Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

duh kaa na mkeo sasa mwambie akuambie ukweli kilichotokea halafu mfanye maamuzi pamoja kama uzae nje uchukue mtoto mleee au iweje? hata me mkinipa milioni kumi nawafanyia favor nakubebea damu yako nakupa mtoto wenu me naendelea na maisha yangu ..... ila kwa sharti la nikisikia mnamnyanyasa i will come back sababu kukupa kiumbe kwa milioni kumi ni ndogo sana hiyo ni matunzo mkuu na wala sijakuuzia
Weweeee[emoji357]

The Great Gatsby
 
Kuna kipande hapa naona nyote mnaojadili mnakiruka.........huyu bwana mbali na kusema kuwa huyu mwanamke wake ni wa ndoa.......kuna swala alisema kuwa alishasikia minong'ono au kuambiwa story za kumuhusu huyu mkewe ambazo hakuziweka bayana ......

Na hapo ndipo nahisi kunaweza saidia kubalance hizi arguments........hebu wewe muhusika weka bayana ingawa mwanzo ulisema hauwezi sema.......funguka na kuwa muwazi kwamba ni mambo gani ambayo hao majirani walikuwa wakikueleza na kukuonya kuhusu huyo mkeo na wewe haukuwasikiliza hadi leo unaonekana kujutia kutokufuata ushauri wao......maana tusije puuza sehemu ndogo hii kumbe hapa ndipo utata umelalia.......tusije muona huyu mwanamke ni victim kumbe yeye ndiye jambazi hapa kuliko jamaa......

Hebu funguka na uwe muwazi na kama hauwezi tuambia basi usingeleta hii story yako ambayo ni wazi haipo balanced imeelezewa nusu.......

Bring the story out tuambie alifanya nini, alikuwa muhuni.....alikuwa anatoa ujauzito sana........alikuwa anatumia dawa za kulevya, ni mshirikina, nini walikwambia hao majirani kuwa muwazi!

SONY Xperia Z5 Premium
Ameshasema mkewe amepimwa amekutwa na uvimbe kwenye uzazi!
Hivi hii nayo huwa ni uamuzi wa mtu kupata uvimbe?
 
mwalimu unadharaulisha fani.unaleta stori za watu walikuambia upuuzi gani.yaani umetudharau sana na ss tuanze kukushauri uchepuke wakati hujaenda hospt.mi niliachwa kisa sizai kwa mateso sana.nimerudi home nikazunguka hospt mayai yanazalishwa,mji wa mimba uko sawa ila mirija iliziba baada ya kuifungua tuu mwezi huohuo mimba kabaki na aibu.tena alijitambisha eti rudisha kadi yangu ya bima natarajia mtoto kumbe alikuwa anatafuta wa nje na sio kunitibia Mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
wewe ulishawahi kwenda kupima? mkeo aliondolewa kizazi au la? kama majibu yote ni "NO" basi usimnyooshee kidole wala usimnyanyase, unaweza kuja kutamani dunia ipasuke. kuna watu walikuwa wamekata tamaa na kuwalaumu wanawake wao kama wewe, wakawaacha wanaenda kuzaa na wanawake nje, mke akaolewa na mtu mwingine akazaa mapacha...yule mwanaume kuja kugundua wale watoto wa nje wote sio wake, na kule mke ameshazaa na dume lingine...ndo mazingira watu huwa wanajinyonga hayo. be careful, tena careful sana. mambo ya uzazi usimlaumu mtu kwasababu yapo beyond our ability, mtu hajipendei. Mungu anao uwezo kukupatia watoto hata kama mtu hana kizazi, labda kama hauamini tu...na watoto wanaotoka kwa Mungu huwa ni wa baraka, wale wasiotoka kwa Mungu wale wa kulazimisha huwa hasara na majuto (majambazi, wauawaji wa wazazi wao, mazezeta etc).
 
Umejuaje kuwa wewe sio mwenye tatizo wakati huna hata mtoto wa kusingiziwa??
 
Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?

1. Kwenye thread yako inaonyesha hamshirikiani katika mambo yenu unaongelea nafsi yako na yake sana tu.....hajafanikiwa badala ya hamjafanikiwa.....nimetafuta badala ya tumetafuta n.k
2. Mkristo wa kweli anajua kuwa mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kwenye mafundisho ya ndoa wanaeleza waziwazi ndoa itavunyika kama utakuta mwanamke hana K ama mwanaume hana rombo lakini sio kukosa mtoto....Swala la kulima bila kupata mazao lipo hata kwenye maisha ya kawaida unalima mvua hainyeshi unalima nyani wanakula unalima mvua inakuwa kubwa kuliko.....ushauri wangu ni kuwa mwombe Mungu kama ni mapenzi yake upate mtoto upate kama si mapenzi yake yote sawa lakini pia kumbuka kuna watu wanapata watoto na wanakufa wote....wakati nataka kufunga ndoa marafiki zangu waliniambia kabla yakufunga ndoa nihakikishe nimempa mwanamke wangu mimba nikawaambia mimi ninaoa kwasababu ninampenda mke wangu either tutapata mtoto ama hatuta pata namwachia Mungu.....nikawauliza kwa hiyo asipopata mimba kabla ya harusi nifanya je nimwache nitafute anaepata mimba walikuwa kimya mpaka nikawaonea huruma
3. Ndoa ni baina ya wewe mke wako na Mungu ukianza ku entertain maneno ya watu hutakaa uwe na ndoa tulivu........
4. Inaonyesha huna mapenzi ya kweli kwa mkeo......ulivyooa ulijua hata zeeka atakuwa kijana milele? na hii inaonyesha ulimuoa kwa vile anavutia ama watu walikuwa wanasema ni mzuri........kitu cha muhimu chakuangalia kwenye kuoa ni personality na character-wachache watanielewa hapa
5. Ukijitambua utaelewa heshima haiji kwa kuwa na watoto ama kutokuwa na watoto........
 
Tafadhari sana confirmation ya kutokua na kizazi utaipata through medical concertations na sio kwa marafiki wala majirani wala ndugu zenu.inawezekana pia wewe mwanaume ukawa hauna uwezo wa kusababosha mimba kwa mujibu wa maelezo yako hujawahi kutoka nje so huna budi wewe na mkeo kwenda hospitalini kuchunguzwa.ni hayo tu kwa leo mungu akusaidie atimize haja ya moyo wako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Kwenye thread yako inaonyesha hamshirikiani katika mambo yenu unaongelea nafsi yako na yake sana tu.....hajafanikiwa badala ya hamjafanikiwa.....nimetafuta badala ya tumetafuta n.k
2. Mkristo wa kweli anajua kuwa mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kwenye mafundisho ya ndoa wanaeleza waziwazi ndoa itavunyika kama utakuta mwanamke hana K ama mwanaume hana rombo lakini sio kukosa mtoto....Swala la kulima bila kupata mazao lipo hata kwenye maisha ya kawaida unalima mvua hainyeshi unalima nyani wanakula unalima mvua inakuwa kubwa kuliko.....ushauri wangu ni kuwa mwombe Mungu kama ni mapenzi yake upate mtoto upate kama si mapenzi yake yote sawa lakini pia kumbuka kuna watu wanapata watoto na wanakufa wote....wakati nataka kufunga ndoa marafiki zangu waliniambia kabla yakufunga ndoa nihakikishe nimempa mwanamke wangu mimba nikawaambia mimi ninaoa kwasababu ninampenda mke wangu either tutapata mtoto ama hatuta pata namwachia Mungu.....nikawauliza kwa hiyo asipopata mimba kabla ya harusi nifanya je nimwache nitafute anaepata mimba walikuwa kimya mpaka nikawaonea huruma
3. Ndoa ni baina ya wewe mke wako na Mungu ukianza ku entertain maneno ya watu hutakaa uwe na ndoa tulivu........
4. Inaonyesha huna mapenzi ya kweli kwa mkeo......ulivyooa ulijua hata zeeka atakuwa kijana milele? na hii inaonyesha ulimuoa kwa vile anavutia ama watu walikuwa wanasema ni mzuri........kitu cha muhimu chakuangalia kwenye kuoa ni personality na character-wachache watanielewa hapa
5. Ukijitambua utaelewa heshima haiji kwa kuwa na watoto ama kutokuwa na watoto........
Asante kwa ushauri mzuri ndugu

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom