Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Wanajukwaa habarini ,natumaini hamjambo na mko poa ...

Nimeleta swala hapa naomba mnishauri au mm ndio namtazamo mbaya kabla sijachukua reaction yoyote

Kuna binti mmoja nipo kwenye uhusiano na yeye kwa muda kama wa miaka 3 ...mwaka jana niliamua niende juzi nilienda kwao kujitambulisha na nikatoa kishika uchumba

Baada ya kurudi maisha yaliendelea kila mmoja akiwa anaishi kwake ...

Kwa kuwa tulikuwa tunaishi mbalimbali nikaona nimuwezeshe mwenzangu nikamfungulia biashara ya jumla kama milion 4 .2

Lengo lilikuwa tuwe tunasaidiana katika maisha na yeye nimpe kazi apate kazi rasmi

Baada ya mwezi mmoja nilianza kuona kama utofauti ...nilienda na kaxi pale ofcn kwa mchumba wangu nikamwambia nifanyie kuprint ....page zilikuwa kama kumi jibu nililopewa nikaambiwa no money no service
Niliingiwa na hasira nikamjibu pale pale hivi vitu vyoye nani alinunua??

Nikaamua kuondoka nikarudi ofcn nikafungua nikaprint ile kazi ofcn japo ilikuwa jion sana

Baada kama ya wiki akaniambia naomba nihamie kwako !! Ili tuanze kuishi pamoja umeshajitambulisha tayari kwetu

Nikamjibu nipe muda nitakujibu....kila tulipokuwa tunakutana alisisitiza jambo lile lile

....Nikamwambia ongea na ndugu zako sio waje wasikie upo kwangu halafu waanze kunisumbua ,akanijibu tayari nimeongea

Siku moja nilisafiri kikazi niliporudi tayari nilimkuta kahamishia vitu vyake vyote vipo kwangu. ..nikapigwa nabutwaa tu kwa kuwa ufunguo wa nyumba huwa tumegawana

Tatizo lilipoanzia
majuzi mama yake kampigia cm walikuwa wanaongea kwa kiruga ila kwa kuwa kilikuwa ni kibantu kuna maneno niambulia kuyasikia baadae akamwambia mpe simu ...mumeo akanipa

Tuliongea vizuri salamu na baadae akaanza sasa wewe umekuja kujitambulisha ,halafu umeenda jumla ...haujarudi tukupangie mahali

Nikamwambia mama swala la mahali bado najipanga nitakapokuwa tayari nitakuja ..akajibu yaani wewe mpaka sasa hivi haujajipanga tu

Ikabidi nimtolee uvivu ...nikamwambia wewe unajua uchumi wangu ? Unajua mipango yangu ...nikamwambia kwani mahali ni lazima au ni zawadi
akanijibu mm naitaka mahali si unajua uko na binti yangu huyo ni binadamu ... Mara nataka nile mahali kabla sijafa

Nikamjibu nimekuelewa ila sifikirii leo au kesho kuleta mahali ...kama kuna mwanaume mwingine anataka kuleta mahali pokeeni binti yenu aolewe

Baada ya kukata cm mchumba wangu aakaanza yaani unamjibu mama yangu hivyo kweli nikamwambia ulitaka nimjibu vipi?

Nilikulazimisha uhamie kwangu ? Mbn ndugu zako sio wastarabu hivi hawaoni juhudi nilizozifanya kwako kukukwamua na kukufungulia ofisi ...kwa sasa sina hela ..

Nikamwambia na wewe kama unaona mm sina dira ya maisha yako chapa mwendo ..hiyo ofisi chukua vitu vyot
Kwa jicho langu la tatu[emoji28] nahisi kuna kitu apo!! Iweje from no where mtu anataka muishi wote alafu ukifikilia na alivyo kujibu siku uliyo mpelekea kazi nadhani huyo binti atakua kashapigwa mimba na akupakazie wewe.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh. Kabila gani hilo wamama wanaongelea mambo ya mahari
 
Godface, ni kweli mahari ni zawadi, na ni kweli pia mawasiliano yako na mamakwe hayakuwa mazui. Lakini, lakini si vizuri kukaa kinyumba na mtoto wa mtu bure, bure kabisa. Utazaa mtoto utapata uzoefu. Labda kwa sasa ujana unawasumbua kidogo .

Ulipomruhusu huyo mama kuhamia kwako , ujue ilitakiwa uyafanye majukumu ya mume . Ikiwa ni pamoja na kumalizana na family yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Odhiambo, jamaa amesema binti alihamia bila ruhusa yake, jamaa alimwambia asubiri kwanza kwasababu pesa aliyokuwa nayo ameitumia kumfungulia ofisi na kwamba anahitaji muda ili kuwa na utayari wa kumchukua kama mke, lakini umesikia aliposafiri akakuta huku nyuma binti amehamia (kwa nguvu), na hii nilishaiona hata mimi, dada anaambiwa na wa kwao hamia kwa jamaa ili tuje tumdai mahali, na mara nyingi mabinti wamekuwa wakufuata maelekezo ya familia zao, (mbaya sana hii) sasa jamaa anapowambia hayuko vizuri kwa muda huu wanamjia juu, maswala ya kulia mahali yanataka maridhiano, namuelewa sana mleta mada, naamini aanaona kama vile anafanywa deal, naamini alikuwa na nia njema sana na ndio maana aliweza kumfungulia ofisi mchumba wake, (hilo peke yake wazazi wa binti walitakiwa washukuru), inaonekana hata akimuoa huyo binti ataishia kwenye conflicts za kila siku na hiyo familia
 
I see mpaka nimesisimka mwili. Wewe hujielewi hata kidogo. Tatizo unalo kubwa. Kwanza umempata binti muelewa,ila wewe ndio unawajaribu watu huna nia ya kuoa,ndio maana hata majibu yako ya ovyo. Nafikiri kiburi chako kinatokana na kipato ulichonacho. Kwa hiyo unajimwambafai kwamba hawa masikini nawawezesha mimi watanifanya nini?. Tukija kwenye swala la kuoa nako umekosea sana. Kwa nini usiwaone kwanza wakushauri ni namna gani inakuwa. Ni yale yale ya kujimwambafai kwamba kwa sbb unazo basi wewe ni kila kitu. Unakosea sana. Kawaida ukishapeleka kujitambulisha,maana yake uko tayari kuoa,maana yake hapo unaomba wakupangie mahali. Na haitakiwi izidi miezi 6. Nina uhakika hata mkioana huyo mke wako atapata shida sana kwako kwa majibu hayo. Una hatua ndefu za kujirekebisha,hata namna ya kumjibu mtu kwa uvumilivu. Bahati mbaya unaweza kukuta ni tabia yako tu,ukiamua kubadirika,utakuwa unabadirika kwa muda unarudia kule kule,ama unabadirika kwa kiasi. Jipange upya muombe msamaha mkeo na mama mkwe pia kwa kwa majibu yako kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Binti anaejilewa "analazimishia" ku move in?
Hapo hamna anaejielewa (wote tuu, bibi, bwana na mama mkwe)
 
Saf Sana mkuu wew ndo mwanaume Hongera kwa roho Ngumu hiyo ndo dalili za uanaume kwanza Hiv kuna watu wanatoaga mahar Mpaka sasahiv
 
Mimi sio mwanamke mkuu. I'd za wanawake zinatafsiriwa vipi? Hicho ni kifupi cha jina langu. Tukija kwenye mada wanaume wengi tunakosea sehemu kama hizo. Ndio maana hata mke ukimuoa,mkaishi miaka labda mitano,siku mkitibuana unamfukuza kama mbwa anaondoka kama alivyo na nguo alizovaa. Je ile miaka mi5 unafikiri hajasaidia kuzalisha chochote?. Je bila wewe kumchukua unahisi asingekuwa amesonga mbele kimaendeleo au hata kuolewa na mwingine?. Tukija kwa huyu,ile hali ya mke kumuambia hela kutoa copy,kuna jambo hapo huyu njemba hajaweka wazi,kuna uwezekano aliongea utani au alitaka kumuonyesha mume kwamba anaijua kuilinda hela aliyompatia,anaijua biashara. Huyu elewa tayari amempotezea muda yule binti kwa kipindi chote kwa kipindi alichompa matumaini ya kuishi nae. Vinginevyo alikuwa anawapata wachumba lakini anawakataa kwa ajili ya huyu. Au angeweza hata kufanya shughuri nyingine ingempatia kipato zaidi ya hicho,au hata kisipofikia hicho. Kwa hiyo huwezi kumuacha aende zake ktk muda wote uliompotezea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, kwa hiyo mleta mada yeye ndio hajapotezewa muda ??
 
Umewahi ongea na Mama yako mzazi kwa kumfokea hata kama yeye ndio kakukosea???Leo umeongea naye ivo, nikwamba hauna mpango kabisa wakumtolea mahari huyo binti???

Nakama upo, utajisikiaje siku sasa ukienda kutoa mahari ???.

Huenda Mama mkwe wako anadhan uchumi upo... mueleweshe tu, mama pesa niliona kwanza nimuwezeshe mwenzangu n.k kisha nijipange nitoe mahari.

So upo tayari kumpoteza mwanamke na uwekezaji uloufanya kwaajili yenu wawili... Sababu tu ya kauli zako????

Kumbuka kua, sio kila siku mwanamke mpumbavu ndio huboa nyumba yake...Siku hizi wanaume ndo wanaongoza kubomoa nyumba.

Baadhi ya mambo usipende tumia 'Ukanda wa ziwa', wacha Busara na Hekima vifanye kazi...... Na muhesabu mwenzako kama Sehem yako.
Hongera sana mkuu. Umemfafanulia maneno yenye busara sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Odhiambo, jamaa amesema binti alihamia bila ruhusa yake, jamaa alimwambia asubiri kwanza kwasababu pesa aliyokuwa nayo ameitumia kumfungulia ofisi na kwamba anahitaji muda ili kuwa na utayari wa kumchukua kama mke, lakini umesikia aliposafiri akakuta huku nyuma binti amehamia (kwa nguvu), na hii nilishaiona hata mimi, dada anaambiwa na wa kwao hamia kwa jamaa ili tuje tumdai mahali, na mara nyingi mabinti wamekuwa wakufuata maelekezo ya familia zao, (mbaya sana hii) sasa jamaa anapowambia hayuko vizuri kwa muda huu wanamjia juu, maswala ya kulia mahali yanataka maridhiano, namuelewa sana mleta mada, naamini aanaona kama vile anafanywa deal, naamini alikuwa na nia njema sana na ndio maana aliweza kumfungulia ofisi mchumba wake, (hilo peke yake wazazi wa binti walitakiwa washukuru), inaonekana hata akimuoa huyo binti ataishia kwenye conflicts za kila siku na hiyo familia
Umeongea vizuri kaka!! Asante sana kwa ufafanuzi
 
Kwanza Ulikosea kumjibu Mama mkwe wako ivo.

Inawezekana kabisa kabisa, ulimfungulia Mradi huo sababu ya mahaba anayokupa nawewe kutamani kumuweka karibu yako zaidi...

SASA ilo haliondoi ukweli yakua unatakiwa Kumtolea Mahari.

Inamaana kwakua umemfungulia mradi , basi usitoe mahari ????

KAMA SHIDA NI PESA, basi Kaa ongea nao kwa heshima tu .

Acha Jeuri zako !!.... na inavyoonekana wewe, Siku akiamua kurudi kwao mpaka utoe mahari, utamnyang'anya na kiofisi ulichompa.

Na hiii unamaanisha, Humchukulii kama Mwanamke wa maisha yako..Bali kama MTU ulomsaidia kutoka ktk maisha magumu .

Akikufia ndani ??? Utawaeleza nn ??

ACHA MARA MOJA UJINGA!!....
Sana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote wewe msichana na mkweo mna makosa....

Mama mkwe hakutakiwa kuongoea na wewe kuhusu lini unaenda kutoa mahari na kukulazmsha kabisa kwamba uende hlo jambo lilitakiwa libakie kwako na huyo dada.

Ila mkuu na wewe inaonekana una ego, just imagine hayo majibu angekua anapewa mzazi wako naamin huyu dada sasa hivi mngekua tayar mmeshaachana...
Hata kama huyu mama alikulazmsha sana kuzungumzia ndoa ila kama mwanaume ulitakiwa ku hold hasira zako kwa maana yule ni mzaz wa msichana wako so kuna heshima lazma iwepo.

Wa mwisho ni huyu msichana inaonekana yuko sana desparate na ndoa kuliko kitu kingne inawezekana kwasababu zake binafsi au presha ya family members, kitendo cha kulazmisha kuhamia kwako tena kipind umesafir haikua busara kabisa alitakiwa kuendelea kubakia kwao mpka muda rasm ila may b pia aliogopa kupoteza future yake.

NB: Sasa mkuu hata kama biashara ni yako ulitaka uende ukafanye printing bure, alikua sahihi kukwambia no money no service ili ujue kutofautisha biashara na mambo binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakazia kwenye NB yako kuna amri moja ya drug dealers inasema "Always keep your family and business completely separated"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,hivi ikitokea tu mwanamke from no where analazimisha kuhamia kwako mazima,kama huna mipango nae utakubali?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww hujawahi kulazimishwa kunywa bia na ulikuwa hauna mpango wa kunywa bia muda huo offer tu ndio zikakupelekea kunywa
 
Mkuu,hivi ikitokea tu mwanamke from no where analazimisha kuhamia kwako mazima,kama huna mipango nae utakubali?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Two wrongs does not make the first wrong right.
Ndo maana nimemaliza kwa kusema wote watatu hawajielewi (mwanaume,mwanamke na mama mkwe). Wewe naona unataka kuwa exempt mwanamke na mama yake kutoka kwenye kutojielewa Swet-R
 
Ww hujawahi kulazimishwa kunywa bia na ulikuwa hauna mpango wa kunywa bia muda huo offer tu ndio zikakupelekea kunywa
Kama sina mpango,siwezi kukubali. Pili kwamba wewe ulipewa offer ya kumtumia huyo demu halafu ukishamjua uanzishe mgomo?. Baada ya huyo ukimpata mwingine nae utampiga chenga hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom