Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,465
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,465 2,000
images-1-jpg.1125684

Salute..
kuna msemo sijui tulifundishwa au tulisoma wenyewe kwenye vitabu vyetu vya dini (Bibble & Qu'ran) msemo huo unasema kua Miaka elfu moja duniani ni sawa na siku moja mbingu, kiukweli kwa uelewa wangu mdogo wa maswala ya Theologia na Physics nasema huu msemo ni uongo ina wezekana waliotufundisha au tulipousoma kwenye vitabu tuliutafsiri tofauti.
Kwanza kama ulisoma uziwangu wa Time Travel kiasi wadau waliweza kuelezea kadri wajuavyo effect ya Time kwenye Maisha/Uhai wa mwanadamu, nilivutiwa zaidi na mchngowa mkuu BASANORARE kwenye comment hii https://www.jamiiforums.com/threads/time-traveling-je-linaweza-kuwa-suluhisho-la-kifo.1585916/post-31526494 sikutaka nimjibu pale nikaona nianzishie mada hii kitu labda kila mtu atoa mawazo yake juu huu msemo/Andiko.
.......
Ref kutoka Qu'ran: Surat Hajj 47, allah anasema kuwa siku moja ya Allah ni sawa na miaka elfu moja "1,000".
Ref from Bible: Zaburi 90:4 Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha kupita, kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku
2Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja
Haya ndio maandiko ambayo yamefanya kuenea kwa msemo ambao mimi kwa muono wangu naona si kweli kwa jinsi watu wanavyo
yatafsiri, mimii naelewa hivi kuhusu haya maandiko and I hope theseare aint Blasphemy kwani the Almighty hapendi wasiotaka kuhoji...Let's go!

Kwanza kabisa Kiasili Mungu ana sifa kuu ambazo ni Omniscience (Ajuaye yote), Omnipotence (Mwenye uweza na nguvu zote) na Omnipresence (aliyoko kila mahalii).
tunaposema kua kwa Mungu/Mbinguni siku moja sawa na miaka 1000 ya duniani msemo huu unauvunja vipande vipande ile sifa ya Mungu ya kua Ana uwezo wa kila kitu na Hana mwanzo wala mwisho.... Kivipi???????????
duniani sababu kuu ambayo inatufanya twafariki ni kwasababu i)Dhambi ya asili (ii)ili kuweza kubalnce nature na kuruhusu existence ya viumbe vingine duniani (iii)time. Yes tunakufa kwakua kuna muda duniani ambao unatuhesabia siku zetu tunazoishi hapa dunia ..Time is the biggest threat to mankind ndio maana nilisema kwenye mada yangu ya time Travelling kua tukiweza kudhibiti muda basi tunaweza kudhibiti KIFO. Kwa mantiki hiyo nachelea kusema kwamba kama kwa Mungu kuna Muda basi Mungu ana mwanzoo, Mbinguni kuna vifo there is no eternal life at all, Yawezekana basi hakuna Mungu mmoja maana watakua wanapita/wanafariki (God Forgive I feel like I'm going too far).
Kwa mujibu Fundamental physical quantity, the SI-Unit of Time is Second and other si-unit are year,day,month,decade,millisecond,century etc...Hivyo basi kama mbinguni Muda basi Mungu atakua ana muda maalumu aliotokea(ana mwanzo) maana ili muda uweze kuhesabiwa lazima kuwe na jua linalo zunguka, haingii akilini kwamba kila ikifika miaka elfu ya duniani basi Mungu hua analala kwakua jua limezama usiku umeingia haiwezekani.

Ninavyofahamu Mimi kwa Mungu hakuna muda (Timeless) hakuna future wala past kila muda kwake ni present, Mungu hawzi eti kesho nitafanya hivi na hivi big Nope ndio maana malaika hawazeeki wala hawafi maana hakuna Muda waliowekewa unaohesabu miaka yaoo labda technically aliyewaumba anajua umri wao. Sie wandamu tumewekewa muda ili tuweze kupanga malengo yetu, ili tuweze kuishi umri fulani tulipangiwa na Muunmba,,ili siku moja tufe that's all..
Kwa hiyo basi kwa kusema hivo yawezekana msemo huu inawezekana kutokna na ambiguity ya kiswahili chetu wakati unatafsriwa kutaka version ya lugha zingine sie tuliuelewa vibaya. au kwa vyovyote vile ulipokelewa kimakosa kama vitabu vinne vya wakorintho ilivyokua..

Mwisho kabisa niseme kua huu ni muono wangu na sio pie kwamba kila mtu alzima aelewe hivyo..Lakini naamini kwa Mungu ni Timeless
Anybody Concur with me......???????????
~Da'Vinci
 
Tlg

Tlg

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
339
Points
250
Tlg

Tlg

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
339 250
ngoja nitafute pakuanzia....

kwanza naunga mkono nadharia ya kwamba duniani miaka 1000 ni sawa na siku 1..
kama tunavyojua kuwa muda unatofautiana kati ya nchi na nchi,sayari na sayari nyingine,,,,
hakuna anayeijua physical location ya mbinguni ipo wapi angani,,
kwa mantiki hiyo mbinguni inaweza kuwa billion miles kutoka kwenye galaxy yetu,,,,

mfano mzuri ni proxima centauri hii ni nyota iliyo karibu na dunia,,,
mwanga wa jua kuufikia ni miaka 4.24,wakati dunia ni dakika 8..

na chombo cha nasa walichokituma voyage 1 mwaka 1977 kwenye space hadi kifike proxima centauri kitatumia miaka kama 80000,,,
hapo tuna assume hakuna error yoyote iliyotokea kwani mpaka sasa kimecover 1/600 light year ndani ya miaka 30,,,
lakini mpaka 2025 kitakuwa kime rest in space sababu energy itakuwa imekwisha.......

na kwa nadharia hii naunga mkono hoja mbinguni kuwa siku 1 ni sawa na miaka 1000 duniani..
kwa sababu hatujui location ya mbinguni ipo wapi.........
Kama Siku ya duniani ni sawa na Siku buku za mbinguni ,na kama muda mbinguni una kuwa measured with the same principle as on earth then we can roughly approximate with a reasonable precision the location of the so called mbinguni .


Tunauwezo wakujua time on other planets through their elliptical distance from the sun. Inversely kama tunajua time relation ya mbinguni na earth. Then we can know the location of mbinguni

Assumption : mbinguni is a physical place( object like other planets revolving around the sun)
 
kingkimbe

kingkimbe

Member
Joined
Jul 11, 2017
Messages
53
Points
95
kingkimbe

kingkimbe

Member
Joined Jul 11, 2017
53 95
Mkuu wewe hauamini nini sasa wanasayansi wako wanakili kuwa Venus ikijizungusha kwenye muhimili wake ni sawa na siku zaidi ya 240 za dunia sasa wewe unajuwa mbingu hipo wapi?? Hadi unaongea hvyo
 
Mwadunda

Mwadunda

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Messages
1,335
Points
1,500
Mwadunda

Mwadunda

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2013
1,335 1,500
Mtu akishasema kwa uelewa wake mdogo huwa ananipa shida sana kuendelea kusikiliza.
 
Waterbender

Waterbender

Senior Member
Joined
Oct 2, 2018
Messages
188
Points
225
Waterbender

Waterbender

Senior Member
Joined Oct 2, 2018
188 225
Njoja nijenge hoja

Mwaka 1 duniani ni sawa na miaka mingapi kwenye sayari ya Jupiter au pluto. Kwa maana ya Jua kuzunguka dunia au sayari ya pluto .

Ukishajibu hapo haishindikani mwaka 1 duniani kuwa sawa na miaka 1000 mbinguni!
Those star are in the same galaxy
 
sande nicolaus

sande nicolaus

Member
Joined
Feb 3, 2015
Messages
13
Points
45
sande nicolaus

sande nicolaus

Member
Joined Feb 3, 2015
13 45
Nilichoelewa mimi na akili yangu ya KVANT KUBWA ni


Wanaposema miaka 1000 kwake ni sawa na siku 1.anatumbusha viumbe wake kuwa yeye hapotezi KUMBUKUMBU.

Kwa binadamu ni rahisi na kawaida kukumbuka ratiba na mizunguko yake yote aliyoifanya jana (tarehe na mwezi wa jana mwaka huu) lakini asikumbuke route au mizunguko,ratiba yake aliyoifanya tarehe na mwezi wa jana ya (mwaka uliopita)..

Mfano wakati una miaka mitatu uliwahi kuiba andazi sokoni(hiyo ni dhambi ulifanya). Lakini leo hii hukumbuki chochote na unaweza ukajiona huna dhambi duniani..kisa ni muda mrefu umepita...lakini kwa Mungu hatasahau atalikumbuka tukio lako lote kama vile limefanyika muda mfupi uliopita(saa au siku moja iliyopita)
Hivo utakumbushwa na kuhukumiwa vile vile...asante ngoja niendele kunywa KVANT yangu
KVANT KUBWA,hongeza nyingine...
 
Musundi

Musundi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Messages
698
Points
1,000
Musundi

Musundi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2016
698 1,000
Njoja nijenge hoja

Mwaka 1 duniani ni sawa na miaka mingapi kwenye sayari ya Jupiter au pluto. Kwa maana ya Jua kuzunguka dunia au sayari ya pluto .

Ukishajibu hapo haishindikani mwaka 1 duniani kuwa sawa na miaka 1000 mbinguni!
Kwa mantiki hiyo hiyo unaweza kucalculate umbali kutoka duniani hadi mbinguni, sio???!!
 
Kaburiwazi

Kaburiwazi

Senior Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
126
Points
225
Kaburiwazi

Kaburiwazi

Senior Member
Joined Jan 1, 2019
126 225
Huwezi kuanza kuandikiwa dhambi kwa umri huo wa miaka mi3.
Nilichoelewa mimi na akili yangu ya KVANT KUBWA ni


Wanaposema miaka 1000 kwake ni sawa na siku 1.anatumbusha viumbe wake kuwa yeye hapotezi KUMBUKUMBU.

Kwa binadamu ni rahisi na kawaida kukumbuka ratiba na mizunguko yake yote aliyoifanya jana (tarehe na mwezi wa jana mwaka huu) lakini asikumbuke route au mizunguko,ratiba yake aliyoifanya tarehe na mwezi wa jana ya (mwaka uliopita)..

Mfano wakati una miaka mitatu uliwahi kuiba andazi sokoni(hiyo ni dhambi ulifanya). Lakini leo hii hukumbuki chochote na unaweza ukajiona huna dhambi duniani..kisa ni muda mrefu umepita...lakini kwa Mungu hatasahau atalikumbuka tukio lako lote kama vile limefanyika muda mfupi uliopita(saa au siku moja iliyopita)
Hivo utakumbushwa na kuhukumiwa vile vile...asante ngoja niendele kunywa KVANT yangu
 
M

MESHACK WARIOBA

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2017
Messages
484
Points
1,000
M

MESHACK WARIOBA

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2017
484 1,000
Jamani, Mbona naona Mbinguni imetawala? Mnaitoa wapi?
Nimesoma Zaburi hiyo ya 90:4 inasema kwamba, "Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha kupita, kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku"

Lakini pia hata hiyo Petro haisemi habari za mbinguni, ninyi wenzetu mnazitoa wapi?
2Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
 
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
6,752
Points
2,000
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
6,752 2,000
Kingine kincho sound tofauti masikioni mwangu ni huu msemo kua ili uelewe maandiko ya biblia inabidi roho mtakatifu akushukie kwanza kwakweli mm sidhani kama ni kweli kwamba inambidi ashuke kwanza kisha ndio akufunulie ...noo asee hapana. Kwanini?

Kwa mujibu wa katekismu au mafundisho yoyote yale ya kikristo inafundisha kua Roho mtakatifu hutupatia mapaji yake saba ambapo kati ya hayo mapaji ni Hekima na Elimu. indi tu binaadamu anapozaliwa Mungu humbarikia kila kitu baadhi ya mapaji tunazaliwa nayo japo sio wote, moja ya paji tunalozaliwa nayo ni paji la Hekima, japo kutokana na malezi au mazingira anayokulia mtoto paji hilo laweza kufifia. Hivyo basi katika kutafsiri maandiko ya bible kinachotumika ni Hekima, paji la hekima ndio linalowezesha kuitafakari andiko la biblia, na ukumbuke anayetoa uwezo huo wa kua na hekima Ni Roho mtakatifu.. Hekima hiyo inakuwezesha pindi unaposoma andiko tu kwa mara ya kwanza mojakwamoja unafahamu kua hili andiko lina ujumbe fulani ndani yake, kama vile darasani kuna mtu akiona swali kwa mara ya kwanza tu bila kucherewa haraka anafahamu hili swali lahitaji nini. Hivyo basi kuna watu wanayo hekima hiyo wengine hawana..katika kutafsiri maandiko pia kuna makundi mawili ya watu ambayo ni (i)Watu ambao wakiona andiko wanalielewa na wanaweza kilielezea mbele ya wengine (ii)kuna wengine wakielewa andiko hawawezi kulielezea kwa wengine kutoka na uwezo mdogo wa kuwasilisha hoja mbele za watu {nipo kundi namba mbili}

kwa mantiki hiyo Roho mtakatifu hakushukii ili uweze fafanua andiko ila anakua ashakujalia kipawa chake toka siku wazaliwa...

pia haya ni mawazo yangu
Unapinga maandiko kwa kuweka upotoshaji mkubwa.

Bwana na akukemee
 
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
3,016
Points
2,000
Iselamagazi

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
3,016 2,000
Mungu daima huzungumza na sisi binadamu ktk metaphorical sense ili tuweze kutambua Ukuu Wake.
Siku 1000 ni KAMA siku 1.
Neno KAMA limetumika kama ufananisho tu, si kitu real.
For your info, kule mbinguni hakuna jua wala mwezi. Hakuna mchana wala usiku, so hakunaga masuala ya time kule (Uf 22:5). Task iliyoko kule ni kuimba tu - haleluya, haleluya, haleluya... up to infinity bila kukoma!
 

Forum statistics

Threads 1,326,252
Members 509,458
Posts 32,215,859
Top