Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

Mkuu wewe hauamini nini sasa wanasayansi wako wanakili kuwa Venus ikijizungusha kwenye muhimili wake ni sawa na siku zaidi ya 240 za dunia sasa wewe unajuwa mbingu hipo wapi?? Hadi unaongea hvyo
 
Mtu akishasema kwa uelewa wake mdogo huwa ananipa shida sana kuendelea kusikiliza.
 
Nilichoelewa mimi na akili yangu ya KVANT KUBWA ni

Wanaposema miaka 1000 kwake ni sawa na siku 1.anatumbusha viumbe wake kuwa yeye hapotezi KUMBUKUMBU.

Kwa binadamu ni rahisi na kawaida kukumbuka ratiba na mizunguko yake yote aliyoifanya jana (tarehe na mwezi wa jana mwaka huu) lakini asikumbuke route au mizunguko,ratiba yake aliyoifanya tarehe na mwezi wa jana ya (mwaka uliopita)..

Mfano wakati una miaka mitatu uliwahi kuiba andazi sokoni(hiyo ni dhambi ulifanya). Lakini leo hii hukumbuki chochote na unaweza ukajiona huna dhambi duniani..kisa ni muda mrefu umepita...lakini kwa Mungu hatasahau atalikumbuka tukio lako lote kama vile limefanyika muda mfupi uliopita(saa au siku moja iliyopita)
Hivo utakumbushwa na kuhukumiwa vile vile...asante ngoja niendele kunywa KVANT yangu
KVANT KUBWA,hongeza nyingine...
 
Njoja nijenge hoja

Mwaka 1 duniani ni sawa na miaka mingapi kwenye sayari ya Jupiter au pluto. Kwa maana ya Jua kuzunguka dunia au sayari ya pluto .

Ukishajibu hapo haishindikani mwaka 1 duniani kuwa sawa na miaka 1000 mbinguni!
Kwa mantiki hiyo hiyo unaweza kucalculate umbali kutoka duniani hadi mbinguni, sio???!!
 
Huwezi kuanza kuandikiwa dhambi kwa umri huo wa miaka mi3.
Nilichoelewa mimi na akili yangu ya KVANT KUBWA ni

Wanaposema miaka 1000 kwake ni sawa na siku 1.anatumbusha viumbe wake kuwa yeye hapotezi KUMBUKUMBU.

Kwa binadamu ni rahisi na kawaida kukumbuka ratiba na mizunguko yake yote aliyoifanya jana (tarehe na mwezi wa jana mwaka huu) lakini asikumbuke route au mizunguko,ratiba yake aliyoifanya tarehe na mwezi wa jana ya (mwaka uliopita)..

Mfano wakati una miaka mitatu uliwahi kuiba andazi sokoni(hiyo ni dhambi ulifanya). Lakini leo hii hukumbuki chochote na unaweza ukajiona huna dhambi duniani..kisa ni muda mrefu umepita...lakini kwa Mungu hatasahau atalikumbuka tukio lako lote kama vile limefanyika muda mfupi uliopita(saa au siku moja iliyopita)
Hivo utakumbushwa na kuhukumiwa vile vile...asante ngoja niendele kunywa KVANT yangu
 
Jamani, Mbona naona Mbinguni imetawala? Mnaitoa wapi?
Nimesoma Zaburi hiyo ya 90:4 inasema kwamba, "Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha kupita, kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku"

Lakini pia hata hiyo Petro haisemi habari za mbinguni, ninyi wenzetu mnazitoa wapi?
2Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
 
Kingine kincho sound tofauti masikioni mwangu ni huu msemo kua ili uelewe maandiko ya biblia inabidi roho mtakatifu akushukie kwanza kwakweli mm sidhani kama ni kweli kwamba inambidi ashuke kwanza kisha ndio akufunulie ...noo asee hapana. Kwanini?

Kwa mujibu wa katekismu au mafundisho yoyote yale ya kikristo inafundisha kua Roho mtakatifu hutupatia mapaji yake saba ambapo kati ya hayo mapaji ni Hekima na Elimu. indi tu binaadamu anapozaliwa Mungu humbarikia kila kitu baadhi ya mapaji tunazaliwa nayo japo sio wote, moja ya paji tunalozaliwa nayo ni paji la Hekima, japo kutokana na malezi au mazingira anayokulia mtoto paji hilo laweza kufifia. Hivyo basi katika kutafsiri maandiko ya bible kinachotumika ni Hekima, paji la hekima ndio linalowezesha kuitafakari andiko la biblia, na ukumbuke anayetoa uwezo huo wa kua na hekima Ni Roho mtakatifu.. Hekima hiyo inakuwezesha pindi unaposoma andiko tu kwa mara ya kwanza mojakwamoja unafahamu kua hili andiko lina ujumbe fulani ndani yake, kama vile darasani kuna mtu akiona swali kwa mara ya kwanza tu bila kucherewa haraka anafahamu hili swali lahitaji nini. Hivyo basi kuna watu wanayo hekima hiyo wengine hawana..katika kutafsiri maandiko pia kuna makundi mawili ya watu ambayo ni (i)Watu ambao wakiona andiko wanalielewa na wanaweza kilielezea mbele ya wengine (ii)kuna wengine wakielewa andiko hawawezi kulielezea kwa wengine kutoka na uwezo mdogo wa kuwasilisha hoja mbele za watu {nipo kundi namba mbili}

kwa mantiki hiyo Roho mtakatifu hakushukii ili uweze fafanua andiko ila anakua ashakujalia kipawa chake toka siku wazaliwa...

pia haya ni mawazo yangu
Unapinga maandiko kwa kuweka upotoshaji mkubwa.

Bwana na akukemee
 
Mungu daima huzungumza na sisi binadamu ktk metaphorical sense ili tuweze kutambua Ukuu Wake.
Siku 1000 ni KAMA siku 1.
Neno KAMA limetumika kama ufananisho tu, si kitu real.
For your info, kule mbinguni hakuna jua wala mwezi. Hakuna mchana wala usiku, so hakunaga masuala ya time kule (Uf 22:5). Task iliyoko kule ni kuimba tu - haleluya, haleluya, haleluya... up to infinity bila kukoma!
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom