Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by BAK, Apr 27, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,703
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Serikali yamgeuka Reginald Mengi kwa kauli ya mapapa wa ufisadi

  * Waziri Sophia Simba asema Mengi kachemsha
  *Mkuchika naye asema wanamchunguza


  Ramadhan Semtawa na Leon Bahati
  Mwananchi

  MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na George Mkuchika jana walimshambulia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi ambaye wiki iliyopita alitangaza majina ya wafanyabiashara watano wenye asili ya Kiasia, akisema ni mafisadi waliokubuhu.

  Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo walisema mfanyabiashara huyo wa jijini Dar es salaam "amechemsha".

  Mengi alitangaza majina ya wafanyabiashara hao Alhamisi iliyopita akisema ni kati ya watu wasiozidi 10 ambao alidai wanaifilisi nchi na kutaka wadhibitiwe mapema kabla hawajaitingisha na kuiyumbisha nchi.

  Hata hivyo, Mengi, ambaye alidai katika taarifa yake kuwa juhudi za Rais Jakaya Kikwete zinakwamishwa na watu hao, hakueleza jinsi watano hao wanavyoitafuna nchi zaidi ya kusema kuwa wanatorosha fedha wanazozipata 'kifisadi'.

  Jana, kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mawaziri hao wawili walitoa kauli za kumshambulia mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, kauli ambazo zinadokeza mtazamo wa serikali katika mjadala unaoendelea wa vita dhidi ya ufisadi na vinara wake.

  Waziri Simba, ambaye wizara yake pia inawajibika katika vita dhidi ya ufisadi, alisema: "Kakosea... watoto wa mjini wanasema kachemsha."

  Simba alitoa msimamo huo jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kufungua semina ya wadau wa vyama vya siasa kuhusu namna ya kuiboresha Sheria ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

  Simba alisema Mengi hana mamlaka hayo ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  Kabla ya kujibu swali kuhusu kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki televisheni ya ITV na kituo cha redio cha Radio One Stereo, kutaja majina ya watu hao aliowaita mafisadi papa, Simba alihoji: " Hapa kuna mtu wa ITV?."

  Baadaye alisema: "Sikilizeni, kwanza kitendo alichokifanya Mengi si sahihi, kakosea hawezi kuhukumu watu, mamlaka hayo anatoa wapi?"

  Simba, huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa akitafuta jukwaa kuzungumzia suala hilo, alisema Mengi amekosea kwa kuwa baadhi ya watu aliowataja wana kesi mahakamani.

  "Anahukumu watu," alisema. "Kuna mtu kama Jeetu (Patel) ana kesi mahakamani (EPA), sasa unapokuja kusema ni fisadi wakati mahakama haijathibitisha, unakuwa na maana gani.

  "Kwanza kwanini awatuhumu wafanyabiashara wenzake tu, ina maana si ana nia mbaya nao."


  Alisema Mengi amechukua uamuzi huo kama vile serikali, wakati serikali ipo siku zote na imekuwa ikifanya kazi zake kwa umakini kwa kufuata misingi ya sheria.

  "Serikali ipo na inafanya kazi kwa misingi ya sheria, sasa yeye kukaa na kutangaza watu nasema si sahihi kabisa. Mahakama pekee ndiyo inaweza kumtia mtu hatiani, lakini huwezi kuhukumu watu kama hakuna mamlaka."


  Waziri Simba, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alisema Mengi hapaswi kutumia vyombo vyake vibaya.

  "Asitumie vyombo vyake kufanya atakavyo yeye. Huwezi kukaa katika chombo chako na kuanza kuhukumu watu. Kila mtu akifanya hivyo itakuaje," alihoji.

  Akiongea na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kauli ya Simba, Mengi alisema: "Namuombea kwa Mwenyezi Mungu na kwa maskini wa Tanzania ili wamsamehe kwa sababu hajui anenalo."


  Mengi hakutaka kuzungumza zaidi kuhusu hatua hiyo ya Mama Simba.


  Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.

  Mkuchika alisema jijini Dar es Salaam jana kwa sasa serikali inafanya uchunguzi juu ya suala hilo na itatumia mikanda ya video pamoja na maelezo ya kimaandishi aliyoyatoa Mengi siku alipokutana na waandishi wa habari.

  "Tumekusudia kupata ule mkanda wa video, pia tusome maelezo yake ya kimaandishi... tukigundua kuna mahala ambapo sheria haikuzingatiwa, (Mengi) atachukuliwa hatua," alisema Mkuchika.

  Mkuchika alisema serikali imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu wengi, wakishutumu hatua iliyochukuliwa na Mengi, ambaye pia anamiliki viwanda vya vinywaji.

  Bila kutaka kuwataja majina, Mkuchika alisema miongoni mwa walalamikaji, wapo walioeleza kuwa vyombo vya habari vya mfanyabiashara huyo havikuwatendea haki watuhumiwa waliotajwa kuwa ni mafisadi wakuu.

