upuuzi tu!hivi mimi nikija na utaalamu wangu wa kipekee utanitaka niende JKT kupoteza muda ndio uniajiri?
hizi ni mbwembwe tu zilizokosa mashiko.....sijui tunataka kuachieve nini?wenzetu wanaimarisha weledi wa kijeshi sisi tunaongeza miguvu isiyokuwa na tija.
Naunga mkono hoja hii hapa nahodha kama kawaida yake amekurupuka kutafuta umaarufu wa kisiasa mara zote husema bila kuwaza, Jeshi letu linahitaji utaalamu sio maguvu, kama tunahitaji askari wa miguu wa mstari wa mbele sawa, lakini kapa tunahitaji utaalamu ndani ya jeshi, basi majeshi yetu pamoja na polisi waajiri kutoka kwenye soko kulingana na na utaalamu uhaohitajika, si wanafanyiwa vetting kabla ya kuajiriwa sasa wasi wasi wake nini, au ndio kuingiza siasa katika majeshi, basi anaonaje turejeshe makamisaa jeshini, kuzaa second version ya akina JK, Kinana, Ngwilizi, Nnauye, na wenzao.
Usiwe mvivu wa kufikiri Nahodha, najua unataka uwe kwenye chati kama akina Mwakyembe na Mangufuli, fanya kazi sio maneno yatakuweka katika chati, nakutabiria uhamisho mwengine JK akipangua baraza la mawaziri huna uliwezalo, sasa ndio inaonyesha wazi Karume alikuwa akikubeba tu, na Dr. Shein hakukosea kukutupa nje ni mzigo tu ndani ya serikali.
Zama za siasa za fitna zimepitwa nawakati sasa ni jinsi utakavyo perform sio kuleta chuki za kisiasa, majeshi yetu yanahitaji utaalamu wa aina mbali mbali sio kufunga na kufungua tuu, unafahamu nini wewe kuhusu jeshi hujawahi kuwa hata mgambo au valantia kule kwenu, na kama unazungumzia uzalendo ulikushinda TVZ ukaenda Arusha kufanyakazi na peace corps, so shut up.