elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,260
- 9,747
Nitajitahid Nishinde MajaribuWengi huwa Wanaweka matarajio makubwa kutoka kwa Dada zetu wa Tanga., mwishoe kwenye Ndoa Matarajio na Uhalisia ni tofauti!
Hapa Nilipo Nipo Moto Na Totoz Za Tanga Acha TuuAmbiele Kiviele ,
Mkuu, karibu sana Tanga, uoe hutakaa ujute.
Binafsi, Poise, sijawahi kujuta, hata nusu sekunde kwa kuoa mke kutoka Tanga.
Nashukuru sana Tanga, kuwa Tanzania!!
Cc: emmyta na wanawake wengine wa Tanga wote heko kwenu kwa kunipeni mke mwema mliyemfunda vyema.
Kila lakheiri bro..,Nitajitahid Nishinde Majaribu
Hapa Nilipo Nipo Moto Na Totoz Za Tanga Acha Tuu
Ambiele Kiviele ,
Mkuu, karibu sana Tanga, uoe hutakaa ujute.
Binafsi, Poise, sijawahi kujuta, hata nusu sekunde kwa kuoa mke kutoka Tanga.
Nashukuru sana Tanga, kuwa Tanzania!!
Cc: emmyta na wanawake wengine wa Tanga wote heko kwenu kwa kunipeni mke mwema mliyemfunda vyema.
Daah. Shukrani sana Shemeji.
Japokuwa saa nyingine huwa nawashangaa sana wale wenye kuipa hila Tanga ila ndio hivyo huwa sina jinsi.
Barikiwa sana Shemeji yangu. Pia nawaombea kwa Allah azidi kuwasimamia.
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
Nakuona katika ubora wakoJoverest kadisco UDSM.
Msifanye mchezo na JF. Alikuwa anaacha kukomaa na chuo yupo na iphon yake anavizia thread mpya.
Siku nzima 24 hrs mnategemea nini?
Na mimi nina mpango wa kwenda huko mwakani, ukifanikiwa uje na mrejeshoTANGA
Bora nikaoe Tanga, tena bint wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.
Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.
Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.
Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.
Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.
Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.
Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.
Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.
Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.
Cc : Mshana Jr
Michezo Ya Kuchezeana Wanafanya Vijana Ndugu Yangu
Maneno Yana Nyama Nyingi Sana HayaDaah. Shukrani sana Shemeji.
Japokuwa saa nyingine huwa nawashangaa sana wale wenye kuipa hila Tanga ila ndio hivyo huwa sina jinsi.
Barikiwa sana Shemeji yangu. Pia nawaombea kwa Allah azidi kuwasimamia.
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
Sijapata Mtu Wa Kunipa Maelekezo HukoBumbuli hupiti mkuu?
Mi Muda Wowote Naweza KwendaNa mimi nina mpango wa kwenda huko mwakani, ukifanikiwa uje na mrejesho
Pole mkuu, ila na wewe upunguze ushirikina ili upate maendeleo
Bibie wewe ni mtu wa digo au segeju (monga,vyeru,kichalikani, kwale)??Kama unapenda laufiudh basi oa m-digo au m-segeju.