Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Sostenes Swila kuendelea kutoa ushahidi wake Februari 9, 2022

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Habari Wakuu,

Leo 08/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Sostenes Swila kuendelea kutoa ushahidi wake Februari 08/2022

Baki nami.

Updates:

Jaji ameingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
Mawakili Wa Serikali Waandamizi Na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
  • Sisty Aloyce
  • Iddi Msawanga
  • Maria Mushi
  • Kadija Aron
  • Lusako Mwaiseke
  • Fredrick Kihwelo
Wakili Nashon Nkungu amepata Emergency Kidogo yupo karibu sana kufika

Jaji: Kabla hatuja endelea Wasiliana naye tujue yupo Wapi

Wakili Peter Kibatala: Sawa Mheshimiwa Jaji

(Anatoka Nje kwenda Kupiga Simu)

Mahakama itasubiri Kidogo, Ukimya Umetawala Wanaingia

Kwa Pamoja sasa Wakili Dickson Matata na Wakili Nashon Nkungu

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa nimtambulishe Wakili Nashon Nkungu,

Nashon Nkungu: Samahani sana nimechelewa Sababu ya Usafiri

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kuendelea Kusikilizwa, Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha Ulikuwa chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Jaji: nakualika Wakili Fredrick Kihwelo

Kiwhelo: shahidi Salaam

Shahidi: Salaam

Kiwhelo: Kwa Mujibu Wa Ushahidi Wako Ulisema Ulipeleka simu Nane

Shahidi: Sahihi

Kiwhelo: nakukumbusha Namba za Simu ulizotaja hapa Mahakamani 0719933386 na 0784779944

Shahidi: Sahihi

Kiwhelo: shahidi Ukienda Dukani Kununua Simu, Je ndani Kuna Kuwa na Line

Shahidi: Hapana

Kiwhelo: kwa hiyo Simu na Line ni Vitu Viwili tofauti

Shahidi: Sahihi

Kiwhelo: Mwambie Jaji ilikiwa Simu 8 ambazo ziliwasilishwa Mahakamani Kama Vielelezo, na Kama line za Simu 8 ziliwasilishwa kama Vielelezo

Shahidi: Ndiyo

Kiwhelo: Mkumbushe Mheshimiwa Jaji ni Vielelezo namba Ngapi, hizo Line 8

Shahidi: Line Za Simu zipo ndani ya Simu Zenyewe

Kiwhelo: Tumeshakubaliana Kuwa Line na Simu no Vitu Viwili tofauti, Sasa nataka Kujua Line 08 ni Kielelezo namba Ngapi

Shahidi: Hapana ziliwasilishwa Simu tuh, Line zipo ndani

Kiwhelo: Unajua Kuwa IMEI Namba haionyeshi line Bali Umiliki Wa simu

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Unafahamu Kuwa namna pekee ya Kuonyesha Umiliki Wa Line ni Kuleta Namba IMCI

Shahidi: Siyo sahihi

Kiwhelo: Unafahamu Kwamba namba ya IMCI ni tofauti na namba za simu

Shahidi: Sifahamu

Kiwhelo: Unaweza Kumwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mmeleta namba za IMCI za line hapa Mahakamani.?

Shahidi: Siwezi kulijibia hilo

Kiwhelo: Kwenye Maelezo Yako Ulisema Mwezi January 2020 Ulipata Uhamishoni Wa Muda Kwenda Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Ni sahihi Mwezi August 2021 ulirudi Katika Kituo chako Cha Kazi TEMEKE

Shahidi: sahihi

Kiwhelo: Uhamisho Wako Ulikuwa wa Muda gani

Shahidi: Mwaka Mmoja Kiwhelo: Unaweza Kumwambia Mheshimiwa Jaji Suala la Uhamishoni ni Mchakato au Tukio

Shahidi: Ni taratibu za Kazi

Kiwhelo: Twende Kwenye taratibu za Kazi, Wakati wa Mahojiano Yako Uliaambia Mahakama hii Kuwa Wakati wa Uhamishoni Ulipitia taratibu Mbalimbali

Shahidi: Ndiyo nilieleza

Kiwhelo: Shahidi nitakuwa Sahihi Nikisema Dalili zote zinasema Kwamba Uhamisho wako Ulikuwa wa Kimkakati na Ulihusu Shauri hili

Shahidi: Si Kweli

Kiwhelo: Wakati wa Mahojiano Ulisema Taarifa za Matendo Ya Kihalifu zilipokelewa na DCI ROBERT BOAZ

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Na Vitendo hivyo Vilikuwa vinahusu uchomaji Masoko

Shahidi: Ndiyo na Matukio Mengine

Kiwhelo: Kukata Miti Barabarani?

Shahidi: Ndiyo na Matukio Mengine

Kiwhelo: na Maandamano?

Shahidi: Ndiyo na matukio Mengine

Kiwhelo: Orodha hiyo Kuna Ugaidi Shahidi Ndiyo upo

Kiwhelo: Ulisema Kuna Viongoz walitaka kudhuliwa, Je Unaweza Kumkumbusha Mheshimiwa Jaji Majina ya hao Viongozi

Shahidi: Lengai Ole Sabaya

Kiwhelo: Mtaje Mwingine

Shahidi: Mwingine Simfahamu

Kiwhelo: Kwahiyo Ulikuwa Unaandika Usichokifahamu

Shahidi: Namjua huyo tu

Kiwhelo: Mtuhumiwa Wa Kwanza hadi wa Nne, Waliandaa Vipi Maandamano

Shahidi: Wanajua Watuhumiwa

Kiwhelo: Wewe Unafahamu Vipi Kwamba Walipanga Maandamano

Shahidi: Wanajua Watuhumiwa

Kiwhelo: Kwani Maandamano ni Kosa

Shahidi: Siyo Kosa Kama Ulifuata Sheria

Kiwhelo: Kwani Walikuwa wameshaandamana au Walikuwa wanapanga kuandamana?

Shahidi: Walikuwa wanapanga

Kiwhelo: Ulijuaje Kama hawato omba Kibali

Shahidi: Hilo siwezi kulijibu

Kiwhelo: Ni sahihi Kwamba Tarehe 18 July 2020 ulifungua Jalada la Kesi ya Kula Njama ya Kutenda Matendo Ya Ugaidi

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Ni sahihi Kwamba Maelekezo hayo Ulipewa na ACP KINGAI

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: nitakuwa Sahihi Nikisema Kwamba Mtu Mmoja anaweza Kuamua ufunguliwe Kosa la Namna gani

Shahidi: Siyo Sahihi

Kiwhelo: Wakati una elekezwa na Ramadhan Kingai Kufungua Shauri hili ulikuwa Umepewa Jukumu la kuwa Mshairi Wake

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Kwani alikwambia Fungua Shauri hili au Mlijadiliana Kwamba Kwa Mujibu wa Ushahidi Huu tufungue Shauri hilo

Shahidi: Ailinielekeza

Kiwhelo: Kwani alikwambia amejadiliana na nani Kwamba Wameona inafaa Kosa la Ugaidi lifunguliwe

Shahidi: Hakuniambia

Kiwhelo: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba Ramadhan Kingai ndiye aliye taka Shauri hilo lifunguliwe

Shahidi: Siwezi Kujibu hilo

Kiwhelo: Ni sahihi Kwamba wewe ndiyo Ulipokea Simu Kutoka Kwa DC Goodluck zilizo toka Moshi

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Unaweza Kueleza Mahakama Taratibu za Makabidhiano

Shahidi: alini kabidhi zikiwa zimeandikwa PF 145 Nikaenda Kuzi hifadhi katika Kabati la Chuma

Kiwhelo: Ni sahihi pia Kuwa Ramadhan Kingai Alimuamuru DC Goodluck akukabidhi Simu za Khalfani Bwire

Shahidi: Ndiyo

Kiwhelo: Ni kweli pia Simu za Luten Denis Urio Ulikabidhiwa kwa Hati ya Makabidhiano

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: na Hati ya Makabidhiano hiyo ipo Mahakamani hapa

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Ni sahihi pia unawasilisha Mahakamani Hati ya Makabidhiano ya Simu za Khalfani Bwire

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: kwa Mujibu wa Maelezo Yako, Ulipokea Taarifa za Uchunguzi wa Simu Kutoka Kwa Inspector Innocent Ndowo

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: na Ulipokea Taarifa hiyo kwa Kusaini Kitabu cha Makabidhiano

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Unaweza Kumwambia Mheshimiwa Jaji ikiwa Umekiwasilisha Mahakamani hapa Kitabu hicho

Shahidi: Sijawasilisha

Kiwhelo: Ni sahihi pia Ulipokea Simu Nane Kutoka Kwa Inspector Innocent Ndowo

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Ni kweli pia Unawasilisha Hati ya Makabidhiano Baina yako na Inspector Innocent Ndowo

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: kwa Mujibu Wa Maelezo Yako Unasema Kuwa Mheshimiwa Freeman Mbowe alikuwa akiwawezesha Watuhumiwa Kwa Fedha na Huduma Mbalimbali

Shahidi: Ni sahihi

Kiwhelo: Tuambie Huduma Mbalimbali ni zipi

Shahidi: Mtuhumiwa Freeman Mbowe ndiye aliyekuwa anawasafirisha, Kuwapatia Maradhi, huko walipokuwa Wanafika Moshi

Kiwhelo: Katika Maelezo Yako Unasema Kuwa Uchunguzi wa Cyber Unaonyesha Mheshimiwa Freeman Mbowe alikuwa anawaelekeza Watuhumiwa nini cha Kufanya, Je ni wapi tutaona hayo Maelekezo

Shahidi: Kwenye Maelezo ya Onyo ya Mshitakiwa

Kiwhelo: Ni sahihi Kwamba Jina la Mheshimiwa Mbowe halikuandikwa Katika Jalada la Kesi, Kwa sababu Kama Mngeandika angejua

Shahidi: Ni sahihi Kiwhelo: na Kama angejua angesitisha Mipango hiyo

Shahidi: Ndiyo

Kiwhelo: Kwani Shahidi Mtu akiwa anataka Kutenda Uhalifu, alafu akasitisha Kuna Tatizo

Shahidi: Hakuna Ila angeweza Kubadili Njia ya Kutenda uhalifu

Kiwhelo: Kwani Mheshimiwa Mbowe ana Mtoto Polisi

Shahidi: Hapana

Kiwhelo: Kwani ana Ndugu Jeshi la Polisi

Shahidi: Sifahamu

Kiwhelo: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwa namna gani Taarifa zingemfikia Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Kwa Kubadilishana Taarifa siyo Kwamba watavujisha

Kiwhelo: ni Kawaida Kwa Jeshi la Polisi Kuficha Majina ya Watuhumiwa

Shahidi: Ndiyo ni Kawaida

Kiwhelo: Ni Matukio gani Mengine ambayo Jeshi la Polisi Wanaficha Majina ya Watuhumiwa

Shahidi: Siwezi Kuongelea hapa

Kiwhelo: ila umesema ni Kawaida Yenu Kuficha Majina ya Watuhumiwa

Shahidi: Ndiyo

Kiwhelo: Ulisema Unafanya kazi Kitengo X

Shahidi: Ndiyo

Kiwhelo: Kwani Shahidi Kuna Makosa Mengine Makubwa ambayo unaona ni Hatarishi Kuya sema hapa

Shahidi: Yapo

Kiwhelo: Tuambie ni Mambo yapi zaidi ya haya Wanayoshtakiwa

Shahidi: Siwezi Kuya sema hapa

Kiwhelo: Mwambie Mheshimiwa Jaji basi Kama hutaki Kutuambia sisi

Shahidi: Siwezi Kusema hapa

Kiwhelo: Ulisema Kwamba Baada ya Kingai Kukupigia Mkutane Polisi Central, Ulisema huluwaona Watuhumiwa ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi, ila nilijua Wapo Central

Kiwhelo: Shahidi Katika Jalada ambalo Jina limefichwa, Nani alikuwa Mtuhumiwa

Shahidi: Freeman Aikael Mbowe

Kiwhelo: Jina lake lilikwepo kwenye Jalada?

Shahidi: Hapana, ila Mtuhumiwa ni Mbowe

Kiwhelo: Katika Maelezo Yako Ya Ushahidi Wako, Unasema Watuhumiwa Wamekiri Makosa yao

Shahidi: Ni sahihi, Baada ya Kusoma Maelezo Yao

Kiwhelo: Na Ulipo wapelekea Karatasi Nane, Walikula Talia kuwa ile Michoro na Maandishi siyo Ya kwetu

Shahidi: Ni sahihi Walikataa

Kiwhelo: Mtu aliyekiri anawezaje Kukataa wakati Wa Sampuli

Shahidi: Inategemea

Kiwhelo: Kwahiyo Katika Maandishi Yao Walikiri au Walikataa?

Shahidi: Mshitakiwa Wa kwanza alikataa, lakini baada ya Sampuli zake kwenda Kwa Mchunguzi Majibu ya Kawa ni Yeye

Kiwhelo: Asante Mheshimiwa Jaji, Ya Kwangu ni hayo tuh

Kibatala: Shahidi Tumeshawahi Kukutana Mimi na wewe Kwa Mara ya Kwanza Leo au Tumeshawahi Kufanya kazi pamoja

Shahidi: Sikumbuki Peter

Kibatala: Hakuna zoezi lolote la Kisheria tulifanya na wewe, Siyo Kwenye hii Kesi, Kuhusiana na Uchukuaji wa Vielelezo

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Wacha tuendelee, Shahidi Unakumbuka Wakati unazungumzia Kuhusu Kidaftari nilisimama Kwamba Mnafanya Zoezi siyo la Umuhimu sana, Baadae tukaambiwa tuache Muendelee

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwenye Process ya Kuku Sanya Data na Sample, Zilikuwa Processed na Baadae zikaenda kwa Expert

Shahidi: Siyo Mimi, Kidaftari kilikamatwa na Mtu Mwingine

Kibatala: Ni kweli Kwamba Sampuli za Mwandiko ulizo chukua ndiyo zilipelekwa kwa ajili ya Uchunguzi

Shahidi: Ni kweli Mimi ndiye niliye chukua Sampuli

Kibatala: Ulichukua Sampuli Kwa Maelekezo Ya Musa Nankaa au Maelekezo ya Ramadhan Kingai

Shahidi: Kwa Maelekezo ya Ramadhan Kingai

Kibatala: Unafahamu Kazi ya Kuchukua Sampuli ni Kazi ya Kisayansi

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Umesomea Mchakato Wa Uchukuaji Sampuli

Shahidi: Nimesomea Kibatala Wapi?

Shahidi: Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Kibatala: Kozi inaitwaje

Shahidi: DEVICE ID COURSE

Kibatala: Ilikuwa Module au ilikuwa ni Main Component

Shahidi: Mimi siyo Mchunguzi

Kibatala: Ndiyo Swali langu hapo sasa, Wewe ni Mtaalamu?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mimi Nimesomea Mambo ya Account for lawyers ila siwezi kujiita Mhasibu, Je Wewe ni Mtaalamu Shahidi: Siyo Mtaalam ila nimesomea

Kibatala: Unajua Maanaa ya Exemplar

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Maana ya Requested writing Sample au Requestes Exaplar

Shahidi: Fafanua hapo

Kibatala: Ni fafanue nini wakati hizo ni Terms za Kisayansi

Shahidi: Sifahamu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji sisi tunaona ni Haki Shahidi akiomba Ufafanuzi, Shahidi apewe Ufafanuzi, Tunaona ni Haki

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hakuna shida, Mbeleni akitaka nimfafanulie nitafanya

Kibatala: Wewe Kwa kuwa Unasema Kwamba umefundishwa namna ya Kuchukua Sample, Je unafahamu Kwamba Ikitokea Ubishani Juu ya Saini yangu, Moja ya Njia Moja wapo ni Kuniambia nilete Nyaraka zingine Zenye sahihi yangu hiyo ndiyo inaitwa Requested Exemplar

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Wakati Unachukua Sampuli kwa Khalfani Bwire, Ulikuwa unafahamu hilo

Shahidi: Nilikuwa nafahamu

Kibatala: Lakini nyie Mlichukua Requested Sample

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulimwambia Kwamba Pamoja na Sampuli zile Nane Mlichukua Nyaraka zingine za Khalfani Bwire

Shahidi: Nilisema

Kibatala: Mlichukua nini? Kitambulisho

Shahidi: Notebook

Kibatala: Kingai alikuwa anajua Kuhusu hiyo Notebook?

Shahidi: nataka Kufafanua

Kibatala: Sitaki Ufafanuzi, Jibu swali

Shahidi: alikuwa hafahamu

Kibatala: Je unafahamu a kwamba hiyo Notebook ni Mali ya Mtuhumiwa

Shahidi: Siyo Mali ya Mtuhumiwa

Kibatala: Hiyo Notebook alikamatwa nayo Nyumbani au Ulimkuta nayo Kituoni

Shahidi: Ninachofahamu ni kwamba Wali chukua Nyumbani Kwa Khalfani Bwire

Kibatala: Na nani alikukabidhi

Shahidi: Sarjent Johnson

Kibatala: Nikienda Katika Maelezo Ya Sarjent Johnson Nitaona kqambaalikikabi Notebook

Shahidi: Ndiyo Kibatala: Na Mlikabidhiana Kwa Utaratibu Upi

Shahidi: Wa Kipolisi

Kibatala: Na Hiyo Nyaraka ambayo Mlikabidhiana hiyo Diary, Ni Muhimu sana Kama Mtaleta hiyo Nyaraka

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji, Tutumie Neno Notebook kuepuka Confusion

Kibatala: Sawa, I apologize, Tutumie neno Notebook

Kibatala: Ni Nyaraka gani Ulionyesha Hapa Mahakamani Kwamba Mlikabidhiana

Shahidi: Sijaonyesha Mahakamani

Kibatala: Wakati Unamkabidhi Mtaalamu Wa Maandishi hiyo Notebook Ulimkabidhi kienyeji au Kwa Maandishi ya Kipolisi

Shahidi: Kwa Maandishi

Kibatala: Maandishi yapi, Mwambie Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Barua na Dispatch Book

Kibatala: Umetoa hapa Mahakamani hiyo Dispatch

Shahidi: Sijaonyesha

Kibatala: Umetoa Mahakamani hiyo Barua

Shahidi: Sijaonyesha

Kibatala: Turudi tena Katika Sampuli, Je unafahamu a kwamba Unapo chukua Sampuli Unatakiwa uchukue Sampuli katika Mazingira ambayo ni Strictly controlled Environment

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je, hayo Mazingira Uliyo yachukulia hizo Sampuli ni Strictly controlled Environment

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu Kwamba ili Ku Create Controlled Environment, ulitakiwa Umpeleke sehemu Nyingine

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Wewe Ulifanya hivyo

Shahidi: Ndiyo nilimuhamisha Kutoka Kituoni Kwemda Jengo la RCO

Kibatala: Majengo ya pale tunayafahamu Wote, Je zinafika Mita 100

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu a kwamba Mwandiko Wa Mtu unaweza Kubadirika Kutiana na Other factors Kama Psychology

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kwamba Ulichukua Mwandiko wa Mtu ambaye amefiwa na Mzazi unaweza Kuwa tofauti

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Mtu akipigwa na Kufungwa Pingu Mwandiko unakuwa tofauti

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Waandishi Wa Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi

Shahidi: Simfahamu yeyote

Kibatala: Unamfahamu Mwandishi Wa Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi anaitwa Garry Breath

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Garry Breath anashauri Kuwa Unapo chukua Sampuli za Maandishi Za Mtuhumiwa lazima Pawe na Mtu Mwingine Kushuhudia

Shahidi: Ndiyo Lakini siyo lazima

Kibatala: Kwani wewe na Garry Breath nani Mtaalamu Wa Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi

Shahidi: Mimi

Kibatala: Kwani Wewe una Certificate hata ya Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi

Shahidi: Sina

Kibatala: Unafahamu Kwamba Garry Breath ni Daktari Wa Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi anatumia Mpaka na FBI Mbali na Kuandika Vitabu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wewe Ulichukua Sampuli ngapi Kutoka kwa Bwire

Shahidi: Nane

Kibatala: Unafahamu kwamba inatakiwa uwe na Sampuli siyo Chini ya 15

Shahidi: Siyo Kweli

Kibatala: Kwani wewe Umepata wapi kuwa Sampuli Unatakiwa uchukue nane

Shahidi: Nilifundishwa Chuoni

Kibatala: Unafahamu Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi unashauriwa Uchukue Upper Case na Lower Case

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unatakiwa Uchukue alphabet, Panctuation Mark, na Namba

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Sasa si Ndiyo Upper case na Lower Case

Shahidi: Nilikuwa Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi inaendana na Sayansi ya INC DATING

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wala Ufahamu Kwamba INC DATING ni Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi Ilikujia Umri Wa wino tangu Maandishi yaandikwe

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je, unafahamu Kwamba kwetu sisi ni Muhimu Kujua Kama Michoro Khalfani Bwire alichora kabla ya Kukutana na Urio na Mbowe

Shahidi: Kwangu siyo Muhimu Kibatala: Kwani Kama Bwire alichora hiyo Michoro kabla ya Kukutana na Mbowe na Urio Je itahusiana na Kesi hii?

Shahidi: Inategemea

Kibatala: Inategemea nini

Shahidi: Unachokisema

Kibatala: Kama Bwire alichora Michoro kabla ya Kukutana na Mbowe na Urio itahusiana na Kesi hii?

Shahidi: Siwezi Kujibia Kibatala: Unaposema huwezi Kujibia ni Kwamba hutaki au hujui Shahidi: Basi rudia Swali

Kibatala: Kama Bwire alichora hiyo Michoro Tarehe 5 May 2020 Je, Kidaftari hicho kitakuwa na Umuhimu katika hii Kesi Shahidi' Hakitakuwa na Umuhimu

Shahidi: Na Bado Unasisitiza Kwamba Kwako Umuhimu ilikuwa siyo kimechorwa lini au Kimechorwa na nani

Shahidi: Umuhimu ilikuwa Kujua kimechorwa na nani

Kibatala: Je, unafahamu Maana ya Confirmation Bias?

Shahidi: Fafanua

Kibatala: Ni hali ya mtu Kufanya Upelelezi akiwa na Dhana yake Kichwani, Ili Kuthibitisha anachokiwaza yeye

Kibatala: Sasa Unafahamu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: huoni Kwamba Inawezekana Kilichorwa siku za Nyuma

Shahidi: Kama Kingekuwa na Nia Njema asingekataa

Kibatala: Unafahamu Kwenye Sayansi ya Upelelezi Maana ya Tool Elevation

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni hali ambayo unachungulia Dirishani au Mlangoni, Kisha Unakuja Kusema Umeona Kuna TV na unaacha Kusema Vingine Ulivyoviona Kama Vile Kabati, Meza na Redio

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mheshimiwa Jaji, Kama shahidi amesema Kwamba hafahamu Kuhusu Tool Elevation, Sasa ni Vizuri kabla hajauliza swali ahakikishe shahidi Kaelewa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji nimepokea Maombi ya Hisani nitafanya

Kibatala: Je, Shahidi Unafahamu Kwamba Katika Sayansi ya Uchunguzi na Upelelezi Wamekatazwa Kufanya Tool Elevation

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Shahidi nimesikia Unasema Kwamba Katika Shauri hili Mlalamikaji ni DCI

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: lakini huyo DCI ni Boss wa

Ramadhan Kingai
Boss wa Inspector Ndowo
Boss wa Inspector Mahita
Boss wa Inspector Swila
Boss wa Jumanne Malangahe
Boss wa DC Goodluck
Boss wa koplo Hafidh
Boss wa Sajenti Nuru

Wote ndiyo wapelelezi na ndiyo mashahidi

Shahidi: Ni sahihi lakini Kuna Vitengo tofauti

Kibatala: Kwani Hao Wa Vitengo Tofauti Hawapo Chini ya DCI

Shahidi: Ni Boss wao

Kibatala: Wakati huo Deputy DCI Alikuwa nani

Shahidi: alikuwa CHARLES KENYELA

Kibatala: DCI kama Yeye alikuwa Ndiye Mlalamikaji, asingemuachia Deputy DCI apeleleze

Shahidi: Si Kweli

Kibatala: Je, RPC akiwa anakutuhumu wewe, Anaruhusiwa Kukupeleleza?

Shahidi: Hairuhusiwi

Kibatala: Kwanini hairuhusiwi

Shahidi: Ni Utaratibu tu wa kazi

Kibatala: Order iliyotoka Kwa DCI unaweza Kui' Challenge

Shahidi: Inategemea

Kibatala: DCI alikupigia Su ufungue Jalada la Ugaidi, Unaweza Kumbishia

Shahidi: kama lipo sahihi nafungua

Kibatala: Kwani Wewe Wakati Unapewa Taarifa Ufungue Jalada la Kesi ya Ugaidi, Ulikuwa na Material gani Mbele yako

Shahidi: Uwepo wa Taarifa

Kibatala: Kwani hiyo Taarifa Ulipokea Wewe

Shahidi: Alipokea Afande Boazi

Kibatala: Mpaka Wakati huo Ulikuwa Umeomgea na Luten Urio au Ilikuwa bado

Shahidi: Ilikuwa bado

Kibatala: kwa hiyo wewe ulifungua sababu ya hear say

Shahidi: Taarifa zilikwepo

Kibatala: Tunataka Kujua Ulipokea Amri au Ulifanya Kazi kama Independent Detective, Je Wakati unafungua Faili ulikuwa Umeshamuhoji na a Kuandika Maelezo ya Afande Boazi

Shahidi: Ilikuwa Bado

Kibatala: Tunakubaliana Wakati wanaongea Urio na Mlalamikaji Afande Boazi wewe hukuwepo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na wewe bado Unasisitiza Kwamba Ulikuwa na Material Wakati unafungua Jalada la Kesi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu a Maana ya Hear say

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Ni sahihi Kwamba wewe Ulifanyia Kazi Hear Say

Shahidi: Ni Hear Say

Shahidi: Mheshimiwa jaji naomba niende washroom (chooni)

Shahidi amerejea

Kibatala: Shahidi tuliishia pale kwamba Yale uliyofungulia Kesi ni hear say

Kibatala: Je aliyekuwa Incharge Wa Upelelezi Wa Kesi hii yote alikuwa huyo huyo ROBERT BOAZ

Kibatala: Je Maelekezo na Taarifa zote Kuhusu Upelelezi Yalikuwa Yanatoka Kwa Robert Boaz

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je Mtu huyo hana Maswahi Binafsi

Shahidi: Hana Maslahi Binafsi

Kibatala: Unafahamu Maslahi Binafsi na Viashiria Vyake

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Na hapa huvioni

Shahidi: Sivioni

Kibatala: Pride, Intergrity, Dignity ya DCI inajadiliwa katika kesi hii

Shahidi: Kinachojadiliwa hapa ni Kesi

Kibatala: Kwani nani alipokea Taarifa akaona Kwamba hapa Kuna Kosa la Ugaidi

Shahidi: DCI Robert Boaz

Kibatala: Unaona Hakuna Maslahi Binafsi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Wewe ulifungua Jalada Siku ya Tarehe 18 July 2020

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni kweli Kwamba ulifungua Jalada bila kuwa na Maelezo ya Robert Boaz

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Uliona Maelezo ya Robert Boaz Tarehe 13 August 2020 kuwa ameandika Chini ya Kifungu cha 3(3) cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Shahidi: Naomba Kuona (Ndiyo)

Kibatala: Unafahamu kwa Mujibu Wa Sheria, Askari anayepokea Taarifa Kwa Mdomo au Kwa Maandishi anatakiwa arekodi kwa Maandishi haraka sana

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Je unataka Kuniambia Kuwa Unaweza Kupokea Taarifa Kwa Mtoa Taarifa, Unaweza Kufungua Faili la Kesi bila Kuwa na Maelezo ya Mlalamikaji

Shahidi: Kama anaye Fungua Kesi ni Raia lazima Uchukue Maelezo, ila Kama Kwa Polisi Maelezo siyo lazima

Shahidi kapewa PGO

Kibatala: Tafuta sehemu inayosema Kwamba Taarifa Hii urekodi Mapema Sana na Taarifa Fulani siyo lazima

Shahidi: Nimekwambia Sikumbuki

Kibatala: Take your time (chukua muda wako) nimekuombea PGO hapo

Shahidi ANAPEKUA PGO

Shahidi: Kwenye PGO sioni mimi

Kibatala: Sasa nakuonyesha Kile Kifungu cha 10 (3) cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai Shahidi amesogezewa Laptop baada ya Mawakili wa Serikali kuihakiki laptop

Shahidi ANASOMA

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Unafahamu Maana hicho Kifungu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Maana yake

Shahidi: Kwamba Askari Polisi ambaye anapokea Taarifa, ataandika Maelezo ya Mtoa Taarifa yoyote

Kibatala: Sheria imeweka Utofauti?

Shahidi: Haijaweka

Kibatala: Haya taja Sasa Mwongozo ambao unakuruhusu Kutoandika Maelezo Ya Mlalamikaji kama Polisi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Sasa Mbona Ulisema Kuna Mwongozo, Lengo lako lilikuwa nini

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Haya nisionekane na Kuharass, Je Maelezo Ya Robert Boaz Uliandika lini

Shahidi: Tarehe 13 October 2020

Kibatala: Ni baada ya Miezi Mingapi

Shahidi: Miezi Mitatu

Kibatala: Bado Mnataka tusione Kuwa Kesi ni ya Kutunga

Kibatala: Haya Maelezo Ya Mtoa Taarifa umeandika lini

Shahidi: Tarehe 11 August 2020

Kibatala: Muda gani Umepita

Shahidi: Wiki Mbili

Kibatala: Kutoka Tarehe 18 July 2020 Mpaka 11 August 2020 ni Wiki Mbili

Shahidi: Ni Wiki 3

Kibatala: kwa hiyo tangu ufungue Faili hata Maelezo Ya Mtoa Taarifa ulichukua baada ya Wiki Tatu, kwanini tusiamini Mlimkamata Luten Denis Urio Mkampiga baada ya kutajwa na Adamoo kisha Mkampa Dili la kuwa Shahidi

Shahidi: Si kweli

Kibatala: Ulisema Kwamba ulifungua P. E file

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, Faili la P.E ulilipa Kosa gani

Shahidi: Lile Jalada ni Jalada la Uchunguzi

(Shahidi anaongea)

Kibatala: Ukimaliza Kuongea Mambo yako Jibu swali Langu Jalada la P.E Uliandika Kosa au halikuwa na Kosa

Shahidi: Jalada la P. E halikuwa limeandikwa Kosa

Kibatala: Wewe Tarehe 14 Kwamba Robert Boaz amekutana na Denis Urio umeitoa Wapi

Shahidi: Nilipata Kwenye Kikaratasi alichonipa Kingai

Kibatala: Kwahiyo Kingai ndiye Kakwambia? Maana Kingai alikuwa katika Kikao cha Robert Boaz na Urio

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Kwanini sasa Robert Boaz katika Maelezo Yake Hakuna Sehemu aliyoitaja Tarehe 14, angalia Maelezo hayo hapo

Shahidi: Hakutaja

Kibatala: Tafuta kwa Kingai Kama alitaja hiyo Tarehe 14

Shahidi: Hajataja

Kibatala: Kingai aliandika lini Maelezo Yake

Shahidi: Tarehe 28 June 2021 Kibatala: Nikisema hiyo Tarehe 14 mmebuni baada ya Sisi Kumuhoji Luteni Denis Urio

Shahidi: Si Kweli, Mimi Ndiye nilifungua faili

Kibatala: Kipi Ulicho Kifanya wewe Kama Mpelelezi Mpaka Tarehe 18 July 2020 Mpaka Ukapandisha Status ya Faili

Shahidi: Kingai alinielekeza nifanye hivyo

Kibatala: kwa hiyo Hakuna Ulicho fanya wewe cha Kupandisha Kupandisha Status ya Faili, zaidi ya Kingai

Shahidi: Ndiyo ilikuwa ni Maelezo ya Kingai

Kibatala: Kwa hiyo Mpaka Unapandisha Status ya Faili Kitoka Kwa Kingai ulikuwa Unawa Jua hao Wakina Khalfani Bwire

Shahidi: Hapana nilikuwa siwafahamu

Kibatala: Je, unafahamu Kwamba Urio na wenzake Kwa Mara ya Kwanza Walikutana Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Ndiyo nafahamu lakini palikuwa na Mawasiliano

Kibatala: Ilikuwa ni Personal Knowledge au Mambo ya Hear say

Shahidi: Ilikuwa ni Hearsay

Kibatala: Na kama siyo hear Say tuambie hapa Denis Urio aliongea kwa mara ya Kwanza na Bwire au Lijenje

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Umeshawahi Kuona Mawasiliano ya Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Shahidi: Kupitia Maelezo ya Onyo

Kibatala: Kwa Maana hiyo unamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mawasiliano ya Urio, Bwire na Lijenje ni Maelezo ya Onyo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nini kilisababisha ukapandisha hadhi ya Faili

Shahidi: Niliambiwa na Kingai nifanye hivyo

Kibatala: Ulisema Kwamba Moja wapo ya sababu ya Kuto weka Jina la Mbowe Mlikuwa mnaogopa Leakage, Je Wakati Mnafungua Faili Kingai aliwaambia Kuwa Kuna tuhuma Za Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nani kati yenu aliye amua kuwa kuna tuhuma Za Ugaidi, Ni wewe au Kingai

Shahidi: Siyo Mimi

Kibatala: Ni lini baada ya Kufungua, Uliform Professional Opinion zako Ukaona Kwamba hapa Kuna tuhuma Za Ugaidi

Shahidi: Baada ya Kumuhoji Luten Denis Urio

Kibatala: Unasema Kwamba wewe ulikuwa Katika Kitengo X. Je, Ulimwambia Jaji Kwamba Wewe na Kingai Mlikaa Ofisi gani

Shahidi: Sikumbuki Kibatala Mimi nikisema hukusema Je utakataa

Shahidi: Sikumbuki

Shahidi: Tarehe 27 July 2020 Nilipokea Faili kutoka kwa DCI Nikampigia Simu Kwamba Jalada hili Mimi na wewe tumepangiwa, na Mimi Ni Msaidizi wako

Kibatala: Je ni Protocol ya Kawaida Faili Kutoka kwa Junior Officer Kwenda Kwa Superior Wako

Shahidi: Ni Jambo la Kawaida

Kibatala: Tarehe ngapi mliamua Kuwa Msiweke Jina la Freeman Mbowe Katika faili

Shahidi: Tarehe 18/7 Kibatala: kwenye Jalada la P. E Jina la Mbowe lilikuwepo

Shahidi: Lilikuwepo

Kibatala: Wakati huo Denis Urio alikuwa anafahamu tayari Kwamba Mbowe ni Mtuhumiwa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Denis Urio alikuwa anaishi Wapi Wakati huo

Shahidi: Morogoro

Kibatala: Je, Denis Urio anakiapo cha Jeshi la Polisi

Shahidi: Hapana lakini ni Askari Wa JWTZ

Kibatala: Je, Denis Urio Mlimuapisha asitoe siri

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Denis Urio alikutana na Moses Lijenje na Khalfani Bwire kawaambia Mnaenda kwa Freeman Mbowe akiwashawishi Mambo ya Uhalifu Mniambie

Shahidi: Mimi sikuupata nafasi Kuongea naye

Kibatala: Je unaona Dhana yako ya Usiri bado upo Wakati Kingai tayari ameshaongea na Watu zaidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je, unafahamu Kwamba Katika Kikosi cha Ramadhan Kingai, Gari yao Ilikuwa na Dereva wa Cheo Cha Chini anaitwa Azizi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je, unafahamu Kwamba Watuhumiwa Walikamatwa na Kupelekwa Kituo cha Polisi Moshi

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Watuhumiwa Walienda Kituo cha Polisi Mbweni, Je bado Kuna sababu ya Usiri

Shahidi: Watuhumiwa walikuwa wameshakamatwa

Kibatala: Freeman Mbowe alikuwa amekamatwa?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa ni Freeman Mbowe Mpumbavu kiasi gani kiasi Magaidi wake Wamekamatwa halafu yeye awe Mtaani

Shahidi: Jukumu letu lilikuwa Kuzuia Uhalifu usitendeke

Kibatala: Unafahamu tofauti ya Kulipua Vituo Vya Mafuta na Kuchoma Kituo cha Mafuta

Shahidi: Ni Mambo Mawili Tofauti

Kibatala: Wewe Ulikuwa na Maelezo ya Mashahidi ya Washitakiwa, Kwamba Kosa lilikuwa ni Kulipua Vituo Vya Mafuta na Kuchoma Masoko

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Lakini Robert Boaz anasema Kwamba Ilikuwa ni Kuchoma Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Lakini haibadilishi Kitu

Kibatala: Haibadilishi Kitu wakati umeshasema ni Mambo Mawili tofauti

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Na Kingai na Denis Urio Wanasema Kulipua Vituo Vya Mafuta, Je Mpaka hapo Kuna Sehemu Mtu kazumgumzi Kuchoma Moto Masoko

Shahidi: Hakuna sehemu ambayo wamesema Watachoma Masoko

Kibatala: Sasa Wewe Taarifa ya Kuchoma Moto Masoko ulitoa Wapi

Shahidi: Ni Terminology tuh

Kibatala: Mwanzoni si umesema Kwamba ni Tofauti, Ila sasa hivi no Terminology tu

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Haya Kwa Jumanne Malangahe anasema Kuchoma Moto Vituo Vya Mafuta na Kulipua Mikusanyiko ya watu

Shahidi: Tuone

Kibatala: SOMA HAPA

Shahidi ANASOMA "Kuchoma Vituo Vya Kuuzia Mafuta na a Kulipua Mikusanyiko ya watu"

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Jumanne anasema Kulipua Masoko

Shahidi: Hakuna sehemu Imeandikwa Kulipua Masoko

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Unasema Moja ya Source zako

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tulikuwa tunajadiliana na Wenzangu hapa, lakini Kuanzia pale alipoenda Kwa Boaz, URIO na Sasa Kwa Shahidi Mwenyewe Sisi Kwa Shahidi Mwenyewe hatuna Tatizo,Mahakama Inakuwa sehemu Ngumu sababu Wale wengine Wameshatoa Ushahidi Wao, Kama wanataka Kuingiza Maelezo Yale, Ilitakiwa Iwe Kwa Wale Mashahidi Kwa Mujibu wa Kifungu 164 cha Sheria ya Ushahidi limeweka Masharti

Sisi tunaona Kwamba Kile Kinachoingia katika Ushahidi, kinaingia Kinyume na Utaratibu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima na Tahadhima, Wao Wenyewe walikuwa wanazungumzia Kidaftari ambacho Hakipo Mahakamani, Kuwa na Usawa Pili kamw hakusimama wakati huo, Basi Kuna Estoppel Hawezi Kuja sasa Kuomba Mahakama Ifute Ushahidi Kwa kazi ambayo hatujaisaidia

Tatu ni kwamba nauliza Kutokana na Majibu wa shahidi Mwenyewe Labda Kama Nita uliza Maswali ambayo hayapo, Hii ni Cross examination Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.

Jaji: Wakati Wakili anauliza Maswali Kuhusu eneo hilo shahidi aliomba Ruhusiwe Kurejea, ili aweze Kujibu Kwa namna ambavyo ameuliza ameuliza akiwa anarejea, na Shahidi amejibu Maswali hayo kwa namna ambavyo alikuwa anarejeshwa na Upande wa Utetezi

Kwa namna ambavyo ameuliza ameuliza akiwa anarejea, na Shahidi amejibu Maswali hayo kwa namna ambavyo alikuwa anarejeshwa na Upande wa Utetezi Ni kweli Nyaraka hazipo Katika Kumbukumbu za Mahakama

Katika Mazingira hayo Mahakama Inaona Kwa nma hiyo Maswali ambayo yameulizwa na Kujibia hayawezi Kuondolewa

Jaji: Mahakama Inaelekeza Wakili wa utetezi (Peter Kibatala) aendelee Kuuliza Maswali.. NATOA AMRI

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Kibatala: Katika Maelezo Yako umeona kuwa Hakuna Kulipua Mikusanyiko ya watu

Shahidi: Ni sahihi, Kwenye Maelezo siwezi Kuandika Kila Kitu

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwenye Maelezo uwezi Kuandika Kila Kitu

Shahidi: Hapana

Kibatala: Katika Maelezo Yako Hakuna Tarehe 14 July 2020 Kama sehemu ya Kufanya Majukumu yako

Shahidi: Ni kweli Hakuna

Kibatala: Ni kweli Shahidi Statement Yako Umerekodi wa Mapema Sana Kuliko Ushahidi Wa Leo hapo Kizimbani

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ni Saa Saba na Dakika 5 naomba Kutoa Hoja tuairishe, nikirudi tuweze Kuendelea na Maswali ya Shahidi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: natoa airisho Mpaka Saa 7 na Dakika 45

Jaji anatoka (1:06 PM)

Jaji amerejea Mahakamani (2:31 PM)


Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile na tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na Mimi sijaarifiwa formally Kwamba Kuna Mtu kaondoka Kuna Kuchelewa tu baadhi yetu, Kwa hiyo tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Hisani ya Mahakama na faida ya Shahidi Naomba Nikumbushwe Jibu letu la Mwisho

Jaji: Kabla ya Kufungua Jalada

Kibatala: Shahidi Nakuonyesha Maelezo Yako hapa Baada ya Kufungua Jalada

Shahidi: Baada ya Kufungua Jalada hilo Afande DCI Robert Boaz alinitaka Mimi Kuwa Mpelelezi Wa Shauri hilo, Baada ya Kupewa Jukumu hilo nilianza Kuandika Maelezo Mbalimbali ikiwemo Denis Urio

Kibatala: Je, Katika Maelezo hayo uliyoyasoma, Kuna Mahala Popote panapo onyesha wewe Ulikuwa Msaidizi Wa Kingai au Kingai Kushirikiana na wewe

Shahidi: Huko sijaandika

Kibatala: Unaendelea kwa Kusema Kuwa Baada ya hapo Uliendelea na Hatua Mbalimbali Ikiwemo Kupeleka Silaha aina ya Pistol A5340 na Risasi tatu ambapo Nilichukua na Kurudisha kwa Sarjent Nuru kwa Kutumia Exhibit Register namba 19/2020

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Hii Exhibit Register ni Mnyororo Wa Kipolisi Kwa ajili ya Kutunza Kielelezo

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Katika Kuonyesha aka ulipokea Kutoka Kwa Sarjent Nuru wewe ulisaini na Yeye akaweka Particular zake

Shahidi: Niliandika Majina na Yeye aKaandika Majina

Kibatala: Hata Tarehe na Muda Tutaona huko

Shahidi: sahihi

Kibatala: Ulitoa Kama Kielelezo Exhibit Register 19/2020 Mahakamani

Shahidi: Sijatoa

Kibatala: Kuondoa Mashaka, Exhibit Register tunayozungumzia ni hii ambayo ina zungumzia Bastola ambayo Umeitambua hapa Mahakamani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwanini Ujaleta

Shahidi: Sikuongozwa Kuleta

Kibatala: Na hii Exhibit Register ni ya Muhimu au Siyo Muhimu

Shahidi: Ni ya Muhimu

Kibatala: Kwa Vyote Vyote Hakuna Mahala ambapo Umeitambua ile Bastola kwa Maneno CZ 100 CALIBRE kutoka Mdomoni Kwako

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni Kwa sababu ile Bastola Ilikamatwa Mahala fulani, I kafika kwa Sarjent Nuru Kupitia Kwa DC Goodluck, Ile Bastola ya Luger A5340 ulitambua Kutoka Kwenye Mlolongo huo

Shahidi: Pamoja na Kuiangalia Silaha yenyewe

Kibatala: zile Risasi Pia Unafahamu Kwamba Kila Risasi Moja Inavitambulisho Vyake Ikiwemo Callibre

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nimeomba wanipatie Bastola na Risasi zake

Kibatala: Bwana Sébastien Madembwe ambaye ni Registar (Mrajisi) wa Silaha, Je Katika Barua Yako Kwenda Kwake ulitaja zile Taarifa za Ziada za CZ 100 CALIBRE

Shahidi: Haikuonyesha

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Kama Mtu atakuwa anaichunguza Kwa Nje hiyo Bastola ataona Maandishi Ya CZ 100 CALIBRE

Kibatala: Je Kuna Mahala Popote umeona Maandishi Ya CZ 100 CALIBRE

Shahidi: Ndiyo Yapo

Kibatala: Na wewe unasema Ulipokabidhiwa Bastola hiyo uliikagua

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ulipokagua Hayo Maandishi Uliyaona au hukuyaona

Shahidi: Niliyaona

Kibatala: Vipi Kuhusu Katika Maelezo Yako, Uliyataja hayo Maneno

Shahidi: Siku yataja

Kibatala: Wakati Unamkabidhi Sarjent Nuru Ulimtajia au hukumtajia

Shahidi: Sikumtajia

Kibatala: Je, anaruhusiwa Kuongeza Taarifa za Ziada

Shahidi: Ndiyo anaruhusiwa

Kibatala: Silaha alikabidhiwa Sajenti Nuru na DC Goodluck, wewe Ukaichukua na Kurudisha Kwa Hati, Swali Je Entry inatakiwa iwe Kama ambavyo Mlikabidhiana au Kutofautiana

Shahidi: Inaweza Kutofautiana

Kibatala: Je, hayo Maneno ya CZ100 CALIBRE ni sehemu ya Utambulisho au Mapambo

Shahidi: Ni sehemu ya Utambulisho

Kibatala: kwa Ruhusa Ya Mahakama Nakuonyesha Kielelezo namba P5 na P4, Hiyo ni Live Catridge, Je Chini yake Kuna namba za Callibre au Hakuna

Shahidi: zipo

Kibatala: Msomee Mheshimiwa Jaji tafadhali

Shahidi: Ni 9mm

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Samahani ninachojua katika Risasi ni palikuwa na Live ammunition, Yeye anatumia Live Catridge

Kibatala: Shahidi Wacha tutumie Neno la Kaka Yangu la Live ammunition

Kibatala: Soma tena Shahidi: 9mm

Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Wako Ulieleza Discription Yake hiyo live Ammunition Kuwa ni 9mm

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Katika Maelezo Yako Ulizungumzia Swala la Kutoa kwa Ballistic ukamkabidhi Sarjent Nuru

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Wakili Mwenzetu Peter Kibatala, alikuwa anaulizia Kuhusu Kupeleka Kwa Mrajisi, As Opposed Kwa Uchunguzi Wa Mlipuko

Kibatala: Wacha nirudie swali Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Shahidi Umeandika Maelezo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, Ulirekodi Tukio la Makabidhiano ya Bunduki na Risasi Baina yako wewe na Sarjent Nuru, Je hiyo Risasi ambayo ipo hai Ulitaja?

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Unaweza Kufahamu Kwanini waliotengeneza hiyo Risasi Waliandika Kwa sababu gani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Mwambie Mhe Jaji Kuwa Maana yake ni nini

Shahidi: Ni Risasi zinazotumika na Bastola (Ukubwa Wa Risasi)

Kibatala: Sawa na kupa sasa na Kielelezo namba P 5, Tafadhali na Zenyewe ziangalie katika Kitako

Kibatala: Anza ya Kwanza, je inamaandishi tambulishi au haina?

Shahidi: Sioni vizuri

Kibatala: Yapo au hayapo lakini

Shahidi: Kuna maandishi

Kibatala: na Unakumbuka upo chini ya Kiapo

Shahidi: Ni sahihi Kibatala Kwamba wewe huoni hapo Neno 9mm Luger PMP. Kama huoni nikuombee Umuonyeshe Jaji, Sababu Chini ya Uangalizi Wake wewe Ndiye Uliapishwa

Shahidi: Nimeyaona

Kibatala: Yanafanana au Yanatofautiana na Maneno Yaliyopo Katika Kielelezo P 4

Shahidi: Ni tofauti

Kibatala: Maneno PMP katika hiyo live Ammunition yanafanana?

Shahidi: Yanatofautiana

Kibatala: Maneno Luger yanafanana?

Shahidi: Kwa Maneno hayo zinatofautiana

Kibatala: Wewe ndiye Uliye Mkabidhi Sarjent Nuru, Je Ulifafanua Kwa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Unafahamu sisi tunatakiwa kulinganisha hizo Risasi ili tujue kama Kweli zilikamatwa kwa Adamoo au Zilikuwa Planted

Shahidi: Siyo Muhimu Kwa upande wa Risasi

Kibatala: Nenda Kwenye hiyo ganda la Risasi

Shahidi:
Kinachoonekana hapa ni 9mm Mengine hayasomeki

Kibatala: kwa Ushahidi Wako huoni Maneno GEKO hapa

Shahidi: Maneno Yapo ila siwezi Kuyasoma

Kibatala: Ngoja Jaji aandike Kwamba Maneno Yapo ila siwezi Kuya Soma

Kibatala: Hizo Spent Ammunition Mbili zinafanama au zinatofautiana

Shahidi: Zinatofautiana

Kibatala: Ulifafanua tofauti Hiyo ya Muhimu kwetu

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Katika Conclusion Zako unasema Ushahidi Mwingine ni Watuhumiwa hao watatu Kukutwa na Silaha na Risasi Tatu Jambo linalo onyesha kweli Walikuwa Wanapanga Uhalifu

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sehemu gani Ambayo Tutaona Kuna tofauti

Shahidi: Kwenye maelezo yangu utaona

Kibatala: Unakumbuka shahidi awali Nilikuuliza Duty yako Unapokutana na Eliminative Evidence Unatakiwa Kuitambua

Shahidi: Fafanua

Kibatala: Unatakiwa Uende Katika Upelelezi Ukiwa Unaenda na Majibu yako

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Ni Wapi tutaona Ukishughulika na tofauti hizo

Shahidi: Tofauti haiondoi zana ya Kwamba Walikamatwa na Silaha

Kibatala: Jibu swali Langu

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Jana ulimtaja Coplo Charles Kumpa Simu 8

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwa Ufahamu Wako wewe Mtu Muhimu Katika Kuonyesha Chain Of Custody na Kupokea Simu zako, Je Katika Kesi hii kwa ufahamu ametajwa Ka Shahidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Nilikuuliza Exhibit Register 251/2021

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Je hiyo Exhibit Register Ilikuwa Mnajaza Kama Mapambo au zoezi la Kisheria

Shahidi: Ni zoezi la Kisheria

Kibatala: Mliandika Katika Exhibit Register hiyo zile CID namba

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kumbe ni nyaraka Moja ya Muhimu sana

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Je Riport Ya Uchunguzi, pamoja na Extraction Riport Mliandika Katika Exhibit Register

Shahidi: Hiyo Sikukabidhi

Kibatala: Je, Ulimwambia Jaji Kwamba Kwanini Hukuleta Mahakamani

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je hii Exhibit Register ni ya Muhimu au Siyo Muhimu

Shahidi: Ni ya Muhimu Katika Utunzaji Wa Vielelezo

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Unasema Kwamba Mtuhumiwa Freeman Mbowe ndiye aliyeanzisha Mchkato wa Kuwatafuta Makomandoo Wa Zamani, Je, Kwa Uthibitisho Upi

Shahidi: Ni Luten Denis Urio ndiyo alisema hivyo

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kwamba ilitupime hili lazima tuangalie Ushahidi Wa Denis Urio na tupime

Shahidi: Na Kwa Kuwakamata wale Watuhumiwa Wanne

Kibatala: Kwani Uliwakamata wewe

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba shahidi apewe muda wa kujibu, maana anajibu hili anaulizwa hili, hajatulia, anaulizwa hili, hajajibu hili anaulizwa hili.. Apewe muda wa kujibu.

Kibatala: Wewe Ulifanya nini zaidi Ya Maneno Ya Denis Urio

Shahidi: Nilifanya Uchunguzi, nikampelela Faili Ngazi ya Juu, Na Mashahidi Kama Justine Kaaya ambapo alisema katika Ushahidi Wake Mtuhumiwa Freeman Mbowe alikuwa anataka Taarifa Bila yeye Kujua ni za nini

Kibatala: Kama Nimeeleza Vizuri ni, Transactions Za Mbowe na Urio, Maelezo ya Urio na Kaaya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Tuanze na Justine Elia Kaaya, Si Alikuwa Mshtakiwa Katika hii Kesi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Alipokamatwa Unafahamu Kwamba aliandikwa Maelezo yake na Jumanne

Shahidi: Siyo Sahihi

Shahidi: Sijui lakini ni Huko huko Arusha

Shahidi: Sijui lakini ni Huko huko Arusha

Kibatala: Lakini Maelezo ya Kaaya Uliyaona

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Maelezo Ya Justine Kaaya Yapo wapi ili tuweze Kuyalinganisha katika yale Ya onyo na Yale Ya Ushahidi

Shahidi: Hayapo Mahakamani

Kibatala: Kama Maelezo Ya Kaaya Yangekuwepo Mahakamani Kama Kielelezo, Tungepata nafasi ya Kuyalinganisha au tusingepata

Shahidi: Hayawezi Kufanana, ila yale Mambo ya Msingi Yanafanana

Kibatala: na hamkuona Umuhimu wa Kuyaleta ili tuone aliachiwa Kwa Ahadi Ya Kuwa Shahidi au aliachiwa kwa sababu Upelelezi umekamilika

Shahidi: Hatukuona Umuhimu

Kibatala: Kama Maelezo Ya Kaaya Yangekwepo Mahakamani Kama Kielelezo, Tungepata nafasi ya Kuyalinganisha au tusingepata

Shahidi: Hakuna hiyo nafasi ya kuyaleta

Kibatala: Narudia tena, Kama Maelezo Ya Kaaya Yangekuwepo Mahakamani Kama Kielelezo, Tungepata nafasi ya Kuyalinganisha au tusingepata

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hilo swali Halipo, Kaaya siyo Mshtakiwa ni Shahidi, Sasa Maelezo Yake yangetoka wapi?

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ukinielekeza nitaenda pengine, ila Swali langu halijajibiwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mheshimiwa Jaji Wakili anauliza Kitu ambacho Shahidi amesha Sema kuwa hakurekodi yeye Maelezo ya Kaaya

Hakuna Namna yoyote Kwenye Procedure au Sheria ambayo wangeweza Kuyaleta

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hakuna Hoja hapo, ni Maoni yake Binafsi tu, Ndiyo Maana Hajataja Sheria Wala Kesi Mbayo ameitumia

Jaji: nimesikia Hoja ambayo Upande Wa Mashtaka Wameleta, Ni kweli Unasema Kwamba Wakili anauliza swali Kuhusu Mtu ambaye ni Shahidi ambaye alikuwa Mshitakiwa Ni wazi Kwamba Maelezo yake ya Onyo Hakuna Namna ambayo yangeweza Kuja Mahakamani

Kwa sababu Wakili ameuliza kwa Haki ya Mteja wake, Wakili yupo Kwenye Cross Examination, Mahakama Inaona kwamba itaona Mbeleni Kama yatakuwa na Back up, Na Itafanya Maamuzi yake

Kwa Mahakama Inaona Kwa Maana hiyo Wakili aendelee Kuuliza Maswali. NATOA AMRI

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Kibatala: Kaaya aliyasema Katika Maelezo Ya 30 July 2021 wewe Kama Mpelelezi Uli Verify Vipi Maelezo Ya Kaaya

Shahidi: Kupitia Maelezo Ya Onyo Washitakiwa, wa Kwanza Pili na watatu

Kibatala: Maelezo ya Mshitakiwa Wa Kwanza hayapo Mahakamani, Ila Kwa Ushahidi Wako ni Kwamba Nikiomba Maelezo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya nitaona Wanasema Walikaa Kikao na Kaaya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P1 (Maelezo Ya Onyo ya Adam Kasekwa) Kibatala Shahidi mimepewa Maelezo ya Onyo ya Adam Kasekwa, Nitafutie Mstari unaosema Kwamba palikuwa na Kikao Kilicho fanyika Adamoo, Ling'wenya, Bwire na Pengine Mbowe

Shahidi: Nimeona Kibatala Soma kwa Sauti Shahidi Mnamo Tarehe 1 August 2020 Saa 11 Alfajiri alituita na Kutuonyesha picha ya Lengai Ole Sabaya

Kibatala: Swali langu umesema Maelezo Yako Kwamba Nikisoma hapo Kwenye Maelezo ya Adamoo anakiri alikaa Kikao na Justine Elia Kaaya

Shahidi: hicho kikao ndiyo walikaa

Kibatala: Nataka unisomee majina

Shahidi: Mimi Ndiyo nishasoma Sasa (anamuonyesha Karatasi Kibatala achukue)

Kibatala: Sasa huo ni Ujeuri, Naona utaki tena tuendelee Kuulizana Maswali Kirafiki

Shahidi: Hakuna Majina yao humu

Kibatala: Kaaya katajwa humo

Shahidi: ajatajwa

Kibatala: Ling'wenya katajwa

Shahidi: hajatajwa

Kibatala: Bwire lilikuwepo?

Shahidi: Nimeona hapa Tarehe 25 August 2020 kwamba Walikutana

Kibatala: Sasa Tarehe 01 August 2020 ndiyo Tarehe 25 August 2020

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa Je, na hapo Kaaya katajwa

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mahala Pengine ambapo Ulisema Kwamba ulipata Taarifa hizo ni Maelezo ya Ling'wenya

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Chukua Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya Nitafutie Mahala Ling'wenya amekiri Kwamba alikaa Kikao yeye, Adamoo, Mbowe na Kaaya, Hata Kama na Bwire pia ni sawa tu

Shahidi: Baada ya Khalfani Bwire kwenda Kumuona Mbowe Waliongea kwa Muda kisha Bwire akatuita, Kwamba Yeye anayetusumbua ni Sabaya, inabidi apewe discipline

Kibatala: Hapo Kuna Mahala Kaaya anatajwa

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wewe Umesema Kwamba Moja ya Viashiria Vyako ni Maelezo ya Kukiri ya haya Washitakiwa hawa wawili, Sasa alichokwambia Kaaya ndiyo Maelezo ya hawa wawili Kukiri

Shahidi: Nishajibu

Kibatala: Ni Mpango upi ambao Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Walikuwa wanatekeleza pale Rau Madukani

Shahidi: Walikuwa hawatekelezi Kibatala Uliyasema Maelezo Ya Onyo la Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: alisema nini Juu ya Uwepo Wake Rau Madukani

Shahidi: Naomba Nikumbushwe

Kibatala: Naomba Kielelezo namba 13, Soma Ling'wenya anasema Rau Madukani ni Kwa nani yake

Shahidi: Nasema nilipo rudi Moshi Mjini, Tukiendelea Kuchunguza Maeneo Mengine, Wakati huo atulufikia Aishi Hotelini, Bali Kwa Dada Yangu anayeishi Rau Madukani

Kibatala: Sasa ni Kweli Kilicho wapelekea Rau Madukani ni Kwa sababu Ndipo walipofikia na Kwa sababu Kuna Dada yake anaitwa Athima D/O kibibi

Shahidi: Ni sahihi ila Hawakukamatiwa Kwa Dada yake

Kibatala: Kuna Mahala ambapo anasema Kwamba Walikamatwa wakiwa Kwenye Maandalizi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwani Ukisoma huko Juu Walipo Kwenda Kufanya Surveillance ni Arusha au Rau Madukani

Shahidi: Hapana

Kibatala: halafu ukiwa unajibu ONGEZA SAUTI wateja wangu wasikie

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi, Justine Kaaya aliwahi Kukwambia Kwamba alipoombwa Taarifa za Kuhusu Sabaya alienda Kuripoti Kwa Mbunge wake

Shahidi: Hakunieleza

Kibatala: Je, aliwahi Kukwambia Kama aliriport Mahala Popote kabla ya Kukamatwa

Shahidi: Hakuwahi kunieleza

Kibatala: Katika Maelezo Ya Justine Kaaya aliwahi Kukwambia Katika Interaction zake alikuwa anafanyia kwenye Land Cruiser ya Mbowe

Shahidi: ajawahi Kuniambia Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Hukuona Umuhimu Wa Kurekodi identity ya hilo gari

Shahidi: Sikuona Umuhimu

Shahidi: Mheshimiwa naomba kwensda washroom (chooni)

Kibatala: Kama Identity ya hiyo Land Cruiser uliona siyo ya Muhimu, Kama Halikuwa Kitu cha Muhimu mbona Uliandika katika Maelezo Yake ya Tarehe 30 July 2021

Shahidi: Kuweka niliona ndiyo Muhimu ila Kufuatilia ndiyo sikuona Umuhimu

Kibatala: Ni sahihi sasa haya aliyokuja Kuya sema Kuhusu Freeman Mbowe aliyasema Baada ya Kuachiwa baada ya Kutoka Kwenye kesi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi baada ya Kuandika Maelezo haya Ndiyo alipewa Vifaa Vyake Ikiwemo pesa (Dola)

Shahidi: Hapana alipewa kabla

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi, Mmoja wa Mtekelezaji wa Mpango Wa Kumdhuru Sabaya Moses Lijenje na Boss wake Bwana Mbowe Master Mind yupo Nje, Je Mlimtaarifu Sabaya au Mamlaka yake ya Uteuzi ili waongeze Ulinzi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mliwa taarifu Mamlaka Wengine Kama TISS

Shahidi: Haikuwa Jukumu langu

Kibatala: Unafahamu alikwambia Viongozi Wako

Shahidi: Hawakuniambia

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Uliwahi Kushauri

Shahidi: Sikuwahi

Kibatala: Ni sahihi Statement hizo Mbili hasa ya Ling'wenya Kwamba Sabaya anamsumbua katika Uchaguzi

Shahidi: sahihi

Kibatala: Ni sahihi Maelezo ya Mohammed Ling'wenya Kwamba ampigie Sabaya ili Kumtia Discipline ili asiendelee Kung'oa Bendera

Shahidi: Naomba nijikumbushe

Shahidi: Yapo hayo ila siyo Kushusha bendera

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Kuna sehemu yoyote Lengo la Mbowe lilikuwa Kuzua Taharuki

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwenye Uchaguzi Mdogo Wa Igunga, Mkuu wa Wilaya Fatma Kimaro alishambuliwa na Watu Waka pelekwa Mahakamani, Je Unakumbuka hilo tulion

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Haya Soma na Maelezo Ya Adamoo

Shahidi: Kuanzia Usiku wa Tarehe 25 July 2020 tulikaa watu watano, Mimi, Ling'wenya, Khalfani, na Freeman Mbowe pamoja na Mtu Mwingine anayeitwa kakobe Mlinzi wa Freeman Mbowe Anaendelea Kusoma

Kibatala: Kwa hiyo ni sahihi Kuwa Motive ya Kikao hicho hata Kama Kweli Walikataa, Lengo la Mbowe la Kumdhuru Sabaya ilikuwa sababu Sabaya anavuruga Wapiga Kura wake

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi kwenye paragraph hiyohiyo Lengo la Kumdhuru Sabaya ni Kwa sababu Sabaya amefanya hujuma na Bendera Nyingi zimeshushwa

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Pia hata Kweli Kikao Kilikaa, Lengo la Mbowe anasema Raia wametishiwa

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Pia Ni Kwa sababu Mbowe anasema Sabaya alikuwa na Mpango Wa Kuiba Kura

Shahidi: Ni Sahihi

Kibatala: Kuna Mahala Mbowe anasema Lengo la Kumdhuru Sabaya ni Kuzua Taharuki

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Kwenye Maelezo ya Adamoo yanasema Kuwa Walipanga Kumdhuru Kwa Kumpiga Spray Ya Sumu

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je, Mbinu hizo Mbili za Maelezo Ya Adamoo na Ling'wenya Vinafanana

Shahidi: Havifanani

Kibatala: Kwa kuwa havifanani, Je Uliwahi Kuandika Maelezo ya Nyongeza Kutoa Ufafanuzi Kwamba iweje watu wawili Wamekiri halafu Maelezo Yapo tofauti?

Shahidi: Sikuwahi Kuandika

Kibatala: Je Uliwahi Kupeleleza Kuhusu hii Dawa yanye Sumu ambayo ilikuwa apuliziwe Sabaya kuwa ingepatikama wapi

Shahidi: Sijawahi

Kibatala: Ni kweli au Si Kweli Mohammed Ling'wenya hakuzungumza Kuhusu hiyo Dawa yenye Sumu katika Maelezo yake

Shahidi: Haja zungumzia

Kibatala: Ulichukua Taarifa Kuhusu hii Dawa yenye Sumu Kwa ajili ya Upelelezi

Shahidi: Sikuchukua

Kibatala: Huyu Sabaya, ambaye Mbowe anasema Kwamba Sabaya anashusha Bendera, Kutisha Raia, na Mpango Wa Kuiba Kura, Je ni sahihi kahukumiwa na Matendo Kama hayo ya Kuwatendea Uhalifu Wananchi

Shahidi: Siwezi Kuzungumzia hilo

Kibatala: hutaki, hufahamu au Jeuri tu?

Shahidi: Sijafuatilia hiyo Kesi Yenyewe

Kibatala: Je Dhumuni la Kukubaliana na Denis Urio Mlikuwa Mnamtafutia Mbowe Vijana walinzi? AU Magaidi? Au Walinzi ambao Watakuja Kugeuka Kuwa Magaidi

Shahidi: Ni Walinzi ambao Watakuwa wanarejesha Taarifa

Kibatala: Kwa Ufahamu Wako wewe Mbowe aliomba Kwa Denis Urio Walinzi au Wahalifu

Shahidi: Denis (Urio) ndiye aliyebuni hawa Waende kuwa Walinzi

Kibatala: Umesema Katika Maelezo Kuwa Freeman Mbowe ndiye aliyeanzisha Mchakato wa Kupata Walinzi au Kupata Wahalifu?

Shahidi: Wakupata Wahalifu

Kibatala: Ila yeye akapelekewa nini

Shahidi: akapelekewa Walinzi

Kibatala: Je Baada ya Mbowe Kuomba Wahalifu kisha Denis Urio Kupeleka Walinzi, Bado Nyie Mlikuwa Mnamuona Urio ni Mwaminifu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hiyo Swala la Kuweka Watu Undercover Ni zoezi la Kisheria au ni Matakwa tu ya DCI na Kingai

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wewe Hukushiriki kwa namna yoyote Katika Mchakato wa Kumuweka Luten Denis Urio Undercover

Shahidi: Sijawahi Kushiriki Mimi Kibatala Unafahamu Kuna Mkanganyiko Denis Urio anasema aliwapa pesa Kuja Moshi, Wakati Hawa wanasema Walipewa pesa Kuja Dar es Salaam

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Kwani wewe Kama Mpelelezi, Baada ya Adamoo na Ling'wenya Kupewa Pesa na Denis Urio walienda wapi

Shahidi: Walienda Hai, Kilimanjaro

Kibatala: Kwanza Maelezo Ya Denis Urio Uliandika Wewe

Shahidi:
Ni sahihi

Kibatala:
Wakati tunamuhoji Denis Urio alisema Kuna Maeneo Kadhaa Ulikosea Kuandika Maelezo yake, Je unafahamu hilo

Shahidi: Sijawahi Kujua

Kibatala: Je ni sahihi Kwamba Ulipokuwa Unaandika Maelezo ya Denis Urio, Kuna sehemu anasema Kwamba Baada ya Kuwapa pesa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya wao Walikwenda Dar es Salaam, Je ulipatia Kuandika au Ulikosea

Shahidi: Nilipatia

Kibatala: Je unaona Kuna Mgongano au Hakuna Mgongano

Shahidi: Rudia swali

Kibatala: Wewe Unasema Ulipopeleleza Kwa ufahamu wako baada ya Adamoo na Ling'wenya Walienda Hai, lakini wewe pia Ukasema Umeandika Maelezo Ya Denis Urio ambayo yanasema Kwamba Baada ya Kupewa Pesa walienda Dar es Salaam. Kuna Mgongano au Hakuna Mgongano

Shahidi: (Kimya)

Shahidi: Naomba nisome Maelezo Ya Watuhumiwa tafadhali...

Shahidi anasoma Maelezo ya Adamoo Anasema:

"Tarehe 24 July 2020 Nilikutana na Mohammed Ling'wenya kasisitiza tuende Morogoro tukakutane na Luteni Urio, ambaye alitumbia kuwa Kuna kazi ya VIP PROTECTION Kumlinda Freeman Mbowe, Akatupa TSh 87,000 kila Mtu nauli ya Kwenda Moshi"

Tulirudi Chalinze Kwa pikipiki na Simu hiyo hiyo tukaanza Safari ya kwenda Moshi..

Kibatala: Kwa Mujibu wa Maelezo hayo, yeye alikwenda Wapi?

Shahidi: Alikwenda Moshi, Na akapolekelewa na Bwire pamoja na Dereva aitwaye Willy

Kibatala: Soma na ya Ling'wenya

Shahidi: Maelezo Ya Ling'wenya yanasema "Baada ya hapo tuliondoka Kurudi Chalinze ambapo Baada ya Kurudi Chalinze tulinunua Shati, Baada ya Muda tulipata Usafiri wa Kuelekea Moshi, Tulifika Moshi Usiku"

Kibatala: Mwambie Mhe Jaji Ling'wenya alipopewa nauli anasema alienda wapi

Shahidi: Alienda Moshi

Kibatala: Sasa nakuuliza Kwamba Kati ya Taarifa ya Undercover Wenu Luteni Denis Urio na Maelezo hayo Kuna Mgongano au Hakuna

Shahidi: Hakuna Mgongano

Kibatala: yaani Shahidi sisi watu wazima Unasema Maelezo Kwamba Watu walienda Moshi na Mtoa Taarifa wenu anasema walienda Dar es Salaam, Hakuna Mgongano?

Wakili wa Serikali Pius Hilla:
Mheshimiwa Jaji Shahidi amesema Kwamba ana ufafanuzi, lakini siyo Kumwambia Shahidi Kwamba ni Mzima..

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ukweli Kabisaaaaaa sijaona Mr. Hilla Kasimama Kwa sababu gani yaani..

Jaji: anasema yale maneno ya ni MTU MZIMA

Kibatala: Shahidi unataka Nikuonyesha Maelezo ya Denis Urio?

Wakili wa Serikali Chavula: Mheshimiwa Jaji sijui kwanini wakili anataka arudie Swali, Wakati Kakataa Ufafanuzi

Kibatala: Mhe Jaji Mimi napokea Maelekezo Kutoka Kwako, Umeniambia Kwamba Unatatizo na Neno wewe ni Mtu Mzima

Kibatala:
Hukusema lolote la Ziada sijui kwanini Wakili Abdallah Chavula kasimama.. Labda kwa sababu sasa ni Saa 11 Ndiyo Maanaa, Naomba tu airishe Mpaka Kesho Wenzetu Watakuwa Wamechoka hawa.. Tena kwa Hoja ya Muda Kama Wenzetu hawatopinga..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naomba kabla hatujahairisha utoe Ufafanuzi

Jaji: Wakili Kibatala Kote Umeuliza kisha Ukataka Shahidi asome Maelezo Ya Adamoo, Kisha Ukataka asome Maelezo ya Mohammed Ling'wenya baadae Ukamuuliza Kama KUNA Mkanganyiko akasema Hakuna

Nafikri kinachofuta sasa ni Kuachiwa Mahakama Kuona Kama Kuna Mkanganyiko au Hakuna..

Kibatala: Sawa Mheshimiwa Jaji Kama nilivyosema Siku zote sin tatizo na Malekezo Yako.. Baada ya hapo naomba nitoe Hoja ya Kuairisha Mpaka Kesho

Jaji: unahairisha Sababu ya muda au?

Kibatala: Ndiyo Mpaka Nitoe Hoja Dakika 5 zitakuwa Imeisha

Jaji: Kufuatia Maombi ya wakili Wa Utetezi, Na airisha Shauri Mpaka Kesho Tarehe 9.2.2022, Asubuhi Saa 3. Shahidi ataendelea Kuwa Kizimbani Kuendelea Kutoa Ushahidi Wake, Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza

Jaji anatoka
 
Naweka kambi hapa. Sipendi kupitwa na neno moja kwenye kesi hii ya kihistoria.

Naamini leo shahidi hajameza dawa kwahiyo safari za kwenda msalani zitapungua
 
Serikali ionyeshe kujali wananchi kwa kuacha matumizi mabaya ya kodi zao. Kodi kubwa, walipa kodi ni maskini, bei za vitu zinapanda, serikali inafuja fedha zao kwa kesi za fedheha kama hii.

Kupitisha muswaada wa polisi kutokushitakiwa wanapofanya makosa, ni declaration ya mwisho wa haki za kuishi kwa watanzania. Rais hata kama anawaogopa ccm, afikirie kwamba ccm si Mungu. Yuko Mungu baada ya maisha ya hapa duniani ambayo si marefu wala.
 
Yanayoendelea mahakamani kwa watuhumiwa kulalamika kuteswa akiwemo Denis Urio ndio imepelekea muswada huu kupelekwa bungeni ili wakina Mahita watese na kuua watu kwa uhuru.
Huu mswada ukipita nitashabgaa sana, utakua ni mwanzo wa mateso ya raia kutoka kwa polisi
 
Back
Top Bottom