Hakuna nadharia yoyote ya Kisayansi inayoelezea kikamilifu chanzo cha ulimwengu

Ahmet

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
1,537
3,404
Habari wapendwa,

Kuna hizi theories zinazoelezea chanzo cha Ulimwengu, kwa uelewa wangu hakuna hata moja inayoelezea kikamilifu chanzo cha huu Ulimwengu, bali nyingi zinaelezea modifications na evolution tu ya Ulimwengu ambapo katika kuelezea huko zinaweza zisiwe sahihi pia.

Tuziangalie kwanza nadharia zenyewe na kivipi zimeshindwa kuelezea chanzo Cha Ulimwengu.

1. Big Bang Theory

Hii ni nadharia maarufu miongoni mwetu, lakini si nadharia pekee inayoelezea chanzo cha Ulimwengu. Kwa mujibu wa big bang, Ulimwengu wote ulianza kama punje ndogo (atom), yenye joto sana, ambayo ilikuwa katika mgandamizo mkubwa usiomithirika (infinitely dense). Kisha punje hii akaanza kutanuka na kutengeneza sehemu na wakati (space and time). Kadri Ulimwengu ulivyotanuka basi ukapoa na kufanya baadhi ya sehemu kuwa ni zenye kukalika na viumbe hai kama ilivyo katika Dunia yetu. Wanasayansi wanadai tulio hili la big bang lilotokea takribani miaka bilioni 13.7 iliyopita.
Wanasayansi wanatumia gunduzi mbili za kisayansi kuthibitisha madai haya.

Kwanza, ugunduzi wa Edwin Hubble miaka ya 1920, ambapo Bw. Hubble kwa kutumia telescope, aligundua kuwa bado Ulimwengu unaendelea kutanuka, ambapo alisema kadri galaxies zipokuwa mbalimbali basi ndio zinazidi kukimbiana (Hubble's law).

Pili, ugunduzi wa Cosmic Microwave Background (CMB). Mnamo miaka ya 1960, wanasayansi waligundua mwanga (radiation) ambao ni wa kale na huo mwanga umetawanyika katika sehemu zote za Ulimwengu. Wanasayansi wanaamini kuwa mwanga huu ulitokana na mlipuko wa big bang na umeendelea kuwepo kwa miaka yote hiyo hadi leo. Inaaminika mwanga huu ni kama mwangi au wimbi la mstuko wa big bang ambalo limeendelea kupoa na hatimae kuonekana katika Microwave domain of electromagnetic spectrum.

Udhaifu wa Nadharia Hii

i. Nadharia hii haielezi chanzo cha hiyo punje ndogo. Yaani hii punje ndogo ilitokea wapi, nini kilipelekea kuundwa kwa hii punje ndogo? Hapa pana maswali mengi ambayo sayansi haiwezi kujibu na itaendelea kusemwa tu kuwa "Ulimwengu ulianza kama punje ndogo". Na kama watasema ulitokana na vitu fulani basi watatakiwa kuonyesha pia hivyo vitu vimetokana na nini.
ii. Nadharia hii haielezi nini kilisababisha mlipuko ambao umeunda Ulimwengu huu.
iii. Je hii punje ndogo ilikuwa katika nini? Je Nadharia inasema nini juu ya uwepo wa mazingira fulani ambayo huweza kubeba kitu? Je hiyo punje ilikuwa ipo yenyewe tu? Je inawezekana kitu fulani kisiwepo juu ya kitu chochote? Nadharia bado haijaeleza.
iv. Hivi karibuni Kuna baadhi ya nyota zimegunduliwa kuwa na umri mkubwa kuliko big bang yenyewe. Mfano, Methuselah ni nyota ambayo inakadiriwa kuwa na miaka bilioni 14.45, yaani hii nyota ilikuwepo kabla ya tukio la big bang.
Kutokana na kutokuwa na majibu juu ya maswali haya, Kuna nadharia nyengine zilitungwa, ambazo zilizidi kuzua maswali mengine.

2. Steady-State Theory

Nadharia inasema kuwa Ulimwengu siku zote unatanuka lakini density (tungamo) ikindelea kubaki vilevile ambapo nyota na galaxies mpya huendelea kutengenezwa kwa kiwango sawa na hupoteaji wa nyota na galaxies za zamani ambazo hupotelea kwenda katika Ulimwengu usioonekana. Watafiti wa nadharia hii wanasema kuwa Ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho katika muda, na density na mpangilio wa galaxies ni sawa kwa muda wote.

Katika nadharia hii, tunaona moja kwa moja wameshindwa kuonyesha chanzo cha Ulimwengu.

3. The Plasma Cosmology

Nadharia hii inaamini kuwa evolution ya Ulimwengu kwa wakati uliopita inabidi ielezewe kwa kuangalia matukio yanayotokea katika Ulimwengu kwa sasa. Yaani inasema, matukio yanayotokea katika Ulimwengu sasa ndio hayohayo yalitokea katika Ulimwengu wakati uliopita. Nadharia hii pia inakataa kuwa Ulimwengu haujatokana na chochote kama inavyoaminika na watafiti wa big bang. Watafiti wa Plasma Cosmology wanaamini kwamba kwasababu tunaona Ulimwengu unaobadilika, basi huu Ulimwengu ulikuwepo siku zote and utaendelea kuwepo and kubadilika milele. Kama ilivyo Kwa steady state theory, Nadharia hii pia inakataa Ulimwengu kuwa na chanzo.

4. Big Bounce Theory

Big Bounce inasema kuwa Ulimwengu umekuwa ukitanuka na kuanguka mara kadhaa. Yaani Ulimwengu umetanuka mara kadhaa na ku-collapse mara kadhaa. Huu Ulimwengu tulionao ni zao la Ulimwengu ambao uli-collapse na kutanuka tena na wanatabiri kuwa huu Ulimwengu uta-collapse tena na pengine kutanuka tena. Kwahiyo Kuna series ya 'crunches and bangs' ambapo Ulimwengu unatanuka na kuanguka. Bado nadharia hii haionyeshi chanzo cha Ulimwengu bali huonyesha mabadiliko tu. Chanzo cha huo Ulimwengu ambao unacollapse na kutanuka ni kipi? Nini ilikuwa sababu ya kutanuka na ku-collapse? Bado hatupati majibu.

5. The Ekpyrotic Model

Nadharia hii inaamini kuwa big bang ilitokea kwa sababu ya mgongano wa branes mbili ambazo zilikuwa sambamba. Sina tafsiri sahihi ya neno branes, lakini branes inaweza kuelezewa kama any of the spatially extended mathematical objects of zero or more dimensions used in string theory. Watu wa Quantum mechanics na General relativity wanaweza wakanielewa. Katika mazungumzo haya, tuzichukulie hizo branes kwa mfano wa kamba, hivyo basi hizo kamba mbili sambamba zilisuguana na kupelekea moto ambao ndio ukazaa big bang na hatimae kuunda Ulimwengu. Hapa tunapata swali jengine, je hizi branes zilitoka wapi? Nini kilifanya zisuguane? Hapa pia Kuna maswali mengi.

Hitimisho: tumeona kuwa nadharia nyingi hazijaelezea hasa chanzo cha Ulimwengu, baadhi zinasema kabisa Ulimwengu hauna chanza na hautakuwa na mwisho na nyengine zinasema Ulimwengu ulianzia na kitu fulani, lakini haziwezi kuelezea chanzo cha hicho kitu. Yaani nini kilikuwa chanzo cha hicho ambacho wewe unakiona kuwa ndio kimeleta Ulimwengu?
Je, Kuna nadharia nyengine ambazo zina majibu mazuri zaidi?
Je, wale wanaopinga uwepo Mwenyezi Mungu wanategemea nadharia hizi katika kuelezea chanzo cha Ulimwengu?
 
Ni kwasababu imejidhatiti kwenye kupata jibu la uhakika na sio kubahatisha kwa kuaminishana

Na ndio maana kila majibu yanayotolewa na sayansi bado yanawekwa kwenye room ya kuendelea kuchunguzwa zaidi.

Sayansi inajua haijakamilika ipo kwenye nafasi kubwa ya kukosea na ndio maana inatoa mwanya kwa wenye mawazo mbadala kupitia uthibitisho wa kuweza kui challenge.

Lakini hata tukikubaliana kuipuuza sayansi je tutasimama na nini kama mbadala?

Dini?

Katika list ya maelfu ya dini itabidi tukubaliane kwanza dini gani ya kuipitisha ambayo tutaitumia kama njia ya kupata majibu.

Jambo ambalo hautakuwa tayari hata wewe kukubali kuona dini yako inaenguliwa na kupitisha dini nyingine.
 
Nadharia hii inaamini kuwa big bang ilitokea kwa sababu ya mgongano wa branes mbili ambazo zilikuwa sambamba. Sina tafsiri sahihi ya neno branes, lakini branes inaweza kuelezea kama any of the spatially extended mathematical objects of zero or more dimensions used in string theory. Watu wa Quantum mechanics na General relativity wanaweza wakanielewa. Katika mazungumzo haya, tuzichukulie hizo branes kwa mfano wa kamba, hivyo basi hizo kamba mbili sambamba zilisuguana na kupelekea moto ambao ndio ukazaa big bang na hatimae kuunda Ulimwengu. Hapa tunapata swali jengine, je hizi branes zilitoka wapi? Nini kilifanya zisuguane? Hapa pia Kuna maswali mengi.

Kwanza kwa nini unadhani ulimwengu lazima uwe na chanzo?

Umewezaje kuamini Mungu usiyemjua Hana chanzo ila una lazimisha ulimwenguni uwe na chanzo?

Kama Mungu huyo ameweza kuwepo bila chanzo, Inashindikana vipi kwa ulimwengu kuwepo bila chanzo?

Kama Mungu ndio chanzo cha ulimwengu, Chanzo cha Mungu ni nini?

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo. Basi hata Mungu lazima awe na chanzo,Na chanzo cha Mungu kiwe na chanzo, Na chanzo cha chanzo cha Mungu kiwe na chanzo mpaka infinity hukooo...

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo chanzo maana kitavuruga muundo mzima wa "ULAZIMA AWEPO CHANZO"
 
Hawa jamaa sijui wanafanya makusudi kuto kuelewa !!!
 
Hivi nikuulize swali chanzo cha yai la kuku ni nini?
 
Nikweli kabisa binadamu hatujaweza kupata definitive answer juu ya chanzo cha ulimwengu. Je, ujinga wetu unatosha kuthibitisha kwamba ulimwengu umeumbwa na sungura mwenye mikia saba?
 
Ni kwasababu imejidhatiti kwenye kupata jibu la uhakika na sio kubahatisha kwa kuaminishana

Na ndio maana kila majibu yanayotolewa na sayansi bado yanawekwa kwenye room ya kuendelea kuchunguzwa zaidi.

Sayansi inajua haijamilika ipo kwenye nafasi kubwa ya kukosea na ndio maana inatoa mwanya kwa wenye mawazo mbadala kupitia uthibitisho wa kuweza kui challenge.

Lakini hata tukikubaliana kuipuuza sayansi je tutasimama na nini kama mbadala?

Dini?

Katika list ya maelfu ya dini itabidi tukubaliane kwanza dini gani ya kuipitisha ambayo tutaitumia kama njia ya kupata majibu.

Jambo ambalo hautakuwa tayari hata wewe kukubali kuona dini yako inaenguliwa na kupitisha dini nyingine.
Sayansi haitakiwi kupuuzwa hata kidogo. Vyombo vya usafiri, mawasiliano, shughuli za kibinadamu, zimekuwa na zimerahisishwa kwasababu ya sayansi. Hakuna mtu mzima mwenye akili katika Karne hii alaf aamini kuwa sayansi haijawa sababu ya maendeleo yetu. Hoja ni kuwa sayansi haiwezi kutupa majibu juu ya baadhi ya mambo.
 
Kwanza kwa nini unadhani ulimwengu lazima uwe na chanzo?

Umewezaje kuamini Mungu usiyemjua Hana chanzo ila una lazimisha ulimwenguni uwe na chanzo?

Kama Mungu huyo ameweza kuwepo bila chanzo, Inashindikana vipi kwa ulimwengu kuwepo bila chanzo?

Kama Mungu ndio chanzo cha ulimwengu, Chanzo cha Mungu ni nini?

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo. Basi hata Mungu lazima awe na chanzo,Na chanzo cha Mungu kiwe na chanzo, Na chanzo cha chanzo cha Mungu kiwe na chanzo mpaka infinity hukooo...

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo chanzo maana kitavuruga muundo mzima wa "ULAZIMA AWEPO CHANZO"
Kuna pande kuu mbili,

Kuna wanaoamini uwepo wa Mungu na wale wasioamini uwepo wa Mungu.

Wasioamini uwepo wa Mungu wanasema, Kila kitu kinacho-exist,uwepo wake lazima uelezewe kisayansi. Swali, kisayansi Ulimwengu ulianzia wapi?

Kundi la pili ni la wale wanaoamini uwepo wa Mungu. Hawa Imani yao inasema si mambo yote yanaweza kuelezewa Kwa akili ya binadamu. Kwaiyo ukimuuliza muumini nini chanzo cha baadhi ya mambo, hawezi kukupa jibu kwasababu msingi wa Imani yake ni kuwa si kila kitu kinaweza kuelezewa na binadamu. Huo ndio Msingi.

Tunapowauliza kuhusu chanzo cha Ulimwengu, na vitu vingine inabidi mtuonyeshe kwasababu msingi wa imani yenu ni kuwa Kila kitu hutokea kisayansi.

Mkituuliza Mungu alianzia wapi, sie jibu letu ni fupi tu kuwa yeye Hana chanzo wala mwisho. Na mkisema hili linawezekana vipi, basi tutasema msingi wa tunachoamini ni kuwa Kuna baadhi ya mambo yana limit.

Nyinyi sasa ambao mnaamini kuwa Kila kitu kinatokea kisayansi mnalo jukumu la kuelezea kila kitu kinachoonekena bila kurukaruka.
 
Wanafanya tafiti wanapata jibu still wanaendelea na tafiti...Kisha uambiwe uiamini tafiti ya swali Hilo Hilo ,kesho waje na majibu tofauti.
Tafitiiiiii😂

Kila mtu afe na chake.
Chagua Upande mwanetu.
 
Sayansi haitakiwi kupuuzwa hata kidogo. Vyombo vya usafiri, mawasiliano, shughuli za kibinadamu, zimekuwa na zimerahisishwa kwasababu ya sayansi. Hakuna mtu mzima mwenye akili katika Karne hii alaf aamini kuwa sayansi haijawa sababu ya maendeleo yetu. Hoja ni kuwa sayansi haiwezi kutupa majibu juu ya baadhi ya mambo.
Hata kabla we haujasema tayari sayansi yenyewe imejielezea.

Sayansi sio jibu la kila kitu na sio kila kitu ambacho hakijaelezewa na sayansi maana yake hicho kitu ni kweli.

Misingi ya Sayansi katika kutangaza madai ya kitu fulani kuwa ni ukweli hutegemeana na uthibitisho ambao umepatikana kwa njia za utafiti.

Kinyume na hapo hicho kitu hakiwezi kukubalika kuwa ni cha kweli.

Sasa katika vitu ambavyo unaviona Sayansi haijavitolea majibu na kusema Sayansi haina majibu, unafikiri kuna vyanzo vingine nje ja sayansi vilivyotoa majibu ya hivyo vitu kwa njia ya uthibitisho?
 
Habari wapendwa,

Kuna hizi theories zinazoelezea chanzo cha Ulimwengu, kwa uelewa wangu hakuna hata moja inayoelezea kikamilifu chanzo cha huu Ulimwengu, bali nyingi zinaelezea modifications na evolution tu ya Ulimwengu ambapo katika kuelezea huko zinaweza zisiwe sahihi pia.

Tuziangalie kwanza nadharia zenyewe na kivipi zimeshindwa kuelezea chanzo Cha Ulimwengu.

1. Big Bang Theory

Hii ni nadharia maarufu miongoni mwetu, lakini si nadharia pekee inayoelezea chanzo cha Ulimwengu. Kwa mujibu wa big bang, Ulimwengu wote ulianza kama punje ndogo (atom), yenye joto sana, ambayo ilikuwa katika mgandamizo mkubwa usiomithirika (infinitely dense). Kisha punje hii akaanza kutanuka na kutengeneza sehemu na wakati (space and time). Kadri Ulimwengu ulivyotanuka basi ukapoa na kufanya baadhi ya sehemu kuwa ni zenye kukalika na viumbe hai kama ilivyo katika Dunia yetu. Wanasayansi wanadai tulio hili la big bang lilotokea takribani miaka bilioni 13.7 iliyopita.
Wanasayansi wanatumia gunduzi mbili za kisayansi kuthibitisha madai haya.

Kwanza, ugunduzi wa Edwin Hubble miaka ya 1920, ambapo Bw. Hubble kwa kutumia telescope, aligundua kuwa bado Ulimwengu unaendelea kutanuka, ambapo alisema kadri galaxies zipokuwa mbalimbali basi ndio zinazidi kukimbiana (Hubble's law).

Pili, ugunduzi wa Cosmic Microwave Background (CMB). Mnamo miaka ya 1960, wanasayansi waligundua mwanga (radiation) ambao ni wa kale na huo mwanga umetawanyika katika sehemu zote za Ulimwengu. Wanasayansi wanaamini kuwa mwanga huu ulitokana na mlipuko wa big bang na umeendelea kuwepo kwa miaka yote hiyo hadi leo. Inaaminika mwanga huu ni kama mwangi au wimbi la mstuko wa big bang ambalo limeendelea kupoa na hatimae kuonekana katika Microwave domain of electromagnetic spectrum.

Udhaifu wa Nadharia Hii

i. Nadharia hii haielezi chanzo cha hiyo punje ndogo. Yaani hii punje ndogo ilitokea wapi, nini kilipelekea kuundwa kwa hii punje ndogo? Hapa pana maswali mengi ambayo sayansi haiwezi kujibu na itaendelea kusemwa tu kuwa "Ulimwengu ulianza kama punje ndogo". Na kama watasema ulitokana na vitu fulani basi watatakiwa kuonyesha pia hivyo vitu vimetokana na nini.
ii. Nadharia hii haielezi nini kilisababisha mlipuko ambao umeunda Ulimwengu huu.
iii. Je hii punje ndogo ilikuwa katika nini? Je Nadharia inasema nini juu ya uwepo wa mazingira fulani ambayo huweza kubeba kitu? Je hiyo punje ilikuwa ipo yenyewe tu? Je inawezekana kitu fulani kisiwepo juu ya kitu chochote? Nadharia bado haijaeleza.
iv. Hivi karibuni Kuna baadhi ya nyota zimegunduliwa kuwa na umri mkubwa kuliko big bang yenyewe. Mfano, Methuselah ni nyota ambayo inakadiriwa kuwa na miaka bilioni 14.45, yaani hii nyota ilikuwepo kabla ya tukio la big bang.
Kutokana na kutokuwa na majibu juu ya maswali haya, Kuna nadharia nyengine zilitungwa, ambazo zilizidi kuzua maswali mengine.

2. Steady-State Theory

Nadharia inasema kuwa Ulimwengu siku zote unatanuka lakini density (tungamo) ikindelea kubaki vilevile ambapo nyota na galaxies mpya huendelea kutengenezwa kwa kiwango sawa na hupoteaji wa nyota na galaxies za zamani ambazo hupotelea kwenda katika Ulimwengu usioonekana. Watafiti wa nadharia hii wanasema kuwa Ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho katika muda, na density na mpangilio wa galaxies ni sawa kwa muda wote.

Katika nadharia hii, tunaona moja kwa moja wameshindwa kuonyesha chanzo cha Ulimwengu.

3. The Plasma Cosmology

Nadharia hii inaamini kuwa evolution ya Ulimwengu kwa wakati uliopita inabidi ielezewe kwa kuangalia matukio yanayotokea katika Ulimwengu kwa sasa. Yaani inasema, matukio yanayotokea katika Ulimwengu sasa ndio hayohayo yalitokea katika Ulimwengu wakati uliopita. Nadharia hii pia inakataa kuwa Ulimwengu haujatokana na chochote kama inavyoaminika na watafiti wa big bang. Watafiti wa Plasma Cosmology wanaamini kwamba kwasababu tunaona Ulimwengu unaobadilika, basi huu Ulimwengu ulikuwepo siku zote and utaendelea kuwepo and kubadilika milele. Kama ilivyo Kwa steady state theory, Nadharia hii pia inakataa Ulimwengu kuwa na chanzo.

4. Big Bounce Theory

Big Bounce inasema kuwa Ulimwengu umekuwa ukitanuka na kuanguka mara kadhaa. Yaani Ulimwengu umetanuka mara kadhaa na ku-collapse mara kadhaa. Huu Ulimwengu tulionao ni zao la Ulimwengu ambao uli-collapse na kutanuka tena na wanatabiri kuwa huu Ulimwengu uta-collapse tena na pengine kutanuka tena. Kwahiyo Kuna series ya 'crunches and bangs' ambapo Ulimwengu unatanuka na kuanguka. Bado nadharia hii haionyeshi chanzo cha Ulimwengu bali huonyesha mabadiliko tu. Chanzo cha huo Ulimwengu ambao unacollapse na kutanuka ni kipi? Nini ilikuwa sababu ya kutanuka na ku-collapse? Bado hatupati majibu.

5. The Ekpyrotic Model

Nadharia hii inaamini kuwa big bang ilitokea kwa sababu ya mgongano wa branes mbili ambazo zilikuwa sambamba. Sina tafsiri sahihi ya neno branes, lakini branes inaweza kuelezewa kama any of the spatially extended mathematical objects of zero or more dimensions used in string theory. Watu wa Quantum mechanics na General relativity wanaweza wakanielewa. Katika mazungumzo haya, tuzichukulie hizo branes kwa mfano wa kamba, hivyo basi hizo kamba mbili sambamba zilisuguana na kupelekea moto ambao ndio ukazaa big bang na hatimae kuunda Ulimwengu. Hapa tunapata swali jengine, je hizi branes zilitoka wapi? Nini kilifanya zisuguane? Hapa pia Kuna maswali mengi.

Hitimisho: tumeona kuwa nadharia nyingi hazijaelezea hasa chanzo cha Ulimwengu, baadhi zinasema kabisa Ulimwengu hauna chanza na hautakuwa na mwisho na nyengine zinasema Ulimwengu ulianzia na kitu fulani, lakini haziwezi kuelezea chanzo cha hicho kitu. Yaani nini kilikuwa chanzo cha hicho ambacho wewe unakiona kuwa ndio kimeleta Ulimwengu?
Je, Kuna nadharia nyengine ambazo zina majibu mazuri zaidi?
Je, wale wanaopinga uwepo Mwenyezi Mungu wanategemea nadharia hizi katika kuelezea chanzo cha Ulimwengu?
1. Sayansi haijawahi kusema nadharia zake zimekamilika. Ukisikia mtu anakwambia nadharia ya sayansi imekamilika, ujue huyo hajui sayansi ni nini.

Mwanafalsafa nguli Kurt Godel aliandika "Godel's Incompleteness Theorems" zinazoelezea kwa undani kabisa suala hili.

Nakushauri uzisome na kuzielewa.

2. Kupinga uwepo wa Mungu ni kitu kimoja, nadharia za kisayansi ni kitu kingine. Mtu anaweza kupinga uwepo wa Mungu kwa kutumia mantiki na falsafa tu, bila kuhitaji nadharia yoyote kati ya hizi za kisayansi.

Kwa mfano, proof by contradiction, using the problem of evil, inaweza kupinga uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote (kama wa Biblia na Quran) bila kuhitaji nadharia yoyote ya sayansi.

Ni sawa na kuweza kujua kwamba 10 si square root ya 2 bila kujua square root ya 2 ni nini.

Ni kama kujua binti mchanga mwenye umri wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, bila hata kumjua mama mzazi wa huyo mwanamme mwenye miaka 30 ni nani.

Ni kama kujua the sum of two even numbers will always give you an even number, without knowing all numbers.

Kitu kikubwa kuelewa ni kwamba, hata katika sayansi, huhitajibsayansi ikamilike, au huhitaji hata kujua jibu sahihi la kisayansi, ili kujua kuwa jibu fulani si sahihi.

Kwa maneno mengine, hata kwenye sayansi, tunaweza kuwa hatujakamilisha jibu la ulimwengu umeanzaje, lakini tukajua kuwa jibu la Mungu yupo na ndiye aliyeumba ulimwengu tukajua si la kweli.

carnage21
 
Binadamu wa kale/ wa mwanzo hawakuweza kuacha nakala/ maandishi ya kueleza walitokea wapi pamoja na Dunia waliikutaje, hii ndio inaleta mgongano siku zote
Lakini sayansi haichoki inazidi kutupatia majibu na kadiri siku zinavozidi kwenda wanazidi kuleta data hivo kwa vizazi vijavo watapata majibu yalio “beyond reasonable doubt” ulimwengu ulitokea wapi na binadamu wa kwanza alitokeaje.
 
Habari wapendwa,

Kuna hizi theories zinazoelezea chanzo cha Ulimwengu, kwa uelewa wangu hakuna hata moja inayoelezea kikamilifu chanzo cha huu Ulimwengu, bali nyingi zinaelezea modifications na evolution tu ya Ulimwengu ambapo katika kuelezea huko zinaweza zisiwe sahihi pia.

Tuziangalie kwanza nadharia zenyewe na kivipi zimeshindwa kuelezea chanzo Cha Ulimwengu.

1. Big Bang Theory

Hii ni nadharia maarufu miongoni mwetu, lakini si nadharia pekee inayoelezea chanzo cha Ulimwengu. Kwa mujibu wa big bang, Ulimwengu wote ulianza kama punje ndogo (atom), yenye joto sana, ambayo ilikuwa katika mgandamizo mkubwa usiomithirika (infinitely dense). Kisha punje hii akaanza kutanuka na kutengeneza sehemu na wakati (space and time). Kadri Ulimwengu ulivyotanuka basi ukapoa na kufanya baadhi ya sehemu kuwa ni zenye kukalika na viumbe hai kama ilivyo katika Dunia yetu. Wanasayansi wanadai tulio hili la big bang lilotokea takribani miaka bilioni 13.7 iliyopita.
Wanasayansi wanatumia gunduzi mbili za kisayansi kuthibitisha madai haya.

Kwanza, ugunduzi wa Edwin Hubble miaka ya 1920, ambapo Bw. Hubble kwa kutumia telescope, aligundua kuwa bado Ulimwengu unaendelea kutanuka, ambapo alisema kadri galaxies zipokuwa mbalimbali basi ndio zinazidi kukimbiana (Hubble's law).

Pili, ugunduzi wa Cosmic Microwave Background (CMB). Mnamo miaka ya 1960, wanasayansi waligundua mwanga (radiation) ambao ni wa kale na huo mwanga umetawanyika katika sehemu zote za Ulimwengu. Wanasayansi wanaamini kuwa mwanga huu ulitokana na mlipuko wa big bang na umeendelea kuwepo kwa miaka yote hiyo hadi leo. Inaaminika mwanga huu ni kama mwangi au wimbi la mstuko wa big bang ambalo limeendelea kupoa na hatimae kuonekana katika Microwave domain of electromagnetic spectrum.

Udhaifu wa Nadharia Hii

i. Nadharia hii haielezi chanzo cha hiyo punje ndogo. Yaani hii punje ndogo ilitokea wapi, nini kilipelekea kuundwa kwa hii punje ndogo? Hapa pana maswali mengi ambayo sayansi haiwezi kujibu na itaendelea kusemwa tu kuwa "Ulimwengu ulianza kama punje ndogo". Na kama watasema ulitokana na vitu fulani basi watatakiwa kuonyesha pia hivyo vitu vimetokana na nini.
ii. Nadharia hii haielezi nini kilisababisha mlipuko ambao umeunda Ulimwengu huu.
iii. Je hii punje ndogo ilikuwa katika nini? Je Nadharia inasema nini juu ya uwepo wa mazingira fulani ambayo huweza kubeba kitu? Je hiyo punje ilikuwa ipo yenyewe tu? Je inawezekana kitu fulani kisiwepo juu ya kitu chochote? Nadharia bado haijaeleza.
iv. Hivi karibuni Kuna baadhi ya nyota zimegunduliwa kuwa na umri mkubwa kuliko big bang yenyewe. Mfano, Methuselah ni nyota ambayo inakadiriwa kuwa na miaka bilioni 14.45, yaani hii nyota ilikuwepo kabla ya tukio la big bang.
Kutokana na kutokuwa na majibu juu ya maswali haya, Kuna nadharia nyengine zilitungwa, ambazo zilizidi kuzua maswali mengine.

2. Steady-State Theory

Nadharia inasema kuwa Ulimwengu siku zote unatanuka lakini density (tungamo) ikindelea kubaki vilevile ambapo nyota na galaxies mpya huendelea kutengenezwa kwa kiwango sawa na hupoteaji wa nyota na galaxies za zamani ambazo hupotelea kwenda katika Ulimwengu usioonekana. Watafiti wa nadharia hii wanasema kuwa Ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho katika muda, na density na mpangilio wa galaxies ni sawa kwa muda wote.

Katika nadharia hii, tunaona moja kwa moja wameshindwa kuonyesha chanzo cha Ulimwengu.

3. The Plasma Cosmology

Nadharia hii inaamini kuwa evolution ya Ulimwengu kwa wakati uliopita inabidi ielezewe kwa kuangalia matukio yanayotokea katika Ulimwengu kwa sasa. Yaani inasema, matukio yanayotokea katika Ulimwengu sasa ndio hayohayo yalitokea katika Ulimwengu wakati uliopita. Nadharia hii pia inakataa kuwa Ulimwengu haujatokana na chochote kama inavyoaminika na watafiti wa big bang. Watafiti wa Plasma Cosmology wanaamini kwamba kwasababu tunaona Ulimwengu unaobadilika, basi huu Ulimwengu ulikuwepo siku zote and utaendelea kuwepo and kubadilika milele. Kama ilivyo Kwa steady state theory, Nadharia hii pia inakataa Ulimwengu kuwa na chanzo.

4. Big Bounce Theory

Big Bounce inasema kuwa Ulimwengu umekuwa ukitanuka na kuanguka mara kadhaa. Yaani Ulimwengu umetanuka mara kadhaa na ku-collapse mara kadhaa. Huu Ulimwengu tulionao ni zao la Ulimwengu ambao uli-collapse na kutanuka tena na wanatabiri kuwa huu Ulimwengu uta-collapse tena na pengine kutanuka tena. Kwahiyo Kuna series ya 'crunches and bangs' ambapo Ulimwengu unatanuka na kuanguka. Bado nadharia hii haionyeshi chanzo cha Ulimwengu bali huonyesha mabadiliko tu. Chanzo cha huo Ulimwengu ambao unacollapse na kutanuka ni kipi? Nini ilikuwa sababu ya kutanuka na ku-collapse? Bado hatupati majibu.

5. The Ekpyrotic Model

Nadharia hii inaamini kuwa big bang ilitokea kwa sababu ya mgongano wa branes mbili ambazo zilikuwa sambamba. Sina tafsiri sahihi ya neno branes, lakini branes inaweza kuelezewa kama any of the spatially extended mathematical objects of zero or more dimensions used in string theory. Watu wa Quantum mechanics na General relativity wanaweza wakanielewa. Katika mazungumzo haya, tuzichukulie hizo branes kwa mfano wa kamba, hivyo basi hizo kamba mbili sambamba zilisuguana na kupelekea moto ambao ndio ukazaa big bang na hatimae kuunda Ulimwengu. Hapa tunapata swali jengine, je hizi branes zilitoka wapi? Nini kilifanya zisuguane? Hapa pia Kuna maswali mengi.

Hitimisho: tumeona kuwa nadharia nyingi hazijaelezea hasa chanzo cha Ulimwengu, baadhi zinasema kabisa Ulimwengu hauna chanza na hautakuwa na mwisho na nyengine zinasema Ulimwengu ulianzia na kitu fulani, lakini haziwezi kuelezea chanzo cha hicho kitu. Yaani nini kilikuwa chanzo cha hicho ambacho wewe unakiona kuwa ndio kimeleta Ulimwengu?
Je, Kuna nadharia nyengine ambazo zina majibu mazuri zaidi?
Je, wale wanaopinga uwepo Mwenyezi Mungu wanategemea nadharia hizi katika kuelezea chanzo cha Ulimwengu?
Kwanza inabidi ufahamu maana ya nadharia (theory)

Katika sayansi kuna theory, facts, laws, principles, etc

Theory/nadharia huwa haina ushahidi isipokuwa ni mawazo tu ya mtu au watu.
 
Ni kwasababu imejidhatiti kwenye kupata jibu la uhakika na sio kubahatisha kwa kuaminishana

Na ndio maana kila majibu yanayotolewa na sayansi bado yanawekwa kwenye room ya kuendelea kuchunguzwa zaidi.

Sayansi inajua haijakamilika ipo kwenye nafasi kubwa ya kukosea na ndio maana inatoa mwanya kwa wenye mawazo mbadala kupitia uthibitisho wa kuweza kui challenge.

Lakini hata tukikubaliana kuipuuza sayansi je tutasimama na nini kama mbadala?

Dini?

Katika list ya maelfu ya dini itabidi tukubaliane kwanza dini gani ya kuipitisha ambayo tutaitumia kama njia ya kupata majibu.

Jambo ambalo hautakuwa tayari hata wewe kukubali kuona dini yako inaenguliwa na kupitisha dini nyingine.
Binadamu siku zote ni dhaifu, hivyo hivyo kwa wanasayansi

Si kila kitu kwenye sayansi ni cha ukweli/uhakika

Sayansi hii hii ndio unatufundisha kuwa binadamu alitokana na jamii ya sokwe, je ni kweli??

Sayansi hii hii inatuambia kwamba twiga wa zamani walikuwa na shingo fupi, nyoka walikuwa na miguu nk,. Je ni kweli??

Sayansi inashindwa kuthibitisha imani za kishirikina, je hazipo

Kuna watu wanashindwa kupona magonjwa mahospitalini (kisayansi) ila wanapona kwa waganga, masheikh au wachungaji, ila bado sayansi haikubali

MWISHO

Sayansi inacover eneo lake, dini ina eneo lake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom