Nabii Frank Kilawah acha kudanganya watu

May 20, 2013
71
151
Huyu nabii juzi kafanya kitu ambacho kimenishtua sana kwenye kipindi chake, katokea mtu anadai ni kipofu kaja na mama yake mzazi, yule mama kaulizwa kadai huyo mtoto wake kazaliwa hana macho kabisa, kabla hajamuombea kamera zilikuwa zinamuonyesha yule kijana akiwa amefumba macho, na ukimwangalia yule kijana alikuwa kama anainama chini muda mwingi.

kuinamisha kichwa chini ni hulka ya binadamu inayoambatana na kuona aibu. Basi nabii akasema huyu mtu tokea kuzaliwa hajawahi kuwa na macho, sasa mungu akimrudishia hata jicho moja si itakuwa safi, basi akachukua maji ya chupa na kummwagia huku akiweka mikono yake kwenye yale macho, eti yule jamaa akafungua jicho moja linaona.

Cha ajabu eti yule kipofu ambaye hajawahi kuona tokea kuzaliwa akapata jicho moja na ye akawa katulia tu kama hamna kilichotokea, yaani fresh tu. Mtu ambaye hajawahi kuona tokea amezaliwa hawezi kuwa vile akiona.

Halafu huu usanii anaofanya nabii anashirikisha hadi wamama watu wazima kuongea uongo mbele ya kadamnasi. Toka lini mungu akamponya mtu nusu kwa kumrudishia jicho moja? Ningekuwepo siku hiyo haki ya mungu ningeomba urudie kuomba ili jicho la pili nalo lirudi.

USHAURI: Katika miujiza ambayo haina longolongo ni upofu, namshauri huyo nabii asiigize tena kuponya mtu kipofu maana kuna siku itamtokea puani. kuna watu kama sisi tukiwa eneo la tukio tutataka tuhakikishe kama huyo kipofu kweli ni kipofu kabla hujamuombea halafu tutakuumbua.

Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.
 
Aisee. Umeanza vema kabisaa ila mwisho uneharibu mbaya kwamba muujiza wa kumpa kipofu kuona Bwana Yesu aliweza mara moja tu na sasa hawezj umechemka sana aisee. Yesu mpaka sasa anaponya kama uamini endelea hivyo hivyo. Mtumishi wa kweli utamjua tu kupitia mafundisho yake ila miujiza sio kipimo cha utumishi kwani inawezekana mtu kuigiza. Hizi ni siku za mwisho aisee. Leo fb nimeona tangazo la nabii mmoja kaweka picha yake kisha kuna maneno yaliyo andikwa kiingeneza kwa capital letters I AM YOUR GOD alafu majamaa fulani yanakoment Amen.
 
ha ha ha i get a lot of things in this life
what open you want to be..? before birth or after death
 
Aisee. Umeanza vema kabisaa ila mwisho uneharibu mbaya kwamba muujiza wa kumpa kipofu kuona Bwana Yesu aliweza mara moja tu na sasa hawezj umechemka sana aisee. Yesu mpaka sasa anaponya kama uamini endelea hivyo hivyo. Mtumishi wa kweli utamjua tu kupitia mafundisho yake ila miujiza sio kipimo cha utumishi kwani inawezekana mtu kuigiza. Hizi ni siku za mwisho aisee. Leo fb nimeona tangazo la nabii mmoja kaweka picha yake kisha kuna maneno yaliyo andikwa kiingeneza kwa capital letters I AM YOUR GOD alafu majamaa fulani yanakoment Amen.
Toa mfano wa mtu aliyeponywa upofu ...Wacheni kudanganya watu nyie
 
Vuka tu boda wapo wengi, sema huku kwetu watu wengi hawajawashtukia...wana saka hela kwa jina la yesu.
 
Usikashifu wala usikatae miujiza ila kama iman hairuhusu acha fata iman yako. Na pia simama mwenyewe. Nilikuwa hivohivo mm wahubiri wanaohubiri miujiza niliwapinga sana nilimwamini mwalimu mwakasege anaekufundisha namna ya kusali ukipatwa Na shida. Ila mjomba wangu alipoooza miaka mnne hatembei alikatisha tamaa miujiza hiyo hiyo aliombewa akapona. Hadi Leo nikabaki nasema Mungu anisamehe yeye ndo anahukumu ila kinywa changu kisimuhukumu mtumishi yoyote
 
Aisee. Umeanza vema kabisaa ila mwisho uneharibu mbaya kwamba muujiza wa kumpa kipofu kuona Bwana Yesu aliweza mara moja tu na sasa hawezj umechemka sana aisee. Yesu mpaka sasa anaponya kama uamini endelea hivyo hivyo. Mtumishi wa kweli utamjua tu kupitia mafundisho yake ila miujiza sio kipimo cha utumishi kwani inawezekana mtu kuigiza. Hizi ni siku za mwisho aisee. Leo fb nimeona tangazo la nabii mmoja kaweka picha yake kisha kuna maneno yaliyo andikwa kiingeneza kwa capital letters I AM YOUR GOD alafu majamaa fulani yanakoment Amen.

upo kama mimi alipofika kumtaja Yesu nimemuona ana mapungufu pia huyu mtoa maada imani yake ni ndogo ataamini makubwa kivipi? imani sio kufufua au kuponya
ishara zipo hata za kishetani halijui hili
 
Toa mfano wa mtu aliyeponywa upofu ...Wacheni kudanganya watu nyie wenye laana
Kulijuwa na wenye ukoma wengi kipindi cha nabii Elisha ila hakuna aliponywa ila Naaman jemedali. Kulikuwa na wajane wengi kipindi cha Nabii Elia ila ni mjane mmoja tu wa Selepta aliyopona kipindi cha njaa kali pale Elia alipozuia mvua isinye juu ya nchi kwa miaka mitatu na nusu.
 
Hivi hamna namna serikali inaweza dhibiti utapeli unaoendelea kwenye haya baadhi ya makanisa?
 
Dah poleni sana makanisani kwenu, sisi hakuna ujinga kama huu, Kwanza tungemtandika bakora Kuanzia Nabii mwenyewe mpaka mgonjwa na mama yake pia
Ni kweli kabisa anakula mboko za kufa alone kuigiza movie kanisani
 
Back
Top Bottom