Kanye2016
JF-Expert Member
- Jun 4, 2016
- 2,474
- 2,445
Habari,
Majuzi kulitangazwa nafasi za ajira katika Bank ya PBZ Kupitia mitandao mbalimbali na pia kwenye website ya PBZ Bank. (Tangazo nime ambatanisha hapo chini).
Kwenye tangazo wamesema wanataka wa Tanzania wenye sifa watume maombi ya kazi kujazia nafasi zilizoachwa wazi.
Changamoto inakuja kwenye kutuma maombi unakiwa utume kwenye website ya tume ya ajira ya zanzibar ambayo ni http://portal.zanajira.go.tz.
Na ukiregister unatakiwa uingize Namba ya utambulisho wa mzanzibari yaani Zanzibar Identification Number, kama inavyoonekana hapo chini.
Sasa je hizi kazi ni za Watanzania wote au ni Wa zanzibari tu?
Kama walikuwa wanataka Wazanzibari ndo watume maombi kwa nini wasingesema tu kwenye tangazo lao kuwa inataka wazanzibari tu ndo watume maombi kama matangazo mengine wanavyofanya.
Kwa nini watu hadae vijana wakitanganyika wenye nia na vigezo vya kufanya kazi walizotangaza ilihali wakijua njia ya kutuma maombi si rafiki kwa ambao sio wanzanzibari.
Kama kuna mtanganyika ameweza kutuma maombi haya kwa kutumia hiyo portal atume ushahidi hapa huenda kuna namna ya ku bypass na kuweza kutuma maombi.
Nawasilisha.