Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Nahisi mama mkwe anatikisa kiberiti

Nimjibu aliyesema akikufia ndani itakuaje ? Ukikaa na mwanamke ndani zaidi ya miezi 6 ni mke wako . Awe mtu mzima aliyeamua mwenyewe kunifuata . Nitamzika kama mke wangu .Ondoa imani za kidini !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry, wanawake wenye kipato kikubwa sasa hivi ni wengi saana, sheria yako hapo inasemaje ?,
Sawa mkuu,mbona iko wazi kama mwanamke ndio kaanzisha mgomo wa kuachana. Yeye mwanamke pia anamlipa mwanaume. Mfano rejea USA wanasanii waimbaji na waigizaji ,wengi tu wanawake wamewalipa fidia wanaume wanaovunja uchumba au ndoa nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea vizuri kaka!! Asante sana kwa ufafanuzi

Kosa la kwanza ulilofanya ni kumfungulia biashara mwanamke ambae sio mke wako. Kitendo hicho kimewafanya ndugu zake wakuone wewe una hela kwahiyo huwezi kushindwa kulipa mahari.
Ndio maana sasahivi ukiwaambia unajipanga na huna hela hawawezi kukuelewa.

Ila pia kutokana na arguments zako nafikiri hujawahi kua na nia ya kumuoa huyo binti. Ungekua na nia kweli ya kuoa, hiyo milioni nne unayodai kutumia kumfungulia steshenari ungeitumia kumlipia mahari na kumuoa, halafu akishakua mke wako ndio muanze kupanga maisha yenu na kuangalia ni kipi cha kufanya kama familia.

Lakini pia tusi-rule out possibility ya kwamba wewe nawe hujielewi wala hujui ni nini unachotaka!
- Umeenda kujitambulisha kwa mwanamke kwa hiari
- Umemfungulia biashara kwa hiari yako
- Amehamia kwako kwa nguvu na umeendelea kuishi nae hadi leo
- Hapo hapo unadai huna mpango wa kumtolea mahari, lakini unaishi nae!
- Ukiulizwa unakua mkali na kutoa majibu ya kejeli
- Umefungua uzi kuomba ushauri ambao kimsingi unaonekana huutaki.

Mimi nafikiri wote tumeshaona tatizo lilipo.
 
Hakuna gharama yeyote kujibu kwa heshima na ustahimilivu. Umepata faida yeyote ulivyojibu hivyo
 
Mi namuangalia tu kwa sasa kama wamedanganyana na binti yake .....itakula kwake yaani hata kama nilikuwa nataka kutoa sitoi mwaka huu wala mwakani ...mpk halimashauri ya kichwa changu itakaporidhia wakiona nazingua wamwambie binti yao aondoke kwangu
Safi sana mkuu ,wee upo kama Mimi mama mkwe anazingua kinyama anajifanya mropokaji sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hay
Kama sina mpango,siwezi kukubali. Pili kwamba wewe ulipewa offer ya kumtumia huyo demu halafu ukishamjua uanzishe mgomo?. Baada ya huyo ukimpata mwingine nae utampiga chenga hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ni mawazo wako sikuzuii kuamini hivyo ila cjawahi kunyenyekea mwanamke sababu ya papunchi wakati zipo zimejaa tele
 
Wanajukwaa habarini ,natumaini hamjambo na mko poa ...

Nimeleta swala hapa naomba mnishauri au mm ndio namtazamo mbaya kabla sijachukua reaction yoyote

Kuna binti mmoja nipo kwenye uhusiano na yeye kwa muda kama wa miaka 3 ...mwaka jana niliamua niende juzi nilienda kwao kujitambulisha na nikatoa kishika uchumba

Baada ya kurudi maisha yaliendelea kila mmoja akiwa anaishi kwake ...

Kwa kuwa tulikuwa tunaishi mbalimbali nikaona nimuwezeshe mwenzangu nikamfungulia biashara ya jumla kama milion 4 .2

Lengo lilikuwa tuwe tunasaidiana katika maisha na yeye nimpe kazi apate kazi rasmi

Baada ya mwezi mmoja nilianza kuona kama utofauti ...nilienda na kaxi pale ofcn kwa mchumba wangu nikamwambia nifanyie kuprint ....page zilikuwa kama kumi jibu nililopewa nikaambiwa no money no service
Niliingiwa na hasira nikamjibu pale pale hivi vitu vyoye nani alinunua??

Nikaamua kuondoka nikarudi ofcn nikafungua nikaprint ile kazi ofcn japo ilikuwa jion sana

Baada kama ya wiki akaniambia naomba nihamie kwako !! Ili tuanze kuishi pamoja umeshajitambulisha tayari kwetu

Nikamjibu nipe muda nitakujibu....kila tulipokuwa tunakutana alisisitiza jambo lile lile

....Nikamwambia ongea na ndugu zako sio waje wasikie upo kwangu halafu waanze kunisumbua ,akanijibu tayari nimeongea

Siku moja nilisafiri kikazi niliporudi tayari nilimkuta kahamishia vitu vyake vyote vipo kwangu. ..nikapigwa nabutwaa tu kwa kuwa ufunguo wa nyumba huwa tumegawana

Tatizo lilipoanzia
majuzi mama yake kampigia cm walikuwa wanaongea kwa kiruga ila kwa kuwa kilikuwa ni kibantu kuna maneno niambulia kuyasikia baadae akamwambia mpe simu ...mumeo akanipa

Tuliongea vizuri salamu na baadae akaanza sasa wewe umekuja kujitambulisha ,halafu umeenda jumla ...haujarudi tukupangie mahali

Nikamwambia mama swala la mahali bado najipanga nitakapokuwa tayari nitakuja ..akajibu yaani wewe mpaka sasa hivi haujajipanga tu

Ikabidi nimtolee uvivu ...nikamwambia wewe unajua uchumi wangu ? Unajua mipango yangu ...nikamwambia kwani mahali ni lazima au ni zawadi
akanijibu mm naitaka mahali si unajua uko na binti yangu huyo ni binadamu ... Mara nataka nile mahali kabla sijafa

Nikamjibu nimekuelewa ila sifikirii leo au kesho kuleta mahali ...kama kuna mwanaume mwingine anataka kuleta mahali pokeeni binti yenu aolewe

Baada ya kukata cm mchumba wangu aakaanza yaani unamjibu mama yangu hivyo kweli nikamwambia ulitaka nimjibu vipi?

Nilikulazimisha uhamie kwangu ? Mbn ndugu zako sio wastarabu hivi hawaoni juhudi nilizozifanya kwako kukukwamua na kukufungulia ofisi ...kwa sasa sina hela ..

Nikamwambia na wewe kama unaona mm sina dira ya maisha yako chapa mwendo ..hiyo ofisi chukua vitu vyot
Una jazba sana kijana, badilika chalii angu,,

Ukiendelea na hyo tabia hakika mahusiano yako yatakuwa up & down

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother it seems your degree of tolerance is second to bad. Unamjibuje hivo mama wa Mpenzi wako! Mama wa mchumba wako!? Ili ionekane kwamba uendeshwi? Ili ionekane kwamba hupangiwi?

Umekosea Sana Kaka, huwezi kuonesha msimamo kwa kumdhalilisha mama wa mwenzako! Yawezekana ni kweli una msimamo lkn Kuna Kuna namna ya kutofautiana na mtu!

Siyo Leo au Kesho? Kweli tata?

" Mama, naelewa vizuri kuhusu Jambo hili, na liko katika vipaumbele vyangu, sema kwa Sasa hali yangu kiuchumi haijakaa sawa! Lakini, najitahidi kupigana nalo, kuhakikisha kwamba nalimaliza. Mungu akinijaalia mama, nitatuma ugeni kwa ajili ya Shukrani hiyo! Naomba unipe muda mama yangu, na nawashukruni Sana kwa kunivumilia"

Hapa ujaonesha kwamba lini utapeleka! Lakn hata mchumba wako, usiku angekupa papuchi mubashara kutokana na kumjibu mama yake kwa heshima! Wakt wew umeenda na moja kichwani Kama zile hesabu za vidudu/chekechea!


Badilika Kaka! Kama una dada nasi tutamjibu hivo mama yako! Pole kwa kupanic, lkn jifunze kuheshimu wazazi wa wenzako!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
binafsi naona kama ulijipanikisha tu bila sabau.yan hakukua na sababu ya kumjibu huyo maza hivyo.Ungemwambia tu mama nitakuja soon.Kila akipiga unamwambia hivyo hivyo.

NB
Kuongea ongea ma vilugha kwangu SITAKI.
 
Kosa la kwanza ulilofanya ni kumfungulia biashara mwanamke ambae sio mke wako. Kitendo hicho kimewafanya ndugu zake wakuone wewe una hela kwahiyo huwezi kushindwa kulipa mahari.
Ndio maana sasahivi ukiwaambia unajipanga na huna hela hawawezi kukuelewa.

Ila pia kutokana na arguments zako nafikiri hujawahi kua na nia ya kumuoa huyo binti. Ungekua na nia kweli ya kuoa, hiyo milioni nne unayodai kutumia kumfungulia steshenari ungeitumia kumlipia mahari na kumuoa, halafu akishakua mke wako ndio muanze kupanga maisha yenu na kuangalia ni kipi cha kufanya kama familia.

Lakini pia tusi-rule out possibility ya kwamba wewe nawe hujielewi wala hujui ni nini unachotaka!
- Umeenda kujitambulisha kwa mwanamke kwa hiari
- Umemfungulia biashara kwa hiari yako
- Amehamia kwako kwa nguvu na umeendelea kuishi nae hadi leo
- Hapo hapo unadai huna mpango wa kumtolea mahari, lakini unaishi nae!
- Ukiulizwa unakua mkali na kutoa majibu ya kejeli
- Umefungua uzi kuomba ushauri ambao kimsingi unaonekana huutaki.

Mimi nafikiri wote tumeshaona tatizo lilipo.
Mkuu umeanza kum crash mtoa mada halaf umeishia kujijibu mwenyewe maswali ambayo nilitaka kukuuliza, binafsi sijaona tatizo kubwa la mleta mada, kama ulivyosema, alienda mwenyewe kujitambulisha, that means alikuwa ana nia ya dhati ya kumuoa huyo binti, kosa limeanzishwa na mama mkwe kuja kufosi alipwe mahali eti aile kabla hajafa, sijui anajua atakufa lini ?!, kuna jamaa yangu mmoja hapa kijijini kwetu ameishi na mwanmake kwa miaka minane na alikuwa hajaenda kwao kujitambulisha (hivi majuzi ndio wamekororfishana wakatengana) naomba mumshauri huyo mamamkwe wa mleta mada ndio ajirekebishe, afuate utaratibu, aombe mahali taratibu atapewa, wanaume wengi sana hawajlipa mahali na wanaishi na wanawake zao vizuri.
 
Brother it seems your degree of tolerance is second to bad. Unamjibuje hivo mama wa Mpenzi wako! Mama wa mchumba wako!? Ili ionekane kwamba uendeshwi? Ili ionekane kwamba hupangiwi?

Umekosea Sana Kaka, huwezi kuonesha msimamo kwa kumdhalilisha mama wa mwenzako! Yawezekana ni kweli una msimamo lkn Kuna Kuna namna ya kutofautiana na mtu!

Siyo Leo au Kesho? Kweli tata?

" Mama, naelewa vizuri kuhusu Jambo hili, na liko katika vipaumbele vyangu, sema kwa Sasa hali yangu kiuchumi haijakaa sawa! Lakini, najitahidi kupigana nalo, kuhakikisha kwamba nalimaliza. Mungu akinijaalia mama, nitatuma ugeni kwa ajili ya Shukrani hiyo! Naomba unipe muda mama yangu, na nawashukruni Sana kwa kunivumilia"

Hapa ujaonesha kwamba lini utapeleka! Lakn hata mchumba wako, usiku angekupa papuchi mubashara kutokana na kumjibu mama yake kwa heshima! Wakt wew umeenda na moja kichwani Kama zile hesabu za vidudu/chekechea!


Badilika Kaka! Kama una dada nasi tutamjibu hivo mama yako! Pole kwa kupanic, lkn jifunze kuheshimu wazazi wa wenzako!


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, unalahisisha saana, wamama wa siku hizi hasa hao wa huko mjini nao midomo yao haina breki, kijana mmoja aliulizwa unalipa lini mahali akajibu bado najipanga, akaulizwa na mamamkwe, Unajipanga wewe umekuwa matofali ?, wamama hawa hawana maana.
 
Hapo kwa upande wa wote kuna shida tena kubwa sana.

Nikiianza na mwanaume, akumbuke kuwa yule mama wa binti ni kama mama yake mzazi hata kama anamapungufu hayo. Kitendo cha kumjibu mama wa binti majibu ya ovyo alimkosea sana, nadhani hata mama yake vile.

Kumbuka binadamu tunatofautina, lakini yeye kama mtu anayetegemea kuwa kichwa cha nyumba na sio mkia, angemjibu kwa lugha nzuri na sio kama alivyomfanyia mama wa binti.

Na kumfungulia mke mtarajiwa biashara, hakufanya kosa isipokuwa isipokuwa kosa kubwa alilolifanya ni kumdhihirishia mchumba kwamba biashara ile anaimiliki kwa 100% na ndio maana kila kitu alikiandika kwa jina lake. Angefanya hivi, ile biashara binti aitambue kwamba ni ya mwanaume au mchumba mtarajiwa na si kama alivyofanya yeye.

Tunakuja kwa binti, kitendo alichofanya cha kuwambia jamaa yake No money No Service ni kitendo cha ubinafsi mkubwa sana, sidhani kama kumfanyia kazi jamaa kungeweza kuleta hasara katika ofisi yake. Inaonekana binti si muungwana kabisa, kuna mambo mengine ni ya utani na kuna mambo mengine si ya utani.

Kitendo alichofanya cha kuhamia kwa jamaa, hapo hakufanya kosa baada ya kuona jamaa tayari nyumbani kwao kajitambulisha na wanamjua, na ndio maana jamaa aliamua kumpokea kwa mikono miwili.

Kikubwa, mwanaume ajitambue na mwanamke pia ajitambue maana hao pamoja ndio watakaoenda kuijenga familia na sio mama mkwe.

Watambue jinsi ya kuchukulian na kuelimishana na sana mwanaume maana yeye ndio kiongozi na atakuwa kiongozi wa familia na wanawake inabidi tuishi nao kwa akili na upendo mkubwa sana kwani kila mmoja tunaishi kwa kutegemea. Mwanaume hawezi ishi peke yake bila mke hali kadhalika mwanamke pia.
 
Umewahi ongea na Mama yako mzazi kwa kumfokea hata kama yeye ndio kakukosea???Leo umeongea naye ivo, nikwamba hauna mpango kabisa wakumtolea mahari huyo binti???

Nakama upo, utajisikiaje siku sasa ukienda kutoa mahari ???.


Huenda Mama mkwe wako anadhan uchumi upo... mueleweshe tu, mama pesa niliona kwanza nimuwezeshe mwenzangu n.k kisha nijipange nitoe mahari.



So upo tayari kumpoteza mwanamke na uwekezaji uloufanya kwaajili yenu wawili... Sababu tu ya kauli zako????


Kumbuka kua, sio kila siku mwanamke mpumbavu ndio huboa nyumba yake...Siku hizi wanaume ndo wanaongoza kubomoa nyumba.



Baadhi ya mambo usipende tumia 'Ukanda wa ziwa', wacha Busara na Hekima vifanye kazi...... Na muhesabu mwenzako kama Sehem yako.
Mkuu ngoja nimtetee mleta mada.
Huyo mama ametoa wapi ujasiri wa kupiga simu kumdai mkwe mtarajiwa aje atoe mahali haraka?
Kwanini huyo mwanamke alilazimisha na kuharakisha kuishi na jamaa?

Hayo mambo ya kuharakisha mambo muhimu kama uchumba na ndoa yanakuja kufanya mmojawapo au wote wajute kwanini ilifanyika hivyo.

Hicho kitendo ni kati ya vitu vibaya sana wanawake wanafanya hasa kwa kushirikiana na mama au dada zao kupanga mkakati wa kumfanya mwanaume flani amuoe ndugu yao hata kabla ya muoaji kuona muda tayari au mambo aliyotaka yamekamilika.

Hapo kuna uwezekano huyu muoaji akashindwa kufanya mambo flani ya kimaendeleo sababu ya kuoa na kuzaa mapema.
Kuna mambo huwezi kujitoa au kujilipua kama umeshaoa au una watoto.

Mleta mada shika msimamo wako hadi mipango yako itakapo kaa sawa au utakapoona muda umefika. Usilazimishwe kuingia kwenye hayo maagano na majukumu mazito kabla hujajiweka tayari kiakili na kimwili maana ikitokea mitihani kidogo tu mtafarakana na kujijengea jina baya kwa jamii.

Jamii zetu za kiafrika zinapenda sana kuweka mashinikizo kwa ndugu, jamaa na marafiki kubeba mzigo wa ndoa wakati wahusika hawajajiandaa kiuchumi, kimwii na akili.

Sema mleta mada nae ajidhibiti mdomo wake, kuna kauli za kuongea na wakubwa zetu hata kama wanakosea na kutukera.
 
Wanajukwaa habarini ,natumaini hamjambo na mko poa ...

Nimeleta swala hapa naomba mnishauri au mm ndio namtazamo mbaya kabla sijachukua reaction yoyote

Kuna binti mmoja nipo kwenye uhusiano na yeye kwa muda kama wa miaka 3 ...mwaka jana niliamua niende juzi nilienda kwao kujitambulisha na nikatoa kishika uchumba

Baada ya kurudi maisha yaliendelea kila mmoja akiwa anaishi kwake ...

Kwa kuwa tulikuwa tunaishi mbalimbali nikaona nimuwezeshe mwenzangu nikamfungulia biashara ya jumla kama milion 4 .2

Lengo lilikuwa tuwe tunasaidiana katika maisha na yeye nimpe kazi apate kazi rasmi

Baada ya mwezi mmoja nilianza kuona kama utofauti ...nilienda na kaxi pale ofcn kwa mchumba wangu nikamwambia nifanyie kuprint ....page zilikuwa kama kumi jibu nililopewa nikaambiwa no money no service
Niliingiwa na hasira nikamjibu pale pale hivi vitu vyoye nani alinunua??

Nikaamua kuondoka nikarudi ofcn nikafungua nikaprint ile kazi ofcn japo ilikuwa jion sana

Baada kama ya wiki akaniambia naomba nihamie kwako !! Ili tuanze kuishi pamoja umeshajitambulisha tayari kwetu

Nikamjibu nipe muda nitakujibu....kila tulipokuwa tunakutana alisisitiza jambo lile lile

....Nikamwambia ongea na ndugu zako sio waje wasikie upo kwangu halafu waanze kunisumbua ,akanijibu tayari nimeongea

Siku moja nilisafiri kikazi niliporudi tayari nilimkuta kahamishia vitu vyake vyote vipo kwangu. ..nikapigwa nabutwaa tu kwa kuwa ufunguo wa nyumba huwa tumegawana

Tatizo lilipoanzia
majuzi mama yake kampigia cm walikuwa wanaongea kwa kiruga ila kwa kuwa kilikuwa ni kibantu kuna maneno niambulia kuyasikia baadae akamwambia mpe simu ...mumeo akanipa

Tuliongea vizuri salamu na baadae akaanza sasa wewe umekuja kujitambulisha ,halafu umeenda jumla ...haujarudi tukupangie mahali

Nikamwambia mama swala la mahali bado najipanga nitakapokuwa tayari nitakuja ..akajibu yaani wewe mpaka sasa hivi haujajipanga tu

Ikabidi nimtolee uvivu ...nikamwambia wewe unajua uchumi wangu ? Unajua mipango yangu ...nikamwambia kwani mahali ni lazima au ni zawadi
akanijibu mm naitaka mahali si unajua uko na binti yangu huyo ni binadamu ... Mara nataka nile mahali kabla sijafa

Nikamjibu nimekuelewa ila sifikirii leo au kesho kuleta mahali ...kama kuna mwanaume mwingine anataka kuleta mahali pokeeni binti yenu aolewe

Baada ya kukata cm mchumba wangu aakaanza yaani unamjibu mama yangu hivyo kweli nikamwambia ulitaka nimjibu vipi?

Nilikulazimisha uhamie kwangu ? Mbn ndugu zako sio wastarabu hivi hawaoni juhudi nilizozifanya kwako kukukwamua na kukufungulia ofisi ...kwa sasa sina hela ..

Nikamwambia na wewe kama unaona mm sina dira ya maisha yako chapa mwendo ..hiyo ofisi chukua vitu vyot

Mkuu Huo ndio uanaume.

Nenda kwenye bar yoyote iliyo karibu and order two bottles of wine and two females, talaka ( bili) Juu yangu.
 
Hay
Hayo ni mawazo wako sikuzuii kuamini hivyo ila cjawahi kunyenyekea mwanamke sababu ya papunchi wakati zipo zimejaa tele
Ndio maana nimesema ulitaka tu kumtumia huyo msichana na papuchi yake umeshaila umeichoka, unataka kuidampo sasa upate nyingine. Tumia busara basi kumuacha kwa amani. Kuna leo na kesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unahisi ndugu zake nakama zake, watajisikiaje ,Ku kufikiria je ikiwa watapata majibu ya kauli zako tena Kwa Mama yao??Ngoja nikuambie ukweli...Sisi wanaume huwa tunakua na utata Wa kijinga tu, MAISHA BILA MWANAMKE UNAYEMPENDA , YANABOA.
hii inategemea na Kabila lenu, huyu kakwambia Mama mkwe ndio kapiga simu kwa mwanae na kataka aongee na kidume (ni KOSA)
nanshauri AMPIGE chini huyo mwanamke na aendelee kuthamini biashara zake zitampa heshima
Kuna makabila mengine Mwanamke anarudishwa nyumbani akakae na Mkwe ajifunze adabu kukutana ni Krismas, sasa huyu hata kuPrint mashine si zake ati pesa kwanza HANA ADABU
kumnyenyekea MCHUMBA ni ulimbukeni atafute mwenye Heshima, na Mama mkwe haruhusiwi kuhoji siri za unyumba, atulie
 
Mkuu Huo ndio uanaume.
Nenda kwenye bar yoyote iliyo karibu and order two bottles of wine and two females, talaka ( bili) Juu yangu.
BRAVOOO kabisa na mimi namchomea nyama Godface ashushie na hizo Bia, ukirudi kulala Mama Mkwe atashika adabu, mwambie aolewe tu huko kwenye haraka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom