Nafasi za kazi nchi za nje

Nafasi za kazi nchi za nje

Bojan

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
259
Reaction score
423
Wadau habarini mm ni mtanzania ninampango wa kwenda kupiga box ughaibuni sasa naombeni ushauri nchi sahihi ya kwenda na jinsi ya kupata kazi kirahisi.nawakilisha
 
Yeyote anayejua upatikanaji wa kazi za kupiga box ughaibuni atufahamishe tupo tayari kwenda hatuchagui kazi
 
Bojan poke ujumbe frsh kutoka Qata...by Pinda,
[h=2]Watanzania kunufaika na ajira[/h]

Na Waandishi wetu

22nd December 2014

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

Pinda-22Dec2014.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema Watanzania watanufaika na kipato na maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira ambazo watapata katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani.

Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla, Pinda alisema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi hiyo inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni wachache.

"Hapa Qatar kuna uwekezaji mkubwa umefanyika, kwa hiyo wanahitaji watu wa kufanya kazi... kwenye mahoteli, viwandani na kikubwa hapa ninachokiona watu wetu watapata kipato lakini pia watapata ujuzi kwa maana ya maarifa yanayoendana na teknolojia ya kisasa."

Maeneo mengine aliyosema wamekubaliana kushirikiana ni kilimo, gesi na mafuta kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania na Tehama.

Alisema wamekubaliana na Sheikh Abdulla al Thani kuunda timu ya pamoja baina ya nchi zao ili ifanye kazi ya kuainisha ni maeneo gani wanataka waanze nayo kwanza kulingana na mahitaji.

CHANZO: NIPASHE
 
Last edited by a moderator:
Kupiga box unamaanisha kazi hizi unskilled?
Hapo panakuwa pagumu maana sidhani kama kuna njia halali ya kwenda huko kufanya kazi hizo inabidi uende kama mwanafunzi so upate shule/chuo kisha upate student visa uweze kuingia huko then una option kadhaa kuzamia (utakuwa unaishi kinyume na sheria ambayo ina matatizo yake), kuoa/olewa na mtu wa huko etc.

Pia ukiwa mkimbizi ni rahisi kuingia baadhi ya nchi za ulaya.

Kama unataka kufanya kazi professional basi kuna options zaidi baadhi ya nchi zina skilled work visas.
Pia nchi kama Canada zinachukua watu wenye skill kwenye "Trades" hizi ni vitu kama welder/carpenter/butcher etc
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako kang lakini nilikua nauliza juu ya upatikanaji wa hizo wanazoita low skilled labour je mtu anayeamua kuishi kwa njia zisizo halali anaweza kupata hizo kazi na kama unafahamu mtu anaweza kutengeneza kiasi gani cha fedha kwa mwezi mmoja
 
Box mbona zipo kibao tu hata hapa Tz hadi vijijini. Zinatupwa tu majalalani karibia na maduka au mahospitalini zinazoishia dawa, unaenda unazipigapiga weee ukichoka unarudi kulala.
 
umechelewa banaa, unachotakiwa sasa sio kutafuta kazi ya kupiga box ulaya maana kwa sasa kumejaa...unatakiwa upambane hapo hapo bongo na ma escrow ili pesa irudi come 2015 UKAWA waingie mjengoni....napita tuu mkuu.
 
Ulaya kumejaa bakini nchini mjenge nchi. Nani atahudumia shuleni, hospitali, benki, migodini, n.k km ukienda piga box?
 
Ulaya kumejaa bakini nchini mjenge nchi. Nani atahudumia shuleni, hospitali, benki, migodini, n.k km ukienda piga box?
mkuu unaroho mbaya sana ukimzuia Mtanzania mkenya au msomari atakwenda funguka kwa jamaa akapige box ili akirudi home 30 watafaidi mkuu

swissme;
 
mkuu unaroho mbaya sana ukimzuia Mtanzania mkenya au msomari atakwenda funguka kwa jamaa akapige box ili akirudi home 30 watafaidi mkuu

swissme;

Sasa roho mbaya yangu ni kuandika ukweli? Ukweli kwa ulaya ya sasa simshauri mtu manake sio rahisi unless una scholarship, au uondoke na mpunga wa kutosha home ukukeep wakati unajiadjust.
Okay njia ya kwanza ni kwenda km student, professional job, kupitia ubeach boy, Kuomba visa ya utalii na kuzamia. Km ni graduate anitafute kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali ( esp renown ones sio vyuo vya kata) anitafute kwa mda wake.
 
Hivi kupiga boksi kunamaanisha kufanya kazi za kubeba boksi kweli au maana yake imebadilika na kuwa kazi yoyote tu ile afanyayo Mtanzania aliyeko ughaibuni?
 
Umeliona hili!?
Litime pale Magogoni, jitumbukize na mikate yako na maji ya kutosha, likitia nanga Liverpool unashuka, kamata East Midlands Trains kamsalimie Malkia Buckingham...

[Mnahisi Ulaya kazi ni zakuokota tu, vijana wa Eastern Europe wamejazana tele. Huko kwa Malkia hadi kazi ya Ulinzi ni lazima uwe registered, na hiyo registration inapitia approvals kibao; hadi visa issuing agencies zinahusika. Bongo hapa JB akianzisha kampuni ya ulinzi anakudaka tu ukalinde. Piga kazi bhana. Hizo kazi za kunyanyua maboksi mbona Bongo zipo tu, au unaona aibu, unataka ukazifanyie mbali na upeo wa Mwasiti?]
 
Attachments

  • DSC04576.JPG
    DSC04576.JPG
    829 KB · Views: 716
Wadau habarini mm ni mtanzania ninampango wa kwenda kupiga box ughaibuni sasa naombeni ushauri nchi sahihi ya kwenda na jinsi ya kupata kazi kirahisi.nawakilisha

Nchi zote ulimwenguni ni poa sana, jiandae na nauli ya kwenda na kurudi, pesa ya kutumia wakati upo huko na vile vile jiandae kufanya kazi yoyote ile itakayokupa mpunga mzuri. BTW lazima uwe na VISA sahihi unakokwenda na kazi unayotaka kufanya. Angalia watoto wa mjini wasikuingize mjini..
 
Sasa roho mbaya yangu ni kuandika ukweli? Ukweli kwa ulaya ya sasa simshauri mtu manake sio rahisi unless una scholarship, au uondoke na mpunga wa kutosha home ukukeep wakati unajiadjust.
Okay njia ya kwanza ni kwenda km student, professional job, kupitia ubeach boy, Kuomba visa ya utalii na kuzamia. Km ni graduate anitafute kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali ( esp renown ones sio vyuo vya kata) anitafute kwa mda wake.
Ntakutafuta na mimi maana naona time inakata tu afu matokeo bado ni bila bila
 
Wadau habarini mm ni mtanzania ninampango wa kwenda kupiga box ughaibuni sasa naombeni ushauri nchi sahihi ya kwenda na jinsi ya kupata kazi kirahisi.nawakilisha

nilikua huko miaka sita nina uzoefu mkubwa sana nicheki0682116396
 
Back
Top Bottom