Nabii Frank Kilawah acha kudanganya watu

Mimi mwenyewe leo nikajikuta naangalia hicho kipindi,nikasema ngoja nione kamali inavyochezwa.Na nilidhamiria kuleta hoja sema mkuu umeshani pre_empty.Lakini usanii unaofanyika ni hatari labda sijui nasikia eti wakisha kuteka kwenye roho huwezi kubeza miujiza
 
Huyu nabii juzi kafanya kitu ambacho kimenishtua sana kwenye kipindi chake, katokea mtu anadai ni kipofu kaja na mama yake mzazi, yule mama kaulizwa kadai huyo mtoto wake kazaliwa hana macho kabisa, kabla hajamuombea kamera zilikuwa zinamuonyesha yule kijana akiwa amefumba macho, na ukimwangalia yule kijana alikuwa kama anainama chini muda mwingi.

kuinamisha kichwa chini ni hulka ya binadamu inayoambatana na kuona aibu. Basi nabii akasema huyu mtu tokea kuzaliwa hajawahi kuwa na macho, sasa mungu akimrudishia hata jicho moja si itakuwa safi, basi akachukua maji ya chupa na kummwagia huku akiweka mikono yake kwenye yale macho, eti yule jamaa akafungua jicho moja linaona.

Cha ajabu eti yule kipofu ambaye hajawahi kuona tokea kuzaliwa akapata jicho moja na ye akawa katulia tu kama hamna kilichotokea, yaani fresh tu. Mtu ambaye hajawahi kuona tokea amezaliwa hawezi kuwa vile akiona.

Halafu huu usanii anaofanya nabii anashirikisha hadi wamama watu wazima kuongea uongo mbele ya kadamnasi. Toka lini mungu akamponya mtu nusu kwa kumrudishia jicho moja? Ningekuwepo siku hiyo haki ya mungu ningeomba urudie kuomba ili jicho la pili nalo lirudi.

USHAURI: Katika miujiza ambayo haina longolongo ni upofu, namshauri huyo nabii asiigize tena kuponya mtu kipofu maana kuna siku itamtokea puani. kuna watu kama sisi tukiwa eneo la tukio tutataka tuhakikishe kama huyo kipofu kweli ni kipofu kabla hujamuombea halafu tutakuumbua.

Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.
Mengine umeandika vizuri, lakini umenichefua sana kwenye kuitimisha eti hata Yesu miujiza aliyotenda ukimwambia arudie leo hawezi!!
 
Aisee. Umeanza vema kabisaa ila mwisho uneharibu mbaya kwamba muujiza wa kumpa kipofu kuona Bwana Yesu aliweza mara moja tu na sasa hawezj umechemka sana aisee. Yesu mpaka sasa anaponya kama uamini endelea hivyo hivyo. Mtumishi wa kweli utamjua tu kupitia mafundisho yake ila miujiza sio kipimo cha utumishi kwani inawezekana mtu kuigiza. Hizi ni siku za mwisho aisee. Leo fb nimeona tangazo la nabii mmoja kaweka picha yake kisha kuna maneno yaliyo andikwa kiingeneza kwa capital letters I AM YOUR GOD alafu majamaa fulani yanakoment Amen.
Hata Mimi nimeangalia leo marudio Channel Ten. But nilichokiona mmmmmh ACHENI tu. But kuhusu YESU naomba Mwandishi afute sentensi hiyo, kwani miujiza ambayo wengine wanaigiza leo yote ilitendwa na YESU KRISTO. Biblia Takatifu imejaa mafundisho ya YESU KRISTU na si usanii wa leo ambao tunaushuhudia.
 
Hao ni manabii au wapiga ramli tu, wengi wao wanatumia mazingaombwe
 
Huyu nabii juzi kafanya kitu ambacho kimenishtua sana kwenye kipindi chake, katokea mtu anadai ni kipofu kaja na mama yake mzazi, yule mama kaulizwa kadai huyo mtoto wake kazaliwa hana macho kabisa, kabla hajamuombea kamera zilikuwa zinamuonyesha yule kijana akiwa amefumba macho, na ukimwangalia yule kijana alikuwa kama anainama chini muda mwingi.

kuinamisha kichwa chini ni hulka ya binadamu inayoambatana na kuona aibu. Basi nabii akasema huyu mtu tokea kuzaliwa hajawahi kuwa na macho, sasa mungu akimrudishia hata jicho moja si itakuwa safi, basi akachukua maji ya chupa na kummwagia huku akiweka mikono yake kwenye yale macho, eti yule jamaa akafungua jicho moja linaona.

Cha ajabu eti yule kipofu ambaye hajawahi kuona tokea kuzaliwa akapata jicho moja na ye akawa katulia tu kama hamna kilichotokea, yaani fresh tu. Mtu ambaye hajawahi kuona tokea amezaliwa hawezi kuwa vile akiona.

Halafu huu usanii anaofanya nabii anashirikisha hadi wamama watu wazima kuongea uongo mbele ya kadamnasi. Toka lini mungu akamponya mtu nusu kwa kumrudishia jicho moja? Ningekuwepo siku hiyo haki ya mungu ningeomba urudie kuomba ili jicho la pili nalo lirudi.

USHAURI: Katika miujiza ambayo haina longolongo ni upofu, namshauri huyo nabii asiigize tena kuponya mtu kipofu maana kuna siku itamtokea puani. kuna watu kama sisi tukiwa eneo la tukio tutataka tuhakikishe kama huyo kipofu kweli ni kipofu kabla hujamuombea halafu tutakuumbua.

Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.
unajaribu kueleza kitu, lakini hapo mwishoni ndo umechafua, Yesu hawezi??????? seriously
 
Dah poleni sana makanisani kwenu, sisi hakuna ujinga kama huu, Kwanza tungemtandika bakora Kuanzia Nabii mwenyewe mpaka mgonjwa na mama yake pia
Hapana usiseme hivo....kuna shehe alitoa tangazo chanel 10 kuwa anaponya na kutoa pepo kwa watoto wakike na akina mama...aliita wote waende kuombewa..tangazo lilikuwa kwa style ya wachungaji....
 
Hayo anaweza kufanyia nyumbani kwake tu Lakini sio msikitini
 
Kulijuwa na wenye ukoma wengi kipindi cha nabii Elisha ila hakuna aliponywa ila Naaman jemedali. Kulikuwa na wajane wengi kipindi cha Nabii Elia ila ni mjane mmoja tu wa Selepta aliyopona kipindi cha njaa kali pale Elia alipozuia mvua isinye juu ya nchi kwa miaka mitatu na nusu.
Naongelea nyakati hizi...
 
Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.[/QUOTE]
hapo sasa umeuvuka mpaka
 
Huyu nabii juzi kafanya kitu ambacho kimenishtua sana kwenye kipindi chake, katokea mtu anadai ni kipofu kaja na mama yake mzazi, yule mama kaulizwa kadai huyo mtoto wake kazaliwa hana macho kabisa, kabla hajamuombea kamera zilikuwa zinamuonyesha yule kijana akiwa amefumba macho, na ukimwangalia yule kijana alikuwa kama anainama chini muda mwingi.

kuinamisha kichwa chini ni hulka ya binadamu inayoambatana na kuona aibu. Basi nabii akasema huyu mtu tokea kuzaliwa hajawahi kuwa na macho, sasa mungu akimrudishia hata jicho moja si itakuwa safi, basi akachukua maji ya chupa na kummwagia huku akiweka mikono yake kwenye yale macho, eti yule jamaa akafungua jicho moja linaona.

Cha ajabu eti yule kipofu ambaye hajawahi kuona tokea kuzaliwa akapata jicho moja na ye akawa katulia tu kama hamna kilichotokea, yaani fresh tu. Mtu ambaye hajawahi kuona tokea amezaliwa hawezi kuwa vile akiona.

Halafu huu usanii anaofanya nabii anashirikisha hadi wamama watu wazima kuongea uongo mbele ya kadamnasi. Toka lini mungu akamponya mtu nusu kwa kumrudishia jicho moja? Ningekuwepo siku hiyo haki ya mungu ningeomba urudie kuomba ili jicho la pili nalo lirudi.

USHAURI: Katika miujiza ambayo haina longolongo ni upofu, namshauri huyo nabii asiigize tena kuponya mtu kipofu maana kuna siku itamtokea puani. kuna watu kama sisi tukiwa eneo la tukio tutataka tuhakikishe kama huyo kipofu kweli ni kipofu kabla hujamuombea halafu tutakuumbua.

Yeye aendelee na miujiza iliyozoeleka ambayo hatuwezi kuthibitisha kama sijui nilikuwa naumwa ukimwi, tumbo, nilikuwa sizai,mapepo, kichwa kuuma, kutokwa na damu, BP n.k ila asicheze kabisa na kumponya kipofu ambaye hana macho, huo muujiza hata yesu ukimwambia arudie te na hawezi.
Kwanza ni wa wapi huyo Frank na kanisa gani?
 
Msilitaje Jina La Bwana Yesu bure. Kwa kukuelewesha katika Jina Hili la Yesu vitu vinavyoonekana na visvyoonekana viliumbwa. Pili. Kila goti litapigwa mbele yake na kila ulimi utakiri kwamba Yesu Ni Bwana ukiwepo wewe uliyesema hata Yesu hawezi kufanya miujiza. Wewe endelea kuchezea Jina Hili maana hakika siku moja utalia na kuomboleza utakapmwona akishuka na mawingu. Kusema kwamba Yesu hawezi kutenda miujiza ndugu yangu umeenda mbali sana. Aliyeumba vitu vyote hatashindwajwe kutenda miujiza. Tatu. Yesu yu hai siku zote maana yeye nimwanzo na mwisho. Yeye na Mungu ni wamoja.
 
tena unakuta mijitu ina PhD inamsikiliza muhubiri kama huyo
 
Back
Top Bottom