Kwanini Februari inakuwa na siku 29?

Powell Gonzalez

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
622
1,276
Karibia kila baada ya miaka minne mwezi wa februari hupata siku ya nyongeza, yaani siku ya 29 ambayo huweza kuitwa ''leap day''. Kama sehemu ya gregorian claendar.

Hii ndio sababu...
Gregorian calendar ilianzishwa 1582 kwenye kalenda hii karibia kila baada ya miaka minne mwezi februari huwa na siku 29, ambapo huo mwaka huitwa ''leap year''.

Dunia huchukua siku 365.24 kuzunguka jua, siku ambazo hakuna kalenda inayoweza accomodate, kawaida kalenda zina siku 365 (hapa kumbuka huwa hazihesabu ile 0.24 ambayo kiuhalisia ipo) sasa kila baada ya miaka minne hizi siku 0.24 zilizokuwa zinaachwa hujumuishwa ili kufidia na hupatikana siku moja ambayo ikiongezwa kwenye siku 365 hupatikana siku 366 siku moja ikiwa imeongezeka, ndio hiyo siku huongezwa katika mwezi februari wa kila baada ya miaka minne.

KWANINI LAZIMA TUONGEZE HIYO SIKU?
Kama nilivyosema hapo mwanzo, dunia hulizunguka jua kwa siku 365.24, na kalenda zetu huwa na siku 365 pekee.

Hivyo kila mwaka mzunguko wetu huwa umeziacha kalenda kwa siku 0.242 kila mwaka, kama hatutatafuta mbinu ya kufidia basi hizi siku zitazidi kuongezeka na kalenda zetu zitazidi kubaki nyuma zaidi kwa kadri miaka inavyokwenda. Hii itasababisha kalenda kutokuwa sahihi kwa sababu kalenda inafuta mzunguko wa dunia.

Ukumbuke tayari binadam tumeshazoea mismu ya mwaka kwa kuangalia miezi au tarehe kwenye kalenda, na misimu hii hutokana na mzunguko wa dunia (waliosoma geography hapa hawahitaji maelezo), sasa kama kalenda ikizidi kuachwa nyuma basi kuna kipindi kalenda zingekuwa zinasema uongo, yaani mwezi fulani ni kiangazi kama ilivyozoeleka ila cha ajabu mvua inanyesha....ndio maana ili isitokee hivi basi hii siku ya 29 katika mwezi februari kila bada ya miezi minne huwa ipo kwaajili ya kufidia zile siku zinazoachwa kila mwaka (yaani 0.24 days x 4 ambayo huja appromimately siku moja)

SIO KILA BAADA YA MIAKA MINNE FEBRUARI HUWA NA SIKU 29
Hata hivyo si kila baada ya miaka minne februari huwa na siku 29, hii ni kwasababu kila tunapoongeeza siku moja katika februari basi tunaifanya kalenda kutangulia zaidi dakika 44.

Ili mwaka upewe hii siku moja basi inabidi ugawanyike kwa nne, kwa miatatu lakini usigawanyike kwa 100.
ndio maana 1700, 1800 na 1900 hazikuwa leap year lakini 2000 ukawa leap year vivyo hivyo mwaka 2100 pia hautakuwa leap year licha ya kuwa utakuwa mwaka wa nne kutoka last leap year ambayo itakuwa 2096.
Hii husaidia kufidia zile 44 minutes.

Hii ni kwa kalenda ya gregorian ambayo hutumika sehemu kubwa ya ulimwengu.

Baadhi ya kalenda zingine pia huwa na utaratibu wake , Kwa mfano.

CHINESE CALENDAR

yenyewe huongeza leap month kila baada ya miaka mitatu.

Naomba kuwasilisha.
I had to write this!
 
Mwaka 1580 huko hakukuwepo vifaa vya kuchunguza mwenendo wa dunia angani sasa inakuwaje utuambie dunia uzunguka mwaka kwa siku 365.24 how..! Ilikuwaje wakapata hizi hesabu miaka hiyo..?

Na km kalenda ilianza mwaka 1582 the hiyo miaka ya nyuma ilifidiwa vipi je km haikufidia kuna usahihi upi kwa kalenda ya sasa?
 
Kwamba Dunia huchukua siku 365.24 kulizunguka Jua....?!

Je,. una ushahidi gani kama Dunia inazunguka na haipo fixed kama tunavyoiona na kuihisi Kwa milango yetu ya fahamu?!
 
SIO KILA BAADA YA MIAKA MINNE FEBRUARI HUWA NA SIKU 29
Hata hivyo si kila baada ya miaka minne februari huwa na siku 29, hii ni kwasababu kila tunapoongeeza siku moja katika februari basi tunaifanya kalenda kutangulia zaidi dakika 44.

Ili mwaka upewe hii siku moja basi inabidi ugawanyike kwa nne, kwa miatatu lakini usigawanyike kwa 100.
Ijapokuwa maelezo yako hapa yako sahihi kwa namna fulani yanapingana pia kwa sababu
Kila baada ya miaka mitatu, mwaka wa nne ni lazima uwe mwaka mrefu. Kwa hiyo kwa sababu tulianza na mwaka wa kwanza baada ya kuzaliwa Yesu, kwa hiyo mwaka wa nne baada ya Yesu kuzaliwa, ulikuwa ni leap year; reference point yenye ikiwa ni mwaka ule wa kwanza baada ya kuzaliwa Kristo

Mbali na hilo, kawaida mwaka una siku 365.25 au siku 365 na masaa 6 na dakika 9 na si siku 365.24


"Earth revolves in orbit around the Sun in 365 days, 6 hours, 9 minutes with reference to the stars, at a speed ranging from 29.29 to 30.29 km/s. The 6 hours, 9 minutes adds up to about an extra day every fourth year, which is designated a leap year, with the extra day added as February 29th"
 
Samahani kaka, ni kama sijaelewa ulilenga kueleza au kuuliza kipi, would you mind to make some clarification please?
 
Back
Top Bottom