Nahitaji msaada wa kufungua bima ya matibabu

Nahitaji msaada wa kufungua bima ya matibabu

Kwa sasa niko mbali kidogo lakini hiyo siyo ishu.

Nikipata mtu wa uhakika naweza kumtumia kupitia MoneyGram halafu yeye akamrushia kwa kupitia local money transfer services.....
Mtu wa uhakika ni Max au AshaDii, kama bado hujafanya hivyo pls do it now, wewe ni Rais wa wazee wa box hii pesa inayotakiwa wazee wa box watano tu member wa JF mnamaliza.

Mimi sijatulia bado niko kwenye wakati mgumu sana nimeshakuwa deputy Father after death of my Father, ila nitamsaidia kupata bima ya NHIF kupitia vikundi.
 
Mtu wa uhakika ni Max au AshaDii, kama bado hujafanya hivyo pls do it now, wewe ni Rais wa wazee wa box hii pesa inayotakiwa wazee wa box watano tu member wa JF mnamaliza.

Mimi sijatulia bado niko kwenye wakati mgumu sana nimeshakuwa deputy Father after death of my Father, ila nitamsaidia kupata bima ya NHIF kupitia vikundi.
Pole kwa maswahibu hayo broh Mungu akutie nguvu uvuke hapo....

aggyjay atashkuru sana kwa msaada wako wa bima
 
Hello,
Kwa jina naitwa Jacqueline mkazi wa Dar es salaam, umri wangu ni miaka 25.Najitokeza kuomba msaada wa matibabu kwa mtu yeyote atakaeguswa kusaidia.

Nilikuwa na mpango wa kufanikisha hili mwenyewe lakini kabla sijafanikiwa nikakumbwa na haya matatizo matatizo yanayonisumbua ni maumivu ya mgongo hasa kwenye pingili za chini za uti wa mgongo(lumbar spine),kulegea kwa misuli ya mguu joint za magoti zina nguvu pungufu na zaidi kwa asilimia hamsini kwenye joint ya kisigino(ankle),tatizo baya zaidi ni foot drop(hali ya kulegea au kuanguka mguu wa chini).

Pia maumivu kama ya kuungua upande wa kulia wa tumbo kwa chini, maumivu haya yanadumu mchana na usiku.

Matatizo haya yalinianza mwezi January rasmi dalili zilianza taratibu mwili unashikwa na uchovu, ngozi ukiigusa inauma,misuli inalegea,maumivu ya tumbo,uoni hafifu(blurred vision) mwili unakosa balance na kuyumba(nina tatizo la sikio linaitwa sensorinurial hearing loss kutokana na damage kwenye cochlea.Sifahamu nililipataje aidha kwa vipigo udogoni au sindano za kwinini).

Tatizo la sikio limeharibu balance yangu lakini hili tatizo jingine la mguu limezidisha.

Mwezi Machi nilipelekwa Muhimbili wakanilaza kwa siku nne na kunifanyia kila kipimo cha damu lakini hawakuona tatizo.Wakafanya ct scan ya ubongo haikuonyesha tatizo.Wakaniruhusu nirudi wakiniandikia ugonjwa waliohisi wao unaitwa Charcot Marie Tooth. Ni ugonjwa wa kurithi(genetical) sababu ugonjwa huu dalili yake kuu mojawapo ni foot drop ambayo ninayo.Lakini huu ugonjwa hushambulia kuanzia utotoni kama magonjwa mengine ya kurithi kama pumu kifafa etc. Nami udogoni sijawah umwa ugonjwa wowote zaidi ya malaria ambayo iliishia nilipofika miaka kumi na mbili, kwa zaidi ya miaka kumi sijawahi umwa wala kwenda hospitali mpaka liliponisibu hili.

Walinipa dawa za kupunguza maumivu miguuni kwani nilikuwa nikilala usiku miguu inauma nakuwa restless hadi asubuhi.
Wakaniandikia nije kufanya kipimo kinaitwa Nerve conducting test..ni cha misuli lakini kufika daktari akabadili akaandika nipimwe MRI ya lumbar spine nayo baada ya wiki nkaletewa majibu hamna tatizo.

Kurudi kwa Daktrai(ni neurologist) akaniandikia dawa za aina tatu fluconazole,amitriptyline na methylpredinisolone.Hiyo dawa ya tatu ni sindano ambayo moja kwa siku ni elfu sitini.Nikaandikiwa kumi ambayo ni laki sita.

Ni hiyo dawa ndio tiba kuu kutokana na ughali wake nikachelewa kuipata lakini nilipoitumia nilipata nafuu ndogo na sikwenda tena tangu mwezi wa tano.

Lakini mpaka sasa matatizo yote bado yapo. Natembea kama vile nataka kupanda ngazi kuepuka kujikwaa sababu sina control ya misuli ya miguu ya chini tena.Siwezi kuchezesha vidole vya miguu, ni kama vimeparalaizi.Siwezi vaa viatu vya wazi kama malapa au sandals sababu vidole havina nguvu ya kushikilia viatu.Navaa raba tu kwani hazihitaji juhudi na nguvu za vidole.mazoezi yananipa relief ya muda tu kwa siku hayaondoi tatizo.

Maumivu ya tumboni bado yapo,nina hofu ni kiungo ndani yangu kina tatizo.Naishi kwa hofu muda wote nina hofu hata nikipita karibu na moto nnaweza nikakosea hatua nikauangukia.

Nasali sana na maombi naombewa sana.Haya yote ni kutokana na watu wangu wa karibu kupotezea suala la afya yangu niliwaomba lakini naona kila mmoja yupo bize na mambo yake wananipita siku zinaenda na manunuzi wanafanya.Siwezi kuwalazimisha tena.

Kama kuna watakaoguswa nikapona sawa nawakaribisha.

Tayari nina mawasiliano ya kampuni ya bima ya Jubilee na kiasi kinachoendana na umri wangu wamenitajia ni 707,475 ambapo ntapata bima ya JCARE kwa mwaka mzima.

Nimeona hiyo sababu tatizo langu ni kubwa bima ya AFYA WOTE wamesema wamesitisha kwa muda
Ntajitahidi kutuma picha za documents za hospital.
nakaribisha maswali kwa yeyote alienayo,japo sitojibu ndani ya mda lakini ntayajibu yote.natumia simu ya mtu.
asanteni.
Pole, patafute hapa
Inst-image-3.jpg
 
huyu nliwahi onana nae..kuomba maombi ya binafsi anataka utoe hela ndo uingie room kuonana nae..na dau lake linaanzia laki tatu na nusu.
sitaki kumuona!!!
Pole sana sister, leo ndo naona andiko lako, nami naahidi kutoa kidogo nilichonacho, pia ukimudu kufika Kimara Korogwe kwenye kanisa la KKKT Ushirika wa Kimara korogwe kwaajili ya maombi itapendeza zaidi.
 
Back
Top Bottom