Mzee Uledi na Msafisha Viatu wamuonya Tundu Lissu vita alioanzisha imeingia kwenye "Grey Zone", kutoka itakuwa shida

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Juzi jioni bila kutarajia niliwakuta hawa wazee mtaa wa Tandamti ndo wanafunga biashara mapema saa 10.

Nawauliza imekuwaje? wakanambia kuna kikao cha dharura.

Nikawauliza kuna nini?

Msafisha viatu akasema alitaka kusoma ujumbe wa WhatsApp ulosema kwamba uvumi na uzushi dhidi ya kiongozi wa juu wa nchi umefikia "highest level" yaani kiwango cha juu.

Nikamwambia vijana wa "cyber crime" wapo kazini masaa 24 na huenda walikuwa wamepata njia moja ya kisosora kwa fundi simu mahali.

Mzee Uledi akaingia akasema " lakini haya yote ni huyu jamaa Tundu Lissu, bila huyu kuleta uvumi pale mwanzo basi tusingefika hapa maana kule juu kati wizara ya katiba na mawasiliano na kwa yule mzee Semu wa TCRA kumekucha."

Mzee Uledi akaendelea, huyu Tundu Lissu ameingia mwenyewe kwenye "Grey Zone".

Sidhani hata kama next-time around anaweza kupata "fair reception".

Ingekuwa vita kamili tungesema mengine lakini kwenye hii hakuna namna kuna mambo kadhaa yanaendelea, akamalizia mzee Uledi.

Msafisha viatu akakazia akasema, mimi nilisema Tundu Lissu hawezi kuwa raisi wa nchi hii na angeshindwa uchaguzi na ikawa. Sasa ameanzisha vita ya mtandaoni amejiingiza kwenye "Grey Zone".

Mimi nikashangaa kusikia hilo neno Grey Zone nikawauliza lamaanisha nini?

Msafisha viatu akasema nenda ukagoogle utapata maana yake.

Hawa wazee ni wale wazee wasomi ambao walisoma hadi Makerere mzee Uledi akifanya kazi TRC ya zamani na Msafisha viatu akiwa bandarini Dar.

Tukaachana hapo na mimi nikaelekea mitaa ya posta kuchukua daladala kuelekea Temeke.

Nikiwa kwenye basi nikagoogle what is Grey Zone.

Nikapata sehemu waeleze uzuri kuhusu hii makitu.

Wanasema Grey zone ni pale kunakuwepo vita baina ya nchi na nchi lakini isohusisha vifaa vya moto vya kijeshi, bali mambo kama udukuzi wa kimtandao au "Cyber hacks" na upotoshaji habari yaani "disinformation" na uchokozi yaani "intimidation".

Ni eneo aambalo adui haonekani wala hajulikani na amesimama kati ya vita na amani.

Kwa maana ingine ni kwamba mstari wa mbele yaani "Front Line" upo kila mahala na mlengwa aweza kuwa ni yoyote yule.

Hili eneo ni uwanja wa vita ambapo majasusi wa aina zote wa kiserikali na wale waitwao "Rogue" yaani ambao wengine wamefukuzwa kazi lakini kwa sababu ya ujuzi mbalimbali bado huitajika kwa shughuli ziitwazo "ad-hock" ndio eneo lao la kujidai.

Humo, wapo majasusi wa kirusi, kichina, kutoka Korea kasikazini, Afrika na kwingine.

Lakini nikawa na interest yaani tashwishi ya kufahamu zaidi kuhusu hii kitu disiformation.

Kwenye hii sehemu kuna vita kati ya ukweli na uongo ambapo mitandao ya kijamii kwa sasa imeanza kubanwa kuhusu kuruhusu habari za kizushi kurushwa kupitia kwenye mitandao yao yaani platforms.

Tanzania imeanza kupigana hii vita katika hili eneo ingawa tumechelewa lakini ni vita endelevu na haiishi leo.

Ni eneo ambalo lina kila kitu ambacho mtu anataka kujifunza na kuelewa.

Mimi nikawakumbuka hawa wazee Uledi na Msafisha viatu, nikajiuliza wamefahamu vipi mambo haya ya Grey Zone?

Hivyo ujumbe ndo huo kwa mtanzania mwenzetu aleamua kujitoa mhanga Tundu Lissu kuwa macho na hili eneo la Grey Zone uloingia.

Inawezekana ikawa ngumu kutoka na kusahau njia uloongilia.

Wataonielewa hawatapata shida.

Jumapili njema.
 
Tundu hana namana ya kuchomoka kwenye hiyo greyzone, sasa ajiandae kisaikolojia, maana zone aliyofika sio shwari kbsa. Kweli kuujua undani wa mtu ina gharama. Aje atuombe radhi watz tutamuelewa.
 
Alipojificha akitoka Kama ni mtu mwenye utashi ataomba radhi kwa kuwatendea watanzania mema,Ataacha kuvunja haki na kuona yupo juu ya Sheria.

Atakumbukwa kwa lipi?

Jema au baya...

Tunaishi tufe...vyeo na madaraka vinaisha tu.
Yuu wapi.. Hitler
Benito Musolini
And the so like...
 
Alipojificha akitoka Kama Ni mtu mwenye utashi ...ataomba radhi kwa kuwatendea watanzania mema,Ataacha kuvunja haki na kuona yupo juu ya Sheria.

Atakumbukwa kwa lipi?
Jema au baya...

Tunaishi tufe...vyeo na madaraka vinaisha Tuu...
Yuu wapi.. Hitler
Benito musolini
And the so like...
Ni ngumu sana kucheza na siasa za mitandao na ukikosea mahala ndo inakuwa mwisho wako kisiasa.

Donald Trump ni mfano mzuri tu, alikotoka na aendako kisiasa sote twafahamu.

Ni kweli twaishi ili tufe lakini staha, ujuvi na namna ya kuogelea kwenye maji yalotulia ni jambo la busara.

Kuna msemo wa zamani kidogo wa kiingereza wasema "Still Waters runs deep".

Ndo maana sisi binadamu watakiwa kuingiza mguu mmoja tu kufanya tathmini.
 
Je, endapo taarifa ya Lissu yakawa hivyo hawa ficha ficha watasema nini mbele ya watanzania?
Pembe la ng'ombe halifichiki buda, waziri mkuu sio fala kutamka yale aliyotamka tena kwa kejeli. Muwe mnasoma hata code watu wazima na wenye mamlaka wakizungumza. Hata kama alikuwa na tatizo, kwa sasa atakuwa fit ndio maana waziri mkuu akalihakikishia taifa.

Achana na viongozi wa taasisi hewa, hazina hata ofisi.
 
Pembe la ng'ombe halifichiki buda, waziri mkuu sio fala kutamka yale aliyotamka tena kwa kejeli. Muwe mnasoma hata code watu wazima na wenye mamlaka wakizungumza. Hata kama alikuwa na tatizo, kwa sasa atakuwa fit ndio maana waziri mkuu akalihakikishia taifa.

Achana na viongozi wa taasisi hewa, hazina hata ofisi.
Mtapiga kelele nyingi lakini ukweli upo palepale, taifa linalovunja haki za kibinadamu huzalisha chuki.
 
Back
Top Bottom