I see mpaka nimesisimka mwili. Wewe hujielewi hata kidogo. Tatizo unalo kubwa. Kwanza umempata binti muelewa,ila wewe ndio unawajaribu watu huna nia ya kuoa,ndio maana hata majibu yako ya ovyo. Nafikiri kiburi chako kinatokana na kipato ulichonacho. Kwa hiyo unajimwambafai kwamba hawa masikini nawawezesha mimi watanifanya nini?.
Tukija kwenye swala la kuoa nako umekosea sana. Kwa nini usiwaone kwanza wakushauri ni namna gani inakuwa. Ni yale yale ya kujimwambafai kwamba kwa sbb unazo basi wewe ni kila kitu. Unakosea sana. Kawaida ukishapeleka kujitambulisha,maana yake uko tayari kuoa,maana yake hapo unaomba wakupangie mahali. Na haitakiwi izidi miezi 6.
Nina uhakika hata mkioana huyo mke wako atapata shida sana kwako kwa majibu hayo. Una hatua ndefu za kujirekebisha,hata namna ya kumjibu mtu kwa uvumilivu. Bahati mbaya unaweza kukuta ni tabia yako tu,ukiamua kubadirika,utakuwa unabadirika kwa muda unarudia kule kule,ama unabadirika kwa kiasi. Jipange upya muombe msamaha mkeo na mama mkwe pia kwa kwa majibu yako kwao.
Sent using
Jamii Forums mobile app