Nafasi za kazi za muda sensa 2022

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA

Serikali imetangaza ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) George Simbachawene amesema Watanzania wote wenye sifa wanaruhusiwa kutuma maombi na wafuate vigezo vilivyo ainishwa.

Aidha, amesema katika mchakato huo wa kutuma maombi, hakuna kiasi chochote cha fedha kinacho tozwa na wananchi wawe makini ili kuepuka kutapeliwa.

Maombi haya yanapatikana katika tovuti zifuatazo:-

1. www.tamisemi.go.tz

2. www.nbs.go.tz

3. www.tamisemim.go.tz

4. www.ocgs.go.tz

Maombi yatumwe kuanzia tarehe 5-19 Mei, 2022 kama ilivyo elekezwa kwenye fomu za maombi.

Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa
 

Attachments

  • FINAL - Tangazo la Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022.pdf
    134.1 KB · Views: 64
watoto wa ma W.E.O, M.E.O, DIWANI, WARATIBU ELIMU, AFISA MIFUGO,NA KILIMO, km huna undugu au ukaribu na hao sahau.
 
Kupotezeana muda tu bila connection hupati
Ishu ya post code ni watoto wa walimu watendaji ndugu jamaa na marafiki
Kama vp wapeni pia na nafasi hizi
Kule Tanga Jimbo la mkinga sehem inaitwa mavovo wamepeka watoto wao wamevulunda Sana kwenye ishu ya post code
 
Kupotezeana muda tu bila connection hupati
Ishu ya post code ni watoto wa walimu watendaji ndugu jamaa na marafiki
Kama vp wapeni pia na nafasi hizi
Kule Tanga Jimbo la mkinga sehem inaitwa mavovo wamepeka watoto wao wamevulunda Sana kwenye ishu ya post code
Tulia bwana tunaupiga mwingiiiii
 
Kupotezeana muda tu bila connection hupati
Ishu ya post code ni watoto wa walimu watendaji ndugu jamaa na marafiki
Kama vp wapeni pia na nafasi hizi
Kule Tanga Jimbo la mkinga sehem inaitwa mavovo wamepeka watoto wao wamevulunda Sana kwenye ishu ya post code
Safari hii walimu wenyewe ndio wahusika maana watakuwa likizo
 

SENSA 2022.​

Nimefanikiwa kujaza form ya maombi ya kazi ya muda kwa ajiri ya kazi ya sensa 2022,lakini nimekosea kuandika majina ya mdhamini mmoja yaani jina la kwanza nimeliweka mwisho na jina la mwisho limekuwa la kwanza.
nimejaribu ku log in kwenye account ili nifanye editing ya majina lakini inaleta nifanye editing ya sehemu inizoja ambazo ziko sahihi ilhali sehemu niliyokosea haileti.

FORM niliyoijaza ya maombi ya kazi ya sensa 2022 ina sehemu tatu yaani sehemu A ni kujaza taarifa zangu binafsi, sehemu ya B ni kijaza taarifa za wadhamini wawili na sehemu C ni kujaza taarifa au viambatanishi vya vyeti.
Sasa nikienda sehemu ya KUHUISHA taarifa kwa ajiri ya kufanya marekebisho ya majina mdhamini, zinatokea sehemu mbili tu yaani sehemu A na sehemu C ambazo zimejazwa kwa ufasaha Ila sehemu B haionekani kwa aijri ya KUHUISHA taarifa ya Wadhamini ambazo nimekosea, nahitaji kufanya marekebisho.

USHAURI WANGU, nikipakuwa form hiyo harafu nikaifanyia marekebisho form kwa kufuta na correction pen na kuandika majina kwa ufasaha kwa mkono harafu nika pakia form mtandaoni, je nitakuwa nimekosea? maana nimewapigia simu huduma kwa wateja wao nao wananambia labda kuna shida ya mtandao kwenye mfumo wao na hawajui wanisaidiaje na muda wa kutuma maombi unakaribia kuisha.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom