Mzee Mwanakijiji: kimya chako kinanitisha

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,499
34,560
Mzee Mwanakijiji u hali gani mkuu....
Naamini umeyaona, umeyasikia na kushuhudia matukio yaliyojiri nchini ndani ya wiki mbili hizi hadi sasa.

Umekuwa mstari wa mbele siyo kwenye kukosoa tu bali hata kuelimisha nini kifanyike pale ambapo watawala wetu wanakwenda nje ya mstari. Leo tunaye *masihi* wetu na hakika tulitamani mtu aina hii ashike hatamu ili tuweze kupiga hatua mbele kama taifa.

sijakusikia wala kukuona ukisema neno dhidi ya matukio tata yaliyojiri ndani ya wiki mbili hizi kuhusiana mwenendo na maadili ya viongozi. Kuna filamu moja niliangalia inahusu kisa cha wanyama ambapo sehemu moja beast anamuuliza warden "are you good guy, bad guy or what guy?" nalirusha swali hili kwako

je KAINZI hakajanusa kashata huko?

Kimya chako kinanitisha mkuu.....
 
Muogope sana mtu asiyedhihirisha upande wake wakati wa maovu!

Bora adui yako kuliko vuguvugu.
Mabandiko ya kumsifu mtukufu yalikuwa mengi, mtukufu akisifiwa kwa kula aina ya tambo na mapambio! Haikutosha tukalazimishwa kisicho tukione ndicho!!! TULIKEMEA HATUKUNYAMAZA. TUKASEMA NJOONI MSIPIGE KELELE ZA MBALI!! HAWAKUJA LEO VIMEROJA WANAKUJA NA MPYA GANI?

HAMKANI MAMBO SI SHWARI TENA!!
 
Hakika kuna tatizo mahala
 
Kabisa Mkuu huyu jamaa alivyobadilika hata kuanza kumpamba dikteta uchwara ni jambo la kushangaza sana. Sijui kama atakuja kukubali kwamba alifanya makosa makubwa sana katika juhudi zake za kumpa kwa mafuta huyu DU ili amrembe.

Muogope sana mtu asiyedhihirisha upande wake wakati wa maovu!

Bora adui yako kuliko vuguvugu.
 
Mbona nimeshaandika jamani na nitaandika. Tatizo ni kuwa kuna watu hawataki kusikia hasa kama nitaandika tofauti. Wanataka wote tuandike na tufikiri namna moja. Kuna ambayo nimeyasema ndani ya wiki hizi chache rafiki yangu Msanii na utaweza kuona kuwa sijawa kimya kama unavyodhania. Ila siandiki kutoka katika hisia - labda mara chache - lakini napenda zaidi kuangalia kwa jicho lenye uhuru zaidi.
 
Magu is becoming more and more indefensible by the day.

Hata kama si yeye aliyewatuma wale watu kwa Nape....the buck stops with him.
Ni kweli Magu asipochukua hatua atapoteza credibility yote.
Asipokuwa makini atapoteza uhalali wa kutawala na wananchi wote watamwona muonezi na mbaguzi.
Kumkubatia Bashite itakuwa na gharama kubwa sana na ya hatari.
 
Hivyo vitu ulivyovitaja hawahi kuwa navyo, kwa hiyo hana cha kupoteza.

Mwenzako anasubiri kuiba kura tu.
 
Mbona nimeshaandika jamani na nitaandika. Tatizo ni kuwa kuna watu hawataki kusikia hasa kama nitaandika tofauti. Wanataka wote tuandike na tufikiri namna moja. Kuna ambayo nimeyasema ndani ya wiki hizi chache rafiki yangu Msanii na utaweza kuona kuwa sijawa kimya kama unavyodhania. Ila siandiki kutoka katika hisia - labda mara chache - lakini napenda zaidi kuangalia kwa jicho lenye uhuru zaidi.
Ni kweli nimesoma mabandiko yako kadhaa lakini ni kama upo inactive katika situations za bongo.
  • Uhuru wa vyombo vya habari
  • Kamatakamata dhidi ya wapinzani
  • Bunge contempt
  • Upungufu wa Chakula na ukame
  • Inflation
  • Illiteracy level kupanda though elimu ni bure
  • Beyond powers wanazotumia wakuu wa wilaya na mikoa
Ni kweli nimesoma lakini naona kama vile you are what guy...

Mimi ni mpenzi wa kusoma makala za uchambuzi ili kuimarisha ufahamu wangu na kuwasaidia wengine.

Je Mwakyembe amekuwa demoted au stationed?
 
Back
Top Bottom