  Alisema ni kutokana na vyombo hivyo kuwataja majina watuhumiwa bila ya kuwapa fursa ya kujibu madai dhidi yao.

  Waziri Mkuchika alipotakiwa kueleza siku ambayo uchunguzi huo utakamilika, alijibu wananchi wanapaswa kuwa watulivu kwa sababu serikali ikimaliza kuchunguza, itawatangazia yale waliyobaini.

  Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi takribani mitatu kwa Mengi kuingia katika mvutano na serikali baada ya kuvutana mapema mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kutokana na kutangaza kuwa kuna mipango ya kumfilisi na kumuua.

  Mengi pia amewahi kujikuta katika malumbano na watendaji wa serikali hasa na waziri wa zamani wa nchi, ofisi ya rais (utawala bora), Wilson Masilingi alipotoa tuhuma kuwa suala la utoaji zabuni ya ununuzi wa hoteli ya Kilimanjaro, hivi sasa inajulikana kama Kilimanjaro Kempiski, kulikuwa na kitu alichokiita "mchezo mchafu".

  Suala hilo liliamsha malumbano makali, lakini liliishia hewani.

  Katika tuhuma za wiki iliyopita, Mengi aliwahusisha wafanyabiashara hao watano na kashfa za wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) na uuzwaji wa jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF).


  Mengi, ambaye kituo chake cha televisheni cha ITV kiliwahi kuendesha mchezo mkubwa wa bahati nasibu ya Jackpot Bingo, pia aliitaja Bahati Nasibu kuwa katika tuhuma hizo, pamoja na mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma.
   
  Last edited by a moderator: Apr 28, 2009
 2. M

  Maua Mazuri Member

  #2
  Apr 27, 2009
  Joined: May 28, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo Mengi bado anaonekana kama ana ajenda ya kisiasa, sidhani kama Serikali imejiridhisha na utetezi wake alioutoa siku za nyuma kuwa hana nia ya kugombea urais. Hadi hapo watawala watakapo amini kuwa Mengi ni Raia mwema, hata afanye jambo jema kiasi gani bado litapokelewa na wakubwa kuwa linalengo la kisiasa. I hope wananchi wengi wanamuelewa anachokipigania.
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mengi ana haki ya kusema atakacho kama raia mwengine. Kama kuna mtu ambae ameona kuwa amechafuliwa jina lake kutokana na kauli yake, ampeleke mahakamani. Serikali ikijiingiza kwenye hili itakuwa imechemsha. Kwa kufanya hivyo wataonekana kama vile wanatumiwa na waliotajwa. Wangejimazia tu.

  Amandla.....
   
 4. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Sofia Simba anafahamiana na Rostam Aziz kwa muda mrefu, hivyo siwezi kushangaa kama atamvalia njuga Mengi.
   
 5. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Ni vizuri tukaanza kugudua kundi la mtandao ambalo limetufikisha hapa tulipo.
  Sofia na wenzake wanamwandama Mengi kwa kuwa amegusa mtandao wao.
  lakini hakuna mapana yasiyokuwa na mwisho,Serikali yetu isitumie rungu ambalo limepewa na wananchi kunyamanzisha watu.je mkuchika na Sofia ndo wasemaji wa wahusika? mbona hawajawa msitari wa mbele kutusaidia kuelimisha umma kuhusu KAGODA kama walivyojitokeza katika hili.
   
 6. M

  Mwakaleli Member

  #6
  Apr 27, 2009
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna watu ambao huwa nawaona hawastahili kabisa kuwa viongozi ni huyu Sophia Simba, hawezi hata kujenga hoja za msingi kama vile hajaenda shule kabisa. Sijui mkuu wa kaya alitumia kigezo gani kumpa uwaziri huyu mama. Maana bado anaonekana ana mawazo ya mtaani. Serikali inafikiria kumchukulia hatua? ama kweli sasa hii serikali inabidi kuisaidia, kwa sababu inafuatilia mambo yasiyo na tija kwa watanzania wasio na uwezo hata wa kununua chumvi na panadol ya sh 100. Bado inaendelea kuwatesa hawa watu wasio na hatia, je walifanya makosa kuzaliwa Tanzania? mpaka hawa wezi na sirikali isiyo jali hawa watanzania. Kama hawa mawaziri walikosa vitu vya kuongea na waandishi wa habari wangekaa kimya kwa sababu wanaendelea kutupa taka kwenye dampo lao la CCM. Na sasa taka zinakaribia kujaa na zinatoa harufu mbaya na ni hatari kwa maisha ya watanzania. Ikiwezekana inabidi watanzania tuamue kulifunga hili dambo la sivyo tutaendelea kupata madhara ya kiafya na kiuchumi.
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Apr 27, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ndio maana nasema,mengi anafikiri kikwete mwenzake ...kumbe atamtosa...kila siku anajifanya kumpigia kikwete debe..sasa sofia simba huyo confidant na mwenza wa kikwete amemtosa......kikwete ni mnafiki....anamchekea mengi jono la pembe!!!
   
 8. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono!
  Nadhani hawa wanasiasa, wanafanya assessment ya maneno ya Mengi bila kumbukumbu kwamba huyu si mwanasiasa. Mengi is just another whistler, bila kujali matumizi ya TV. Maneno yake yanaweza kutumiwa na serikali kama njia ya kupata ushahidi, kama atashirikishwa.

  Wanatakiwa wasijali kujulikana kwake maana huyu sidhani kama kwa nafasi yake anaweza kuingilia uhuru wa mahakama.

  Sasa naanza kuwa na mashaka na serikali ktk kupambana na ufisadi. Hivi kweli wangekuwa wanachunguza tuhuma za Mapinduzi ya serikali na jamaa akatoa tahadhari kama hiyo, leo hii asingelindwa kwa nguvu zote ili awape taarifa muhimu kama hizo?
   
 9. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Walivyo na miguu myepesi kuchunguza mambo yanayotetea uhafidhina! wangekuwa wepesi kuchunguza upotevu wa pesa si tungekuwa tumefika mbali kimaendeleo! Kwanza Sophia asituchefua maana ofisi yake ndio kichaka cha mafisadi.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapa ndo pa kujua nani yuko upande upi?, badala wafatilie tuhuma wao wana dili na mtoa tuhuma? Serikali ndo itakuwa imechemsha big time, kujiingiza kuwatetea mafisadi, Ila wana sahau kwamba kuna nguvu kubwa ya umma nyuma ya wanao pambana na mafisadi! They want to see it, haya jaribuni kumgusa mzalendo Mengi!
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama kuna mtu aliyechemsha hapa basi ni Sofia Simba.
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  whatever happened to presumption of innocence?
   
 13. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii ndio sifa ya mawaziri mabwege hulopoka tu na ni vigumu kuwatofautisha bosi wao aliyewapa madaraka. Naamini kama waziri anaweza kuwa ***** kiasi hiki, basi bosi wake hawajibiki vyema. Lkn katika mapambano yoyote ya kudai haki, wasaliti huwa hawakosekani. Ndio hawa mawaziri mabingwa wakujikomba kwa wahindi wakiwasaliti maskini watanzania wenzao.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kangaroo court haina hiyo presumption.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Apr 27, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,789
  Likes Received: 5,048
  Trophy Points: 280
  ..alichotamka Sophia ndiyo msimamo wa serikali na CCM.

  ..tuliwaambia kwamba CCM na SERIKALI ni MAFISADI lakini hamkusikia.
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  court ipi hiyo?
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Na hawa mawaziri waache kuwatisha na kuwafunga mdomo wananchi!
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mengi kawa out hawa watu kama mafisadi, kama mtu anataka kumtaka Mengi ushahidi ili ku substantiate maneno yake nitaelewa.

  Lakini habari ya kusema Mengi kachemka bila hata ya kujua Mengi ana ammunition gani, kesho keshokutwa unaweza kuaibika ukashindwa hata kumuomba radhi.

  Mengi si mahakama na hana wajibu wala mamlaka ya kupitisha hukumu, yeye anatoa maoni yake kama mtanzania huru, kama mtu anajiona kapakaziwa na Mengi mahakama ziko, anaweza kufungua mashtaka.

  Yaani hao walioitwa mafisadi wenyewe hawajasema viwaziri visharukia issue? Whats wrong with this picture, some puppeteering going on here?
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani huyu sofia simba ni hawara ya rostam aziz kwa sababu kama ana akili asinge tetea wahindi wanaoiba mali ya watanzania maskini na kupeleka canada na kwingineko. Hivi huyu mama ana mume kweli??au ana mume *****?? si ajabu rostam ndo ngoma yake!!!

  Ah.... mpaka inachefua. Hivi rais alitoa wapi viwaziri pambafu kama hivi???
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hawa ndiyo Mawaziri wetu, Sasa kama akigundua sheria imefuatwa na aliowataja mengi ni mafisadi kweli atafanya nini?. Mbona hawa watu wanakuwa watumwa wa mafisadi wa ki..... kiasi hiki kwenye nchi yao?, Hawa ndiyo wanaoshirikiana na hawa mafisadi kuuza nchi. They are so biased, so bulled. Mengi yeye kaongea kama Mengi na kaitisha vyombo vya habari ambavyo hata hao mafisadi waliotajwa wana haki ya kuviita na kuongea navyo. Kinacho wachokonoa hawa mawaziri njaa ni nini hasa?. Kisa gwiji katajwa ?
   
  Last edited: Apr 27, 2009
Loading...