Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

hii inategemea na Kabila lenu, huyu kakwambia Mama mkwe ndio kapiga simu kwa mwanae na kataka aongee na kidume (ni KOSA)
nanshauri AMPIGE chini huyo mwanamke na aendelee kuthamini biashara zake zitampa heshima
Kuna makabila mengine Mwanamke anarudishwa nyumbani akakae na Mkwe ajifunze adabu kukutana ni Krismas, sasa huyu hata kuPrint mashine si zake ati pesa kwanza HANA ADABU
kumnyenyekea MCHUMBA ni ulimbukeni atafute mwenye Heshima, na Mama mkwe haruhusiwi kuhoji siri za unyumba, atulie
Umeongea vizuri sana mkuuu...asante kwa ushauru murua
 
mleta mada Naona kama ulianza kuji-deffence kwa wasomaji ambayo ni sisi


million 4.2


labda ulete picha hapa
 
Odhiambo, jamaa amesema binti alihamia bila ruhusa yake, jamaa alimwambia asubiri kwanza kwasababu pesa aliyokuwa nayo ameitumia kumfungulia ofisi na kwamba anahitaji muda ili kuwa na utayari wa kumchukua kama mke, lakini umesikia aliposafiri akakuta huku nyuma binti amehamia (kwa nguvu), na hii nilishaiona hata mimi, dada anaambiwa na wa kwao hamia kwa jamaa ili tuje tumdai mahali, na mara nyingi mabinti wamekuwa wakufuata maelekezo ya familia zao, (mbaya sana hii) sasa jamaa anapowambia hayuko vizuri kwa muda huu wanamjia juu, maswala ya kulia mahali yanataka maridhiano, namuelewa sana mleta mada, naamini aanaona kama vile anafanywa deal, naamini alikuwa na nia njema sana na ndio maana aliweza kumfungulia ofisi mchumba wake, (hilo peke yake wazazi wa binti walitakiwa washukuru), inaonekana hata akimuoa huyo binti ataishia kwenye conflicts za kila siku na hiyo familia
Ok , hata hivyo kuishi naye kama mke bila kukamilisha taratibu napo si sawa.

Wanawake wote ni wajanja, na hasa wanapokabiliwa na matatizo ya kiuchumi na wakati mwingine ujauzito . Lakini pia wanatumia udhaifu wa wanaume kuwaonea aibu kutimiza malengo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mk
Mkuu mm nilimkatalia kuwa kwa sasa sijajipanga subiri siku nikikutolea mahali ndio uhamie kwangu kwangu kaongea na ndugu zake na akawaaga ....iweje tena niingie kwenye majukumu ambayo sina bajeti nayo
Ulipokubali kuubeba msalaba basi na majukumu yakupasayo uyakabili mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasukuma mna tabu sana ndo maana Mama yetu huwa Hana raha kwasababu ya majibu nakupenda ubabe.

KILL soft MANENO MATAMU ila action wanasema huyuu atakuwa kalogwa.
 
mama wakwe usipowakazia watakupangia hata jinsi ya kumla tunda mtoto wao..

hongera usio Kwa shuruti.
 
Wanajukwaa habarini ,natumaini hamjambo na mko poa ...

Nimeleta swala hapa naomba mnishauri au mm ndio namtazamo mbaya kabla sijachukua reaction yoyote

Kuna binti mmoja nipo kwenye uhusiano na yeye kwa muda kama wa miaka 3 ...mwaka jana niliamua niende juzi nilienda kwao kujitambulisha na nikatoa kishika uchumba

Baada ya kurudi maisha yaliendelea kila mmoja akiwa anaishi kwake ...

Kwa kuwa tulikuwa tunaishi mbalimbali nikaona nimuwezeshe mwenzangu nikamfungulia biashara ya jumla kama milion 4 .2

Lengo lilikuwa tuwe tunasaidiana katika maisha na yeye nimpe kazi apate kazi rasmi

Baada ya mwezi mmoja nilianza kuona kama utofauti ...nilienda na kaxi pale ofcn kwa mchumba wangu nikamwambia nifanyie kuprint ....page zilikuwa kama kumi jibu nililopewa nikaambiwa no money no service
Niliingiwa na hasira nikamjibu pale pale hivi vitu vyoye nani alinunua??

Nikaamua kuondoka nikarudi ofcn nikafungua nikaprint ile kazi ofcn japo ilikuwa jion sana

Baada kama ya wiki akaniambia naomba nihamie kwako !! Ili tuanze kuishi pamoja umeshajitambulisha tayari kwetu

Nikamjibu nipe muda nitakujibu....kila tulipokuwa tunakutana alisisitiza jambo lile lile

....Nikamwambia ongea na ndugu zako sio waje wasikie upo kwangu halafu waanze kunisumbua ,akanijibu tayari nimeongea

Siku moja nilisafiri kikazi niliporudi tayari nilimkuta kahamishia vitu vyake vyote vipo kwangu. ..nikapigwa nabutwaa tu kwa kuwa ufunguo wa nyumba huwa tumegawana

Tatizo lilipoanzia
majuzi mama yake kampigia cm walikuwa wanaongea kwa kiruga ila kwa kuwa kilikuwa ni kibantu kuna maneno niambulia kuyasikia baadae akamwambia mpe simu ...mumeo akanipa

Tuliongea vizuri salamu na baadae akaanza sasa wewe umekuja kujitambulisha ,halafu umeenda jumla ...haujarudi tukupangie mahali

Nikamwambia mama swala la mahali bado najipanga nitakapokuwa tayari nitakuja ..akajibu yaani wewe mpaka sasa hivi haujajipanga tu

Ikabidi nimtolee uvivu ...nikamwambia wewe unajua uchumi wangu ? Unajua mipango yangu ...nikamwambia kwani mahali ni lazima au ni zawadi
akanijibu mm naitaka mahali si unajua uko na binti yangu huyo ni binadamu ... Mara nataka nile mahali kabla sijafa

Nikamjibu nimekuelewa ila sifikirii leo au kesho kuleta mahali ...kama kuna mwanaume mwingine anataka kuleta mahali pokeeni binti yenu aolewe

Baada ya kukata cm mchumba wangu aakaanza yaani unamjibu mama yangu hivyo kweli nikamwambia ulitaka nimjibu vipi?

Nilikulazimisha uhamie kwangu ? Mbn ndugu zako sio wastarabu hivi hawaoni juhudi nilizozifanya kwako kukukwamua na kukufungulia ofisi ...kwa sasa sina hela ..

Nikamwambia na wewe kama unaona mm sina dira ya maisha yako chapa mwendo ..hiyo ofisi chukua vitu vyot
Mkunje Samaki angali mbichi kwani akishakauka ukimkunja atavunjika na hilo siyo jambo jema kwa mja.
 
Umepanic mkuu sipati picha siku rasmi ukienda kutoa mahari mama mkwe wako utamuangalia kwa jicho gani?ila na hawa wa mama sio wastaarabu
 
hii inategemea na Kabila lenu, huyu kakwambia Mama mkwe ndio kapiga simu kwa mwanae na kataka aongee na kidume (ni KOSA)
nanshauri AMPIGE chini huyo mwanamke na aendelee kuthamini biashara zake zitampa heshima
Kuna makabila mengine Mwanamke anarudishwa nyumbani akakae na Mkwe ajifunze adabu kukutana ni Krismas, sasa huyu hata kuPrint mashine si zake ati pesa kwanza HANA ADABU
kumnyenyekea MCHUMBA ni ulimbukeni atafute mwenye Heshima, na Mama mkwe haruhusiwi kuhoji siri za unyumba, atulie
Ukwajuu >>>>>>>>
 
Nahisi tunataka tufanane kimajibu ila hata mimi nimejichunguza ila sio vizuri lazima tujenge mazoea yakujizuia kutoa majibu yasiyopendeza.

