Mzee Mwinyi alikuwa na nafasi ya kuwa Baba wa Taifa wa pili baada ya Nyerere ila maboko yake yalimkosesha hadhi hiyo

Nyerere alikuwa na akili ila akishindwa kutumia akili zake kipindi cha mwisho kuwa na maono juu ya uelekeo wa dunia kutoka ujamaa kwenda ubepari. Kiburi chake ndio kimesababisha hadi sasa tupo nyuma kimaendeleo.
Kwamba maendeleo huletwa na mfumo wa ujamaa au ubepari?. kwamba huwezi kuendelea ukiwa Mjamaa au huwezi kuendelea ukiwa Bepari?. au nini haswa tafsiri ya maendeleo uliyonayo kichwani? maana mimi ninatizama maendeleo kwa mlengo tofauti.

Mimi nilidhani maendeleo ni Elimu ya kujua kwamba nyumba lazima iwe bora, iwe na madirisha ya kutosha, kula chakula bora, kufahamu kanuni za kilimo uvune mazao ya kutosha n.k.

Tatizo hapa ni kutafuta tu Mtu wa kumlaumu kwa matatizo yetu wenyewe....hivi nchi iwe ya kijamaa au kibepari inakuzuia vipi vichwa vyenu kubuni mashine za kubadilisha pamba mliyolima kuwa nguo?.

Kuishi kwa kutegemea akili za wengine kutatua matatizo yetu ndio tutaishia kukaa vijiweni kusubiri Kiongozi anachagua mfumo gani wa kuendesha nchi.

Kiongozi akifanikiwa kusimamia Amani, Usawa, Elimu, Huduma za Afya n.k nadhani inatosha sana tu...tuliobaki tutimize wajibu wetu tutaendelea.
 
Watoto wa generation hii hamuwezi kujua mchango wa Mzee Mwinyi katika nchi ya Tanzania, Sisi ndio tunajua, chuki zako dhidi ya rais wa sasa usizitumie kumchafua mzee wetu,
Kaa na wazazi wake wakupe historia ya nchi yako vizuri.
Ipo haja ya kuandaa uzi watu wafahamu makubwa aliyoacha Mwinyi
 
Swali , jee inawezekana Marehemu Mzee Mkapa sababu ya kifo chake inaweza kuwa ni STRESS, iliyofanya immunity yake kwenda chini.
Kila kifo kina sababu. Cha muhimu ni kukumbuka tu kwamba kila mmoja atakufa.
 
Ipo haja ya kuandaa uzi watu wafahamu makubwa aliyoacha Mwinyi
kweli mkuu, inasikitisha sana rais aliyeibadili taswira ya tanzania leo vitoto vinambeza hivi...

mwinyi alikubali kuingia ugomvi kwa kuibadili baadh ya mifumo ya kijamaa na kuanzisha soko huria, watu wakaruhusiwa kumiliki biashara binafsi, mashart ya uingizaji bidhaa toka nje na manunuzi yakapunguzwa, kubwa zaidi 1991 mfumo wa vyama vingi ukaasisiwa baada ya makelele ya wafadhili..

note: vijana msikurupuke kumnanga rais bora wa wakati wote Tanzania, huyu ndo rais pekee aloruhusu watu wafanye kila kitu bt wasivunje tu sheria.
 
Unafahamu kwamba inasemekana kuna vikongwe wachawi kupindukia?

Kiimani Wakati mwingine binadamu tunapewa nafasi ya kuishi miaka mingi ili tupate nafasi ya kuacha maovu na kutubu.

Please, nisiwekewe maneno kwamba namuongelea mzee mwinyi. Nimekujibu tu ishu ya kuishi miaka mingi.
Wewe ni wa imani ipi? maana kwenye vitabu vyetu huku imeandikwa "Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako".....KUT. 20:12
 
WEWE NI MTANZANIA? ULIFUATILIA HOTUBA YA HUYO MZEE JUZI KWENYE MKUTANO WA CCM DODOMA KUMCHAGUA RAIS WA ZANZIBAR NA KUMPITISHA M JIWE KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM? KAMA HUJUI JAMBO USIJIDHALILISHE HADHARANI.


Hivi wewe unajua kiswahili vizuri??

NI LINI NA WAPI RAIS MSTASFU ALLY HASSAN MWINYI ALISEMA KATIBA IVUNJWE ILI MAGU AENDELEE KUONGOZA BAADA YA MIAKA KUMI YA KIKATIBA??

👆🏻Hilo ndilo swali langu, kumbuka maneno ya msisitizo ni haya; "KATIBA IVUNJWE".

Sitaki porojo hapa, jibu swali.

Msifuatilie mambo kwa mihemuko yenu ya kisiasa.
 
Wewe ni wa imani ipi? maana kwenye vitabu vyetu huku imeandikwa "Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako".....KUT. 20:12
Nilishajibu hili swali, mkuu Sentensi yangu imeanza na neno wakati mwingine. Kila kitu kina exceptions, vipi kuhusu watoto wachanga wanaofariki? Hawajawaheshimu wazazi?
 
Hivi wewe unajua kiswahili vizuri??

NI LINI NA WAPI RAIS MSTASFU ALLY HASSAN MWINYI ALISEMA KATIBA IVUNJWE ILI MAGU AENDELEE KUONGOZA BAADA YA MIAKA KUMI YA KIKATIBA??

👆🏻Hilo ndilo swali langu, kumbuka maneno ya msisitizo ni haya; "KATIBA IVUNJWE".

Sitaki porojo hapa, jibu swali.

Msifuatilie mambo kwa mihemuko yenu ya kisiasa.
NA MIMI NAKUULIZA ULIFUATILIA HOTUBA YAKE HIYO NILIYOISEMA? KAMA ULIFUATILIA NIAMBIE ALISEMA NINI NA HICHO ALICHOSEMA WEWE UNAKIELEWAJE? SITAKI POROJO JIBU SWALI ILI NA MIMI NIKUJIBU.
 
NA MIMI NAKUULIZA ULIFUATILIA HOTUBA YAKE HIYO NILIYOISEMA? KAMA ULIFUATILIA NIAMBIE ALISEMA NINI NA HICHO ALICHOSEMA WEWE UNAKIELEWAJE? SITAKI POROJO JIBU SWALI ILI NA MIMI NIKUJIBU.


Mwinyi hakusema "katiba ivunjwe", alisema katiba "ifikiriwe kubadilishwa" kipengele cha ukomo wa raisi ili Magu aendelee,--- hayo yalikuwa ni maoni ya Mwinyi kama Rais mstaafu, kama raia mwenye haki zote za kutoa maoni kama jinsi wewe unavyotoa hapa.

Katiba inaweza kubadilishwa na imeshafanyika hivyo mara kadhaa kukidhi haja ya wakati, Katiba sio Qur'an au Biblia, katiba ni sheria zilizotungwa na Bunge, hoja ni hii; ni Bunge gani lingekaa kwa wakati ule/ huu kubadilisha hiyo katiba, kimsingi Mwinyi alikuwa anamfurahisha Magu (kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa) ili kumtengenezea njia Hussein.

Hata kama ingewezekana katiba ibadilishwe mimi binafsi sikubaliani na mawazo ya Mwinyi ambayo yasingeweza kutekelezeka.
 
Muacheni mzee wa wetu atuchekeshe wajukuu zake. Aliwakuta baba/babu zetu wanavaa likundou,kaniki na viatu vya mairi ya gari,wanapanga foleni ya sukari,sabuni na mafuta ya taa,TV alikuwa nayo Nyerere tu pale Ikulu. Akatufanya tujue duniani watu wanaishije ili na sisi tuishi kama wao.
Tatizo ni pale ukijifanya uko upande wa jiwe, utachukiwa na watanzania wote, refer Bashite
 
Nakumbuka enzi zake, mke wake aliifanya ikulu kuwa ofisi ya wapiga deal, mpaka Nyerere akasema
Kwa mantiki hiyo, hiyo kama Nyerere angekuwepo enzi zile Mama Mkapa alipoanzisha na kuendesha NGO yake binafsi iitwayo EOTF akiwa ikulu angemshushia makombora ya maneno???
 
kila mtu anahaki kutoa maoni yake alimradi hajavunja Sheria. Actually hatamm ninaunga mkono MAGU kuongezewa muda maana amefanya vitu vyakipekee Hakuna rais alowahi kufanya:
- kujenga reli
- kusafisha Ccm
- kujenga ikulu na makao makuu dodoma
- kuishinda vita ya corona majirani wakihaha
- kununua mindege ndani yamuda mfupi
- kutoa haki ya elimu (elimu bila malipo)
- kuzuia wizi wa madini
- kujenga Nyerere dam
- kukomesha mgawo wa umeme na kuusambaza spidi
achilia mbali yale ya kawaida Kama barabara, maji, vituo vya afya nk.
Nchi nyingine zimewahi kuwaongezea muda marais mahiri mf. Urusi, china nk.
tuache upumbafu wakudhani wengine hawastaili kutoa maoni Mwinyi anajua vyema ugumu wakazi ya urais kuliko majinga kadhaa yanayong'ang'ana kuingia ikulu na ujuzi sifuri walionao
Matanga katika ubora wako, 1.5 tr
 
Hivi wewe unajua kiswahili vizuri??

NI LINI NA WAPI RAIS MSTASFU ALLY HASSAN MWINYI ALISEMA KATIBA IVUNJWE ILI MAGU AENDELEE KUONGOZA BAADA YA MIAKA KUMI YA KIKATIBA??

Hilo ndilo swali langu, kumbuka maneno ya msisitizo ni haya; "KATIBA IVUNJWE".

Sitaki porojo hapa, jibu swali.

Msifuatilie mambo kwa mihemuko yenu ya kisiasa.
Wewe utakuwa matanga tu, so nikisema katiba ibadilishwe/Iruhusu Jiwe abaki madarakani then mtu akasema nimesama katiba ivunjwe wewe hapo utapinga kuwa sijasema hivyo kwa sababu tu msemaji katumia neno kuvunja badala ya maneno yangu,
 
Mkuu tz haijawahi na haitotokea kuwa na baba wa taifa namba 2 kwa mfumo huu wa CCMism labda uishee!
Mpaka sasa tuna baba wa taifa 1 tu, wengine waliofuata ni mababa wa chama.
2. Baba wa CCM
3. Baba wa CCM
4. Baba wa CCM
5. Baba wa CCM loading ila ni baba wa CCM zaidi ya wote walotangulia.
Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika!
 
Wewe utakuwa matanga tu, so nikisema katiba ibadilishwe/Iruhusu Jiwe abaki madarakani then mtu akasema nimesama katiba ivunjwe wewe hapo utapinga kuwa sijasema hivyo kwa sababu tu msemaji katumia neno kuvunja badala ya maneno yangu,


Maneno "Kuvunja katiba" na "kubadilisha katiba" ni sawasawa???!
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom