...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

Nape Nnauye tunaomba wewe mwenyewe kwa mikono yako utuwekee video nzima na kwa nini unamsubili security guard aweke? Naomba uweke yote si vipande na kama unayo kwa nini umechelewa? Nape kwanini usiweke video nzima hapo juu? Au twambie uliongea nini kuhusu wazee wetu?

Nape Nnauye kwa nini hutaki Wazee wetu waendelee kuishi?
 
Last edited by a moderator:
Hii kauli ya huyu nape ya kutaka wazee wafe inawezekana ikawa ni matokeo ya frustration alizokua nazo kwa kutomjua baba yake

Na hata pale alipokua anaing'ang'ania familia ya nnauye, hiyo familia ilimkataa na kujitenga nae. Ushaidi ni lile tangazo la kumbukumbu ya mzee nnauye

Hapa mtapoteza muda kumjadili mtu mwenye frustration

Nape anapaswa kuwaomba radhi wazee wetu yani hata wazee waliomlea wakina MAKAMBA NA MANGULA HATAKI WAENDELEE KUISHI
 
Nape kwanini unawakosesha wazee wetu usingizi?
 
Mkuu Nape Nnauye.
Kweli kabisaa..mwisho wa uongo ni aibu kama ulivyoabika kwenye kuvuana Magamba

Du! Kumbe hata big baby umevundua mwisho wa uongo ni aibu? Afadhali. Pengine utajirekebisha. Unatakiwa vilevile kujua. Kuwa mwisho wa kuropoka ni aibu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nadhani Nape Nnauye anatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kudai tunatumiwa/tunatumwa bila kuja na uthibitisho wowote.Pia kama mnataka hilo litimie Mwambie Nape alete video ambayo imethibitishwa kuwa ni original maana video hii haionyeshi alipoanzia wala alipoishia.Je hiyo video haijawa edited na kukatwa baadhi ya vipande?If you come,come correctly otherwise don't come at all!

Zako/Zenu mnazoleta huwa ni Original?!Hizi ni fikra zinazoongozwa na watembea na sumu mifukoni kwa ajili ya kuteketezan wenzao.
 
Si uilete wewe hiyo utuhakikishie kuwa ulikuwa si muongo, unangoja nini? Unanchekesha!

Unajua huyu Dogo ana matatizo sana,tangu atuhumiwe kutembea na sumu mfukoni kwa ajili ya kutaka kuwauwa wenzake amekuwa na matatizo sana,sijui mwisho wake utakuwaje,lakini nilishasema kwamba huyu naye mwisho wake utakuwa mbaya kama wale wenzake ambao aliwasababishia matatizo mpaka wakaondolewa,huu ndio uzuri wa kutumika!.
 
Ninashindwa kuelewa mtu anavyotoa hoja, akajibiwa kwa hoja anaishia kutukana bila kujitathimini ni wapi amekosolowa ili ajirekebishe baadae akijua siasa zipo kila siku....

Nape! Mwanasiasa mzuri ni yule anayeyafakari kabla ya kuongea, ni yule anayejiandaa na kupangilia agenda za kuzungumza kabla hajapanda jukwaani,ni yule anayethamini na kutathimini aina ya hadhara/wahusika anaotaka kuwa-address siku hiyo, ni yule anayesoma upepo wa siasa upo upande gani na unavuma kuelekea upande gani, lazima ujue unatumia chanel gani kufikisha ujumbe. Hayo ni machache tu, naomba nizungumzie kidogo.

1.Kutafakari kabla ya kuongea. Hapa ni lazima ujue aina ya topic iliyoko mezani, lazima ujue umuhimu wa topic hiyo kwa mahali hapo, manufaa, changamoto na suluhu kwa wanaosikiliza. Usipende kuongelea topic bila kuangalia umuhimu, manufaa yke na jns ya kukabidhiana na changamoto zitakazojitokeza wakt au baada ya kuzungumza!

2. Aina ya hadhara, ni lazima ujue ni watu gani unawapelekea ujumbe wako, ni wazee, vijana, watu wa kati, wasomi au watoto! Lazima ujue mwitikio wao, je wanapokeaje ujumbe wako? Je wananielewa? Wana idea na hiki ninachokizungumza? Wanafaidka kwa sasa au ni baadae, watakuwa na subira? Mood zao ziko je katika kuniskiliza? Wamekula wakashiba,? Ni wahusika? Usije ukaingiza mguu wa kulia kwenye kiatu cha mguu wa kushoto.

3. Upepo wa siasa unavuma vipi ni suala la msingi sana, kwa mfano upepo wa siasa kwa Tanzania ni wa mageuzi na macho ya watu wengi hata wanasiasa wanalenga zaidi kujua je huyu au chama hiki kitatufanyia nini iwapo kitapewa serikali, sasa lazima ujue kila unachozungumza watu wanakitafsiri mara mbili yako, wanaangalia faida ya moja kwa moja, muda wa hiyo faida na madhara yake! Je huyu ni nani? Anataka nini na ni kwa faida gani kufanya hvyo?

4. Chanel au lugha ya kufikisha ujumbe wako kwa hadhara. Lazima ujue lugha unayotumia kama ni vijana unatumia lugha ya ujana, kama ni wasomi kuna lugha yao, kama ni akina mama kuna lugha yao, KAMA NI WAZEE KUNA LUGHA YAO, watu wa kati na watoto wote wana lugha yao. Kwa mfano refer Mbunge wa mbeya mjini Mh. Sugu alitumia lugha gani kuwatuliza vijana/ wamachinga waliokuwa wanavutana na polisi kule mbeya.

Tatizo ninalo liona kwa ndugu zangua hawa wanasiasa , hawajui kama siasa ni science pia wanashindwa kujua kwamba wao ni viongozi na siku zote psychology ya watu wengi wanaamini kwamba kiongozi anajua zaidi kuliko wale anaowaongoza hata kama wamemzidi kielimu au uzoefu! Ndugu yangu Nape najua labda ni kutokujua au makusudi kamili huwa napenda sana kumsikiliza sana lakin kuna kitu anakosa kati ya hivyo nilivyovitaja hapo juu! Yeye mwenyewe akitafakari atajua au wenzangu walionielewa watamsaidia.

Inawezekana mbinu iliyoasisiwa kihalali kwamba hata kama nikiongea kitu ambacho hakijafurahisha wazee au vijna hakuna wakuniuliza, kwa kuwa mimi ni mimi watake wasitake wataheshimu tu na watanipigia makofi. Kwa hili la kusema wale wote wanaoshabikia serikali tatu ni wazee wanaokaribia kufa... Hata mimi lilinishutua sana japokuwa kila mtu atakufa..... Jaribu kufanya siasa sa kisomi kwa kuzingatia taaluma yako...

Asanteni
 
Unajua kuwajibu nyie ni kupoteza muda. Namshukuru securitygurd kwa kuweka kipisi cha kwanza. Video hizi zilikuwa kwenye mitandao siku ya pili tu baada ya stori kuchakachuliwa. Wengine hapa wanadai ilikua wapi!! Weka hiyo video yako,usitishie nyau hapa!Lakini cha kufurahisha hata walioandika walishaikanusha lakini kwakukisa hoja mnahangaiaka sanaaaaa! Poleni sina muda wa kupoteza kuwajibu tena kwa hoja mfu!

"Kaka hawa kazi yao ni kutembea na sumu mifukoni,wamejaza sumu kwenye mifuko ya nyuma ya suruali,mbele kulia na kushoto,kwenye mifuko ya shati na hasa ukizingatia mashati yao yalivyo na mifuko mingi,wameijaza hadi kwenye soksi kwa ajili tu ya kuwasaka wenzao kwenye baa!,hii ni hatario sana halafu unaambiwa eti kijana msomi?!"
 
Jahazi linazama jipangeni upya. Namheshimu sana mzee Mengi asinge andika uwongo.
 
Kama kawaida ya CCM, Naona hapa Mkuu umeshachakachua hii video. Kwa nini usiweke video nzima watu wachambue wenyewe?
Au unadhani sisi ni TBC wakuambiwa 'weka hiki', 'toa hiki'!
 
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!




- Yaani this is the best of JF, yaani FACTS zunawekwa hapa wananchi wanapewa mchele na pumba ahsante sana Katibu wa Uenezi wa Chama changu this is just super!!

KIDUMU CHAMA CHA MAPUNDUZI!!

Le Mutuz
 
Last edited by a moderator:
Zahazi linazama jipangeni upya. Namheshimu sana mzee Mengi asinge andika uwongo.

Hapo kwenye red vipi wakati unaandika sumu ilikuwa imedondoka kutoka mfukoni mwako ukawa unaiokota ili wasikuone?!
 
Zahazi linazama jipangeni upya. Namheshimu sana mzee Mengi asinge andika uwongo.

- Mzee Mengi kwenye hili alichemka maana hata gazeti lake Nipashe halikukubali uongo huu wa gazeti la Mtanzania ambao baadaye wao wenyewe wameomba radhi kwamba sio kweli, kurusha rusha Majina kama kina Mengi ni dalili za kukosa hoja.

Le Mutuz
 
Kama ccm imekufa kiasi hiki basi inatisha sana,kwa kauli hii ya Nape bas alitakiwa awe ametoswa kutoka kwenye nafasi yake kitambo,lakini kwa sababu ccm ni la kufa sishangai sana kuona bado anadunda kwenye nafasi yake.
 
Nape anaweweseka, kila kitu kipowazi.

Hawezi kukujibu,inaonekana wakati anaandika Sumu ilidondoka kutoka mfukoni mwake akawa anawahi kuiokota ili watu wasiomuone,si unajua kazi yao ni kutembea na sumu mifukoni wakiwasaka wenzao hadi kwenye baa?!,na leo kwa sababu ni EID,sijui?!
 
- Yaani this is the best of JF, yaani FACTS zunawekwa hapa wananchi wanapewa mchele na pumba ahsante sana Katibu wa Uenezi wa Chama changu this is just super!!

KIDUMU CHAMA CHA MAPUNDUZI!!

Le Mutuz

Dude, Please !!!!

Is this the best you can do ? You guys.....!
 
Back
Top Bottom