Nafasi ya ushirikina kwenye mapenzi!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,644
Habari zenu ndugu zangu,
Najua wazi tuko makundi tofauti kuhusu hoja hii ninayoiweka jukwaani,
tupo ambao hatuamini ushirikina kabisa, tupo ambao tunaamini lakini
hatuutaki kwa sababu za imani nyingine, tupo ambao tunaamini na
tunaupenda pia tupo ambao tunaupinga mdomoni lakini moyoni
tunaamini.

Tuachane na hayo, kuna usemi wa kiswahili LISEMWALO LIPO......
kwa hali ilivyo sasa ni wazi kuwa baadhi ya watu hutumia dawa (ushirikina)
Kuboresha mapenzi yao.

Je! Ni kweli ipo dawa ya kuboresha mapenzi? umewahi kutumia au
Kushuhudia? Tueleze. Una ushauri gani kwa watu wanaotafuta dawa kwa ajili ya
kuboresha mapenzi yao kama vile kumfanya mume asiende nje n.k

NAWASILISHA
 
Mkuu mimi naishi Kiwalani, nimepanga nyumba ambayo mama mwenye
nyumba ni mtaalamu wa tiba kama hizo. Anatoa dawa ambayo inaitwa
dawa ya pendo. Huwa naona wanawake ndo wanakuja pale kuchukua hizo
dawa. Wengi wao huja usiku na magari yao.
Kuwa zinafanya kazi au hapana hilo Sifahamu, Pia sijawahi kumuona
Mwanaume anatafuta dawa ya mapenzi ni wanawake tu,
 
Mmmmmmhh hii kali....Ni vidonge au syrup? au sindano? mmmh haya
 
Huwa wanaingia chumba fulani kwenda kuogeshwa na huyo mama. Sina uhakika ni dawa gani nyingine wanapewa baada ya hapo. Kuna mtu kani PM anataka nim pe namba ya huyo mama au nimuelekeze vizuri anakopatikana. Panda gari za Jet/Lumo - Kariakoo shuka kituoni kwa GUDE ukifika hapo uliza kwa mama msambaa!
 
Huku uswazi mambo ya kawaida hayo mkuu
ukitiwa kwenye chupa.. hata wapige kelele vipi! husikii
 
Zipo sana haujawahi kusikia limbwata kwa watu wa pwani?Shuntama Bukoba,Kichwa cha perege Ifakara nk..Usiombe yakufike baba utakoma mtu wangu.Wife akisema lala hata kama ni saa 5 asubuhi wewe kitandani tu.Nitarudi kesho wewe kutikia ndio mama Boke nk.
 
Duh! hii ya kutiwa kwenye chupa ndo kwanza naisikia ingawa niliwahi
kuiona kwenye filamu za kinaijeria!
 
Zipo sana haujawahi kusikia limbwata kwa watu wa pwani?Shuntama Bukoba,Kichwa cha perege Ifakara nk..Usiombe yakufike baba utakoma mtu wangu.Wife akisema lala hata kama ni saa 5 asubuhi wewe kitandani tu.Nitarudi kesho wewe kutikia ndio mama Boke nk.
Duh! Hizo zenye Red ndio kwanza nazisikia.
 
asilimia 94 ya watanzania ni washirikina...

tena hasa wale wanaojifanya hawajui lolote kuhusu mambo hayo
 
Mtoa mada kama ni mwanamke, dawa ya mapenzi hii hapa. Mumeo akirudi jioni mpokee kwa upole na ukarimu. Mwambie pole na kazi. Ikifika saa ya utakaso, shughulika sawasawa huku ukimpigia vigelegele laini karibu na sikio lake na aksante nyingi kwa kazi nzuri anayofanya. Mwisho unamalizia na pole kwa kazi ngumu. UTAONA MATOKEO.
 
mhhhh nasikiaga na natamani wakati mwingine, ila kila nikifikiria
nitakuwa nimependwa kwa ajili ya madawa nakataa, kwa kweli watu wengi
hushiriki haya mambo, ila nasikia pia huwa yanawageukia badae yanaisha
inabidi mtu awe mtumwa wa ibada hizo,tuachane na hizi ibada ni za kishetani sana
 
Mtoa mada kama ni mwanamke, dawa ya mapenzi hii hapa. Mumeo akirudi jioni mpokee kwa upole na ukarimu. Mwambie pole na kazi. Ikifika saa ya utakaso, shughulika sawasawa huku ukimpigia vigelegele laini karibu na sikio lake na aksante nyingi kwa kazi nzuri anayofanya. Mwisho unamalizia na pole kwa kazi ngumu. UTAONA MATOKEO.
<br />
<br />

Mimi ndo kilichonimaliza
 
Dawa ya Kuboresha Mapenzi...

  • Kupenda kwa dhati...
  • Kua bingwa wa compromise..
  • Kujituma 6/6
  • Kujua kua yeye ni bora kuliko Mwanaume/mke yeyote yule...
  • Kumjua hasa Mpenzi wako... nini ufanye akichukia...
nini ufanye akifurahi... nini ufanye kurudisha vibe kama inalega...
nini anafurahia katika mahusiano yenu...

Short Cut:- Kwa Mganga... hapo unapata galasha.. sio mtu mwenye akili yake...
 
Mtoa mada kama ni mwanamke, dawa ya mapenzi hii hapa. Mumeo akirudi jioni mpokee kwa upole na ukarimu. Mwambie pole na kazi. Ikifika saa ya utakaso, shughulika sawasawa huku ukimpigia vigelegele laini karibu na sikio lake na aksante nyingi kwa kazi nzuri anayofanya. Mwisho unamalizia na pole kwa kazi ngumu. UTAONA MATOKEO.

Wanaume wengine hata ukiwaramba nyayo hawaridhiki ngó!
 
Mtoa mada kama ni mwanamke, dawa ya mapenzi hii hapa. Mumeo akirudi jioni mpokee kwa upole na ukarimu. Mwambie pole na kazi. Ikifika saa ya utakaso, shughulika sawasawa huku ukimpigia vigelegele laini karibu na sikio lake na aksante nyingi kwa kazi nzuri anayofanya. Mwisho unamalizia na pole kwa kazi ngumu. UTAONA MATOKEO.
Kuna tukio nimelishuhudia LIVE Mke wa mjomba'angu alisafiri
aliporudi sijui ilikuwaje lakini akakamatwa na dawa za mizizi na
hirizi ambapo baada ya kubanwa sana alitoa siri kuwa hiyo dawa
aliichukua kwa mganga ili apendwe na amtulize mumewe ambaye
alionekana kutotulia. Kilichonishangaza zaidi ni kuwa hata kabla ya
kuchukua hiyo dawa alikuwa anapendwa lakini baada ya tukio
Kaachwa!
 
Mtoa mada kama ni mwanamke, dawa ya mapenzi hii hapa. Mumeo akirudi jioni mpokee kwa upole na ukarimu. Mwambie pole na kazi. Ikifika saa ya utakaso, shughulika sawasawa huku ukimpigia vigelegele laini karibu na sikio lake na aksante nyingi kwa kazi nzuri anayofanya. Mwisho unamalizia na pole kwa kazi ngumu. UTAONA MATOKEO.
Si bure we ni mjuvi wa mambo yale au??????????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom