Haya ndiyo mapambano ambayo nina hamu kuyaona kwa mwaka huu 2024

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,454
21,158
Hakika mwaka jana (2023) ulikuwa mwaka mzuri sana kwenye upande wa boxing ,tulishuhudia mapambano ya kukata na shoka, linatoka hili linakuja lile, mfano Terence Crawford vs Errol Spence, Gervonta Davis (Kwa sasa Abdul Wahid) Vs Ryan Garcia, Devin Haney vs Vasily Lomachenko nk.

Mwaka huu Sasa haya ndio mapambano ambayo nina hamu nayo sana kuyaona.

1) Artur Beterbiev vs Dmitry Bivol
Artur rekodi yake imetakata sana, amepigana mapambano 20 na yote 20 ameshinda kwa K.O , ametoka kupigana juzi dhidi ya Callium Smith na ameshinda kwa K.O raundi ya 7.

Binafsi karata yangu nampa Bivol , huwa Sina imani sana na hawa K.O artist.

2)Jason Ennis vs Terence Crawford.

Hili pia litakuwa pambano kali sana na ni ngumu mno kutabili.

3) Hassan Mwakinyo vs Asemahle Wellem.

Wellem anapambano March 1 dhidi ya Selemani Kidunda , japo binafsi nampa 66% Wellem kushinda.

Wellem na Hassan pambano litakuwa kali sana na litavutia mno.

4) Devin Haney vs Gervonta Davis.

5) Shakur Stevenson vs Gervonta Davis/Devin Haney.

6) Oleksandr Usyk vs Tyson Fury.

7) Nasibu Ramadhan Vs Said Bwanga.

8) Anthony Joshua vs Tyson Fury.

9) Natasha Jonas vs Claresa Shields

10) Benavidez vs Canelo.

Naoya Inoue apande uzito kutafuta challenge mpya, kwenye Bantamweight hana mpinzani.
 
Uyo wellem ndo yule msouth alimtandika kiduku? Kidunda ngumi zake nzito sana akilenga target vizuri mpinzani lazima aende chini tatizo ni mzito halafu hayupo vizuri kwenye kukwepa ngumi za mpinzani. Hivi Itawezekana kweli uyo msauzi kupigana na mwakinyo? maana naona kama wanatofautiana sana uzito.
 
Wellem ndiye aliyempiga Kiduku .

Wellem kupigana na Mwakinyo inawezekana kabisa.

Kitakachofanyika Wellem ashuke kidogo na Mwakinyo apande kidogo wakutane kati kwenye Super Welterweight.
 
Ingekua tayari wapo kwenye uzani sawa ingekua rahisi ila iyo ya kufosi sidhani kama watakubali hata ivyo mwakinyo anaweza akapigwa maana jamaa atatumia faida ya urefu kama alivyofanya kwa kiduku.
 
Wellem ndiye aliyeanza kusema anahitaji pambano na Mwakinyo
 
Hatimaye tarehe 17 feb ,Tyson Fury vs Usyk.

Tarehe 20 Apr Devin Haney vs Ryan Garcia.

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
 
Fury anaruka ruka sijui anaogopa pambano

King Ryan naona kabisa anakwenda kupoteza pambano kwa Devin..... baada ya kipigo toka kwa Tank angepata mapambano kama matatu hivi ya mabondia daraja la B kisha aje kucheza sasa na akina Devin, Shakur nk
Fury na Usyk mbona walishasaini kitambo ilibidi wapigane kabla ya pambano na Francis.

Wiki ijayo wanakiwasha kupata undisputed champ +lineal champ (Fury ni lineal champ pia ana mkanda wa WBC , Usyk ni unified champion ana mikanda mitatu,WBA,WBO na IBF) hivyo wataunganisha mikanda yote mikubwa zaidi kidunia kumpata undisputed +lineal champ.

Kuhusu Ryan, ni kweli angeanza na wapinzani daraja B kurudi kwenye peak kabla ya kum face Devin Haney.

Ila lolote linaweza kutokea.

Hakuna mnyonge kati yao.
 
Haya mapambano yakifanikiwa kufanyika yataingiza mkwanja mrefu sana

Mkuu msaudia kaamua anataka mapambano yote yanayotamaniwa na watu yatokee basi ana hakikisha yanatokea na kufanyikia kwao

Mabondi wengi wanakwepa kupigana kwa kisingizio cha kushindwa kukubaliana kwenye mafao
Tanks vs Shakur kila mmoja alikua anashikilia apate 60% kwa 40% wakashindwana

Sasa waarabu wao wanakupa mpunga wako plus % ya ppv na viingilio

Just imagine Furry vs usky kila mmoja anakula 50m usd na hapo ni nje ya ppv na kiingilio

Ngannou na ugeni wake alikula 10m usd plus pvv na kiingilio

Kwa mihela hii tutaona mapambano makali sana
 
Waarabu wameamua sana kuhusu suala la michezo.

Na maandalizi yao huwa ni mazuri sana.

Kama sikosei pambano lao kubwa la kwanza kufanyika kwao lilikuwa lile la AJ vs Andy Ruiz , lilikuwa pambano la rematch.

Mpaka sasa wamefanikiwa kuandaa mapambano mengine mengi makubwa na mengine makubwa zaidi yatakuja.

Crawford anamtaka sana Canelo waoneshane kazi.
 
Timu ninazotaka zifutwe
1707562034952.png
 
Fury na Usyk mbona walishasaini kitambo ilibidi wapigane kabla ya pambano na Francis.

Wiki ijayo wanakiwasha kupata undisputed champ +lineal champ (Fury ni lineal champ pia ana mkanda wa WBC , Usyk ni unified champion ana mikanda mitatu,WBA,WBO na IBF) hivyo wataunganisha mikanda yote mikubwa zaidi kidunia kumpata undisputed +lineal champ.

Kuhusu Ryan, ni kweli angeanza na wapinzani daraja B kurudi kwenye peak kabla ya kum face Devin Haney.

Ila lolote linaweza kutokea.

Hakuna mnyonge kati yao.
Pambano kati ya Fury na Usyk limesogezwa mbele mpaka May 18 kutokana na Fury kuumia mazoezini.
 
Wellem ndiye aliyempiga Kiduku .

Wellem kupigana na Mwakinyo inawezekana kabisa.

Kitakachofanyika Wellem ashuke kidogo na Mwakinyo apande kidogo wakutane kati kwenye Super Welterweight.
Haupo sahii hapa. Mwakinyo tayari yupo Middle na wellem yupo super middle. Kwahyo wellem akishuka wanakutana Middle. Uzito wa mwakinyo wa muda mrefu ni superWelter weight
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom