Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Dada yangu aliolewa mwaka 1996 akapata mtoto mwaka 2010... Kuna dada mwingine nilisoma naye alikaa ndani ya ndoa miaka tisa bila kupata mtoto ila baadaye akazaa watoto kama wawili hivi.
Kuna watu wanachelewa kupata watoto kutokana na matatizo ya uzazi. Nendeni hospitali mkapimwe mpatiwe ufumbuzi. Kama mji wa mimba upo na kama mayai (ovary) zipo that means kama anapata period then kuna uwezekano mkubwa huko mbele akaja kuzaa...
asante kwa ushauri rafiki, ila kusubiri miaka mingi kiasi hicho si ntaitwa babu? Anaingia period kama kawaida
 
mliouliza kuhusu majibu ya hospitali ni kuwa tuliambiwa ana uvimbe kwenye mfuko wa uzazi. Tulipouliza matibabu yake wakasema mpaka operesheni ili kuutoa huo uvimbe. Ambayo gharama yake ilikuwa nje ya uwezo wa kazi zetu za serikali, Pia kwa kusoma saikolojia ya aliyenipa haya majibu kuna kitu alinificha. Alinipa moyo na kuniambia kama nina haraka nifanye hiyo op, lkn pia atapona taratibu naweza subiri.
 
Boss hebu soma hapa kidogo - haya si maneno yangu.

Mwanzo 16:1-4

1 Sasa Sarai, mke wa Abramu, hakuwa amemzalia watoto wowote; lakini alikuwa na mjakazi Mmisri na jina lake lilikuwa Hagari.

2 Ndipo Sarai akamwambia Abramu: “Tafadhali sasa! Yehova amenifunga nisizae watoto.Tafadhali, lala na mjakazi wangu. Labda ninaweza kupata watoto kutokana naye.” Basi Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.

3 Ndipo Sarai, mke wa Abramu, akamchukua Hagari, mjakazi wake Mmisri, mwishoni mwa miaka kumi ya kukaa kwa Abramu katika nchi ya Kanaani, naye akampa mume wake Abramu kama mke wake.

4 Basi akalala na Hagari, naye akapata mimba.
Na hili ni Neno la Mungu...

Tatizo kuna Wayunani hapa kina espy Shunie aggyjay Sakayo geniveros Heaven Sent Heaven on Earth Curious gal Numbisa Maserati cute b dark angel et el wanaweza wasikuelewe...

Ila Wakorintho wenzangu Sky Eclat Madame S husna muba wanaweza kukuelewa....

Sina uhakika kama Wagalatia snowhite gfsonwin Madame B Evelyn Salt wako upande upi.

Neno hili liwafikie watumishi wenzangu Kaizer Daby Bonny na Saint Ivuga Popote pale walipo kwa ajili ya kuwavuvia wananakondoo ili wasipotee.
 
Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
Nenda kapime naye kwa daktari, kuna watu wametoa ushauri mzuri tu. Usihofu heshima,kuna hata mkuu WA mkoa Fulani naye ilibidi aende nje kupandikiza mbegu. Hats hivyo bado na yeye. Ila hauko peke yako, wasio na watoto ni wengi kama ambavyo wanaotoa mimba walivyo wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, ila nendeni kwa madaktari bingwa na wao watawapa ukweli. Ikibidi tafuta mbinu mbadala. Ila isije kuwa tatizo lipo kwako.
 
Mungu aniepushe na mwanaume mwenye hasiye na akili kama wewe aisee kwa lugha hyo Mungu akurehemu kwanza ndio mengine hayo akupe.una roho mbaya sana wewe jamaa..mkeo nampa pole we hujui kina Rebeka kina Sarah huko kanisani sijui unaenda Fanya nn..
Wanaume wanaoheshimika kanisani ndivyo walivyo wao no wakamilifu Ila wengine wore waovu
 
Kuna mambo mengi yamejificha ktk suala hili.

Mtoa mada unajua kabisa tatizo liko wapi, umetuficha ili upate kujua kama kuna mtu atataja sababu hiyo au hizo.

Pili, nahisi wewe ni mwongo kwa sababu huwezi jua kwamba wewe uko vizuri kama hujatoka nje ya mkeo.

Nina mengi but nikushauri uvumilie hadi kifo kiwatenganishe maana uliambiwa hivyo siku ya ndoa na hiyo si sababu ya msingi kwa ninyi kuachana.
 
MKUU MIMI SIKUPI USHAURI KWA KUWA UMEMKASHIFU MKEO KUWA ANAKUZEEKEA, KWANI ULIVYOMUOA HUKUJUA KAMA ATAZEEKA?
 
Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
pole! maisha tu jinsi yalivyo....sio kila kitu unaweza ukawa nacho (ukabarikiwa nacho)!
kiufupiii hamjajaaliwa kupata mtoto lkn pia kuna wapo ambao wana wanatupa watoto na kuna ambao wazazi wanafariki wanaacha watoto hawana wazazi! sio mbaya mkakubaliana na mkeo kutafta mtoto kwa njia hiyo...mkamlea km mtoto mliemzaa na mkampa mapenzi yote! na pengine akaja akawa mtoto mwema mwenye kuwaji kuliko hata huyo mtoto wa kumzaa mwenyewe! kila kitu kinatokea kwa sababu...na Mungu ndie anaejua zaidi! ushauri tu km nmekosea...naomba radhi

asante kwa ushauri wako mzuri
 
Kiongozi,
»Mmehangaika wapi, hospitali au kwa babu?
»Ni matatizo gani uliyoambiwa kuhusu yeye ukapuuza, wao walijua kuwa huyo mkeo ni mgumba?
»Wewe umeangalia afya yako na kujiridhisha kuwa upo sawa na kwamba unaweza kusababisha mimba?

Anyway, umeenda mbali sana kusema anakuzeekea, kwani wewe huzeeki? Unamfedhehesha mke wako wakati unajua hilo jambo linamuumiza, it's not right.

Ushauri; Nendeni hospitali yenye department nzuri ya gynecology na andrology, wawafanyie vipimo kuona tatizo liko wapi. Pesa itahusika kwa sana.

mie aliponichosaha ni pale amesema anamzeekea tu ,hapo nikaona nipite kimya
 
Jamaa huyu ni dogo na Ana roho mbaya.mtoto ni Baraka kutoka kwa Mungu.badilika kwanza mpende mkeo mtapata mtoto.mke hana tatizo.mtoto hapatikani kama mwanamke Ana stress. Baada ya kurudisha upendo.nendeni mkapime na kupata ushauri wa kitaalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom