Mzee Kikwete: Unapokuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais basi unakuwa na nguvu sana

Nimesikiliza maoni ya aliyewahi kuwa Rais wa JMT Mh. Jakaya Kikwete kuwa hatarajii chama cha chake kuweza kutenganisha nafasi ya urais na ile ya uenyekiti wa CCM kwa watu wawili tofauti. Ninaheshimu mno mawazo yake, isipokuwa kutenganisha nafasi hizi ni jambo ambalo linazungumzika...
Mkuu huyo mwenye exclusive rights ndio boss wa chama!!!!!!!🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Unakuwaje mwenyekiti ila maamuzi ya mwisho anafanya mtu mwingine??

waliweka makusudi ili asitimuliwe.....CCM ikimfukuza Samia leo, mnarudia uchaguzi wa urais kwa mujibu wa katiba mama

ndio ikawekwa bora awe mwenyekiti pia....
 
Nimesikiliza maoni ya aliyewahi kuwa Rais wa JMT Mh. Jakaya Kikwete kuwa hatarajii chama cha chake kuweza kutenganisha nafasi ya urais na ile ya uenyekiti wa CCM kwa watu wawili tofauti. Ninaheshimu mno mawazo yake, isipokuwa kutenganisha nafasi hizi ni jambo ambalo linazungumzika...
Hii hoja ilikua inatumika Kama fimbo ya kumzingua JK wakati ule JK akitaka kutenganisha Siasa na Biashara
 
CCM inamhitaji zaidi Rais kuliko Rais anavyoihitaji CCM hasa nyakati za uchaguzi.

Suala la kutenganisha hizo kofia mbili litawafanya CCM wapate kazi ya ziada ya kufuata matakwa ya wananchi wakati wao hawataki.
Hii concept yako sidhani kama iko hivyo, Rais na mwenyekiti wote wanategemeana, hasa pale Rais anapotaka kugombea muhula wa pili, kama pakiwa na ushindani chamani anaweza toswa akizidiwa nguvu na wajumbe.

Kuna issue kama Katiba Mpya, hii wote hawaitaki kwasababu inawabeba wote kwenye kuunda serikali.
 
Hii concept yako sidhani kama iko hivyo, Rais na mwenyekiti wote wanategemeana, hasa pale Rais anapotaka kugombea muhula wa pili, kama pakiwa na ushindani chamani anaweza toswa akizidiwa nguvu na wajumbe.
Sizungumzii ushindani wa chama.

Rais ndio muundaji wa machinery yote ya wasimamizi wa uchaguzi
  • DEDs
  • NEC
  • Msajili wa Vyama
  • IGP
-

So, Kwa lugha rahisi ukitenganisha hizo kofia mbili maana yake CCM kushinda kura, itategemeana na kukubalika kwake kwa haki kabisa kwa wananchi. Sasa CCM unayoiona iko tayari kwa hilo?!
 
Wakuu ndiyo maana nimelinganisha na nafasi ya Rais ndani ya Bunge la JMT. Tunatambua hadhi na madaraka ya Spika wa Bunge lakini pia tunaona jinsi mchakato ulivyo mgumu wa kikatiba wa kuweza kumthibiti Rais aliyepo madarakani.
 
Sizungumzii ushindani wa chama.

Rais ndio muundaji wa machinery yote ya wasimamizi wa uchaguzi...
Lakini huyu Rais ni zao la chama, na ili awe Rais na kuunda hizo taasisi au kuteua wasimamizi unazosema lazima chama kimridhie, ndio maana nimekupa mfano kama atakutana na ushindani akitaka kugombea muhula wa pili wajumbe wasimpitishe, hizo machinery unazosema atateua vipi wakuu wake?
 
Lakini huyu Rais ni zao la chama, na ili awe Rais na kuunda hizo taasisi unazosema lazima chama kimridhie, ndio maana nimekupa mfano kama atakutana na uzhindani akitaka kugombea muhula wa pili wajumbe wasimpitishe, hizo machinery unazosema ataziundia wapi?
Huo mkutano wa wajumbe watakaokuwa kinyume na Rais utafanyikia ndani ya nchi humu humu??
 
Huo mkutano wa wajumbe watakaokuwa kinyume na Rais utafanyikia ndani ya nchi humu humu??
Ukifika wakati wa vyama kutafuta wagombea kisheria lazima mkutano ufanyike, no way out, wajumbe watake wasitake utafanyika.
 
CCM ni chama kikongwe, ni vyema kisijenge tabia ya kuishi kwa mazoea eti tu ni kwa sababu ya kudumisha fikra za waasisi wake. Ni lazima kiwe na uthubutu wa kufanya mabaliko na kuishinda dhana ya "fear of unknown" pale inapopasa kufanya hivyo.

Kuna nyakati zinahitaji "paradigm shift" ili kuboresha mifumo ya uongozi ndani ya chama. Kumlimbikizia mtu mmoja madaraka makubwa ndiko kunapelekea kuleta watawala madikteta.
 
Kikwete ni mnafiki sana. Hakumtaka kabisa Magufuli awe rais ni zali tu mwendazake ilimuangukia. Au bwashee unatetea hoja yako wakati hule mamia ya container ya mama salma yalizuiwa na Jiwe bandarini hadi yalipiwe ushuru maza akamshukia Jiwe kwa kumuambia ujue hata huo urais bila sisi usingeupata.

Jiwe nafsi ilimsuta na kumuuma sana akaamua kumpoza festledi wa awamu ya nne kwa ubunge na kumuachia mamia ya container zake
Wewe ni mpumbavu. Kama aliweza kumkata LOWASSA unadhani alishindwa nn kwa MAGUFULI?
 
Kikwete ni mnafiki sana. Hakumtaka kabisa Magufuli awe rais ni zali tu mwendazake ilimuangukia. Au bwashee unatetea hoja yako wakati hule mamia ya container ya mama salma yalizuiwa na Jiwe bandarini hadi yalipiwe ushuru maza akamshukia Jiwe kwa kumuambia ujue hata huo urais bila sisi usingeupata.

Jiwe nafsi ilimsuta na kumuuma sana akaamua kumpoza festledi wa awamu ya nne kwa ubunge na kumuachia mamia ya container zake
Umejichanganya hapa naomba uniweke sawa. Umesema kuwa Kikwete hakutaka Magufuli awe raisi isipokuwa ni zali tu lakini mwisho wa sentensi yako unasema kuwa Mama Salma akamahukia jiwe kwa kumwambia kuwa huo uraisi bila wao asingeupata.

Kwa hii kauli tu inaonesha ni wazi kuwa uraisi wa jiwe umetokana na kikwete na ndio maana jiwe akanywea baada ya kuambiwa hivyo.
 
Sasa kuwa na hiyo "prominent member" na "exlusive rights" si ndio uenyekiti wenyewe? au zaidi ya uenyekiti.

Naona kuna kamchezo mnataka kukafanya kumnyima huyo mama uenyekiti bila sababu za msingi, hii inathibitisha hata ule urais hakuupata kirahisi, ndio maana kila siku mama wa watu anasisitiza mimi ni Rais mwenye jinsia ya kike.
Labda wafuate mfumo wa ACT wazalendo Rais awe ndio KC!
 
Akizungumzia namna yeye binafsi alivyohakikisha Dr Magufuli anakuwa Rais wa JMT mwaka 2015 JK anasema " unajua unapokuwa mwenyekiti wa CCM na Rais unakuwa na nguvu kubwa "...
Hata asemeje, hakuna asiyejua kuwa yeye alikuwa team Membe na kila mtu anajua damu ni nzito kuliko maji! Aliyembeba Magufuli alikuwa ni Mkapa.
 
Kwa hili ni bayana kuna sintofahamu kene hilo la uwenyekiti na hii inatokea kipindi hiki tunachoelekea kwenye huo mchakato wa kumpa kijito mama awe sasa na nguvu kamili kiserikali na kichama ambapo km ilivyobayana kwass viongozi wanahesimu zaidi chama kuliko hata serikali yenyewe.
 
Wewe hlkijua nguvu ya chairman wa CCM?!
Nguvu ya mwenyekiti wa ccm iko ndani ya madaraka ya urais. JK anajua fika bila mwenyekiti wa ccm kuwa rais, ni dhahiri ccm itaondoka kwenye siasa za ushindani hapa nchini. JK hataki kuwa mnafiki, anajua ni kwa jinsi gani madaraka ya urais yanavyotumika kuibeba ccm, hivyo anajua ccm wakifanya kosa hilo ndio mwisho wake.

Mimi naomba ccm ifanye hilo kosa la kutenga hizo kofia ili ikose support ya vyombo vya dola, hapo ccm ndio itajua ilikuwa madarakani bila ridhaa ya umma bali madaraka ya urais.
 
Juzi Mzee Msuya kalisemea hili jambo leo Kikwete naye kazungumza jambo hilo hilo, kuna nini kinafukuta huko ndani?

F0636996-564C-4CCA-866C-D90F42E431B5.jpeg
 
Back
Top Bottom