Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
Unajuaje kwamba ni mke wako na si wewe?

Kwani heshima kuwepo ni kazima upate mtoto?

Sent from my Kimulimuli
 
Waingereza wanasema "it takes two to tango". Hivyo mimba inatungwa na wote wawili (me &ke ). Tatizo linaweza pia kuwa kwako (matatizo katika utengenezaji na usafirishaji wa mbegu za kiume) au kwa mkeo (matatizo ya kutoa yai "ovulation", magonjwa ya mishipa inayounganisha kiwanda cha mayai (ovaries) na nyumba ya mimba(uterus), mfuko wa uzazi (cervix), magonjwa ya tezi ya shingo (hypo and hyperthyroidism), unene wa kupindukia (obesity) nk.

Poleni na nendeni mkwapimwe, wewe (sperm analysis- upimaji wa mbegu za kiume), mkeo- ultrasound-nyumba ya uzazi na kipimo cha damu ,homoni ya progesterone siku saba kabla ya siku zake za mwezi (mvua kunyesha), hiki kipimo kitaonyesha kama mkeo anatoa yai (Ovulates), pia kuna vipimo vingine vya homoni kama vile FSH, LH, Testosterone, SHBG, TFT na DHEA , vifanywe katika siku ya 2,3 au 4 ya mwezi, Dakatri wako atakufanulia zaidi.

Ni vyema kufahamu kuwa, asilimia themanini ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa "reproductive age" watatunga mimba si zaidi ya mwaka mmoja wa kugegedana. Na asilimia kumi watatunga mimba chini ya miaka miwili. Waliobaki 10% ndio hao wanaotakiwa kufanyiwa uchunguzi.

Hata ikitokea kwa bahati mbaya madaktari wako hawawezi kukusaidia basi, mshukuru Mungu kwa yote.
 
Mungu aniepushe na mwanaume mwenye hasiye na akili kama wewe aisee kwa lugha hyo Mungu akurehemu kwanza ndio mengine hayo akupe.una roho mbaya sana wewe jamaa..mkeo nampa pole we hujui kina Rebeka kina Sarah huko kanisani sijui unaenda Fanya nn..

Yaani, binafsi ni mwanaume, ila kwa kweli jamaa huyo ametumia maneno machafu sana kwa mkewe.
Nilitamani, kuwa karibu naye nimpe vibao vya uso , na kanisani nimuondoe hata hiyo kazi ya ualimu ningemfuta kabisa.

Eti, oooh. Mimi Mwalimu, mara mkirsto , eti huduma kansani , naenda Kanisani, yaani ameniudhi sana.

Nina wasiwasi na kanisa lake na huo ualimu wake sijui anawafundisha watoto kitu gani kwa kweli!!
 
Nimesoma nimejikuta nashindwa kushauri kabisa dah leo akili haipo ngoja nisijichoshe
 
Sasa hivi teknolojia imekua...nendeni hospitali ijulikane haswa nini kati yenu wawili....
With tym mtapata mtoto.
Muombeni Mungu...anawatest ujue
 
Kuishi bila mtoto ni stress mkuu. Hata kama sasa hivi unaona sio ishu itafika wakati utaona ni ishu sana, na ndoa itakuwa haina Amani. Kwa sababu mijitu hainaga simile aisee, kila unapoenda mtakuwa mnaulizwa mna watoto wangapi sasa hivi? Mnangoja nini? Kwanini msiongeze? Na maswali mengine ya kijinga kama hayo. Kama kweli unampenda mkeo, zaa nje kimya kimya, utaungama mbele ya safari. Halafu huyo mtoto atakuwa wako na mkeo, sawa? Maisha yatakuwa poa tu. Ni bora uzae nje kuliko kumwacha mke unayempenda kwa ajili ya kutozaa. Angeweza kuzaa na watoto wote bahati mbaya wakafa, ungemuacha? Zaa tu sehemu maisha yasonge! Lakini wewe uko sawa? Isije kuwa na wewe hauzai aisee! Mi nimeishi miaka kibao bila mtoto kwa kujua kuwa mke hazai, kumbe mke alipotibiwa tatizo likaisha mimi ndio nikawa nina tatizo. Nilipotibiwa mimi nikapata watoto wawili kwa mpigo. KWA KIFUPI, KAMA UKO FIT, ZAA NJE TU, ENDELEZA MAISHA NA MKEO UMPENDAYE. ULIMPENDA AKIWA HANA MTOTO!
Asante kwa ushauri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje kwamba ni mke wako na si wewe?

Kwani heshima kuwepo ni kazima upate mtoto?

Sent from my Kimulimuli
Mimi sina tatizo ni mwanamke... nilipewa angalizo mapema nikadhani ni wivu. Sina mtoto wa nje ya ndoa kwa sababu ya uaminifu
 
Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
Kupata mtoto/watoto ni majaaliwa yake mwenyewe Mungu muombe Mungu atakusaidia
 
SEMEN ANALYSIS FOR MEN (UPIMAJI WA SHAHAWA NA MBEGU ZA KIUME)

Volume

2 5 milliliters is a normal volume. A very low volume indicates that the seminal vesicles may not be making enough fluid or that these ducts may be blocked. It may also indicate a problem with the prostate gland.

Sperm Count
40 million to 300 million is the normal range for the number of sperm per milliliter. Counts below 10 million are considered poor; counts of 20 million or more may be fine if motility and morphology are normal.

Motility and Velocity
2 aspects of motility will be evaluated

  • The number of active cells as a percentage of the total number of cells (rated from 0-100%, at least 50% should be active)
  • The quality of the movement of the sperm (rated from 0-4. A score of 2 or more is satisfactory.)
Morphology
At least 30% of cells should be of normal shape according to the WHO (world health organization)

Kruger (strict) morphology test
Examines the shape and size of the sperm head. Normal results are when 14% or more of the sperm have normal shaped heads. Men with less than 4% of normal shaped sperm may have a significant infertility problem.

Liquefaction
Normal semen which is liquid at ejaculation immediately coagulates into a pearly gel that liquefies within 20 minutes. Failure to coagulate and then liquefy may indicate a problem with the seminal vesicles, as would increased thickness or the presence of white blood cells.

Seminal Fructose
If no sperm are present, the semen will be tested for seminal fructose, normally produced by the seminal vesicles. If no fructose is present, congenital absence of the vas deferens or seminal vesicles or obstruction of the ejaculatory duct

Cultures
Your Doctor may test the semen and/or the urethra for the presence of ay STD's/STI`s (magonjwa ya ngono) or any other bacteria.
 
Ni inbox nikwambie kitu!
Mungu aniepushe na mwanaume mwenye hasiye na akili kama wewe aisee kwa lugha hyo Mungu akurehemu kwanza ndio mengine hayo akupe.una roho mbaya sana wewe jamaa..mkeo nampa pole we hujui kina Rebeka kina Sarah huko kanisani sijui unaenda Fanya nn..
 
Ni inbox nikwambie kitu!
Mungu aniepushe na mwanaume mwenye hasiye na akili kama wewe aisee kwa lugha hyo Mungu akurehemu kwanza ndio mengine hayo akupe.una roho mbaya sana wewe jamaa..mkeo nampa pole we hujui kina Rebeka kina Sarah huko kanisani sijui unaenda Fanya nn..
 
Mkuu kabla hujafanya maamuzi jiweke kwanza kwenye viatu vya mkeo seriously kabisa

Then ujiulize ungekuwa wewe u katika hali hiyo ungependa mkeo akutendee vipi??

Ungejisikiaje mkeo akiwa anaongea kwa watu anasema mume ananizeekea na hanizalishi???

Ungekuwa katika hali gani kuishi na mke ambaye unafahamu kabisa anaona unamzeekea afu humzalishi???

Fikiria sana mkuu na jitahifi kuishi kwa akili na mkeo kwa maana hakuna kitu kinamuuma mwanamke kama kukosa kumzalia mumewe watoto

Then tafuteni tiba ya tatizo lenu kwa ushirikiano mkitiana moyo coz ninyi ni mwili mmoja sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wanawaume wadharirishaji sana kwa wake zao!
Eti anazeeka tu
Lugha kweli hizi ndiyo za kumuelezea mkeo hata kama hajakupa mtoto?
Wewe umeisha pima kuona kama hauna tatizo?Una mtoto wa nje kujua kama unaweza zalisha?
Labda ambaye huzai ni ww unamsingizia mkeo?
 
Dada yangu aliolewa mwaka 1996 akapata mtoto mwaka 2010... Kuna dada mwingine nilisoma naye alikaa ndani ya ndoa miaka tisa bila kupata mtoto ila baadaye akazaa watoto kama wawili hivi.
Kuna watu wanachelewa kupata watoto kutokana na matatizo ya uzazi. Nendeni hospitali mkapimwe mpatiwe ufumbuzi. Kama mji wa mimba upo na kama mayai (ovary) zipo that means kama anapata period then kuna uwezekano mkubwa huko mbele akaja kuzaa...
Kuna rafiki yangu pia wamepata mtoto mwaka 2012 baada ya kukaa miaka hata wakaanza kuzeeka, sasa hv wana watoto wawili ila ukiwaona yule baba yao utadhani ni babu yao.
 
Back
Top Bottom