Kuwashwa Kwa kiganja cha mkono na kucheza Kwa jicho kunakupa taarifa itakayotokea

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,905
KUWASHWA KWA KIGANJA CHA MKONO NA KUCHEZA KWA JICHO KUNAKUPA TAARIFA ITAKAYOTOKEA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nafsi yako inañamna mbalimbali za kuwasiliana na wewe(mwili wa nje) Kwa namna mbalimbali.
Namna maarufu ni pamoja na ndoto za Usiku ukiwa umelala. Hutumia ndoto kuwasiliana na wewe kuhusu Jambo Fulani.

Ni ndoto pekee ambayo Nafsi inaweza kuzitumia kukupa taarifa zilizokwisha kupita zamani, iwe ulikuwepo au haukuwepo. Na NI ndoto hizohizo ambazo Nafsi inaweza kukupata taarifa Fulani ya Jambo linalokuja bila kujali utakuwepo au hautakuwepo.

Tofauti na ndoto, Nafsi hutumia Viungo vya mwili kutoa taarifa ya kile kitakachotokea na sio kilichotokea.

Nafsi yako na mfumo wa ufahamu (ubongo) hufanya kazi Kwa ukaribu Sana.

Zingatia, ubongo wako ndio unaotawala mwili wako, unaotawala Maisha yako. Hii ni Kwa sababu ubungo ndio kiungo pekee ambacho ufanyaji kazi wake niwa Siri, complicated, na ndio unaolinda utu Wako.

Mtu hawezi kujua nini unachofikiri, namna Akili yako inavyochambuka na kufanya kazi. Sio ajabu ubongo ndio kiungo pekee ambacho ni nyeti, na ambacho kimelindwa na kufunikwa na mfupa mgumu kuliko kiungo chochote kile.

Katika kujihami, Nafsi inatoa alerts Fulani Kwa mwili wako ili kujihami au kujiandaa kwaajili ya Jambo Baya au zuri ambalo litatokea katika Maisha yako.
Tofauti na ndoto ambazo unaweza kumuotea mtu mwingine ndoto lakini alerts za mwili wako zipo kwaajili yako mwenyewe na Yale yanayokuhusu ambayo yatakuathiri.

Mfano Mkeo au Mumeo, wazazi, Watoto, Ndugu na watu wako wa Karibu ambao wanakuathiri wewe moja Kwa moja basi Mwili wako utapewa notification ya Jambo zuri au Baya ikiwa litatokea.

Huwezi pewa alerts ya mwili Kwa Watu ambao huna uhusiano nao, mfano Ajali ya Gari ambayo hakuna hata mmoja ambaye humjui, au Au kuanguka au kufanikiwa Kwa kiongozi Fulani ambaye hakujui na wala hauna uhusiano naye.

Moja ya Viungo vya mwili vinavyopewa Signal, Alerts au notifications na Nafsi yako ni kama ifuatavyo;

1. Jicho Lako (Macho yako)
Macho ndio taa ya Nafsi. Kinachoona NI ubongo wako Ila kinachomulika ni macho yako.
Lipo jicho la kulia na jicho la kushoto (Kwa kuzingatia mkono). Chunguzi zangu zinaonyesha kuwa katika macho yako mawili lipo jicho moja lenye nguvu kuliko jicho jingine. Kama vile mkono wa kulia(kuume) na mkono wa kushoto. Unaweza kufanya majaribio kuona ni jicho lako lipi linanguvu kuliko jingine. Kisha uendelee kusoma.

Kucheza Kwa jicho la kulia(lenye nguvu) kunamaanisha kuna Jambo la bahati, zuri, Jema, la kheri linaenda kutokea kwenye Maisha yako hivi karibuni. Na haitozidi siku ishirini na nane katika za mwezi, na likicheza jicho lako la kushoto (lisilo na nguvu) hiyo itamaanisha kuna Jambo Baya, la hatari, mkosi na hasara inaenda kukutokea hivi karibuni. Na haitazidi siku ishirini na nane za mwezi.

Zingatia; jicho la Kulia kwako linaweza kuwa jicho la kushoto Kwa mwenzako. Hapo kitachozingatiwa ni lenye nguvu na lile lililodhaifu.

Zingatia pia, Jinsia yako pia itamata, itazingatiwa. Kwenye jinsia pia kuna jinsia yenye nguvu na jinsia dhaifu. Mwanaume ndiye mwenye nguvu na Mwanamke ni dhaifu Kwa habari za jinsia.

Hivyo Ikiwa wewe ni Mwanamke basi jicho la kushoto(dhaifu) likicheza jua kuna bahati, habari njema, uzuri au chochote kizuri kinaenda kutokea katika Maisha yako ndani ya siku za mwezi kulingana na mzunguko wako wa hedhi. Na kama litacheza jicho la kulia(lenye nguvu) basi hiyo itamaanisha kuna janga, tatizo, mkosi au taarifa Mbaya utaipata ndani ya siku za mzunguko wako wa mwezi.

Ieleweke kwamba, Wanawake wao mzunguko wao unategemea mzunguko wake wa hedhi. Yaani mwezi wa Mwanamke mmoja ni tofauti na mwezi wa Mwanamke mwingine. Wapo ambao mwezi kwao unasiku 28 wapo wa siku 29, 30 mpaka 37.
Wakati Kwa wanaume Sisi miezi ya siku itafuata mzunguko wa Setilaiti Mwezi unaowaka angani Usiku.

2. Viganja vya Mikono yako
Mikono yako inakazi kuu mbili, moja kufanya mambo au vitu, pili, kutoa na kupokea. Kuna mkono wa kulia(wenye nguvu) na mkono wa kushoto (wenye udhaifu). Lakini elewa kuwa kushoto yako dhaifu inaweza kuwa kulia ya mwenzako yenye nguvu. Yaani kuna Watu mikono Yao ya upande wa kushoto(wengi tumezoea kuiita hivyo lakini sivyo) inanguvu kuliko mikono Yao ya kulia. Yaani matumizi.

Ikiwa kiganja cha mkono wako kinawasha, basi elewa kuna signal, alerts au notifications Nafsi yako inajaribu kukupa kuwa kuna Jambo linaenda kutukia.

Mkono wako wa kulia (wenye nguvu) ukiwasha, hiyo itamaanisha unaenda kupokea maokoto, Pesa, Kupata faida, au kuna dili Fulani linakuja Huko, au kuna kazi unaenda kuipata, au kazi unayoifanya itapata Mafanikio ndani ya siku ishirini na nane au tisa za mwezi(Kwa wanaume). Hapa Pesa haitakuja Kwa tabu. Yaani Pesa haitakusumbua ukiifanya kazi hiyo. Na utakayemfanyia atakufurahia.

Lakini mkono wa kushoto ukikuwasha, hiyo itamaanisha unaenda Kupata hasara, kupoteza Dili, kuharibu kazi Fulani, au kucheleweshewa malipo, au Kupata ajali iwe ya kibiashara au ya kimwili. Mnaenda kugombana na watu wako WA Karibu labda ni Mkeo, Watoto au wazazi, Ndugu na mwajiri wako. Yaani mtu ambaye inauhusiano naye ambaye anaathari za moja Kwa moja.

Kama ni fundi elewa kuwa kazi utakayoifanya au unayoifanya Wakati kiganja cha mkono wa kushoto kimewasha basi aidha uzingue wewe au azingue mteja wako. Ilimradi hasara itokee na kugombana.

Hiyo itakuwa kinyume na Viganja vya jinsia ya Kike, Wanawake ambao wao ni kinyume na Viganja vya wanaume.

Sitaki kuwachosha. Ishara zingine ni pamoja na Kujikwaa au kujigonga Kwa bahati Mbaya. Kugongana na maneno na MTU Kwa pamoja Kwa wakati mmoja. Au ulikuwa unataka kuongea Jambo Fulani lakini likakutoka Kwa namna ya ajabu. Hiyo inamaanisha sio Wakati sahihi au hao sio Watu au MTU sahihi kusikia kile ambacho ulitaka kusema.

Elewa kuwa mambo yote hayo hutokea naturally, automatically, yaani huwezi kuamua kuchezesha jicho au kiganja chako kuwasha.

Muhimu zaidi, sio kila kuwasha au kucheza Kwa jicho ni notification au alerts Kutoka kwenye Nafsi. Wakati mwingine inaweza kuwa matatizo ya kiafya.

Zingatia kuwa, pale unapopata ishara hizo, chukua kitabu chako cha kumbukumbu andika hiyo tarehe na saa na jicho au mkono husika uliofanya hivyo. Kisha Subiri nini kitatokea, na iwe ndani ya siku ishirini na nane au tisa za mwezi wa Setilaiti inayowaka hapo angani, na Kwa Wanawake iwe katika siku zako za mwezi kadiri ya mzunguko wako.

Mimi Acha nipumzike sasa.
Ni Yule Mtibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mimi kikiwasha kiganja cha kulia najua kuna dili nono linakuja lakini inaweza pita hata wiki,lakini kikiwasha kigole gumba cha mkon cha kulia hata siku mbili haipiti ni dili nono.Kinyume chake ikiwa kushoto lazima pesa ndefu initoke kwa njia yoyote.
 
Fikra za kimaskini... Fanya kazi acha kuendekeza vitu vya kusadikika
 
Nina uhakika haunizidi sio tuu kielimu hata kifedha.
Sasa sijui Mimi na wewe Nani afanye Kazi
Elimu yako darasa la ngapi..
Ungekuwa na Elimu ungeacha kuleta mada za kusadikika, Pesa haina formula. Unaleta utabiri tambitambi kwenye mambo ya fedha

Ni mara ngapi jicho limecheza au mkono kuwasha na haujapata pesa?
 
Elimu yako darasa la ngapi..
Ungekuwa na Elimu ungeacha kuleta mada za kusadikika, Pesa haina formula. Unaleta utabiri tambitambi kwenye mambo ya fedha

Ni mara ngapi jicho limecheza au mkono kuwasha na haujapata pesa?

Unaposema mara ngapi unamaanisha nini kwenye Akili yako ndogo?
Unaniuliza Mimi badala ya kujiuliza wewe mwenyewe.

Nimekuambia, kuhusu Elimu na Pesa itabidi utafute washirika wenzako ili angalau uweze kunipata.
 
Ulichoandika ni Sahihi kisayansi. Lakini ikiwa vinginevyo utaelezeaje matukio hayo?
Unachotaka kusema hata mtu akitoka chooni aja kubwa, akafika nje akapata pesa napo utasema kwamba ukinya unapata pesa...

Kitu unachosema hakina mashiko, kuwashwa mkono na kupata pesa ni coincidence tu, na hakuna uhusiano wa moja kwa moja kwa sababu kuna siku mkono hauwashi au jicho halichezi na unapata Pesa vizuri tu. Hali ya kuwasha au jicho kucheza ni mwili tu kujaribu kujirekebisha wenyewe na haina uhusiano na nadharia zako. Fanya kazi usitegemee Mkono kuwasha
 
Back
Top Bottom