Nchi ambayo inasemekana inalipa vizuri duniani na kadiri ya utafiki kwamba mtu unaishi bila stress ni nchi ya Norway. Wastani wa malipo kwa saa ni kama $20. Kwa mswahili wa kibongo asiyejua maisha ya huko ataona hapo akienda atageuza maisha haraka na amepata kumbe atakuja kupatikana na kujutia.
Nchi hizo za ukanda wa Scandinavia zina vimelea vya ujamaa, na hivyo serikali inakamua kodi balaa. Ununuzi wa vitu ni ghali sana mfano kikombe cha kahawa ni $5 wakati nchi kama Marekani ni $1.50. Utakashoshtukia pesa unayolipwa inaishia kulipa gharama za kuishia vinginevyo ni full mzuka wa kubana matumizi ndo unabaki na cha kurudi nacho bongo.
Nchi za magharibi wanataka ujifunze kwanza lugha yao, maana kazini kunahitajika sana communication iwe ni oral or written. Hivo lazima ujifunze kama ni kijerumani, kiswiswi, kidenmark, kinordic nk.