Nahitaji msaada wa kufungua bima ya matibabu

Kwanza nikupe pole, tena pole ya kutoka moyoni.

Kwa sasa upo na dawa gani? Au mbali na bima umepanga kufanya nini kingine kwa ajili ya matibabu yako?
 
Nakupa pole na pia nikujulishe kuwa mimi huwa nipatapo nafasi uombea wagonjwa wote ambao Hupitia majaribu ila huwa ni mitihani tu huwa nawaombea Mungu awasamehe dhambi zao nankuwaponya tafahdl tutakuombea pili kuwa waz mimi naisi maradhi yako sio ya kutibiwa hospital kwa hishu pingili plz kuna mitishamba inatibu kabsa mkuu.
 
Hello,
kwa jina naitwa Jacqueline mkazi wa Dar es salaam.umri wangu ni miaka 25
najitokeza kuomba msaada wa matibabu kwa mtu yeyote atakaeguswa kusaidia.
nlikua na mpango wa kufanikiaha hili mwenyewe lakini kabla sijafanikiwa nkakumbwa na haya matatizo
matatizo yanayonisumbua ni maumivu ya mgongo hasa kwenye pingili za chini za uti wa mgongo(lumbar spine),kulegea kwa misuli ya mguu joint za magoti zina nguvu pungufu na zaidi kwa asilimia hamsini kwenye joint ya kisigino(ankle),tatizo baya zaidi ni foot drop(hali ya kulegea au kuanguka mguu wa chini).
Pia maumivu kama ya kuungua upande wa kulia wa tumbo kwa chini.maumivu haya yanadumu mchana na usiku.
matatizo haya yalinianza mwezi January rasmi..dalili zilianza taratibu mwili unashikwa na uchovu.ngozi ukiigusa inauma,misuli inalegea,maumivu ya tumbo,uoni hafifu(blurred vision) mwili unakosa balance na kuyumba(nina tatizo la sikio linaitwa sensorinurial hearing loss.kutokana na damage kwenye cochlea.sifahamu nililipataje aidha kwa vipigo udogoni au sindano za kwinini)
tatizo la sikio limeharibu balance yangu lakini hili tatizo jingine la mguu limezidisha.
mwezi march nlipelekwa muhimbili wakanilaza kwa siku nne na kunifanyia kila kipimo cha damu lakini hawakuona tatizo.wakafanya ct scan ya ubongo haikuonyesha tatizo.wakaniruhusu nirudi wakiniandikia ugonjwa waliohisi wao unaitwa Charcot Marie Tooth.ni ugonjwa wa kurithi(genetical)..sababu ugonjwa huu dalili yake kuu mojawapo ni foot drop ambayo ninayo.lakini huu ugonjwa hushambulia kuanzia utotoni kama magonjwa mengine ya kurithi kama pumu kifafa etc.nami udogoni sijawah umwa ugonjwa wowote zaidi ya malaria ambayo iliishia nlipofika miaka kumi na mbili..kwa zaidi ya miaka kumi sijawahi umwa wala kwenda hospital mpaka liliponisibu hili.
walinipa dawa za kupunguza maumivu miguuni kwani nlikua nkilala usiku miguu inauma nakuwa restless hadi asubuhi.
wakaniandikia nije kufanya kipimo kinaitwa Nerve conducting test..ni cha misuli.lakini kufika doc akabadili akaandika nipimwe MRI ya lumbar spine nayo baada ya wiki nkaletewa majibu hamna tatizo
kurudi kwa doc(ni neurologist) akaniandikia dawa za aina tatu fluconazole,amitriptyline na methylpredinisolone .
hiyo dawa ya tatu ni sindano ambayo moja kwa siku ni elfu sitini.nkaandikiwa kumi ambayo ni laki sita.
ni hiyo dawa ndio tiba kuu kutokana na ughali wake nkachelewa kuipata lakini nlipoitumia nlipata nafuu ndogo.na sikwenda tena tangu mwezi wa tano.
lakini mpaka sasa matatizo yote bado yapo.natembea kama vile nataka kupanda ngazi kuepuka kujikwaa sababu sina control ya misuli ya miguu ya chini tena.siwezi kuchezesha vidole vya miguu.ni kama vimeparalaizi.siwez vaa viatu vya wazi kama malapa au sandals cz vidole havina nguvu ya kushikilia viatu.navaa raba tu kwani hazihitaji juhudi na nguvu za vidole.mazoezi yananipa relief ya mda tu kwa siku hayaondoi tatizo.
maumivu ya tumboni bado yapo.nna hofu ni kiungo ndani yangu kina tatizo.naishi kwa hofu mda wote..nna hofu hata nkipita karibu na moto nnaweza nkakosea hatua nkauangukia.
nasali sana na maombi naombewa sana.haya yote ni kutokana na watu wangu wa karibu kupotezea swala la afya yangu..nliwaomba lakini naona kila mmoja yupo bize na mambo yake.wananipita siku zinaenda.na manunuzi wanafanya.siwezi kuwalazimisha tena..kama kuna watakaoguswa nikapona sawa nawakaribisha.tayari nina mawasiliano ya kampuni ya bima ya Jubilee.na kiasi kinachoendana na umri wangu wamenitajia ni 707,475 ambapo ntapata bima ya JCARE kwa mwaka mzima.nimeona hiyo sababu tatizo langu ni kubwa.bima ya AFYA WOTE wamesema wamesitisha kwa mda
Ntajitahidi kutuma picha za documents za hospital.
nakaribisha maswali kwa yeyote alienayo,japo sitojibu ndani ya mda lakini ntayajibu yote.natumia simu ya mtu.
asanteni.
Dah pole sanaaa tena sanaaaa Mungu ata kufanyia wepesi
 
Pole sana mpendwa Mungu atakisikia kilio chako. Labda ungeomba michango kwa watakaoguswa ili mwenye mia 2 mia 5 kupitia mitandao ya simu watoe mpaka ifike hiyo pesa ya bima ya afya unayatamani kuipata asante.
 
asante mkuu.niko tayari kwa hilo pia
 
Kwanza nikupe pole, tena pole ya kutoka moyoni.

Kwa sasa upo na dawa gani? Au mbali na bima umepanga kufanya nini kingine kwa ajili ya matibabu yako?
kwa sasa sina dawa yoyote zaidi ya kufanya mazoezi tu.licha ya bima nna mpango wa kuwa na biashara hata ndogo ntaifanyia zaidi online na kumtumia mtu wa kudeliver mzigo cz hali yangu hainiruhusu kutembea mbali.siwezi.
ila bado sina
 
Nakupa pole na pia nikujulishe kuwa mimi huwa nipatapo nafasi uombea wagonjwa wote ambao Hupitia majaribu ila huwa ni mitihani tu huwa nawaombea Mungu awasamehe dhambi zao nankuwaponya tafahdl tutakuombea pili kuwa waz mimi naisi maradhi yako sio ya kutibiwa hospital kwa hishu pingili plz kuna mitishamba inatibu kabsa mkuu.
asante mkuu.maombi yako nayahitaji.huo wote ndo ukweli nloandika sijaficha kitu..kama madawa ya mitishamba unayajua pia sawa unsweza nisaidia siyafahamu
 
Pole sana kwa maumivu unayopata, ila hongera kwa juhudi ulizochukua ili kujua tatizo liko wapi.

Nashauri uongee na jf admins/moderators, wapate uhakika wa unachosema ili waruhusu uweke contacts zako hapa, mwenye nacho kidogo akusaidie. Naamini utasaidika ili upate unachohitaji.

Again, pole sana.
 
asante mkuu.ntafanya hivyo
 
Kweli aisee tufanye jambo
 
Back
Top Bottom