Mzee Mwinyi alikuwa na nafasi ya kuwa Baba wa Taifa wa pili baada ya Nyerere ila maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo

Ni Jambo lililo wazi kwamba Mzee Mwinyi ni mtu mwema mpole mnyenyekevu na mkarimu asie na makuu. Alipaswa kuwa na nguvu baada ya Mwalimu kuondoka kwasababu ya kigezo cha seniority list.

Lakini maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo na kupewa Mkapa. Hebu fikiria mfano huu mdogo.

Eti yeye Mzee Mwinyi anamhusudu Magufuli na kwamaneno yake anaongoza nchi vizuri sana. Mbaya zaidi, anatamani hata tuvunje katiba ili Magufuli abaki madarakani. Kweli hii ni hadhi ya mtu kuwa na hadhi ya pili next from Nyerere?

Mkapa deserved it kwasababu alithubutu kumkemea JPM waziwazi kama tu Mwalimu alivyofanya kwa Mwinyi.
Baba wa Taifa huwa ni mmoja tu ,wala Mzee hana Sifa ya kuwa Baba wa Taifa
 
Jana mbona alimuombea sana marehemu msamaha. “Alikosea Baba yetu Adam ijekua siye, yote aliyokosea ya marehemu asamehewe”. Ni yepi hayo yaliyoikosesha amani nafsi ya Mzee Mwinyi mpaka kumuombea marehemu mzee Mkapa msamaha?
 
Huyu mzee mwenye enzi Mungu amemjalia maisha marefu ana miaka 94 na bado yuko vizuri akili yake iko timamu kuliko sehemu kubwa ya member wa JF. Je hakuna cha kujifunza? Tafakari
Unafahamu kwamba inasemekana kuna vikongwe wachawi kupindukia?

Kiimani Wakati mwingine binadamu tunapewa nafasi ya kuishi miaka mingi ili tupate nafasi ya kuacha maovu na kutubu.

Please, nisiwekewe maneno kwamba namuongelea mzee mwinyi. Nimekujibu tu ishu ya kuishi miaka mingi.
 
Vipi ile ahadi aliyoitoa Mungu? Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na kheri duniani? Tuanzia hapa
 
Rip mkapa we will miss you
IMG-20200729-WA0001.jpeg
IMG_20200730_000025.jpeg
IMG_20200728_193257.jpeg
 
Vipi ile ahadi aliyoitoa Mungu? Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na kheri duniani? Tuanzia hapa

Kuishi miaka mingi hakutokani na ahadi hiyo pekee. Kila kitu kina exceptional zake, hata MUNGU naye ana exceptional zake, wapo watoto wachanga wanafariki bila kujua kuwa kuna ahadi ya kuishi miaka mingi.
 
Unakumbuka jina la aliyempiga kibao?

Ingawa niliona kwenye tv hata sura sikumbuki nakumbuka jamaa alikua na baraghashia ila vazi sikumbuki kama ilikua kanzu ya hughurungi au shati jeupe na suruali nyeusi
Aliempiga mwinyi Kofi alikufa mwaka juzi.
 
Nyerere alikuwa na akili ila akishindwa kutumia akili zake kipindi cha mwisho kuwa na maono juu ya uelekeo wa dunia kutoka ujamaa kwenda ubepari. Kiburi chake ndio kimesababisha hadi sasa tupo nyuma kimaendeleo.
Mmmmh
 
Mbona umesahau kusema enzi yake ndio Baba yako aliacha kuvaa midabwada kwa kuwa sasa nguo hazikuwa tena bidhaa adimu, aliacha kupanga folen usiku kucha akiwa na kupuni ya Mjumbe wa Ccm ili aruhusiwe kununa bidhaa kama sukari. Umesahau enzi zake ndio jamaa zako waliruhusiwa kumiliki Friji kwa kuwa kabla yake ilikuwa ni uhujumu Uchumi n.k
Nakumbuka enzi zake, mke wake aliifanya ikulu kuwa ofisi ya wapiga deal, mpaka Nyerere akasema
 
Jana kwenye hotuba yake nilipatwa na mshangao, alimsifia sana mkapa kwa kukuza sana uchumi, then akaja kumsifia Magufuli kwa kuipeleka nchi mbele kwamba aliitoa nchi kubaya. Hii inamaanisha yeye Mwinyi na Kikwete waliiharibu nchi au sio?
Na nyerere umemsahau mbona?
 
Ni Jambo lililo wazi kwamba Mzee Mwinyi ni mtu mwema mpole mnyenyekevu na mkarimu asie na makuu. Alipaswa kuwa na nguvu baada ya Mwalimu kuondoka kwasababu ya kigezo cha seniority list.

Lakini maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo na kupewa Mkapa. Hebu fikiria mfano huu mdogo.

Eti yeye Mzee Mwinyi anamhusudu Magufuli na kwamaneno yake anaongoza nchi vizuri sana. Mbaya zaidi, anatamani hata tuvunje katiba ili Magufuli abaki madarakani. Kweli hii ni hadhi ya mtu kuwa na hadhi ya pili next from Nyerere?

Mkapa deserved it kwasababu alithubutu kumkemea JPM waziwazi kama tu Mwalimu alivyofanya kwa Mwinyi.
Sasa tumwombee JK maisha marefu, maana huyu chakubanga wa Sasa bila JK ataizamisha nchi shimoni
 
kila mtu anahaki kutoa maoni yake alimradi hajavunja Sheria. Actually hatamm ninaunga mkono MAGU kuongezewa muda maana amefanya vitu vyakipekee Hakuna rais alowahi kufanya:
- kujenga reli
- kusafisha Ccm
- kujenga ikulu na makao makuu dodoma
- kuishinda vita ya corona majirani wakihaha
- kununua mindege ndani yamuda mfupi
- kutoa haki ya elimu (elimu bila malipo)
- kuzuia wizi wa madini
- kujenga Nyerere dam
- kukomesha mgawo wa umeme na kuusambaza spidi
achilia mbali yale ya kawaida Kama barabara, maji, vituo vya afya nk.
Nchi nyingine zimewahi kuwaongezea muda marais mahiri mf. Urusi, china nk.
tuache upumbafu wakudhani wengine hawastaili kutoa maoni Mwinyi anajua vyema ugumu wakazi ya urais kuliko majinga kadhaa yanayong'ang'ana kuingia ikulu na ujuzi sifuri walionao
 
Back
Top Bottom