Mzee Kikwete: Unapokuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais basi unakuwa na nguvu sana

Haitakaa itokee kwa katiba hii ya Tanzania Rais kuzidiwa nguvu na yeyote.
Hyo haipo ,na haitakuja kutokea boss!!! Mwenyekiti wa chama atakuwa na nguvu kuliko raisi....chama kikihtaji msaada na Raisi asifanye , mwenyekiti anamtupia lawama Kwa wajumbe ......
 
CCM ni chama kikongwe, ni vyema kisijenge tabia ya kuishi kwa mazoea eti tu ni kwa sababu ya kudumisha fikra za waasisi wake. Ni lazima kiwe na uthubutu wa kufanya mabaliko na kuishinda dhana ya "fear of unknown" pale inapopasa kufanya hivyo...
Raisi awe mwenyekiti tu, hakuna dikteta atakayetokea akaishi milele, ila mfumo wa kakikundi kumwendesha raisi kupitia mwenyekiti unaishi.
 
Nape, JK na Makamba hawatakubali
Tunataka uongozi wa chama na rais utenganishwe ili mwenyekiti wa chama amuwajibishe na ikibidi amvue uanachama SSH kwa kuonyesha udhaifu katika uongozi ili tupate rais mwingine strong kama magufuli.
 
Wanataka Mama asiwe Mwenykiti ili waweze mbana....
Akipewa Uenyekiti ataachana na ya hayati
Wakifanya hivyo CCM ndio utakuwa mwisho wao
manake siku raisi aliyepo madarakani akipingana na mwenyekiti wa chama anaweza kuunda chama chake akiwa madarakani
 
Tunataka uongozi wa chama na rais utenganishwe ili mwenyekiti wa chama amuwajibishe na ikibidi amvue uanachama SSH kwa kuonyesha udhaifu katika uongozi ili tupate rais mwingine strong kama magufuli.

Siku ccm itatenganisha kofia ya uenyekiti na urais ndio itakuwa mwisho wa hilo dubanwa liitwalo ccm. Naomba hiki unachokitaka kitokee ndio utajua ccm nguvu yake inategemea madaraka ya urais.
 
Hapa tulikofikia bado samia hatujamuona kama kamudu urais,sasa mnataka kumuongezea tena uwenyekiti wa Chama?
Ili ionekane kamudu urais ni mpaka aanze kuteka wapinzani na kuwaua? Naona bado mna hangover ya utawala wa dhalimu. Mtakula kwa jasho, yale mambo ya kupita bila kupingwa yamefikia mwisho.
 
Hyo haipo ,na haitakuja kutokea boss!!! Mwenyekiti wa chama atakuwa na nguvu kuliko raisi....chama kikihtaji msaada na Raisi asifanye, mwenyekiti anamtupia lawama Kwa wajumbe.
Mkuu mwenyekiti wa chama awe na nguvu kuliko rais? Sio kwa katiba hii, labda huyo rais awe dhaifu. Kwa taarifa yako hata vikao tu vya chama vinaweza kukaliwa kwa ruhusa ya rais pekee, na akapanga nini kijadiliwe, na kitendo cha kwenda kinyume na maagizo yake kikao kikapigwa mabomu. Kinachoibeba ccm ni cheo cha urais kupewa mwenyekiti wa ccm. Ili ccm ibaki hai au ipotee ni hapo kwenye kofia ya urais na uenyekiti.
 
Wasipompa awe mwenyekiti hawatashinda uchaguzi .....majimbo nusu kwa nusu...safi sana badilini katiba ccm twende sawa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom