Jihadharini kuabudu wachungaji Wanadamu!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,502
19,303
Kuna imani ilianzia Marekani huko miaka ya 1960s, imesambaa hadi Tanzania, Arusha nimeona wapo na pia DSM na maeneo mengine ya nchi, hii ni imani ya Branhamites, wafuasi wa mtumishi mmoja wa Mungu mkubwa sana aliyeitwa William Marrion Branham. Wengi mtakuwa mmeshawafahamu, wengine wanabandika hadi picha za huyu mhubiri kwenye magari, na wanaamini (kama walivyoelekezwa naye mwishoni wa uhai wake) kwamba yeye ndiye Eliya aliyekuwa anakuja kuisafisha njia ya Yesu Kristo; bahati mbaya, Yesu mwenyewe alishasema kuwa Eliya alishakuja, na ni Yohana Mbatizaji, na ujio wa Eliya mara ya pili ilikuwa ni kuisafisha njia ya kuzaliwa kwa Yesu. Kama Yesu alishakuja 2000 years ago, miaka ya 1965 angekuja kusafisha nini sasa, hapo ndio unaona hili lilikuwa fundisho la uongo, aliteleza na wafuasi wake wamedondoka yeye aliokolewa na Mungu kwa moto.

William Marrion Branham alizaliwa huko Kentucky Marekani mwaka 1909, hajawahi kusoma shule, ila alitokewa na malaika akiwa mdogo akienda kuchota maji, akamwambia kuwa autunze mwili wake usinajisiwe kwasababu atakuwa mtumishi wake ukubwani. Ni kweli, alipofika umri wa miaka kumi na, alianza kuhubiri, Mungu alishuka kwa kiwango kikubwa sana miaka ile baada ya vita vya pili vya dunia miaka hiyo ndani ya kanisa la Baptist, na inasemekana hakuna mtumishi ambaye rekodi iliwekwa kushuka Nguvu za Mungu kama ilivyokuwa kwake hadi sasa, kwasababu kuna siku alikuwa anahubiri, ndimi za mwanga wa moto ukaonekana kabisa kwa macho juu ya kichwa chake, na watu walipiga picha hizo ndimi, zipo hadi leo. Hiyo picha ndio wafuasi wake wanatembea nayo kwenye magari hadi leo.

Kila palipo na wahubiri, Mungu huwa anainua watu na kugawa madaraka (specialization), kwake kwasababu alikuwa hajasoma shule kabisa, alimpa karama ya kuhubiri kidogo ila kufanya miujiza ya uponyaji kwa wingi mno, na baada ya watu kuokoka kwa matendo makuu ya Mungu, ila Gordon Lindsay alikuwa kama mfundisha semina, kama ilivyo kwa Mzee Kulola na Mzee Lazaro.

Lindsay, Kenneth Hagin na watumishi wengine waliokuwa wameinuliwa tangia wakati huo, wanashuhudia kwamba, kutokana na umaarufu mkubwa kumpata, udhaifu wa kibinadamu ulianza kumwingia, akawa hafurahii watumishi wengine kuinuka, alianza kuwakosoa kina Oral Roberts, Kathlyn Kuhlman, Billy Grahm na wengine. Hata kama wewe ni mtumishi wa Mungu, ukifungua mlango adui akiingia huwa anaharibu kabisa, hivyo alipoanza kufungua milango hii ya mashindano, akaacha wito wake wa kuponya wagonjwa, akajitangaza kwamba yeye ndiye aliyetabiriwa kwenye Malaki 4:5-6 kwamba yeye ndiye yule Eliya aliyetabiriwa kuja kuisafisha njia kwa ajili ya ujio wa Yesu. Kuna uwezekano mkubwa kwasababu alikuwa hana kisomo, hakuiona hata mistari (ambayo nimeweka hapa chini) ambayo Yesu alisema Eliya alishakuja, ni Yohana Mbatizaji. Fundisho hilo limebaki hadi leo kwa wafuasi wake.

Kenneth Hagin, Gordon Lindsay na wengine walionyeshwa maono na Mungu, akiwaambia kwamba mtumishi huyo ameiacha njia yake, lakini kuna kitu kitampata ili hata kama mwili wake utaumia basi roho yake ipone ili asiendelee kusambaza upotofu huo. Siku moja akawa anaendesha gari akiwa na mkewe na kijana wake, walienda kulivaa trekta njiani, mkewe akawa kama amepoteza maisha palepale, na yeye akaumia sana kiasi cha kutoweza kufanya lolote, ila sauti inatoka, akamwelekeza kijana ambaye walikuwa naye pale ambaye hakuumia hivyo, kwamba auchukue mkono wake (yeye William) auweke kwa mkewe aliyekuwa ameshapoteza fahamu, alipofanya hivyo, kwasababu alikuwa anaweza kuongea, akamwombea, mkewe akawa mzima, na aliishi miaka kadhaa mbeleni, ila yeye baada ya kufanya hivyo akafa palepale.

SOMENI MISTARI HII KUHUSU UJIO WA ELIYA vs YOHANA MBATIZAJI

Malaki 4: 5-6
na Isaya 40:3 zinatabiri kwamba, kabla ya kuja kwake Kristo (Yesu) alitakiwa kutanguliwa na Eliya awe mhubiri ili kusafisha njia ya Kristo ambaye angezaliwa.

Luka 1:17 Malaika alimtokea Zakaria mume wa Elizabeth (wazazi wa Yohana Mbatizaji), walikuwa tasa kwa miaka mingi na wakapata ujauzito uzeeni. Yule malaika alimwambia Zakaria kwamba mkewe angezaa mtoto kwa ajili ya kusafisha njia ya Masihi (Yesu) kwani mtoto wake huyo atakuwa na roho ya Eliya juu yake.

Marko 9:11-13 Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba, Eliya tayari ameshakuja ila watu hawakumtambua, na alimaanisha Yohana Mbatizaji ndiye Eliya.

Yohana 1:23 yeye Yohana mbatizaji alipoulizwa kwamba yeye ndiye Eliya, alisema yeye ni yule aliyezaliwa kwa ajili ya kuitengeneza njia ya Bwana kabla ya ujio wa Masihi kama ilivyotabiriwa katika Isaya 40:3.

Pamoja na kwamba kuna maeneo mengine (eg. YOHANA 1:19 – 28) Yohana mbatizaji alikuwa aidha anajificha watu wasimjue na alijaribu kujifanya/kukataa kwamba yeye sio Eliya, lakini ilifika mahali ukisoma mistari hiyo kama Yohana 1:23 alikiri kwamba yeye ndiye aliyekuja kusafisha njia ya ujio wa Kristo (ambaye ndiye Yesu). Na wakati mwingine walipomuuliza alijificha asionekane kama ni nabii, lakini aliendelea kuhubiri watu watubu kwasababu ajaye mbele yake ana nguvu kuliko yeye, ambaye yeye hana hata hadhi ya kumfungua kamba za viatu vyake; ila bado alifumbwa macho hajui ni nani manake Yesu aliposhuka ila abatizwe naye Yohana alimuuliza wewe unakuja mimi nikubatize (akiona hana hadhi) Yesu akasema ni lazima nifanye hivi ili kutimiza haki yote, na alipobatizwa Roho Mtakatifu akashuka juu yake kama hua na sauti ikatoka ikisema huyu ndiye mwanangu mpendwa msikieni yeye.(Mathayo 3:13 – 15) , hii inamaanisha kwamba Yohana alikuja kujua kwamba Yesu ndiye masihi na kwamba yeye alitangulia kumsafishia njia, (though watu wanaweza kushangaa kwanini tena aliwatuma wanafunzi wake wakamuulize Yesu yule aliyeona Roho akishuka juu yake kama ndiye au siye? Ni kwasababu wakati huo Yohana alikua amewekwa gerezani na aliamini moyoni mwake kwamba ujio wa Yesu pengine angekuja kama mtu mwenye mamlaka kama mfalme Daudi au nabii mwenye kutumia nguvu za kimwili afanye kitu cha ajabu kumtoa gerezani, alitegemea masihi angefanya kituko haraka kuonyesha nguvi ili amtoe kwenye mateso ya gereza, aliona Yesu anachelewa kufanya hivyo hadi akawa na mashaka naye, hakujua ufalme wa Yesu ni ufalme wa rohoni au wa mwilini, ila ukweli ni kwamba Yohana alijijua yeye ni nani na alijua Yesu ni nani. Hivyo maandiko hayo yamethibitisha pasi na shaka kwamba Yohana Mbatizaji ndiye alikuja kama Eliya.

USHAURI: Nawaagiza kwa Jina la Yesu, achene kumwabudu huyu mhubiri wa marekani, yeye alishaokolewa na Mungu tena kwa moto, na hakuwahi kuwaelekeza mmwabudu, pia fundisho la Eliya ni potofu na ndilo lililomuua, msijisogeze wenyewe kwenye upotofu ule uliomwondoa hata yeye duniani. Ukiokoka, mtazame Yesu, wachungaji ni wanadamu, kuna wakati huwa wanasimama vizuri na wakati mwingine wanateleza, angalia wakiteleza usije kuteleza nao kwa kuwasikiliza kila kitu bila kupima kupitia Neno la Mungu. Ukiokoka, soma Neno na ukiona umeshasimama omba Mungu akufundishe ili usiende na upepo wa watumishi wanaoanguka. Achene kuabudu wanadamu, mtazameni Yesu ndiye aliyewafia msalabani, wengine wanaabudu wanadamu hadi wanawatandikia nguo wapiti juu, wengine wanalala chini mhubiri apite juu yao, wanawapa wanadamu utukufu wote badala ya kumpa Mungu aliyetoa garama kubwa ya ukombozi wao, hili ni onyo kwenu kwa Jina la Bwana, iweni macho, iweni macho! Mungu awabariki.
 

Attachments

  • JIHADHARINI NA KUABUDU WACHUNGAJI WANADAMU.pdf
    105.5 KB · Views: 4
Uko sahihi lakini nadhani karibu dini zote zinaabudu manabii wake kwa namna fulani. Mungu hana ubia wowote kwenye umungu wake. Na pia ana wivu kwenye umungu wake. Ila cha kushangaza sisi binadamu ni kama manabii/mitume wa Mungu tumewaweka daraja fulani la kulingana na Mungu. Kwa mfano hapo uliposema "nawaagiza kwa jina la Yesu" inaleta ukakasi. Kwa nini isiwe unatuagiza kwa jina la Mungu moja kwa moja?
 
lakini wanashindwa kuelewa hili jambo, na wanaamini yeye ndiye eliya, na hawajui eliya alikuwa anatakiwa kuja kufanya nini. ajabu ni kwamba, wanamwita ni eliya na wakati huohuo wanaamini wanamwamini Yesu, kivipi sasa kwamba mtangulizi wa Yesu aje miaka 2000 baada ya Yesu kuwepo duniani? kuna mpare mmoja nimeona anazunguka nchi nzima kufungua haya makanisa, na ili kupata wafuasi amekuja na mtindo kuyaita makanisa ya wanaoamini kuokoka ni makanisa ya malkia wa zinaa. hajui hili neno William alilitaja kwa ajili ya nini.

alitokea mtumishi mmoja anaitwa Kathlyn Kulhman, huyu ndiye aliyekuwepo kabla ya kina Benny Hinn na wengine aliibuka sana enzi zeke, yeye alipoona mtu mwingine anakuja kupata umaarufu, bahati mbaya akaanza kuhubiri kwamba wanawake wasihubiri kabisa, hao wanaohubiri ni malkia wa zinaa ili kuua kabisa imani kwa wahubiri wanawake, ni bahati mbaya hata baada ya kufanya kazi kwa uzuri mwishoni alianza kupotoka, ashukuriwe Mungu aliyeokoa roho yake lakini.
 
Kuna tofauti gani kati ya aliyokuwa akiyafanya William Branham na hawa Televangelists kina Mwamposa,"Kuhani" Richard Mussa,mwingira,Kakobe , hawa mitume feki n.k.?

Hao wote mnawaabudu kwa kufuata uongo wanaowauzia kwa thamani ndogo ya pesa ambayo hupelekea kuwatajirisha matumbo yao.
 
Uko sahihi lakini nadhani karibu dini zote zinaabudu manabii wake kwa namna fulani. Mungu hana ubia wowote kwenye umungu wake. Na pia ana wivu kwenye umungu wake. Ila cha kushangaza sisi binadamu ni kama manabii/mitume wa Mungu tumewaweka daraja fulani la kulingana na Mungu. Kwa mfano hapo uliposema "nawaagiza kwa jina la Yesu" inaleta ukakasi. Kwa nini isiwe unatuagiza kwa jina la Mungu moja kwa moja?
wewe ni adui, umekuwa ukifuatilia post zangu tangu kitambo ili kuzichafua, nakushauri uokoke, sikuombei mabaya, naomba Mungu walau aokoe roho yako, siku moja macho yako yapate nuru uone umuhimu wa wokovu. hata hiyo avatar yako uliibandua kwangu ukaweka kwako ili tu kuharibu ukweli wa Neno la Mungu, nikakuachia nikaweka nyingine, na ukiiba tena nitakuachia na kuweka nyingie, ili tu iwe ushuhuda kwamba nimenawa mikono juu yako. Mungu akusaidie. sijaenda kwenye point kwasababu nimeona wewe sio wa kujibu kwa point ila kwa namna hii.
 
Kuna tofauti gani kati ya aliyokuwa akiyafanya William Branham na hawa Televangelists kina Mwamposa,"Kuhani" Richard Mussa,mwingira,Kakobe , hawa mitume feki n.k.?

Hao wote mnawaabudu kwa kufuata uongo wanaowauzia kwa thamani ndogo ya pesa ambayo hupelekea kuwatajirisha matumbo yao.
of course, hao uliowataja, hauhitaji mtu aje akwambie na feki au sio feki, Yesu alisema mtawatambua kwa matunda yao. yale maangamizi ya roho anayafanya kuhani musa pale kimara temboni, anapeleka watu wengi motoni, na wengi wao ni wahitaji na masikini. mwamposa pia anajua yeye mwenyewe anachofanya, grace zoazoa na mumewe mangi wajajua wanachokifanya, ngurumo ya upako anajua anachokifanya. ila pimeni ninyi wenyewe, na muwakimbie wale ambao Mungu anawashuhudia kuwa ni manabii feki, kwasababu mkiungana nao mtaenda nao motoni. msikubali kuungua moto pamoja nao, wakimbieni.
 
imagine, unamheshimu aliyeokolewa kuliko mwokozi. tuwe makini, mchungaji atabeba furushi lake mwenyewe na wewe la kako, kila mtu atatoa hesabu yake. hata ukiona mtumishi anakosea leo usimfuate, kwasababu kila mtu atahukumiwa kivyake.
 
Uko sahihi lakini nadhani karibu dini zote zinaabudu manabii wake kwa namna fulani. Mungu hana ubia wowote kwenye umungu wake. Na pia ana wivu kwenye umungu wake. Ila cha kushangaza sisi binadamu ni kama manabii/mitume wa Mungu tumewaweka daraja fulani la kulingana na Mungu. Kwa mfano hapo uliposema "nawaagiza kwa jina la Yesu" inaleta ukakasi. Kwa nini isiwe unatuagiza kwa jina la Mungu moja kwa moja?
Mungu ni cheo/hadhi. Jina lake ni Yesu.


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Back
Top Bottom