Nadhani wimbo huu utafanya vizuri sana mwaka 2023

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
Huyu mwanadada Libianca ni mwanamuziki wa Cameroon, na mwaka huu ametoa wimbo uitwao PEOPLE. Binafsi nimeusikiliza mara kadhaa na kutambua kwamba huyu dada ana kipaji kikubwa mno cha uandishi na uimbaji. Mashairi ya huu wimbo yana ujumbe mzito sana na ametumia mahadhi ya Afro-Fusion (Huku akichanganya Blues, Soul, RnB na Highlife) kama ambavyo Burna Boy anafanya.

Mziki una mahadhi mengi lakini bado unausikia Uafrika kwa kiwango kikubwa na kufahamu kabisa huyu ni mwanamuziki kutoka Afrika Magharibi. Kiukweli amejitahidi mno.

Yanaweza yakawa ni maoni yangu binafsi na nimeandika kwasababu ya mahaba na huu wimbo, lakini kama wewe ni mdau wa muziki naomba umsikilize. Kila siku huwa nasema wasanii wetu wanahitaji kujifunza na kubadilika sana kama wanataka kulifikia soko la kimataifa.

Nimeusikiliha kupitia andiko lako, ngoja tuupe wiki mbili hadi tatu alafu tuangalie viewers maana hao ndiyo watakaombeba hata mapato yake, vinginevyo wimbo unaweza kuwa mzuri ila arena wakamfanyia yale ya Rick Ross majuzi huko amerika!
 
Naam, mimi binafsi huwa nasema hivi "MUDA NI MWALIMU"
 
Nimeusikiliha kupitia andiko lako, ngoja tuupe wiki mbili hadi tatu alafu tuangalie viewers maana hao ndiyo watakaombeba hata mapato yake, vinginevyo wimbo unaweza kuwa mzuri ila arena wakamfanyia yale ya Rick Ross majuzi huko amerika!
Nadhani umejionea wenyewe jinsi wimbo unavyosumbua kwenye charts nyingi za duniani.
 
Back
Top Bottom