Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,891
NABII MUSA HAJAWAHI KUMTAJA SHETANI MAHALI POPOTE KATIKA MAANDISHI YAKE; UASI NI UAMUZI WA MTU NA SIO SHETANI.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
Mhusika Shetani amekuwa zaidi maarufu katika vitabu vya Injili kuliko vitabu vya Torati, Zaburi na vitabu vya manabii wadogo kama kina Daniel, Yona, Habakuki n.k.
Vitabu vya Musa ambavyo ni Mwanzo, Kutoka, mambo ya Walawi, Hesabu na kumbukumbu la Torati havijamtaja Mhusika Shetani Kwa namna Yoyote Ile.
Ni kitabu cha mwanzo pekeake ambacho kinamtaja Mhusika Nyoka pale Edeni akimdanganya Eva. Wakristo wanadai nyoka ndiye Shetani Jambo ambalo sio Kweli. Sio kweli kwa hoja zifuatazo;
1. Maandishi ya Musa Kwa 99.9% hayakuandikwa kifasihi na kifalsafa, yaliandikwa Kwa Lugha ya moja Kwa moja.
Musa ni mwandishi wa Historia pamoja na Mwanasheria (aliyeandika sheria/Torati) kikawaida Historia haiandikwi kimafumbo na wala sheria haiandikwi kimafumbo.
Hivyo wanaosema neno Nyoka lilitumika kama Lugha ya picha kubeba taswira ya Ibilisi wanakosa mantiki.
Ndio haohao wanaosema pia tunda ni Lugha ya picha Jambo ambalo sio kweli. Tunda lilikuwa tunda Kutokana na nature ya maandishi ya Nabii MUSA.
Hii ni tofauti na Nabii Yesu au ISSA bin Mariam ambaye uhusika wake ulikuwa ni mwalimu na mara kadhaa alitumia mbinu ya Brainstorming Kwa kutoa metaphor (visa vya kifasihi vyenye mafumbo). Lugha atakayoitumia mtu wa kifasihi na Falsafa inaweza Isiwe Lugha ya moja Kwa moja na ikawa na matawi mengi ya tafsiri kulingana na Msikilizaji au msomaji.
2. Nyoka anayetajwa na adhabu alizopewa hazina uhusiano wowote na mhusika Shetani anayetajwa katika vitabu vya Injili.
Yule alikuwa Nyoka Halisi kama hawa tunaowaona hivi Leo. Kwa sababu ni kweli Nyoka anajongea Kwa tumbo mpaka hivi SASA.
Ushahidi WA wanyama kuongea upo mpaka hivi leo kwani hata Kasuku anaongea licha ya kuwa Hana Ala Sauti nzuri zinazomwezesha kuzungumza kama binadamu. Ila akiongea anaeleweka.
Wanyama wengine waliowahi kuongea ni pamoja na Farasi aliyepandwa na Balaki.
Hivyo kusema shetani(kama mhusika) alimuingia Farasi au Nyoka pale Edeni na kuzungumza hakuna mantiki yoyote Kwa sababu Mungu ndiye anaamua Kiumbe hiki kiongee na hiki kisiongee. Ukizingatia wapo binadamu wasioweza kuongea (Mabubu).
Maandishi ya Musa hayamtambui Shetani kama chanzo cha Uasi au dhambi hapa Duniani. Isipokuwa yanatambua Uhuru WA kuchagua wa viumbe wenyewe.
Yaani binadamu anayohiyari ya kuchagua kutenda Mema na Mabaya pasipo kusingizia Wahusika wa Kiroho wasioonekana. Yaani suala la Uasi NI ishu ya Uhuru binafsi WA MTU.
NABII MUSA ambaye ndiye Nabii namba moja Duniani aliyejenga msingi WA dini zenye asili ya Uyahudi(Ibrahim) ambaye ndiye Nabii pekee maandishi yake yanaeleza asili ya Mwanadamu na jinsi alivyoamua Kutumia Uhuru wake kuchagua kuasi, hatambui kitu kinachoitwa SHETANI kama Mhusika.
Bali anatambua uchaguzi hasi na nguvu hasi iliyomo ndani ya mtu.
Musa hakumtaja Shetani kama Mhusika Bali binadamu Kwa sababu;
1. Mwanadamu ndiye aliyewekewa sheria na ushahidi WA sheria hizo tunazo mpaka hivi leo.
Kusema shetani aliasi Mbinguni na hatujui sheria za Mbinguni hata Moja ni dalili ya kuongea vitu Kwa Uongo.
Huwezi sema Shetani aliasi Mbinguni alafu muda huohuo ukiulizwa utaje sheria hata mbili za Mbinguni huna unachojua.
2. Matokeo ya Uasi na adhabu za Uasi zinampata Mwanadamu mtendaji Kwa mujibu wa sheria na sio Shetani kama Mhusika.
Matokeo ya uzinzi, ubakaji, uuaji, wizi, n.k. Anayewajibika nayo ni Mwanadamu kama Mhusika aliyewekewa sheria.
Vitabu vya Musa MTU anapokosea au kufanya dhambi hajawahi kusingiziwa Shetani Bali mhusika akiyetenda na anayewajibishwa na mhusika.
Hii inafanana na Dini zote Duniani za Asili zikiwemo dini za kiafrika ambapo hakuna Mhusika Shetani, isipokuwa MTU akiamua kuwa Mbaya ndio huchukuliwa kama Mbaya na mwenye nguvu Hasi.
Hata kwenye Mahakama za kiulimwengu hawatambui Mhusika Shetani wala Mungu katika ishu ya Uasi au kufanya Makosa Bali wanajua MTU ndiye anamaamuzi ya kufanya Makosa au kutokufanya.
Kuwa Mwema ni maamuzi na kuwa Mbaya ni maamuzi pia ya MTU.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam