...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

Ni kweli Nape Nnauye hata wewe vua Gamba ilikuaibisha na sijui hatima yako Lowassa akiingia

Ana muogopa sana hadi anatamani afe.

Hivi Nape Nnauye hawa wazee wetu wame kukosea nini?

Malecela,WARIOBA,SALIM,MAKAMBA,KINGUNGE,LOWASA,MANGULA,SITTA,MAKINDA,MKAPA,MTEI,MAMA MARIA NYERERE,KARUME.

Nape Nnauye TAFADHALI TUWEKEE VIDEO KUANZIA MWANZO AU UKISHINDWA HIVYO ITISHA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUWAOMBA MSAMAHA WAZEE.

HII KAULI YA NAPE INAWAKOSESHA USINGIZI WAZEE WETU,TAFADHALI NAPE RUDISHA USINGIZI WA WAZEE WETU.
 
Last edited by a moderator:
Nape Nnauye hana exposure au ameamua kupotosha akijua kuwa anaoongea nao hawana uelewa wa dunia hii.
Hoja zake ni nyanya zisizo na mashiko.
Tutamjibu hoja moja baada ya nyingine, tunachomtaka asikimbie.

Ninajiuliza hivi hawa ndio viongozi waliompokea Nyerere kijiti kweli!
 
Last edited by a moderator:
Bila kutumia uongo na ahadi za kitapeli Chadema hawawei kupata wateja

Ili ahadi ionekane ni ya kitapeli ni pale itakaposhindwa kutekelezwa na yule aliyeahidi. Chadema wanatoa ahadi za kutekelezwa endapo wataingia madarakani na hawajapata hiyo nafasi ya kuingia madaarakani ili waitekeleze, sasa iweje uziite ni za kitapeli? Je zile ahadi walizo ahidi waliopo madarakani na hazijatekelezwa utaziitaje? Najaribu kupanua upeo wa kufikiri!
 
Nadhani Nape Nnauye anatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kudai tunatumiwa/tunatumwa bila kuja na uthibitisho wowote.Pia kama mnataka hilo litimie Mwambie Nape alete video ambayo imethibitishwa kuwa ni original maana video hii haionyeshi alipoanzia wala alipoishia.Je hiyo video haijawa edited na kukatwa baadhi ya vipande?If you come,come correctly otherwise don't come at all!
Ben kama kama kuchukuliwa hatua za kinidhamu ungetakiwa kuchukuliwa wewe

kwasababu kuna siku ulileta taarifa za uongo kuhusu kijana aliyepigwa katika uchaguzi

mdogo wa madiwani kata ya kaloleni nikakwambia habari ile ni ya uongo lete uthibitisho

hukuleta lakini siku shangaa hapa si upo "home ground" na walio kuletea taarifa nawajua.

Cc.Mungi,Crashwise,Arushaone
 
Nape jipangeni upya. Ccm mumeshaiua wenyewe. Laana inayoonekana sasa itaendelea kuwatafuna siku zote. Chama kikiendelea kukutumia wewe na mwigulu hamtakifikisha 2015. Siasa chafu dharau zenu ndizo zinaharakisha msiba wenu.
 
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!



Yaani kweli kabisa hoja ya Saanane ndo unaijibu na haka kavideo chako ambacho hakana hata punje ya majibu kwa maswali aliyouliza Ben?
Ningekuelewa haraka sana kama ungeweka hoja baada ya hoja kwa yote aliyoainisha Ben.
Inaitwa ukomavu wa kiakili na fikra na nguvu ya hoja hususan kwa mtu kama wewe unaeongea na vijana wengi Tz hii kupitia ofisi uliyopewa.
Jipange. La sivyo utashangaa vijana wadogo zaidi wanapewa kazi yako hiyo ya uenezi hapo mbeleni.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
MwanaDiwani; Embu muulize kaka yako Nape, ni kwanini amekata kipande cha video badala ya kuiweka yote au alishuka ghafla kama Malaika kutoka mawinguni bila utangulizi wala hitimisho lolote?
 
Last edited by a moderator:
Yaani kweli kabisa hoja ya Saanane ndo unaijibu na haka kavideo chako ambacho hakana hata punje ya majibu kwa maswali aliyouliza Ben?
Ningekuelewa haraka sana kama ungeweka hoja baada ya hoja kwa yote aliyoainisha Ben.
Inaitwa ukomavu wa kiakili na fikra na nguvu ya hoja hususan kwa mtu kama wewe unaeongea na vijana wengi Tz hii kupitia ofisi uliyopewa.
Jipange. La sivyo utashangaa vijana wadogo zaidi wanapewa kazi yako hiyo ya uenezi hapo mbeleni.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Hana uwezo wowote wa kupambana na Kamanda Ben Saanane kwa hoja.
 
Last edited by a moderator:
fikiria tena ulichosema labda utafuta kauli yako.vipi wale waliotuambia maisha bora kwa KILA mtanzania?hakuna uongo hapo na hali halisi?
 
Kama wewe unajua imechakachuliwa, lete ya kwako ambayo haijachakachuliwa tuione.

Jenga hoja kwa evidence na siyo mihemko ya kibavicha.

Hizi kelele unazopiga ni kelele za debe tupu. Huoni huyo aliyeleta uwongo kuhusiana na hili swala ameamua kufunga thread yake haraka na kuukimbia uongo wake.
.....Naunga mkono kuwa Video ni muendelezo wa uchakachuzi wa Magamba. Kama mliweza kuchakachua mkanda wa Lwakatare mkaonekana hakuna kesi ya ugaidi, mtashindwa hiyo clip ya dakika kadhaa. Hivi katika huo mkutano Nepi alihutubia dakika 11?
 
By Ben Saanane
Ushahidi kamili ni upi ikiwa hawezi kututhibitishia kuwa video haijawa edited?

Weka wewe iliyo halisi
Mkuu mshauri Nape Nnauye aweke video yote kuanzia mwanzo.

Hivi Nape Nnauye kwanini unawakosesha wazee wetu usingizi kwa kauli zako za kuwaombea vifo? Hivi unajua kwa nini tuliumbwa na mdomo mmoja na masikio mawili?

Nape wazee wetu wamekukosea nini?
 
Last edited by a moderator:


Sehemu nyingine ya Video hii hapa...

Ukiwa mtu mzima na unaelewa nchi utajenga hoja kwa misingi ya kuboresha, Nape ni moja ya vijana wanaoelewa na siasa zake zimekuwa safi na kukubalika tumsikilize na hapa.
 
Last edited by a moderator:
Isingekuwa kupigwa ban ningewatukana wajinga fulani hivi kama Chris Lukosi,mwanawadiwani,wa wapumbavu wengine ambao wanatetea ujinga,si mmesoma tweet ya Mzee Mengi? Inamaana alikuwa anamzulia Nape? Kwa kipi alicho nacho hadi Mengi amzulie kwamba muache Mungu afanye kazi yake? Hivi nyie mnaotetea mnatetea mama zenu? Mbona ukweli mnaujua lakini mnajidai hamnazo?

Mnajipendekeza nini sasa mtu ameongea Tanzania nzima wamesikia,eti kuna wapumbavu wachache wanabisha ili iweje?

Bahati mbaya wazee wenyewe wamesikia alichokisema Nape nyie mnamtetea simply mnapewa posho,ukweli uko palepale na hautafutika hata akija na usanii na utapeli hautakubalika,alishasema na wamelisikia sasa nyie wapambe ambao hamna kazi mnaomsafisha sijui mtaelewekaje na inawezekana wooote mnaomsafisha hamna wazazi ni watoto wa mitaani hivyo hamjui thamani ya wazee

UKWELI UTABAKI PALEPALE PAMOJA NA CLIP FAKE HAUTABADILIKA wewe Nape hauna wazazi uliokotwa au ulitolewa kwenye mti
 
Jamani tusikimbilie hoja dhaifu ya kudai video imeeditiwa tafuteni ushauri kwa wataalamu wa video.
Siasa si kila jambo kupinga kwa sababu wewe ni mpinzani kuna wakati kuna hoja za msingi inabidi mkubaliane.
 
Nape haishii tu kumwita Dr. Slaa kibabu kwamba hana faida na asisikilizwe, amenukuliwa "wazee wanaopendekeza serikali 3 wanasumbuliwa na uzee na wanasubiri kufa", 'kama ni wanaccm ni oil chafu'

chanzo:Mawio

My Take:kama ni kweli
nape hana wazazi?
hana heshima na anajitabiria kifo ujanani na kutoufikia uzee

Nape ni janga! Nilitegemea kabla ya kuja kumkanusha saanane aje kulikanusha gazeti la chama chake "Uhuru" lililo andika kuhusu kauli zake tata ikiwemo ile "wazee wanao taka serikali 2 ndio wenye akili timamu"

Ukiipima hiyo kauli maana yake ni kwamba wazee wote wasio taka serikali mbili ndio watakufa bali wenye kutaka serikali ndio wataishi milele, akaongeza "wenye kutaka serikali mbili ndio wenye akili timamu", maana yake wote wasio taka serikali mbili wana matatizo ya akili.

Hivi kati ya Nape na Ben nani anatakiwa kuambiwa "mwisho wa uwongo ni aiubu?" Tuhukumu kupitia video clip ya dakika 11 ambayo haina mwanzo wala mwisho au tuamini kauli kupitia tweet za mzee Mengi na gazeti la chama chake kuwa nape ana kauli tata?!
 
Back
Top Bottom