaji wanapaswa kuwa na vyeti halisi vya kuzaliwa na vya elimu, na wasiwe wamewahi kuhudumu katika taasisi nyingine za ulinzi na usalama kama Polisi au Magereza.
Wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanahimizwa kuomba, isipokuwa wale waliopo makambini kwa sasa.
Kwa mujibu wa utaratibu huo, maombi yote yataandikwa kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi yaliyopo Msalato, Dodoma, kuanzia Aprili 15 hadi Aprili 28, 2026, yakiwa na nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya NIDA, vyeti vya kuzaliwa na elimu, pamoja na namba ya simu ya mwombaji.
Maombi hayo yatatumwa kwa anwani ya Mkuu wa Utumishi Jeshini, Makao Makuu ya Jeshi, S.L.P 194, Dodoma.