Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

Nahitaji ushauri, mke wangu hana uzazi

ndege joni

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
689
Reaction score
1,126
Habari zenu watu wa Mungu,

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 30, naishi mkoa wa Arusha wilaya (mabano). Ni mwalimu wa sekondary, nilioa miaka kadhaa iliyopita na bahati mbaya mpaka sasa mke wangu hajafanikiwa kupata mtoto.

Nimetafuta namna nyingi za matibabu sijafanikiwa. Mbaya zaidi mke wangu nionavyo mimi kuna kitu anakijua ndani ya hili tatizo. Kuna watu walishawahi kuniambia kabla kuwa hana uzazi na haitatokea azae, ila niliona ni wivu tu.

Pia waliniambia kuwa amenidanganya vitu vingi ambavyo siwezi kuweka wazi. Kutokana na hali hii saivi mke wangu hana amani na hata sura yake imeanza kuchoka. Ninachojiuliza kwanini nilime na nisipate mazao miaka mingi?

Nahisi kukata tamaa, na huyu mwanamke anajulikana kama nini kijijini kwetu. Amenifanya nisipate mwanamke mwingine, kila nikijaribu nahisi atajua.

Naombeni ushauri, mimi mkristo mshika maadili na naheshimika kanisani. Huyu mwanamke ameanza kunizeekea na saivi sina hata mtoto wa kusingiziwa kutokana na uaminifu wangu. Naona wenzangu waliooa juzi tu wanapata watoto, mimi naumia tu.

Nifanyeje nipate watoto na heshima yangu iendelee kuwepo?
 
Haya mambo yahitaji akili ya ziada wala si ushauri,
Tafuta mwanamke pembeni azisha mausiano kama mchepuko wako na atakuzalia tu tena arusha mbona wapo wengi sana!
Ila angalizo mschana yoyote utakayekuwa naye nje ya mkeo usimweleze chochote kuhusu mambo yanayohusu ndoa yako wala akishika mimba yako muone kawaida wewe mpe matunzo ya kutosha.
 
Kiongozi,
»Mmehangaika wapi, hospitali au kwa babu?
»Ni matatizo gani uliyoambiwa kuhusu yeye ukapuuza, wao walijua kuwa huyo mkeo ni mgumba?
»Wewe umeangalia afya yako na kujiridhisha kuwa upo sawa na kwamba unaweza kusababisha mimba?

Anyway, umeenda mbali sana kusema anakuzeekea, kwani wewe huzeeki? Unamfedhehesha mke wako wakati unajua hilo jambo linamuumiza, it's not right.

Ushauri; Nendeni hospitali yenye department nzuri ya gynecology na andrology, wawafanyie vipimo kuona tatizo liko wapi. Pesa itahusika kwa sana.
 
Hivi sumu itokanayo na kuchomwa sindano za uzazi wa mpango hutibiwa kwa dawa gani?
 
Dada yangu aliolewa mwaka 1996 akapata mtoto mwaka 2010... Kuna dada mwingine nilisoma naye alikaa ndani ya ndoa miaka tisa bila kupata mtoto ila baadaye akazaa watoto kama wawili hivi.
Kuna watu wanachelewa kupata watoto kutokana na matatizo ya uzazi. Nendeni hospitali mkapimwe mpatiwe ufumbuzi. Kama mji wa mimba upo na kama mayai (ovary) zipo that means kama anapata period then kuna uwezekano mkubwa huko mbele akaja kuzaa...
 
Pole sana...

Jaribuni kutafuta ufumbuzi hospitali...

Umesema anajulikana sana... Labda anajulikana sana kwa kipi au yapi?

Cc: mahondaw
 
Watu wengi wanaamini kukosa watoto Ni kufeli maisha.Si kweli.
Mpende mkeo hata msipozaa mtasaidiana hata katika uzee wenu.Mbona Kuna wazee wengi omba omba mitaani waliozaa Hadi watoto 10.
Kuzaa sio guarantee ya kufanikiwa maisha,watoto sio benki yako Bali wewe ndiye benki ya watoto.
Ridhika na Hali.Je Kama wewe ndiye mwenye tatizo,akikudump utahisije?
 
Umepita hospital?
Kama bado naona tatizo liko kwako.
Umeshashindwa kumpa suport mkeo anaishi kwa stress unadhani hata mwili utakaa sawa kupokea mimba?
Kama hamjafanya vipimo kafanye.
Ukishapima uje hapa nitampatia mkeo dawa free of charge kama tatizo lake linatibika.

love thé love or hâte thé love.....
 
Boss hebu soma hapa kidogo - haya si maneno yangu.

Mwanzo 16:1-4

1 Sasa Sarai, mke wa Abramu, hakuwa amemzalia watoto wowote; lakini alikuwa na mjakazi Mmisri na jina lake lilikuwa Hagari.

2 Ndipo Sarai akamwambia Abramu: “Tafadhali sasa! Yehova amenifunga nisizae watoto.Tafadhali, lala na mjakazi wangu. Labda ninaweza kupata watoto kutokana naye.” Basi Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.

3 Ndipo Sarai, mke wa Abramu, akamchukua Hagari, mjakazi wake Mmisri, mwishoni mwa miaka kumi ya kukaa kwa Abramu katika nchi ya Kanaani, naye akampa mume wake Abramu kama mke wake.

4 Basi akalala na Hagari, naye akapata mimba.
 
u mean ...........
apewe housegirl ikiwezekana?
 
Mungu aniepushe na mwanaume mwenye hasiye na akili kama wewe aisee kwa lugha hyo Mungu akurehemu kwanza ndio mengine hayo akupe.una roho mbaya sana wewe jamaa..mkeo nampa pole we hujui kina Rebeka kina Sarah huko kanisani sijui unaenda Fanya nn..
 
Boss hebu soma hapa kidogo - haya si maneno yangu.

Mwanzo 16:1-4

1 Sasa Sarai, mke wa Abramu, hakuwa amemzalia watoto wowote; lakini alikuwa na mjakazi Mmisri na jina lake lilikuwa Hagari.

2 Ndipo Sarai akamwambia Abramu: “Tafadhali sasa! Yehova amenifunga nisizae watoto.Tafadhali, lala na mjakazi wangu. Labda ninaweza kupata watoto kutokana naye.” Basi Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.

3 Ndipo Sarai, mke wa Abramu, akamchukua Hagari, mjakazi wake Mmisri, mwishoni mwa miaka kumi ya kukaa kwa Abramu katika nchi ya Kanaani, naye akampa mume wake Abramu kama mke wake.

4 Basi akalala na Hagari, naye akapata mimba.

UNAMAANISHA NINI HAPA
 
Kwa kweli umetumia lugha mbaya sana dhidi ya mkeo.

Natamani ngekuzaba vibao ndiyo maudhi uliyonisababishia yangenitoka.

Any way, mpende mkeo hata yeye atakuwa hafurahii hali hiyo na ndiyo maana unamuona ana huzuni.

Kwa kifupi, ukimuacha mkeo kwa sababu hiyo, usitarajie kuwa na mtu mwingine utakaye kuwa na raha. Unaweza ukapata watoto ila ukakosa amani.

Be careful.
 
Back
Top Bottom