Msaidizi wa Mwl. Nyerere (Mzee Kasori) alivyowashukia viongozi wa serikali ya awamu ya nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidizi wa Mwl. Nyerere (Mzee Kasori) alivyowashukia viongozi wa serikali ya awamu ya nne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ilboru1995, Jan 31, 2008.

 1. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  USHAURI KWA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI – AWAMU YA NNE, HUSUSANI MHE MEGHJI, KARAMAGI, MRAMBA, YONA N.K KUHUSU UWAJIBIKAJI NA UADILIFU.

  Baada ya kufuatilia kwa karibu sana matamshi mazito ya kukemea ufisadi na ufujaji wa rasilimali nchini Tanzania, yaliyotolewa hivi karibuni na Mhe Rais J.M Kikwete, Kadinali Pengo, Askofu Kilaini, Padri Victus Sichwale, Askofu Thadeus Ruwa, Sheikh Suleiman Gorogosi, Sheikh Mkuu Sheikh Shaaban Bin Simba, Askofu Dr. Valentino Mokiwa, Mhe Jaji Mstaafu Sinde Warioba, Waheshimiwa waandishi wa habari k.m Jenerali Ulimwengu, Joseph Mihangwa, Mbwambo, Conges Mramba, Jackton Manyerere, Said Kubenea, Ayubu Rioba, Majid Njengwa, Innocent Mwesiga, Padri Privatus Karugendo, D. John, Muhingo Rweyemamu na wengine wengi wakiwemo wananchi, na hasa kutokana na umma wa Watanzania kuguswa na yaliyotokea BoT, nimeona ni busara nami ni ungane na wote hao ktk kupaza sauti ya kuchukizwa na matendo haya yenye kurudisha nyuma juhudi za maendeleo ya nchi yetu.

  Nianze kwa kusema mimi ni mtumishi mstaafu niliyekuwa nimeajiriwa na serikali ya Tanzania kuanzia tarehe 01.01.1969 hadi tarehe 02.06.2005. Ngazi ya juu niliyofikia ni kubahatika kuwa katibu ( msaidizi mkuu kiserikali ) wa Mwalimu J.K Nyerere. Nimeishi naye hadi alipofariki dunia 14.10.1999. Kubwa nililozingatia katika utumishi wangu serikalini katika kufanya maamuzi madogo na makubwa ni kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za serikali ambazo msingi wake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Sheria mama). Niharakishe kusema mapema kuwa nilipotambulishwa na kupokelewa na Baba wa Taifa kama msaidizi wake mkuu , baada ya Butiku na Batao , Baba wa Taifa kwa maneno yake mwenyewe aliniasa kwa kusema " KASORI, KARIBU SANA. NAOMBA USIFANYE KAZI KWA KUNIOGOPA. MUNGU AKUSAIDIE KTK KUNILEA KISERIKALI; KUWA MWAMINIFU NA JASIRI KTK KUNISHAURI"

  Jambo jingine ambalo lilinisaidia katika utumishi wangu serikalini ni kujitahidi mara kwa mara kudurusu kurasa za nyuma na madokezo katika kila jalada liliokuja mezani kabla ya kufanya maamuzi ya suala jipya ndani ya jalada hilo. Nilizoea kufanya hivyo kwa lengo la kuepuka kutoa maamuzi yenye kuleta utata ambayo labda huko nyuma tayari yalikwisha kutolewa maamuzi ya busara na kufangwa. Nathubutu kusema kuwa hili ni moja ya yale yaliyonijengea heshima kubwa kwa Baba wa Taifa.

  Jambo la tatu nililoliweka maanani daima ni kutambua na kuheshimu alama kuu za serikali ambazo ni taasisi kama vile URAIS, UWAZIRI, UKATIBU MKUU, na KATIBA ya Jamhuri yetu. Niliishi kwa kutambua kuwa Rais au Waziri au Katibu mkuu n.k wote wanafanyakazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na siyo "hisia" au "mawazo yao".

  Kwamba Mhe. Meghji mwenye dhamana kubwa ya KAPU la fedha za serikali anatuambia Watanzania na dunia nzima kuwa aliidhinisha malipo ya Tsh billion 40 kwa kampuni ya Kagoda Agricultural ltd kwa kumuamini Gavana Ballali, inatia kichefuchefu hasa inapozingatiwa kuwa Meghji naye alihudhuria semina elekezi Ngurudoto na kupata heshima ya kutembelewa wizarani kwake na Rais J.M. Kikwete. Ni kweli kufanyakazi kwa kuaminiana ni moja ya vigezo vyenye kuleta ushirikiano mzuri katika sehemu za kazi. lakini kuaminiana siyo mbadala wa sheria, kanuni na taratibu za serikali. NAKATAA! Mhe Zakia Meghji si mgeni katika kazi za uwaziri. Haiingii akilini eti baada ya Boss ( Rais) kukasirishwa na yale yaliyojiri BoT, yeye Meghji anasema alidanganywa na gavana. Mhe Meghji ofisini kwake katika makabati au mezani anazo sheria, kanuni za utawala wa fedha. Pia Waziri anao wasaidizi, manaibu mawaziri wawili, katibu mkuu, manaibu katibu mkuu wawili, wakurugenzi, makamishna na wengine wengi, tena wasomi wazuri tu. Hivyo anao uzoefu wa kutumia hizo rasilimali nzuri za serikali( wataalam na nyaraka)! Mhe. Mgonja (KM) ni mtaalam mzuri tu wa masuala ya BoT na uchumi. Meghji anamtumia vizuri?

  Nimesoma barua na taarifa za Mhe. Meghji katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 16-22 Jan.2008 toleo la 012, uk. 12. Nimeshikwa na butwaa maana zote hazina nukuu za sheria , kanuni na taratibu za serikali ndani ya maelezo yake yote. Katika uandishi wa barua za serikali, unapoandika; kinachokupa mamlaka kwa hoja yoyote ile mara zote ni nukuu za sheria, kanuni na taratibu za serikali. Lazima zitajwe. Kinyume chake ni ngonjera na mawazo binafsi tu! Ndiyo maana barua za serikali nyingi siku hizi ni ndefu mno!

  Hata alipo omba ukaguzi kwa Mthibiti Mkuu wa Hesabu za serikali alipashwa kunukuu vifungu vya kanuni za ukaguzi wa mahesabu ya serikali. Mhe Utoh alifanyakazi kizalendo. Nampongeza. Mwandishi mmoja kati ya hao niliowataja mwanzoni aliwahi kuandika kuwa "baadhi ya viongozi wetu wanapoteuliwa kushika madaraka makubwa hujiona kuwa wana akili maalum, nzuri kuliko za walio chini yao" Ni ukweli usiopingika kuwa leo hii tunao viongozi wenye tabia ya kudharau kutumia nyaraka rasmi za serikali na ushauri wa wataalam walionao. Tabia hii imefikisha taifa letu kukodi kwa gharama kubwa wataalam wengine wenye sifa duni kutoka nje kuja kushughulikia hata matatizo madogo! Ni kwanini hao wanaaminiwa na kuheshimiwa kuliko wataalam wetu na sheria zetu, mimi sijui! Ni aibu kwa Mhe. Meghji na hata prof. Maghembe kusema kuwa walidanganywa!

  Angalia hawa mawaziri ni wasomi wenye hata makabrasha muhimu ya Ngurudoto ambapo fedha nyingi zilitumika kuwa gharamia! Je, waliyaacha Ngurudoto? Nadhani kwa siku za usoni ni busara kuanza na kozi za Ngurudoto kabla ya kugawa madaraka ili wasio elewa wasipewe madaraka KABISA. Serikali makini haijengwi na viongozi wenye kubahatisha juu ya uendesheji na uongozi wa serikali, HAPANA! Ndiyo maana tuna Permanent Secretaries. Eti anafanya hisani kupata ushauri wa katibu mkuu! Mawaziri hawapashwi kufanyakazi na permanent secretaries kwa misingi ya hisani. Kila mmoja analazimika kuona kuwa anamhitaji mwenzake katika uendeshaji wa serikali. Wote wanapashwa ku-review flimsy files kila wakati, kujua ni nini kinaendelea ndani ya wizara/idara.

  Watanzania wamechoka kuona/ kusoma maamuzi ya cabinet na wizara au idara yanakinzana. Pia ni muhimu mawaziri wetu wajenge tabia ya kuelewa kuwa maamuzi ya wizara moja yanagusa wizara nyingine na serikali kwa ujumla. Inauma sana kuona warsha/semina za mara kwa mara hata pale Bungeni wanalipana posho za Jumamosi juu ya posho za kila siku wawapo bungeni, baada ya hapo hakuna tija ya maana na badala yake mtu anaishia kumwambia Rais na watanzania kuwa "nilidanyanywa" Kumbukumbu zinapofutika haraka ng'atuka. Ni Mhe. Meghji huyo huyo alituletea mwekezaji wa kununua shamba la mikoko yetu. Wataalamu wa misitu na waandishi wa habari Mungu bariki walipaza sauti kweli kweli na agenda hiyo mufilisi ikafa kifo cha mende. Katika hilo nani alimdanganya? Kwa tabia hii kuzoea kudanganywa, hivi mhe.Rais wetu hajadanganywa na wakubwa hawa? Ndiyo! Kwani Msabaha hajadanganya juu ya umeme? Je alijiuzulu?Ona! Mwaka jana wakakwepua posho na kuzunguka nchini eti wanaeleza ubora wa bajeti! Mungu wangu! Danganya ya aina yake tu. Sasa kazi ya wabunge wetu ni nini? Si hao ndio wenye kujua lugha na shida zetu? Si walikuwepo Bungeni na ndio walioichambua? Meghji na wenzake wanafikiri hatujui somo la URAIA? Mhe. Meghji, kwa vile ni fundi wa kiingereza naomba nimwambie kuwa "People can be fooled for a while, they can for a while believe stories (rhetorics), that while the pain is here to-day, the gain is around the corner but after a quarter century or more, such stories lose their credibility"

  Ya BOT tumeyaona! Dr. Slaa na Hamadi walipo anzisha sakata la BOT, hadithi, ngonjera kutoka kwa Meghji na Wenzake zilikuwa nyingi. Mimi ni mwana CCM mwenye kadi Na. Ab1478743 kwa vile niliyajua kiasi fulani wote hao wawili Hamad na Slaa niliwatumia message kuwa semeni kwa nguvu tu bungeni. Nilifanya hivyo kwa mapenzi makubwa niliyonayo kwa nchi yangu. Tanzania si nchi ya viongozi tu. Ni yetu wote. Hapa nimethubutu kutaja namba yangu ya CCM kwa kujiamini sana kwa vile nilifundishwa kusema ukweli tu na marehemu J.K. Nyerere – nitatoa mfano hai. Waulizeni wahusika nitakao wataja hapa.

  Siku moja Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Ameir akifuatana na Mhe.Maokola Majogo walikuja Butiama bila taarifa. Walipofika nilikwenda kumwita Mwalimu shambani na njiani alisema kwa masikitiko kwa nini nilichelewa kumpa taarifa kuhusu ujio wa wakubwa hao. Nilimwambia wamekuja ghafla. Kabla ya kuwasalimu Mwalimu alikwenda kusali chumbani kwake na alipotokea aliwauliza kuna jambo gani kubwa ambalo liliwaleta pasipo taarifa. Walijibu kuwa wametumwa na Kamati kuu ya CCM kumweleza kuwa anaaibisha CHAMA kwa kuzungumza na wapinzani Mrema na Sharif. Mwalimu aliuliza walikuja kwa njia gani? Wakajibu kuwa kwa ndege. Akauliza ndege gani? Wakajibu Jet ya Rais. Akauliza tena: ile ambayo nilikuwa natumia? Wakasema ndiyo! Mwalimu aliuliza hivi mnapo niita Baba wa Taifa nilileta maombi (application) serikalini au katika chama niitwe hivyo? Hivi Mrema na Sharif siyo watanzania? Hivi kuunda vyama vya upinzani ni usaliti? Hivi nyinyi CCM kama hamnihitaji kwa ushauri kwa vile mnajua kila kitu basi nisizungumze na vyama vingine? Hivi hamjui kuwa mimi Baba wa Taifa ni above political parties? Mmesema nina kadi namba moja, sawa kwa hiyo mmekuja kunikamata hapa kwetu nilipozaliwa? Maana wewe Ameir ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Majogo Ulinzi? Aliendelea kwa kusema kuwa, kama hilo ndilo lililowaleta na kama mmetumwa na mwenyekiti Mhe.Ali Hassani Mwinyi na kamati yake ya CC basi kuleni chakula na baada ya hapo nitawapa kadi yenu kisha ondokeni! Mimi naijali na kuipenda Tanzania kuliko vyama vyenu, mnasikia?

  Hapo Mhe. Maokola Majogo alijiengua haraka kwa kusema kuwa Mhe. Mwalimu mimi nilipata lift tu kwenye ndege ili nije kukagua ujenzi wa nyumba mpya tunayokujengea wanajeshi. Kisha nilimfuata Mwalimu chumbani kwake na kumsihi asirudishe kadi na akakubali. Hakurudi kuwaaga!

  Nimelazimika kutoa mfano huu wa kweli kwa kuenzi hekima/busara hizo za Baba wa Taifa kwamba wapinzani wanapojenga hoja za msingi zenye maslahi ya Taifa mimi huwapa shime kwa kuongea nao. Hata CCM pia huwapa shime. Nilifanya hivyo kwa mbunge wa Mbarali kupinga ubinafsishaji na kuuzwa kwa mwekezaji wa nje mashamba ya mpunga, pia nilimpongeza kwa simu Mhe. Beatrice Shelukindo katika hoja ya uteuzi wa mabalozi kuwa baadhi hawana sifa na hawaandaliwi. Katika haya niliyoyasema kama yameudhi viongozi wa CCM basi kama Mwalimu alivyofanya kwa Mhe. Ameir nami nitakuwa tayari kurudisha kadi ya CCM!

  Naipenda na kujali Tanzania kuliko vyama ambavyo havina uchungu na UBAKAJI WA RASILIMALI ZETU na vyenye viongozi waliojaza pamba masikioni na macho yasiyoona ukweli! Tunaimba kumuenzi Baba wa Taifa lakini matendo hayafanani! Nasema nje ya nchi yapo mataifa yanayomuenzi Mwalimu kuliko sisi. Nendeni kwa Mhe Kagame. Pamoja na matatizo ya vita uchumi wao haupangwi na kuendeshwa kisanii kama Tanzania. Hata wanavyo sherehekea Mwalimu DAY utafikiri alikuwa Rais wao! wametumia mawazo yake vizuri zaidi kuliko sisi! Na hayo mnayo yafanya (BOT) kwenye rasilimali za nchi kama Madini n.k angekuwa hai, nasema huo ndio ungekuwa ugonjwa wa kumua haraka kuliko ugonjwa wa LUKIMYA. Kuna wakati aliniambia juu ya mambo ya ovyo yanayofanywa na viongozi serikalini na akalia machozi. Tusema nini ndipo msikie sasa? The poor in Tanzania are now left to fend for themselves. When they speak no one listerns. When someone listerns they are told nothing can be done! Tunaambiwa sisi ni wavivu!

  Naomba niseme kwa msisitizo mkubwa kuwa CCM na serikali, vyote vina taratibu nzuri tu. Maandishi hayo kimsingi yanalenga viongozi maalum kama hao wanaovuruga nchi hii kwa rhetorics za kuondoa umasikini kudumisha amani na mshikamano….eti Tanzania kisiwa cha amani n.k. huku wakitumia kiburi kuvurugwa kwa raslimali za nchi.

  Kwa mfano wote hao wamekopeshwa magari (mawaziri, makatibu wakuu) wote. Lakini kwenda kazini na kurudi nyumbani bado wanatumia magari ya serikali, pia wanazurura nayo hata likizoni bila aibu. Hata kama ni stahili je hizi zina morals?. Katika hili nashauri viongozi wetu waende kwa Mhe KagameRwanda waone magari ya serikali yanavyotumika. Kule hakuna mzaha!. Kwetu hapa katika Wizara moja tu utakuta aina ( miundo) zaidi ya sita na hili limeshuka hadi kwenye halmashauri za Wilaya n.k. Nani katuloga? Je, katika haya huwa tunafanya faithful decisions? kwanini tumekuwa ni mafundi wa kuiga mambo ya hovyo kila wakati? Bungeni kwanini tumeharakisha kutunga sheria za ugaidi na haya tunayapuuza? Hivi ni lazima kila kitu tuaambiwe na mataifa makubwa au mashirika ya wakubwa? Hivi ndivyo tunavyojenga amani na mshikamano? Stahili zao ni pamoja na kuishi nyumba za serikali bure, wanalipiwa umeme, maji, simu, watumishi wawili, dereva wa kuendesha gari binafsi na samani za nyumba na vyombo vya chakula. Ona sasa tumepandishiwa bei ya umeme wakati tunalalamikia mafuta ya taa!

  Hawa tukiwasema ati wanajibu kwa kiburi tunatukana serikali au CCM! Hapana huo ni uhuni. Ni ukweli CCM na serikali hawako hivyo. Hawa ni wahuni waliojificha katika CCM na kana kwamba hayo hayatoshi wanachezea kapu kuu la fedha zetu za serikali (BOT). Kweli tunyamaze??

  Ona alivyosema CASTILLO wa Guatemala kuhusu wabakaji/wakwepuaji wa raslimali za nchi; namnukuu kiingereza (naomba radhi): -"One day the apolitical intellectuals of my country will be interrogated by the simplest of our people. They will be asked what they did when their nation died out slowly like a sweet fire small and alone. No one will ask them about their dress their long siestas after lunch. No one will want to know about their sterile combats with the ideas of nothing. No one will care about their higher financial Learning. They won't be questioned on Greek mythology or regarding their self disgust when someone within them begins to die the coward's death. They will be asked nothing about their absurd justifications born in the shadow of total lie. On that day the simple men will come.Those who have no place in the books and poems of the apolitical intellectuals but daily delivered their bread and milk, their tortillas and eggs those who mended their clothes, those who drove their cars, those who cared for their dogs and gardens and worked for them and they will ask: WHAT DID YOU DO WHEN THE POOR SUFFERED WHEN TENDERNESS AND LIFE BURNED OUT IN THEM? We, the African students and intellectuals, what shall we say when we are asked by simple MEN AND WOMEN; WHAT DID YOU DO WHEN THE POOR SUFFERED, WHEN TENDERNESS AND LIFE BURNED OUT IN THEM?

  Oneni hekima hiyo. Meghji kasoma ana elimu nzuri tu. Pamoja na hayo ya elimu yake, je ana hekima kusema alidanganywa? Na wote wale wanaofanana naye ni vema wakazingatia pia mawaidha ya Charles Mloka (16/01/1983) aliposema: "Ingawa elimu ni bora, hekima bora zaidi. Hekima ndiyo heshima, ya elimu ikafaa. Hii ndiyo sifa njema, hata ukisoma sana. Hekima huleta jibu, watu linalovusha. Babu zetu hapo zamani hekima walithamini.Uongozi wa hekima ulileta kuungana. Watu waliishi vema, wakiwa wanapatana. Hii tushike sana, utu ufike kilele. Hekima ndiyo uhuru wa watu wowote wale hekima huleta nuru, ya watu kuenda mbele ingawa elimu bora. Hekima bora zaidi!" (nimenukuu vipengele vihusuvyo mada yangu tu)

  Marehemu Baba wa Taifa katika mojawapo ya hotuba zake kwa viongozi wenzake kuhusu maadili na uwajibikaji aliwahi kusema "Mtu unapofanya kosa na ukalikubali na kuomba radhi bila kusingizia wengine… wewe unahesabika kuwa una hekima, uungwana na busara ni mtu wa kutumainiwa kwa kupewa hata madaraka makubwa hapo baadaye". Mwishoni mwaka jana katika taasisi moja Uingereza zilipotea nyaraka muhimu. Waziri mkuu G. Brown alikwenda Bungeni haraka kuomba nchi radhi. Huu ndio uadilifu. Ndiyo uungwana. Kwa vile mada yangu inahusu UADIIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI WETU.

  Sasa kwa kuzingatia yote haya na hekima za Baba wa Taifa nachapisha hapa kikamilifu barua ya Mhe. Ali Hassani Mwinyi kwa yale yaliyotokea shinyanga mwaka 1975 yeye akiwa Waziri wa Mambo ya ndani kwa lengo la kuona kama huo utakuwa ni msaada wa mwisho kwa Mhe. Meghji na wenzake kufuata nyayo. Barua yenyewe inasema hivi; tufuatane kwa kuisoma kwa makini tafadhali.

  Baada ya kusoma barua ya mhe. Ali Hassani Mwinyi, unaona uadilifu, uwajibikaji na unyenyekevu uliotukuka? Hiyo ndiyo hali halisi inavyotakiwa yaani; hayo yaonekane yakitendeka! Hivi tunaposema kuenzi busara za viongozi wetu maana yake nini hasa? Ni kweli tunawaenzi kwa vitendo? Yetu ni masikio na macho. Kujiuzulu kama alivyofanya Mhe. Ali Hassani Mwinyi sio ujinga. Ni uungwana , ustaarabu na ni kusafisha njia ili haki iweze kutendeka pasipo kuharibu imani ya wanachi ndani ya taasisi husika. Kurudisha imani iliyopotea kuna gharama kubwa. Wakubwa hili mnalijua.

  Sambamba na barua ya Mhe. Mwinyi hapo juu, Professor Joseph Stiglitz, mtaalamu wa uchumi, ona aliyoyafanya kwa kuona kuwa Ikulu Marekani sera za Rais Clinton juu ya utandawazi zilikuwa zinakandamiza nchi masikini sisi tukiwemo. Kwa maneno yake anasema: " When I was about to leave the white house for the world bank, President Clinton asked me to stay on as chairman of his council of Economic Advisors and as member of his cabinet. I declined, because I thought the task of designing policies and programs that would do something about the abject poverty which plagued the less developed world was a far more important challenge… I had seen countries where poverty was increasing rather than decreasing, I had see what that meant-not just in statistics but in real lives of people".

  Huyu sasa ni mwalimu tu-professor of economics and finance University of Columbia. Catrina ilipotokea marekani nako viongozi kadhaa walijiuzulu.

  Unaona wenzetu wanavyojiuzulu kistaarabu. Msabaha, Mramba, Karamagi, Meghji, Ballali nchini Tanzania wamekataa kujiuzulu. Hapa kwetu hotuba zimejaa takwimu ambazo hazina uhusiano kabisa na hali halisi ya maisha ya watanzania! Tunazunguka nchi eti tuna bajeti nzuri n.k na uchumi unapaa! Tunamdanganya Rais na tunawadanganya Watanzania mchana kweupe na kwa kiburi. Vipaumbele katika bajeti zetu vinatisha! Kana kwamba hayatoshi Mramba juzi juzi kama Karamagi kaweka sahihi mkataba wa hovyo wa EPA. Huyu sasa kaleta sumu kali - TINDIKALI MACHONI ya kuua biashara na viwanda vyetu. Tarehe 26/01/2003 Rais Lula Da Silva alisema;
  Any export we might make will be worth nothing if rich countries continue to preach free trade and practice protectionism.

  Mhe. Mramba ona; Nothern governments now spend $ 1 billion a day on agricultural subsidies. Amounting 6 times their spending on aid. Subsidies generate large surpluses that are dumped on world markets at prices bearing nothing to production costs. Millions of farmers in developing countries receive lower prices for their products and get pushed out of markets of the powerful nations. To add insult to financial injury, rich countries impose higher taxes on processed goods than on raw materials. Mramba ajue kwamba advanced industrial countries which dictate the direction of globalization have not yet developed the underlying sympathies which are necessary to make the global economy work. Kwanini Mramba hatumii wataalam ofisini au chuo kikuu kabla ya kukurupuka?

  Hivi haya, Mhe. Mramba na ujanja wote alionao wa kutwambia tule majani hayajui kweli? Amuulize Prof Samwel Wangwe MNEC, prof Ndulu, prof Shivji, prof Baregu, Iddi Simba kwa yaliyojiri DOHA, Joseph Mihangwa, prof Joseph Stiglitz na prof A.Safari maana ya nukuu hiyo hapo juu. Kwa hapa watanzania walipofikia sampuli hii ya mawaziri na watendaji wanaofanana nao ni muhimu wakajua kuwa kama nchi tayari kuna idadi isiyo haba ya informed citizensary which is more likely to provide some checks against abuses of power/ office! Si busara kumkasirisha Rais, si busara kukasirisha viongozi wa dini. Si busara wananchi kupoteza imani kwa serikali waliyochagua. Bunge letu lina wasomi wengi wazuri . Muhimu wachangamkie maendeleo. Serikali ijue wajibu wake katika kuleta maendeleo. Muhimu kwa akina Mramba, Karamagi, Meghji wasaidiwe kuona njia sahihi ya maendeleo.

  Mwisho nasema watu walipokufa shinyanga mwaka 1975, mhe. Mwinyi kwa kusutwa na dhamira yake ya kukosa amani moyoni ( yeye hakushiriki mauaji wahusika walimficha) kwa hiari yake na kwa unyenyekevu mkubwa tarehe 22/01/1977 aliandika barua kwa Rais Nyerere ya kujiuzulu uwaziri. Tayari tumesoma hapo nyuma. Katika hili sakata la BOT na uporaji wa raslimali zetu ikiwa ni pamoja na wanyama kuuzwa kwa bei za kutupwa, waheshimiwa Meghji, Mramba, Karamagi, Yona, Msabaha tayari wamekwisha fanya mauaji makubwa ya watanzania kuliko yale ya Shinyanga. Kuua si lazima iwe kwa silaha au sumu tu. Unaweza kuua kwa kutotoa fedha za kununulia dawa na zana nyingine za tiba kwa wakati. Kwa kipindi ambacho mabillioni hayo ya fedha yalipoibwa BOT na kwingineko, hospitali zingetoa takwimu za watanzania waliokufa kwa kukosa nyenzo muhimu za tiba taifa letu lingetikisika. Kwa kutojali sasa ni kawaida mawaziri na vigogo wengine wanatibiwa India, Marekani na ulaya hata kwa ugonjwa wa mafua tu. Mwalimu alianzisha mradi wa hospitali ya Lugalo (JWTZ) kwa lengo la viongozi pamoja na Rais kutibiwa hapo kama inavyofanyika Marekani, lakini nani anajali kupaendeleza? Yawezekana nako tukabinafsisha, nani ajuae kwa staili hii ya viongozi wenye kuabudu utandawazi (MJOMBA MWEKEZAJI)! Tunao madaktari wenye ujuzi mkubwa tu lakini shida ni vifaa na miundo mbinu. Someni hotuba ya Mwl JK. Nyerere bungeni ya mwaka 1985

  Fedha zilizoporwa na tunazopoteza kupitia mikataba mibovu zimeua/zimedhoofisha asilimia kubwa tu ya watoto wetu waliostahili kupata elimu nzuri/bora hapa nchini. Fedha hizo kama walivyokwisha sema waandishi wa habari (tunaowadharau na kuhujumu juhudi zao na kusifia waandishi wa nje) zingesaidia kuboresha majengo ya vyuo vikuu vya mlimani (DSM), Muhimbili na Sokoine. Hali ilivyo sasa mlimani, binafsi naona aibu kusema kuwa nilisoma hapo! Kwa taarifa yenu yale majengo ya awali ya mlimani yalikuwa na hadhi ya kimataifa ikiwa ni pamoja na chakula tulichokuwa tunapata kama wanafunzi. Hata Baba wa Taifa ilikuwa ni kawaida yake kuja kushiriki nasi katika chakula cha jioni kila mwaka-ANNUAL DINNER! Pia ilikuwa ni kawaida yake mara nyingi kuja kuzungumza nasi (siyo kutuhutubia na kufoka).

  Mwaka jana nilibahatika kutembelea chuo kikuu cha sokoine morogoro. Ukiona majengo ya kitengo cha mifugo, karakana na sehemu za kuhifadhi vyakula vya mifugo n.k. hutaamini kuwa hiyo ndiyo taasisi namba moja ya kutoa wataalamu wa kilimo tunacho imba kuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Madaraja muhimu yaendayo kwenye mashamba muhimu ya majaribio ndani ya chuo yamekatika. Gharama za kuyarejesha katika hali yake chuo hakiwezi kumudu. Lakini wakubwa wamekwapua BOT. katika hatua ya kuchukiza sana utakuta baadhi ya viongozi wakitembelea chuo hicho au mkoa wa Morogoro wanachota miche, madume au mitamba yenye ubora wa hali ya juu ati kama zawadi! Kuna wakubwa fulani wamezoea kutumia raslimali za vyuo vikuu kuendeshea kampeni zao za uchaguzi. Hali ya sekondari zetu hasa zile za kabla na baada ya uhuru sina la kusema!! Nilibahatika pia kutembelea sekondari za Musoma, Ilboru, Mzumbe, Pugu, Bwiru, Old Moshi na Minaki. Niliyoyaona ndani ya madarasa, maabara, mabweni na nyumba za walimu ni siri yangu yenye kusababisha kilio cha machozi ya damu. Basil Davidson aliwahi kuandika kitabu chake cha historia akakiita WHICH WAY AFRICA, Hayo niliyo yaona katika shule zetu na sasa kusikia ukwapuaji wa mabillioni BOT natamani kuandika kitabu na nikiite WHICH WAY TANZANIA! Kabla sijafanya hivyo niombe tu kwa unyenyekevu kuwa fedha hizo zitakaporejeshwa, na iwe mapema, basi nyingi zimwagwe kwenye kuwekeza katika elimu na afya.

  Sambamba na hayo nitoe ushauri tu kuwa ili kufanya gawio la busara katika wizara mbali mbali, Waziri wa fedha ajenge tabia ya kutembelea maeneo yenye matatizo makubwa. Pia wakuu wa mikoa/wilaya waache taabia za kumpangia Rais ratiba zenye mafanikio tu: sehemu kubwa ya ratiba zao wamwonyeshe yeye na Waziri Mkuu mambo yenye utata ili wakuu wetu waachane na aibu ya kutumia fedha za wafadhili kujengea vyoo shuleni n.k

  Naomba kuhitimisha kwa kutoa mchango wangu kwa chief Whipp, Mhe Dr. Batilda na Mwanasheria Mkuu Mhe Mwanyika kuwa kwa haya yaliyotokea BoT na tatizo la madini. Si busara kumfanya Rais kuchukua nafasi zao bungeni. Wao walishiriki kwa nguvu kubwa kuua sauti za wabunge wa upinzani Bungeni. Kwa haya yaliyotokea wanalo la kusema? Mijadala yenye maslahi ya nchi siyo ya kufanyia usanii/mzaha Bungeni. Ni muhimu hawa wawe " focused" wamsaidie spika na Taifa. Kwa wabunge kama Gallinoma, Dr Mwakyembe, Anne Kilango, W. Shelukindo, Ibrahim Sanya, Hamad, Dr Slaa, Zitto hawa ni watu very serious, tujifunze kutoka kwao tafadhali.

  Kwa waandishi wa habari nawashukuru kwa dhati na nawatakia kazi njema. Katika kitabu chake " UONGOZI NA HATIMA YA TANZANIA" marehemu baba wa Taifa alisema: "OLE WAKE TANZANIA TUSIPOISAIDIA" Niwezalo nimefanya, kushauri na kuonya. Nasi tumsaidie (Rais J.M. Kikwete) Mhe. Meghji na wenzake kwa unyenyekevu nawaomba mtafakari haya tafadhali. Haitoshi kutuambia Ballali alidanganya. Mlikuwa wapi? Watanzania bado tunasubiri kuambiwa na Meghji ni kikao gani cha serikali na ni sheria zipi za serikali zilimruhusu Meghji kutenda aliyoyatenda. Hata anaposema maswala nyeti yenye usalama wa nchi – hayo yote atueleze ni kwa mujibu wa sheria na vikao vipi? Je barua hiyo ya Mhe. Mwinyi itakuwa ya msaada na angalizo mwafaka katika medani za uadilifu na uwajibikaji? TAFAKARI!!

  S. H. Kasori

  0754372141
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 24, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  How did we miss this.. ! ? duh kuna makubwa yalitupita hapa..
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  MKJJ,

  tulishaiona hiyo, nahisi ilipostiwa mara mbili......moja ikiwa ktk mjadala mkali kuhusu kumtaka Bi Meghji na wenzake wajiuzulu.

  Kwa hili Mzee Kasori alizungumzia right on time!!..........na post yake ni valid mpaka leo hii kwani bado wako viongozi wengi tunahitaji wawajibike/wawajibishwe na kuwaachia wachapa kazi waadilifu.
   
 4. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Mbona sijaiona barua aliyoandika Mzee Mwinyi kwa Mwalimu in 1975 kuhusu mauaji?
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Mar 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwili umenisisimka.... Duh, kumbe tupo wengi tunaoipenda Tanzania.
  MUNGU AKULINDE, AKUBALIKI... Mh. ndugu yetu KASORI
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa Mkandara,

  inatia moyo kuona kuwa watu kama hawa bado wanaishi huko Tanzania ambako Manji, Rostam, na Viti-rada wanakula nchi kama hawana akili vile na kupewa baraka zote na top brass ya nchi!
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nimefurahi sana kuona maoni ya Mzee Kasori, namfahamu mzee huyu first hand na katika pitapita siku moja alinichachafya sana, ni very smart kwenye kazi, kwenye gari lake na hata mavazi yake. Na sasa naona hata dhamira yake na roho yake. Thank God wazee wetu wenye akili na kutupenda vijana wao na nchi yao wanatufundisha ukweli. Tunashukuru kwa maoni yako mzee.
   
 8. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Yes we can... Yes we can... Yes we did ... Yes we did... Shukrani kwa Wapiganaji wote popote mlipo! hakika hii si nchi ya Mafisadi peke yao, Tanzania itabaki kuwa Tanzania ya Watanzania Daima...
   
 9. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #9
  Nov 26, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Ndugu Kasori,
  That is what I was saying ,kwamba kuna irregularities in what you are writing,inconsistency and ambiguity.
  Ingawa sasa hivi I cannot accuse you of ambiguity. Huyu Valentine Mokiwa is a straight talker. If you talk to him,you will not go away guessing at his meaning,what he was trying to say to you.

  What you are writiing now is very clear. Unaandika maneono ya kumkashifu Mwalimu Nyerere.
  Wewe ulikuwa umeajiriwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere. You were a servant in his house. We cannot always call people like you Civil Servants,you are just hired servants. Kwa hiyo ulitakiwa kuonyesha loyalty kwa Mwalimu.

  Sasa unatuambia Lowasa alitaka kuamuru Mwalimu aende Monduli kulisafisha jina lake.
  Halafu sasa unatuambia,CCM haikupendezwa Mwalimu kuongea na Wapinzani,hususan, Mrema,na Seif Hammad. Kwa hiyo,siku moja,wakatuma ndege Butiama to arrest Mwalimu,
  Ameir,waziri wa mambo ya ndani,na majogo,waziri wa ulinzi.

  Hizi story ni kashfa tu. We have heard enough. If you have any more such stories,keep them to yourself. Mambo ya zamani yasizungumzwe,zipo statute of limitation laws. Watu kama ni waouvu,lama walitenda uovu zamani,watatenda uovu leo pia. Tusahau ya zamani.

  Let us focus our minds on these people,ambao inaelekea wameliibia Taifa.Let us be united in what we want to do,tusiongee kuhusu" agreeing to disagree."
  Pia tusiongee juu ya tindikali,lest we be sent to the psychiatrist.
  Tuna matatizo ya uchumi,and we have to clever like Prof. Stiglitz
   
 10. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Ganesh, Naona Mzee kasori anakupa maumivu yasiyokuwa yakawaida... kama hujui ulikotoka si rahisi kujua uendako!!!
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Someone:
  Gimme a Gun. I wanna kill.
   
 12. M

  Mama JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Why? This statement can lead you to a ban from Silencer. You can modify or delete the post if you like.
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mama,

  To Mama, How about this - I feel like I wanna tear somebody apart with my bare hands.

  To Ganesh - you must be the luckiest sob on earth, how I wish I could lay those hands on you.

  To fellow Tanzanians it time for me and you to be asked by the simplest of peoples:-

  - what did we do when their nation died out slowly like a sweet fire, small and alone ?

  - What did we do when the poor suffered, when tenderness and life burnt out in them ?

  Yeah it is time and thank you Kasori, may you live long enough to see the tide turn against all those that have driven our beloved country to its knees.
   
 14. M

  Mama JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  That one is good any way.
   
 15. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Makubwa yanawapita Kijijini kwa kukosa uhondo kama huu, hivyo basi MKJJ jaribu kutoa nakala kwenye CHECHE
   
 16. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #16
  Nov 27, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  No.I do not agree. A Silencer is not needed to silence this mama mag3. I do not have a problem,about what she is saying to me.that she would like to tear me apart with her bare hands.
  That is what happens with these discussion forums,people take them too seriously.
  It is obvious kwamba umehadaiwa na huyu Kasori. As that other fellow was saying,kwamba anamfahamu Kasori,ni mtu maridadi,katika mavazi yake na gari lake. Hiyu Kasori ni smooth,sleek,and untrustworthy. Anamtukana Mwalimu Nyerere katika makala zake,halafu anazivisha makala zake na joho kubwa za bla bla nyingi za uzalendo.
  Huyu ni Civil Servant,sasa hivi yupo Arusha anafanya kazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,ambaye,nadhani ni Isidore Shirima. Sasa anaandika mambo ambayo yanaonyesha kwamba hana loyalty kwa CCM,au kwa Serkali. Loyalty ni kitu cha kwanza kwa mfanya kazi yoyote,popote anapofanya kazi. Not just integrity,but also loyalty. Watu wanapandishwa vyeo kwa kuwa na loyalty. Watu wanaopanda cheo katika Serkali ya Kikwete,ni wale wanaomsifu Kikwete,hata kama wamelewa chakari bado wanmsifu Kiwkete.
  It is not, without reason,kwamba Kasori anasema kwamba,ikiwa vipi au nini,yuko tayari kuirudusha kadi yeke ya CCM. Kwa sababu akianza kuongea mambo kama hayo,ni lazima awe tayari kuiruduisha kadi,kama ikibidi.
  Kasori yupo Arusha,na Lowasa yupo Arusha. How do we know that he is not writing these things and later going to laugh and chat with Lowasa? I am not suggesting that he does not have the right to laugh and chat with any one he likes.

  What I am saying is that he probably was attracting these abusive persons to come and abuse Mwalimu. It is unlikely kwamba Butiku au Batao wanazo hadithi nyingi juu ya watu kuja kubishana na Mwalimu wakati wao walipokuwa wanafanya kazi pale.

  Haimsaidii mtu yeyote kwa Kasori kuongea maneno kama haya sasa. Na CCM wakigundua,labda kuna mtu atakwenda kumpigia hodi Kasori,usiku wa manane.
   
 17. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Tunajua kuwa Mafisadi mmezoea kuua na mara nyingi mkikosa damu za watu huwa mnatetemeka!! Ganesh Tafadhali zudia kuzisoma upya alichokiandika Mzee Kasori then Linganisha na hali halisi ya Maisha ya Mtanzania...
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Did I read the same article you read or are there 2 articles by Kasori?
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Im also confused!
   
 20. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #20
  Nov 28, 2008
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sipati picha kumbe mwenzetu umeikimbia nyumba yako? Hali ikiwa shwari tusikusikie unakuja kugombea Ubunge huku. wanaume tumekomaa tutapigania haki za vizazi vyetu TUKIWA HAPA HAPA TABORA.
   
Loading...