Mzigo wa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzigo wa nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Jul 8, 2010.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  ...kina dada hunishangaza, pamoja na kutaabika kujibebesha mizigo kama hii, kwanini Khanga haikosekani kwenye mikoba yenu???

  Eti watu wazima wenzangu, nini siri ya Khanga hizo, wanaenda nazo wapi au kwa matumizi gani? ....mtihani walaaaahi, ha ha...

   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahahahaha We Mbu! mchokozi sana lol! Kwanini lakini hutaki wabebe vijaluba vyao? Halafu siku hizi vijaluba vinazidi kuongezeka ukubwa ukilinganisha na miaka iliyopita. Nilipita duka moja juzi nikakuta limejaa mno nikasema hebu nichungulie hapa kulikoni? Kumbe vijaluba vipya vilikuwa vimeshuka wenyewe wanadai vikali sana na cha bei ya chini kilikuwa kinaanzia $350. Unaweza kukuta kijaluba kilivyosheheni kimekosa sana kina vitu vya kilo tatu sasa huu ni mzigo mzito kwa bega na unaweza kabisa kuleta hata matatizo ya mgongo.
   
 3. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbu, kanga muhimu kwa mwanamke, anaweza kuihitaji anywhere, any time. thats why mwanameke atakua na kanga katika pochi yake kama hana atabeba kikoi.

  ukubwa wa pochi ni kuweza kuweka mahitaji yote humo, mfano hiyo kanga, makeups na vinginevyo.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mh! Nasikia hizo kanga ni kwa ajili ya dhalula ya yule 'mgeni wao' anaewatembelea kila mwezi. sometimes huwa anaibuka tu bila taharifa wala apointment.
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hehehe hivi ni kweli watu wanatembea na kanga mkobani? mie na walionizunguka wote hawafanyi hivyo au ndio influence za culture za nje?!

  anyway mimi nafikiri akina dada lazima mikoba isheheni kwa kuwa kuna vitu muhimu vya kubeba kila utokapo kwako

  makeup (kama lipstick na sunscreen lotion, hand lotion, perfume ndogo...n.k)
  Vitu vya matumizi ya kike kama panty liners and pads (wengine sio zao hanina utaratibu maalum inabidi wawe na bidhaa full time)
  dawa (ya kichwa, ya maumivu, ya mafua, ya pumu)
  miwani ( ya jua au ya kuonea)
  Sewing kit (vifungo, uzi na sindano, mkasi)
  Stationery kit ( kalamu, flash drive, small note pads n.k)
  jamii ya tissue ( tissue, wet tisues, handkerchief)
  jamii ya candies ( chewing gum, chocolates, sweets)
  wallet
  simu
  n.k

  sasa vitu vyote hivyo lazima kibegi kijae ati au unanambiaje?
   
 6. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  na kanga pia kwa wabongo hasa tunaotembea kwa miguu na kupanda daladala zenye vumbi
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mom kwa hiyo kanga unaitandaza kwenye daladala kwanza ndo unakaa au inakuwaje?

  hebu nipe shule kwanza kuhusu matumizi ya hizi kanga mikobani :D
   
 8. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hii ni kwa mm gaijin. nikiingia kwenye daladala yenye vumbi hasa kama nimevaa nguo nyeupe nitafunga hii kanga ndio nikae then nikishuka nakunja na kurudisha kwenye pochi.

  au imgn ni mvua inanyesha nawe uko mbali na hom, then inapita gari na maji machafu yanakurukia nguo inaonekana ina madoa mabaya nitajisetiri kwa kanga mpaka nifike sehemu ambayo naweza pata option nyingine.
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hiyo ya khanga nadhani sio wanawake wote, cjakuaga nawazo la kubeba khanga kabisa, sema handbag yangu haiishi makorokoo, yaani nikitupa fones humu kuzipata ni mpaka ni beep, cjui hata kwanini...lol
   
 10. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,228
  Trophy Points: 280


  Kwanini kwenye hiyo list hakuna hela/ ATM card?

  Mi nilizani ndo vitu vya muhimu mwanamke kuanavyo na vingesaidia kupatikanika kwa nafasi kwenye dalalala.

  Sa mfano unafanya kazi Kariakoo, kunaulazima gani wa kubebelea saduku wakati vitu vyote vinapatikanika madukani?
  Najua nitajibiwa eti dharula mf MP au kuchanika kwa nguo kunaweza kutokea ghafa, sa kama ni ivyo, itakushinda nini kumtuma mtu wa hapo ofisni akakununulie sindano ,uzi au always?

  Afu hayo mabengi msiwe mnakuja nayo kwenye sherehe, kwani hutumika kuibia vinywaji.
   
 11. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa wanyaji wa BEER - zile "take away" zinawekwa humo! Pale mwamamke anapopewa "OFA" wakati anawahi nyumbani huo mkoba unamsaidia kuweka vile vichupa vidogo na kuondoka zake!
   
 12. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
   
 13. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 14. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Nijuavyo mie... kwenye party hatubebi mabegi haya makubwa tunabeba clutches
  ( kipimajoto) or purses - vipochi vidogo KWA AJILI YA LIPSTICKS, MINIATURE PERFUMES, HANKY, NA PESA YA DHARURA..
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,037
  Likes Received: 23,816
  Trophy Points: 280
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wallet kaka yangu ndo ina hizo pesa na atm cards
  but hakuna faida ya kuwa kila nguo yangu ikichanika kifungo nikanunue mpya wakati naweza kuikarabati kirahisi.............au nisubiri mpaka nipate siku zangu kazini nimtume mtu pedi! agggrrr

  kwenye sherehe tunabeba clutch bags..............na mara nyingi yangu huwa inaingia simu, pesa, lipstick na tissue tu
   
 17. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
   
 18. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 19. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,228
  Trophy Points: 280

  Mbona c wanaume hatuna hofu ya kuchanika suruali zetu wala hatubebi cherehani?
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,037
  Likes Received: 23,816
  Trophy Points: 280
  Unajitahidi usiingie wapi na kanga? Gesti au?
   
Loading...