Nafasi ya ushirikina kwenye mapenzi!

Huwa wanaingia chumba fulani kwenda kuogeshwa na huyo mama. Sina uhakika ni dawa gani nyingine wanapewa baada ya hapo. Kuna mtu kani PM anataka nim pe namba ya huyo mama au nimuelekeze vizuri anakopatikana. Panda gari za Jet/Lumo - Kariakoo shuka kituoni kwa GUDE ukifika hapo uliza kwa mama msambaa!

Yeah.. Namfahamu huyu mama ni maarufu sana hapo kwa Gude, unajua watu wa Tanga ( kama wako humu watakubaliana na mimi) wana dawa yao maarufu inaitwa Ndele, hiyo ni Kiboko, wenyewe wanaijua........ labda anayefahamu namna inavyofanya kazi atujuze zaidi..... mie nilisimuliwa na jamaa yangu mmoja mwenyeji wa huko Tanga
 
Habari za jumapili ndugu zangu,

Naomba kuuliza hivi kweli mtu anaweza kutumia ushirikina ili apendwe? Nimekuwa nikisikia kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia ushirikia ili wapendwe. Nimeona leo nilete swali hili kwenu.

Karibuni tujadili
 
Nijuavyo Ushirikina au Uchawi Mkubwa Ktk Mapenzi Ni HELA / PESA Tu Na Huko Kwingine Ni Mbwembwe Tu Na Kupotezeana Muda!
 
wapo ndugu wanaotumia tena wengi tuu
kama unataka mtafute maalim hussein
 
Ushirikina upo na unatumika sana lakini ni short term tuu. Matokeo yake dawa ikikata nguvu huwa ni aibu kubwa sana aisee.

Ila uchawi kwa sasa pesa tuu, although sio mahala pote pesa itakuwa na nguvu katika mapenzi.
 
sikuizi kuna waganga au mazingaombwee? wanganga zamani sikuizi unambiwa lete mbuzi lete jogo ,mara chano
zamani ukipewe siku3 basi 3 naam...
Mmmh !! Sasa hao pataamu.... hebu tiririka taalum nasi tupate uelewa wa haya mambo... hivyo hao wanyama (mbuzi,jogoo nk..) inahusihajee !! masikini viumbe.....
 
hebu nenda Tanga ukapate majibu huko mapenzi ya aina yote yapo huko

Ninatoka Tanga lakini ninaamini penzi la kweli linatoka kwa Mungu. Alichokipanga Mungu binadamu hawezi kubadilisha.
 
ZZ mie nikupe au weye uwape wenzioo,au niwambie nyie ndio mlikua mnafuga majini sasa mie jamani naanzaje..
Mpendwa ee, Siye ya kwetu ni Jimi wa kusafiri,kusafirisha fast fasta na kuleta tende za Mfungo na mavazi ya sikukuu tu !!

Lakini zenu ni za mahabaat !! Yala yala Khaloo usiniangushe.....!
Sky Eclat nae yupo mnazi mmoja !!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom