Nafikiria kuishi hivi...... naomba ushauri.

Dada nakushauri sana usifanye hayo unayotaka kufanya kikubwa muombe sana Mungu akuponye madonda yako kisha muombe akupe yule wa kufanana naye! A vivid example from I have been pasing through the same situation for some years lakini nilimulilia Mungu na amenipa wa kufanna naye na sasa niko ndani ya ndoa iliyojaa furaha ya Mungu na nafurahia mno kuwa naye kwani Mungu amenikumbuka na kunisahaulisha madonda yangu yoooooooooooooooooooooooooooooooooote!
 
Nakushauri utulie kwanza, jipe likizo ya miezi sita hadi mwaka, kisha fanya maamuzi sahihi....huwezi kusema sitapenda wakati ndoa za wenzio utaziona siku zote, uamzi wako si sahihi kuna hatari ya kuja kufa kabla ya wakati..acha kabisa hayo maamuzi.....Mapenzi si Sheria.
 
Dada nakushauri sana usifanye hayo unayotaka kufanya kikubwa muombe sana Mungu akuponye madonda yako kisha muombe akupe yule wa kufanana naye! A vivid example from I have been pasing through the same situation for some years lakini nilimulilia Mungu na amenipa wa kufanna naye na sasa niko ndani ya ndoa iliyojaa furaha ya Mungu na nafurahia mno kuwa naye kwani Mungu amenikumbuka na kunisahaulisha madonda yangu yoooooooooooooooooooooooooooooooooote!

Asante kwa ushauri. Usinisahau kwenye sala zako!
 
Mikwara tu hakuna lolote. Hasira zikiisha " Ooooh Dear nimekumic niliover react my sweetie, nisamehe ila na wewe bwana achana na huyo mwanamke" ahahahahahahahaha

Ndugu yangu usitukane mamba na hujavuka mto maisha unayoyataka utayaweza? Matoy si mazuri kama msuri original lile nyama lenyewe lile nafikiri unalijua!!!!!. Na kumbuka maisha unayoyataka yana class yake si kila mtu tu anayaweza mama. We penda ila usipende kizoba unajiachia moyoooo wooooooooote ndo mana jamaa akikuwaza tu unaanza kusema maneno ambayo badaye unakuja kujilaumu. Penda but uwe 50 50 mapenzi bongo kwenye hiki kizazi cha sasa ni ishu ukijifanya umefika saanaaaa umekwisha,, unatakiwa unakuwa mguu ndani mguu nje kudadadekii,,, :bathbaby:

Asante. Nimekuelewa kwamba nipende nusu nusu. Huoni kama nitakuwa najiumiza? nitabalance vipi 50/50 ili nisiumie wala nisiumize mtu? mmmmh hebu nambie wewe unafanyaje?
 
Usikiri vibaya maana vile unavyokiri ndivyo utapokea hasa kwenu kian dada muwe waangalifu sana na maneno yanayowatoka kinywani hasa baada ya kuumizwa au katika hali ya kawida kama unafahamu kitabu kinaitwa biblia kitafute na usome kitabu cha HESABU 30;2-16
INASEMA

2. Mtu atakapomwekea Bwana nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.

3. Tena mtu mke atakapomwekea Bwana nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aketi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake;

4. babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika.

5. Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na Bwana atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza.

6. Tena kama amekwisha kuolewa na mume, wakati huo wa nadhiri zake, au wa neno hilo alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia;

7. na mumewe akasikia, naye akamnyamazia siku hiyo aliyosikia neno hilo; ndipo nadhiri zake zitathibitika, na vile vifungo ambavyo ameifunga nafsi yake vitathibitika.

8. Lakini kama mumewe akimkataza siku hiyo aliyolisikia; ndipo ataitangua nadhiri yake iliyo juu yake na neno alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na Bwana atamsamehe

9. Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyeachishwa mume, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake.

10. Tena kama aliweka nadhiri nyumbani mwa mumewe, au kama aliifunga nafsi yake kwa kifungo pamoja na kiapo,

11. na mumewe alisikia akamnyamazia, wala hakumkataza; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichojifungia kitathibitika.

12. Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na Bwana atamsamehe.

13. Kila nadhiri, na kila kiapo kifungacho, ili kuitaabisha nafsi ya mwanamke mumewe aweza kuthibitisha, au mumewe aweza kutangua.

14. Lakini mumewe akimnyamazia mkewe kabisa siku hata siku ndipo azithibitisha nadhiri zote za mkewe, au vifungo vyake vyote vilivyo juu yake; yeye amezithibitisha, kwa kuwa alimnyamazia mkewe siku hiyo aliyozisikia nadhiri zake.

15. Lakini akizibatilisha na kuzitangua baada ya kuzisikia; ndipo yeye atachukua uovu wa mkewe.

16. Hizi ndizo amri, ambazo Bwana alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, ali nyumbani mwa babaye.

Asomaye na afahamu hasa kina dada chunga sana matamshi yenu.

Nakushukuru kwa kunikumbusha maneno la Biblia.

Nasikitika hukuelewa ninachokielezea. Mimi sijaweka Nadhiri bali nimefikiria tu moyoni mwangu na kabla sijayafanyia kazi mawazo yangu nimeomba ushauri kwa wana JF wote. Nitafurahi endapo utaendelea kunishauri, usinihukumu kwa kosa ambalo sijalifanya. Hata hivyo nimeyapenda maneno hayo, naamini yatawasaidia na wengine.
 
Love is the answer to all of your problems,but come to those who believe it

Umeniwashia mataa ya njano, sielewi nikae au nilale, nisimame au nichuchumae, nikimbie au nitembee!!! SIJAKUELEWA
 
Soma vizuri. Nimesema nafikiria kuishi hivyo, sio nimeamua kuishi hivyo. Ushauri wako bado nauhitaji

Najua ipo siku upweke utakuzidi utahitaji kuwa na mtu by your side, sio swala la kuamua huwa inatokea spontaneously na unajikuta una walk kwenye aisle unajishangaa umefikaje.
 
si mara zote binaadamu hukamilisha anayoyapanga,tumuache apumzike,mpaka hapo anayetekeleza mipango ya binaadamu amuamulie kivingine,ninamaana muumba.
 
Aaah... Kuishi bila mpenzi ni kuidhulum nafsi jamani.... Wapo wengi wametendwa tena wewe cha mdoli, lakini wanapenda tena...! Asikwambie mtu, maisha ya kuwa na mpenzi ni mazuri kuliko ya kuwa single..! Usikate tamaa, endelea kuamini yupo atakaye kupenda kwa upendo wa dhati..!
 
Dada yangu nadhiri sio mpaka useme naweka nadhiri,unachotamka kwa hasira baada ya kuwa umeumizwa yaweza kuwa nadhiri bila wewe kujua kuwa umeweka nadhiri mara nyingi kina dada wanapoumizwa kuna maneno mnatamka hayo maneno unayotamka kwa kurudia rudia yanatosha kuwa nadhiri kwako,nadhiri sio lazima useme kuwa leo naweka nadhiri hata ukitamka na moyo wako ukinuia kufanya hilo jambo hiyo ni nadhiri,kwa mfano kwenye ujumbe wako umesema "Nafikiria kuishi single sitaki kuolewa" unaweza ukawa umesema neno hili zaidi ya mara moja na nafsini mwako umeamua hivyo hata kama ni kutokana na hasira hiyo tayari unakuwa unaifunga nafsi yako unatakiwa kutubu na kuomba Mungu akusamehe maana hukumaanisha hivyo huenda ni hasira tu.Mara nyingi katika maisha yetu tunafungwa na mambo mengi ambayo hatujui ni kwa nini kumbe kuna vifungo tumejiwekea wenyewe bila kujua.Nakutakia kila la heri
 
Asante nimekuelewa. usinisahau kwenye sala zako..
 
Back
Top Bottom