Hivi kupiga boksi kunamaanisha kufanya kazi za kubeba boksi kweli au maana yake imebadilika na kuwa kazi yoyote tu ile afanyayo Mtanzania aliyeko ughaibuni?
Maisha ya ulaya yana raha yake na kalaha yake. Kuna watu wanaenda Ulaya wanafanya hizo kazi wanapata hela wanarudi Bongo, maisha yanakuwa magumu, wanatamani kurudi Ulaya wanashindwa kwani walishanyea kambi kwa kuzidisha muda wao wa viza. Mifano hiko mingi.
Kwa mara nyingine tena nachua fursa hii kuwasilisha mada katika jukwaa hili lenye watu wenye mitizamo tofauti ya kimaisha hiyo basi nitapokea maoni yenu. Hitaji langu nikupata mtu anayeweza kunisaidia kupata kazi zisizo hitaji kiwango kikubwa cha elimu (low skilled labour) maarufu kama kupiga box nje ya tanzania kwenye nchi za uarabuni ulaya magharibi marekani na ocenia(Australia na New Zealand) kwa mwenye uzoefu tasaidiane mawazo nawasilisha ahsanteni.
Muone Kuveta atakusaidia
Habari wana JF
KWA MARA NYINGINE TENA naweka bango langu la kuelezea nia yangu ya kuelekea ughaibuni.
Hivi majuzi niliweka bango huku kuelezea nia yangu hii lakini nashangaa sikuliona tena yaani limefutwa sasa najiuliza kwani tatizo liko wapi mimi kueleza nia yangu hii.
Kwa kifupi nilimaliza kidato cha nne mwaka 2010 then nikajiunga na colege moja ya clinical asistance na kumaliza mwaka 2013 nikapangiwa kituo huko mkoani iringa kwa kweli katika ufanyaji kazi wangu sijaona faida yoyote kwani mshahara wenyewe ni mdigo kiasi kwamba ukichanganya na makato ya kodi mifuko ya jamii na bima unakua huja save chochote hivyo basi nikaona bora nitafute njia ya kuingia ughaibuni hata kama nitafanya kazi za hadhi ya chini lakini nikaweza kusave angalu kiwango kidogo
Hivyo basi kwa wale wenye uzoefu na huko hebu nipeni mbinu za kuweza kufika huko...