Ipo hivi, mimi nipo kwenye mahusiano ila mwanzo mwanzo mama mkwe aliniletea pigo kama hizo...... Mwanzoni nilimvumilia ila mwisho wasiku nilichoka nikaanza kumpa faka kama hizo mpaka akanihara in short kwasasa heshima anapoongea namimi inshu yoyote lazima ajipange vizuri.

Ila nimegundua sio vizuri yaani nimetokea kujishtukia jinsi mama mkwe anavyoniogopa mpaka natamani nipate manzi mpya namama mkwe mpya ili nianzishe mahusiano mapya yenye misingi yakuheshimiana nafamilia ya mwanamke toka mwanzo.

Ila yote yayote hayakuwa makosa yangu nimakosa yamama mkwe wangu natabia yake aliyokuwa nayo yakunivaa nakusahau mimi nimkwe wake.

Ila mama mkwe wako nayeye nikiboko kwanini asiwasiliane nawashenga wako kwa inshu kama hizo zamahari au kwanini asimtumie mtoto wake kuongea nawewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wewe ndiye mwenye utata! Kwanza ushasema mpo katika mahusiano kwa takribani miaka 3, Je ndani ya miaka yote hiyo bado hujajipanga tu?? Pia kama uliweza kumpatia demu huyo mtaji wa Miln hizo 4.2 , kwanini usingeanza na kulipa mahari kwanza?...Sasa hapo kwa misimamo yako hiyo mkitibuana nae akaolewa dume mwingine huoni kuwa itakula kwako? Pia uwe adabu na adabu unapoongea watu wa rika la wazazi wako hata kama unawazidi cheo au kipato lakini kule kuwa wazazi wa mwenzako tayari ni wazazi wako, hivyo wanapokukosea jaribu kuchuja majibu unayoyatoa! Wakati mwingine majibu au matusi kwa wazazi wetu hupa laana zisizokuwa za lazima! Kaa chini ujitathmini upya, kama vipi shirikiana na wife mdundulize pesa , mmalizane na wazazi, tambua kuwa kitendo tu cha kumgegeda bint yao kwa miaka yote hiyo bila asante kwa wazazi ni makosa!
 
Ukwajuu >>>>>>>>
mm na hawa mamawakwe siwapendi kabisa (na huenda ni single mother au naye kamkalia babamkwe kwenye paji la uso)
jamaa hajaoa kaanza kubanwa
akioa ndio kafa kabisa
papuchi hapewi mpaka akajenge kwa wakwe
bao ni usiku tu mara moja kwa mwezi malipo kitenge
hapo dogo hajajenga, ila duka pesa asiulize atafute ingine
AMPIGE CHINI asipojirekebisha
 
nimekuelewa vema...kamatia hapo hapo.....wasikuzowee......
 
Hapo kwa upande wa wote kuna shida tena kubwa sana.

Nikiianza na mwanaume, akumbuke kuwa yule mama wa binti ni kama mama yake mzazi hata kama anamapungufu hayo. Kitendo cha kumjibu mama wa binti majibu ya ovyo alimkosea sana, nadhani hata mama yake vile.

Kumbuka binadamu tunatofautina, lakini yeye kama mtu anayetegemea kuwa kichwa cha nyumba na sio mkia, angemjibu kwa lugha nzuri na sio kama alivyomfanyia mama wa binti.

Na kumfungulia mke mtarajiwa biashara, hakufanya kosa isipokuwa isipokuwa kosa kubwa alilolifanya ni kumdhihirishia mchumba kwamba biashara ile anaimiliki kwa 100% na ndio maana kila kitu alikiandika kwa jina lake. Angefanya hivi, ile biashara binti aitambue kwamba ni ya mwanaume au mchumba mtarajiwa na si kama alivyofanya yeye.

Tunakuja kwa binti, kitendo alichofanya cha kuwambia jamaa yake No money No Service ni kitendo cha ubinafsi mkubwa sana, sidhani kama kumfanyia kazi jamaa kungeweza kuleta hasara katika ofisi yake. Inaonekana binti si muungwana kabisa, kuna mambo mengine ni ya utani na kuna mambo mengine si ya utani.

Kitendo alichofanya cha kuhamia kwa jamaa, hapo hakufanya kosa baada ya kuona jamaa tayari nyumbani kwao kajitambulisha na wanamjua, na ndio maana jamaa aliamua kumpokea kwa mikono miwili.

Kikubwa, mwanaume ajitambue na mwanamke pia ajitambue maana hao pamoja ndio watakaoenda kuijenga familia na sio mama mkwe.

Watambue jinsi ya kuchukulian na kuelimishana na sana mwanaume maana yeye ndio kiongozi na atakuwa kiongozi wa familia na wanawake inabidi tuishi nao kwa akili na upendo mkubwa sana kwani kila mmoja tunaishi kwa kutegemea. Mwanaume hawezi ishi peke yake bila mke hali kadhalika mwanamke pia.
Asipokuelewa hapa basi atakuwa anashida jamaa yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binafsi naona kama ulijipanikisha tu bila sabau.yan hakukua na sababu ya kumjibu huyo maza hivyo.Ungemwambia tu mama nitakuja soon.Kila akipiga unamwambia hivyo hivyo.

NB
Kuongea ongea ma vilugha kwangu SITAKI.
Hapo kwenye mavilugha ndo wamesababisha wanaficha nini sasa?hata mi ningezingua tu inawezekana walikuwa wananiteta
 
Mkuu ngoja nimtetee mleta mada.
Huyo mama ametoa wapi ujasiri wa kupiga simu kumdai mkwe mtarajiwa aje atoe mahali haraka?
Kwanini huyo mwanamke amlezimisha na kuharakisha kuishi na jamaa?

Hayo mambo ya kuharakisha mambo muhimu kama uchumba na ndoa yanakuja kufanya mmojawapo au wote wajute kwanini ilifanyika hivyo.

Hicho kitendo ni kati ya vitu vibaya sana wanawake wanafanya hasa kwa kushirikiana na mama au dada zao kupanga mkakati wa kumfanya mwanaume flani amuoe ndugu yao hata kabla ya muoaji kuona muda tayari au mambo aliyotaka yamekamilika.

Hapo kuna uwezekano huyu muoaji akashindwa kufanya mambo flani ya kimaendeleo sababu ya kuoa na kuzaa mapema.
Kuna mambo huwezi kujitoa au kujilipua kama umeshaoa au una watoto.

Mleta mada shika msimamo wako hadi mipango yako itakapo kaa sawa au utakapoona muda umefika. Usilazimishwe kuingia kwenye hayo maagano na majukumu mazito kabla hujajiweka tayari kiakili na kimwili maana ikitokea mitihani kidogo tu mtafarakana na kujijengea jina baya kwa jamii.

Jamii zetu za kiafrika zinapenda sana kuweka mashinikizo kwa ndugu, jamaa na marafiki kubeba mzigo wa ndoa wakati wahusika hawajajiandaa kiuchumi, kimwii na akili.

Sema mleta mada nae ajidhibiti mdomo wake, kuna kauli za kuongea na wakubwa zetu hata kama wanakosea na kutukera.
Hapo mwisho nimekuelewa chief,,

Ila ktk kumtetea bado aisehh,,

Kumbuka mama ni mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye mavilugha ndo wamesababisha wanaficha nini sasa?hata mi ningezingua tu inawezekana walikuwa wananiteta
siipendi kabisaa hii tabia.Mtu unakuta mmekaa mob halaf wadau wawil out of no where wanaanza kutwanga kilugha..siipendi hii tabiaa.
 

Attachments

  • images(2).jpg
    images(2).jpg
    8.3 KB · Views: 10

Similar Discussions

Back
Top Bottom