Nabii Suguye: Kufunga ndoa kanisani ni upagani

Nabii Suguye: Kufunga ndoa kanisani ni upagani

Ni upagani kulingana na dini ya Ukristo kwa sababu sio fundisho lililo kwenye biblia, yuko sahihi.
Ndio maana nimesema huyu nabii kuna baadhi ya mambo yupo sahii 💯%, likiwemo hili la kufunga ndoa kanisani.
 
Uwe hai
Yesu yu hai

Mm ni mfuatiliaji wa mahubiri yake kupitia WRM TV
MM NI MUANGLIKANA, LAKINI HUYU NABII KANIZINDUA MAMBO MENGI SANA.
Nabii kuna wakati anasema ukweli bila kumumunya maneno. Ndio maana serikali ilimfungia kanisa lake.
 
Ukristo kwa asilimia tisini ni upagani kwa sababu unafuata mafundisho yasiyo ya kibiblia nikupe mifano;

1. Sadaka na zaka ni zawalawi na makuhani.
Wakristo sadaka wanawapa wachungaji.
Wachungaji wengi hawana sifa za ukuhani.

2. Siku ya ibada ni Sabato jumamosi. Lakini Wakristo wanaabudu jumapili.

3. Biblia inatuhusu talaka. Wakristo wanakataza talaka.

4. Biblia inaruhusu kuoa wake wengi. Wakristo wanakatazwa kuoa Wake wengi.

5. Biblia inakataza Kula nguruwe na baadhi ya wanyama. Wakristo karibu madhehebu yote wanaruhusiwa Kula Nguruwe.

6. Biblia inamzuia mwanamke mwenye Siku zake asiende kuabudu kanisani au hekaluni.
Wakristo hiyo Sheria hawaifuati.

7. Biblia inatambua Mungu ni mmoja.
Wakristo wanaamini Miungu(Mungu mmoja katika nafsi tatu) ambalo ni fundisho la kikafiri/kipagani

Yapo mengi
Nakubaliana na ww
 
Upo sahihi mkuu. Mandoa ya sasa hivi ni upuuzi mtupu. Ndoa zilikuwa zamani.
Kwa ujumala hata mapenzi yenyewe yamekuwa upuuzi mtupu, inafikia mahala mtu unaamua kuwa unakata kichwaa unatupa kuleee
 
Kwa ujumala hata mapenzi yenyewe yamekuwa upuuzi mtupu, inafikia mahala mtu unaamua kuwa unakata kichwaa unatupa kuleee
Kweli kabisa mkuu. Dunia inaelekea kubaya sana
 
Sitaki kuwachosha, hebu twende kwenye mada moja kwa moja. Nabii na mtume mkuu wa kanisa la WRC amewaambia wafuasi wake na jamii kwamba kufunga ndoa kanisani ni upagani.

Mtume huyo, ambaye ni maarufu kwenye kauli tata, amesema hayo wakati akiwahubiria waumini wake huko Matembele, Kata ya Kivule, na mahubiri hayo yamesambaa nchi nzima hadi kwa raia wa kawaida. Wengi wa wananchi niliowashirikisha hii video, wamesema mtume yupo sahihi kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Siongezi neno. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapo chini mkuu:

View attachment 3592197

MAONI YANGU
Ijapokuwa sikubaliani na huyu nabii katika mambo mengi, kwa hili la ndoa, namuunga mkono 💯%. Kama kufunga ndoa kanisani ndiyo deal, basi hata Mungu angewafungisha Adam na Hawa ndoa ya kanisani. Vinginevyo, ufungishaji ndoa unaosisitizwa na viongozi wa dini na kuvalishana mipete mbele ya mchungaji au askofu, ni ubatili na uopagani mtupu. Hawa viongozi wanalazimisha kufungisha ndoa kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Nawasilisha.​
Yupo sahihi 💯%
 
Back
Top Bottom