Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Nionacho mimi wala sio FAME, bali ni pale jambo linapokugusa kwa karibu. Ufisadi watu wengi hawau-feel directly na ndio maana sio wengi wanaopiga kelele.

Alichofanya Mengi ni kukoroga kidogo jambo lililopelekea kuwa na muendelezo wa vita dhidi ya MAFISADI. Sio mbaya watu wakiendelea kutetea "keki zao" hadharani, maana hapa ndipo tunapogutuka nani yuko upande upi na kutambua upana wa tatizo hili. Kwa njia hii utatuzi utakuwa rahisi.

Hatimaye mwananchi wa kawaida naye ataguswa kwa karibu, hapo ndipo atapotetea keki ambayo amekuwa akiikosa. Baada ya Mengi - maji kwenye mtungi yakitulia, tunahitaji mdau mwingine kulikoroga kidogo. :)
 
Hapa ndio nikasema kuna makundi utaona Pinda yupo na Mengi ,CCm Yanga wapo na Manji na sijui CCM Tabora wapo na Rostam ,Chadema wapo na Mengi ,Je huu ni upinzani hamuoni kuwa mnachezeshwa gwaride la kushoto na kulia.

Ni lazima upinzani ujitenge kabisa na watu hawa ,mnapoambiwa kuwa CCM yote ni corruption basi muwe na mkakati wa kweli kusimamia hoja hio na isionekane mnayumba ,

Ni lazima upinzani uende kivyakevyake iwatenge wananchi na Sultani CCM kwa kutumia vyanzo vyake na sio kutegemea vita vilivyomo ndani ya mitandao ya CCM.
 
``He (Mengi) has exercised freedom of speech enshrined in the constitution. It is for those implicated to react. If they want to go to court it’s upon them to decide. It is better for Tanzanians to be careful when commenting on issues pending in court,`` Pinda said.


Very diplomatic. Sophia Simba sijui ni member hapa JamiiForum asome hii? :)
 
``He (Mengi) has exercised freedom of speech enshrined in the constitution. It is for those implicated to react. If they want to go to court it’s upon them to decide...

Sofia Simba na Mkuchika hapa wameumbuliwa na bosi wao... Km mengi anavyouliza hawa mafisadi wamepata wapi kiburi cha kuendelea kunyanyasa wananchi, ndivyo hivyohivyo tujiulize Mengi kapata wapi ujasiri wa kuendelea na anayoendelea nayo sasa?? Kwa statement hiyo ya Pinda mhhh.... hili sakata bado bichi!
 
Natamani hivyo kaka, natamani niandamane uchi kutoka Gongolamboto, kupitia buguruni, kariakoo, , niingie bibi titi nimalizie IKULU, natamani dunia ijjue mtamsema weeeeeeeeeeeeee RA, kumbe cha mtoto kuna watu wanakula fedha kila kona, rangi zao nyeusi tii kuliko mimi, ! CCM has to GO!!! that is solution!!!!!! tukilala tukiamka hakuna kumsifia Mwakyembe wala Kilango wote wako dampo, wote waondoke madarakani! tumewapa mika 40 inatosha, inatosha, inatosha uuuuuuuuwiiiiii!

Mimi na wewe tukipambana ipasavyo tutaing'oa madarakani
 
Nataka Kumjua baba wa Mafisadi,Nani anawalea mafisadi?

Mie nimeona sasa Mengi ameenda mbali sana,Katumia Vyombo vyake vya habari vibaya sana na mpaka sasa nashindwa kuelewa ni kwanini Jukwaa la Habari limekaa kimya kuhusiana na habari hii.Tukiachia mambo kama haya siku mtu anweza kuamua kuwatangazia UMMA mambo ya ajbu ajabu tu!

Kama anajua Kila "flani" ni mapapa basi atuambie baba yao ni nani?hauwezi kuwa papa kama haujazaliwa na papa,na hauwezi kuishi kwa ujanja tu bila ya kulelewa na PAPA.Kwa maana nyingine aseme tu kuwa Na "flani" ni papa,awaorodheshe!

Inawezekana Mengi anawaju wazazi wa hawa Mapapa,ila kwa suala hili la kuchonga juzi mie nasema mzee amechemka,na maejenga chuki kati ya watu na pia ameleta "Ukaburu"!

Kama asipotaja baba wa Mapapa,anayawealea mapapa mie nitandelea na msimamo wangu kuwa Mengi ameamua kuwachafua kina RA na wenzake!

Tabia ya mtu kutaka Sympathy kwa wanachi imepitwa na wakati,

Yes,Mengi najua unaweza kuwataja wazazi wa hao mapapa.Come on do it Now!
HI Gembe,
You are here again, sioni kama proposal yake iko constructive ukichukulia nchi yenyewe unayoiongelea.

1. Wewe unataka evidence gani zaidi ya evidence zote zilizotolewa (EPA, KAGODA, RICHMOND, RADAR, NDEGE YA RAIS) kuwa Rosatm ni fisadi au hao aliowataja kuwa ni mafisadi? Hao wote waliotajwa aidha kesi zao zipo mahakamani au washasemwa na mafaili yao yapo kwa prosecuotor ameyakalia tu. What kind of evidence you want? or you're just jumping on the Sophia Simba wagon as a member of payroll?

2. Kama tungekuwa makini; nyie mnaotetea kuwa Tanzania kuna vyombo vya sheria na usalama kwa usalama wa Taifa; mmeshaona FBI wanvyofanya kazi lakini? Wakisikia rumours tu kama zile ambazo amezitoa Mengi, wangeshaenda zamani na kumtengenezea faili Mengi ili awape habari zaidi. Kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya vyombo vya Usalama. Sasa hapa kwetu allegations kubwa kama hizi kwa nini hizi FBI zetu ziko kimya? Usimlaumu Mengi laumu system ambayo ni mbovu!!

3. You know exactly, the biggest culprit of all these events and the beneficiary; the man at the top!
 
Pinda alichosema ndicho cha kweli. Hawa viongozi njaa wakina Simba na Mkuchika sijui wanaugonjwa gani. Wameng'ang'ania tu kwamba Mengi katumia media yake kuwasema mafisadi papa wakati Mengi aliita waandishi kutoka media zote na ku release statement yake. Matangazo yote yalitoka katika vyombo vyote vya habari na si vile vya IPP pekee kama wanavyotaka kutulazimisha tuamini mawakili wa Mengi akina Simba.
Binafsi niliona kwa mara ya kwanza habari hii kwenye TBC1 ingawa nilikuja kuiona kwa kirefu ITV sasa kosa la Mengi ni lipi? Watu wana behave kama hawakwenda shule vile?
Pinda alichosema ndicho Mengi alichosema alipoulizwa je hadhani anajiweka katika hatari ya kushitakiwa mahakamani kwa kuwataja kwa identity zao hao wezi wakubwa wa nchi hii?
Bravo Pinda hapo umesema sawia. Aliyeumia including wapambe wa wahindi wezi hawa waende mahakamani na wasimshitaki Mengi tu bali waishitaki hata jf na hata mzee mwanakijiji kwa kuwasema wazi wazi katika Cheche.
 
Very diplomatic. Sophia Simba sijui ni member hapa JamiiForum asome hii? :)

Hivi huyo Sofia kweli zimo? manake hata kama angekuwa anataka kuongea jambo la msingi kwanini atumie ushangingi namna ile utadhani yuko kitchen party?

Just imagine waziri mzima anaanza, IPP wapo hapa?... watupishe..
...Nasema kachemsha!!!..

What .. what ? Huyo ndo waziri mwenye dhamana???
 
Sasa hapa katika watu wanaojua misingi ya utawala ya "collective responsibility" inabidi Sofia Simba aombe radhi, kwa sababu mkulu wake (PM Pinda) kashatoa msimamo unaopingana na wake (Simba).Hii ni muhimu ili tujue kuwa msimamo wa Pinda ndiyo official stand ya serikali.

Ama kama Simba anaona hakubaliani na msimamo alioutoa Pinda, anaweza kujiuzulu, lakini hatuwezi kuwa na serikali iliyo shaghalabaghala, huku Waziri Simba kasema moja na Waziri Mkuu Pinda kasema kingine.

Waandishi wako wapi, story hiyo.
 
Hapa ndio nikasema kuna makundi utaona Pinda yupo na Mengi ,CCm Yanga wapo na Manji na sijui CCM Tabora wapo na Rostam ,Chadema wapo na Mengi ,Je huu ni upinzani hamuoni kuwa mnachezeshwa gwaride la kushoto na kulia.

Ni lazima upinzani ujitenge kabisa na watu hawa ,mnapoambiwa kuwa CCM yote ni corruption basi muwe na mkakati wa kweli kusimamia hoja hio na isionekane mnayumba ,

Ni lazima upinzani uende kivyakevyake iwatenge wananchi na Sultani CCM kwa kutumia vyanzo vyake na sio kutegemea vita vilivyomo ndani ya mitandao ya CCM.

Kama ndiyo tafasiri, basi unaweza kusema pia LIpumba yupo na Simba na Mkuchika, kwa hiyo dots zingaungana na linakuwa duara.
Mimi nadhani jambo la msingi ni pale panapokuwa na ukweli basi hatuna budi kusimama katika kweli!
 
Kama ndiyo tafasiri, basi unaweza kusema pia LIpumba yupo na Simba na Mkuchika, kwa hiyo dots zingaungana na linakuwa duara.
Mimi nadhani jambo la msingi ni pale panapokuwa na ukweli basi hatuna budi kusimama katika kweli!

Kama ni Lipumba yule yule ninayemfahamu aliyesema niliyosoma na kuyasikia kuhusu Mengi, basi kafu imekwisha, kwani imebadilisha muelekeo ya vita na sasa wanapiga risasi ovyoooooooooooooo. Jamani kuweni macho nao maana risasi inaweza kumpata hata mwa kafu mwenyewe. Mwiba, wasaidie viongozi wako waelewe kuwa kama wataendelea kupambana kwa jinsi hii hawataweza kushinda uchaguzi wowote asilani. Vita ya ufisadi ni ngumu na si maneno ya uoga uoga tu. Hapa ni lazima uwe kinyume nao kwa kila namna na ikiwezekana jela uonje lakini iko siku ya kufanikiwa tu na kula matunda ya mapambano.
 
Ni lazima Pinda amtetee Mengi. Atamtetea nani. Hana political weight Tanzania. Ni lazima ajitengenezee mkakati wa kubakia kwenye nafasi hiyo hata baada ya uchaguzi ujao. Mtaona mwaka huu na mwaka ujao kila mwenye uwezo atakayejitokeza atamtetea ili mradi naye atengeneze force kwa maandalizi ya uchaguzi ujao na kurtetea nafasi yake ya uwaziri mkuu. Vinginevyo mtamlaumu akianza tena kulia hadharani.
 
Hapa ndio nikasema kuna makundi utaona Pinda yupo na Mengi ,CCm Yanga wapo na Manji na sijui CCM Tabora wapo na Rostam ,Chadema wapo na Mengi ,Je huu ni upinzani hamuoni kuwa mnachezeshwa gwaride la kushoto na kulia.

Ni lazima upinzani ujitenge kabisa na watu hawa ,mnapoambiwa kuwa CCM yote ni corruption basi muwe na mkakati wa kweli kusimamia hoja hio na isionekane mnayumba ,

Ni lazima upinzani uende kivyakevyake iwatenge wananchi na Sultani CCM kwa kutumia vyanzo vyake na sio kutegemea vita vilivyomo ndani ya mitandao ya CCM.

Waambie waambie hao. Na Lipumba na CUF wako na Rostam na Manji kumsulubu Mengi.

.....ndiyohiyo
 
Where are leaders like Edward Sokoine during times like this? I guess they are there kama wakina Dr. Slaa but we need a man like that who is within the government. Which leader within the government is going to stand up & say enough is enough. Nadhani neno "uzalendo" halipo kwenye vocabulary zetu tena.
 
Nipashe ya leo tarehe 1 mei 2009 imeandika kichwa cha habari kifuatacho."Kilango awashukia wanaotetea mafisadi" na aya ya tatu imeandikwa ifuatavyo :
Pia ,hafla hio licha ya kumpongeza Mwenyekiti wa IPPkwa ujasiri wa kutaja Watanzania wenye asili ya kiasia na madhara yao hadharani,.....Huu ni ubaguzi tena wa Hitler kwa kuwa wapo waasia wengi tu ambao hawana tatizo na mtu
 
Nipashe ya leo tarehe 1 mei 2009 imeandika kichwa cha habari kifuatacho."Kilango awashukia wanaotetea mafisadi" na aya ya tatu imeandikwa ifuatavyo :
Pia ,hafla hio licha ya kumpongeza Mwenyekiti wa IPPkwa ujasiri wa kutaja Watanzania wenye asili ya kiasia na madhara yao hadharani,.....Huu ni ubaguzi tena wa Hitler kwa kuwa wapo waasia wengi tu ambao hawana tatizo na mtu

Kwa hiyo unataka kutueleza kuwa Utanzania wao hauna asili ya Kiasia, au siyo Watanzania Wahindi?.
 
Granted, Nipashe si New York Times (ambao nao hukosea pia, lakini husahihisha) lakini hili wamezidisha.

Waliotajwa na Mengi hawakutajwa kwa sababu ya "uTanzania wao wa asili ya Asia" hasha.

Wametajwa kwa sababu ya ufisadi.Kwa hiyo kama wametokea kuwa Watanzania wenye asili ya Asia, hii haimaanishi wamekuwa mafisadi kwa sababu wao ni Watanzania wenye Asili ya Asia, tuna mafisadi wengi Watanzania weusi, na watanzania wenye asili ya Asia wengi ambao si mafisadi.

Kwa hiyo hilo andiko la Nipashe, ambalo linaweza kutafsirika kuwa "Mengi kawatolea uvivu watanzania wenye asili ya Asia" lina mislead kwa kuonyesha tatizo kuwa ni utanzania wenye asili ya Asia, badala ya kusisitiza vita dhidi ya ufisadi.

Mengi naye analeta maswali mengi kwa kutaja Watanzania wenye asili ya Asia tu, ina maana wao tu ndio mafisadi?
 
Pamoja na wachache watakaokereka ukweli ni kwamba kituo cha ITV kimepotosha kabisa kile kilichotokea kwenye Press Conference( Habari Maelezo) ukweli ni kwamba baada ya tamko kutolewa na mjumbe wa Baraza kuu Uvccm Taifa toka Tabora Ndg Patrick Kabaye, yaliulizwa maswali manne, na yalijibiwa yote na Katibu mhamasishaji Uvccm Mkoa wa Tabora Ndg Daniel Mhina kwa ufasaha swali ambalo halikujibiwa ni moja tu ambalo kuna mwandishi alitaka kujua endapo Bw Mengi hatawaomba radhi vijana wa Tabora watamchukulia hatua gani? viongozi hao waliokuwepo walijibu kuwa kwa heshima aliyonayo Bw mengi lazima tu ataomba radhi, ndipo mwandishi mmoja aliposisitiza tena je asipoomba? kibaya zaidi majibu yote fasaha yaliyojibiwa vizuri na Mhamasishaji wa mkoa ITV hawakuonyesha kabisa kwa maana walikata sauti huo nao si UFISADI? mbona vituo vingine kama DTV, chanel Ten nk vimerusha kile kilichojiri bila upendeleo!
 
viongozi hao waliokuwepo walijibu kuwa kwa heshima aliyonayo Bw mengi lazima tu ataomba radhi, ndipo mwandishi mmoja aliposisitiza tena je asipoomba? kibaya zaidi majibu yote fasaha yaliyojibiwa vizuri na Mhamasishaji wa mkoa ITV hawakuonyesha kabisa kwa maana walikata sauti huo nao si UFISADI? mbona vituo vingine kama DTV, chanel Ten nk vimerusha kile kilichojiri bila upendeleo!

Majibu yepi yaliyojibiwa vizuri? Ni upotoshaji gani huo?
 
Majibu gani yalijibiwa vizuri, mbona mie niliangalia channel ten sikusikia wakijibu maswali
 
Back
Top Bottom