Mzee Butiku aigeuza Mwalimu Nyerere Foundation kutoka kuwa taasisi kubwa ya kimataifa mpaka level ya kikao Cha ukoo wa Nyerere. Ikabidhiwe UDSM

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,683
Mwalimu Nyerere Foundation wakati inaanzishwa, ilikuwa na malengo makubwa sana. Ilivutia wafadhili, ilivutia serikali kuweka fedha. Na Kila mtu alitarajia kwamba itakuwa ndio kisima Cha mawazo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kidiplomasia kwa Kila namna.

Mwanzoni ilianza vizuri, kabla haijawekwa mikononi mwa Butiku. Hapo ndipo tulishuhudia taasisi hii ikiporomoka umaarufu wake.

Kwa Sasa taasisi hii haina inalifanya, iko kwenye makaratasi tu, hakuna mijadala inaendeshwa na taasisi hii, hakuna scholarship inatoa.

Taasisi inapokea mabilioni, lakini anayejua ziko wapi ni Butiku pekee.

Nashauri taasisi hii ikabidhiwe Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ufanisi.
 
Binadamu ye yote mkweli anayejua historia ya Tanzania; aliyeshuhudia Tanzania ikiwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi kadhaa; aliyeshuhudia Tanzania tukiungana kuikomboa nchi yetu Idd Amin alipotuvamia; aliyeshuhudia Tanzania ikiheshimiwa kwenye duru za kimataifa hata kuogopwa na baadhi ya nchi kwa misimamo yake ya uhuru na haki ya kila mtu kuishi; hawezi kukosa kusononeka akiona Uongozi wa Tanzania, Bunge na CCM ya leo ilivyo kinyume na tuliyoyapigania na kuyaenzi. Hata shetani hawezi kuamini anachoona na kusikia kwenye uongozi wa leo hapa Tanzania. Tunashuhudia hata askari anamtisha raia anayetetea mstakabali wa Tanzania? Njaa ndiyo imekuwa mwongozo na dira ya mtu kutetea jambo? Je bado Watanzania tunawasha mwenge juu ya Mlima Kilimanjaro, Ili uoneshe nini? Hii ni aibu? Wazee na heshima zao ambao hawakemei maovu haya wanafikiria zaidi na kujilinda ili wazikwe vizuri kwa heshima zote siku ya kufaa itakapowadia, siyo? Mnaomdhihaki Mzee Butiku jipimeni! Mwenyezi Mungu Aamshe roho ya kweli ya Tanzania turudi kwenye Tanzania yetu na maadili tuliyojijengea!
Wazee kama akina JK na Mwinyi hawawezi Sema kwa sababu ya mikataba yao mibovu na Wizi walioufanya huko nyuma. Akina Butiku au Warioba ambao wako safi wakiongea wanaundiwa fitina. Hii nchi dawa ni katiba mpya tu kuliko kuegemea huu ukoo wa Panya.
 
Mleta mada utakuwa ni moja ya majambazi .baada ya Mzee kuwachana ITV naona ndo unatiririka. Mnufaika wa diiii piiii wodi
 
Binadamu ye yote mkweli anayejua historia ya Tanzania; aliyeshuhudia Tanzania ikiwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi kadhaa; aliyeshuhudia Tanzania tukiungana kuikomboa nchi yetu Idd Amin alipotuvamia; aliyeshuhudia Tanzania ikiheshimiwa kwenye duru za kimataifa hata kuogopwa na baadhi ya nchi kwa misimamo yake ya uhuru na haki ya kila mtu kuishi; hawezi kukosa kusononeka akiona Uongozi wa Tanzania, Bunge na CCM ya leo ilivyo kinyume na tuliyoyapigania na kuyaenzi. Hata shetani hawezi kuamini anachoona na kusikia kwenye uongozi wa leo hapa Tanzania. Tunashuhudia hata askari anamtisha raia anayetetea mstakabali wa Tanzania? Njaa ndiyo imekuwa mwongozo na dira ya mtu kutetea jambo? Je bado Watanzania tunawasha mwenge juu ya Mlima Kilimanjaro, Ili uoneshe nini? Hii ni aibu? Wazee na heshima zao ambao hawakemei maovu haya wanafikiria zaidi na kujilinda ili wazikwe vizuri kwa heshima zote siku ya kufaa itakapowadia, siyo? Mnaomdhihaki Mzee Butiku jipimeni! Mwenyezi Mungu Aamshe roho ya kweli ya Tanzania turudi kwenye Tanzania yetu na maadili tuliyojijengea!
Nimependa saana ulichokiandika. Tanzania ya zamani si ya sasa. Tanzania badala ya kupiga hatua mbele inarudi nyuma. Ukikosoa unaonekana mbaya watu wanakushambulia.

Ila kwa upande mwingine, Mzee Butiku apumzike kwenye swala la kuongoza Nyerere Foundation. Angebaki kuwa mshahuri. Nyerere Foundation ilitakiwa iwe mbali sana. Na hata iwe foundation si tu ya makaratasi bali hata inatoa ajira ili indeshwe vizuri na wataalamu.

Ninajua mzee Butiku alipigwa vita saana na awamu fulani haikutaka hata wajenge lile jengo ikazuia kila kitu. Ni Rais Magufuli aliye wawezesha na hata jengo kukamilika.

Nyerere alikuwa na heshima yake duniani, aliifanya Tanzania ikaheshimika. Penye ukweli tuwe wakweli. Butiku ana haki ya kutoa maoni. Asiandamwe kwa maoni alotoa. Ila nae pia basi asibweteke kuiacha Nyerere Foundation kuwa ya mfukoni.

Nakumbuka lengo mojawapo ilikuwa ni kutoa scholarship, Lakini Foundation imekuwa kimya. Kujihusisha ktk kuleta amani na maelewano na hasa utatuzi wa migogoro. Usikii wakiongolea lolote kama Taasisi. Ethiopia kumekuwa na migogoro, na baadhi ya nchi lakini Foundation haina project yoyote kuleta michango ya utatuzi wa migogoro.

Imebaki tu kuitwa kwenye makongamano ya kigoda cha Nyerere chuo Kikuu Dar es Salaam. Na Butiku akitoa maoni anatoa yeye kama yeye si Taasisi.

Ninapinga Uuzwaji wa bandari kwa mkataba usiyo na manufaa kwa Tanzania. Ila Butiku nae ajipime katika kuendesha Nyerere foundation. Hadi hii leo hawana website, ukitaka habari hupati.
 
Hahahahahahaaa!! Yamekua hayo leo kisa Bandari. Mlikua wapi kusema hayo cku zooote?
 
Ninakusikia unachosema. I hear you Sir!
 
Back
Top Bottom